Ufafanuzi: Nafuu ya kodi unapoagiza/kununua gari za Afrika Kusini

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Habari wakuu.

Naomba kutoa angalizo ama ufafanuzi kidogo kuhusu nafuu ya kodi pale utakapoagiza gari zilizotengwa South Afrika.

Nimeona mijadala mingi humu watu wakisema kuna unafuu mkubwa wa kodi ukiagiza gari South Afrika kuliko Japan.

Hilo jambo linaweza kua sahihi ama linaweza kua na ukweli ndani yake ila kuna masharti magumu ya kufanya ili kupata hiyo nafuu.

Ni kweli South Afrika wanatengeneza baadhi ya models za magari 'exclusively' ya makampuni makubwa Duniani, kuna assembly plants za magari kama Toyota, Ford, Hammer, Benz, BMW, Nissan nk.

Ni kweli pia kwamba kuna makubaliano ya nchi za kusini mwa Afrika ama SADC kupeana nafuu ya kodi iwapo hicho kitu kimetengenezwa ndani ya nchi wanachama. Tanzania na South Afrika ni wanachama hivyo mikataba hiyo iko halali kabisa.

Pamoja na hayo, sharti la kupata nafuu ya kodi ni iwapo tu gari utakayoiagiza ni brand new zero kilometers, haijawahi kutumika mahala popote.

Iwapo utaagiza gari yoyote used kutoka kwa Mandela, hata kama ni ya mwaka huu 2022 ila used basi utalipa kodi kama vile ukiagiza Japan ama mahala popote Duniani.

Hivyo, usidanganywe na mtu kwamba South Afrika kuna nafuu ya magari, ni magari mapya tu.

Jambo lingine, kwa uzoefu wangu, Magari ya south Afrika hasa used yamechoka kuliko ya Japan ama Thailand. Kukuta gari ya South Afrika ya mwaka jana leo hii ina Kilomita 100,000 ni kawaida sana ila kwa Japan ni ngumu sana.

Wakuu, nimeona nijaribu kuchangia uzoefu wangu.

Nashukuru sana.
 
Huu uzoefu umeupata wapi mkuu gari za SA hata maroli ni imara sana kwa nini mnapenda kupotosha jamii ili iweje humu nikituma Gari za SA ukiambiwa ni used utakataa na pia ili upate huo unafuu wa kodi ni lazima uwe na karatasi za export za SA ambazo wanatoa Sunnyside pale...
 
Hizi gari ndio unasema zimechoka sana..
 
Attachments

  • IMG-20221109-WA0084.jpg
    IMG-20221109-WA0084.jpg
    228.3 KB · Views: 106
Mtoa hoja hii acha kupotisha watu humu, gari za SA hasa used ni bora mno kuliko makachakacha kutoka Japan na elewa hizi used cars kutoka SA nyingi haziji kwa kubebwa hapa,zinatambaa zenyewe hadi hapa ,from jhb hadi Dar ni zaidi ya 3500km,gari mbovu haifiki umbali huo
 
Huu uzoefu umeupata wapi mkuu gari za SA hata maroli ni imara sana kwa nini mnapenda kupotosha jamii ili iweje humu nikituma Gari za SA ukiambiwa ni used utakataa na pia ili upate huo unafuu wa kodi ni lazima uwe na karatasi za export za SA ambazo wanatoa Sunnyside pale...
Unachoongea ni kuhusu unafuu wa kodi ama uchakavu?

Kuhusu unafuu wa kodi hiyo ndio fact, haijalishi una document gani lakini ili upate nafuu lazima gari iwe mpya.

Kwa uchakavu hayo ni maoni yangu na uzoefu wangu.

Ahsante.
 
Mtoa hoja hii acha kupotisha watu humu, gari za SA hasa used ni bora mno kuliko makachakacha kutoka Japan na elewa hizi used cars kutoka SA nyingi haziji kwa kubebwa hapa,zinatambaa zenyewe hadi hapa ,from jhb hadi Dar ni zaidi ya 3500km,gari mbovu haifiki umbali huo
Kuna hoja mbili, uchakavu na kodi, wewe umekomalia uchakavu ila hoja ya msingi ya unafuu wa kodi umeikwepa.

Anyway, kuhusu uchakavu hayo ndio maoni yangu kwa uzoefu wangu ila kuhusu unafuu wa kodi huo ndio ukweli.

Shukrani sana.
 
Unachoongea ni kuhusu unafuu wa kodi ama uchakavu?

Kuhusu unafuu wa kodi hiyo ndio fact, haijalishi una document gani lakini ili upate nafuu lazima gari iwe mpya.

Kwa uchakavu hayo ni maoni yangu na uzoefu wangu.

Ahsante.
Pick up land Cruiser ya Japan inalipiwa 30m mpaka 33milion wakati ya kutoka SA ni 18m mpaka 25m inategemeana na mwaka na gari hiyo hiyo ikitumika Malawi wakipiga hesabu za depreciation inalipiwa si chini ya 22m nalipia gari mara kwa mara Kasumulu au mpaka wa Tunduma...sema kuanzia mwezi wa saba zimeongezeka hata tractor hawataki used ya kutoka Nje kodi ni kubwa bora ununue jipya bovu linalotengenezwa ndani...
 
Kuna hoja mbili, uchakavu na kodi, wewe umekomalia uchakavu ila hoja ya msingi ya unafuu wa kodi umeikwepa.

Anyway, kuhusu uchakavu hayo ndio maoni yangu kwa uzoefu wangu ila kuhusu unafuu wa kodi huo ndio ukweli.

Shukrani sana.
Chuga pana dogo kaagiza gari imefika 28m Rav 4 sijui ya 2006/2007 wakati SA Rav 4 ya 2012 kuendelea ndio itaingia kwa gharama hiyo SA gari ni cheap tofauti na Nchi zingine na wao wanazingatia sana mwaka wakati Japan wanazingatia soko lipoje..gari ya mufa mrefu itakua na bei ndogo sokoni tofauti na hizi za miaka ya karibuni..
 
Tuunganishe juhudi tupige hii kazi boss. We si upo SA? Mie nipo dsm.
 
Tafuta wateja tuu Mkuu gari yeyote inakuja iwe Lori mpaka hizi gari ndogo...gari za Friedge Truck zilifutwa Kodi mwaka huu huyo jamaa mwenye uzi huu atakua ajui pia tukimwambia na hiyo ni fursa ataikataa...iwe tani moja pick up walitoa nadhani VAT utalipia vitu vingine...
 
Back
Top Bottom