BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Kama ni mfuatiliaji wa aina za Magari yanayomilikiwa na Watanzania walio wengi, utagundua kuwa asilimia kubwa wananunua Magari ambayo ni "Used" tena kwa miaka 10 au 15 nyuma, na yote ni sababu ya wingi wa Kodi za ajabu ajabu kutoka Mamlaka za nchi hii.
Tofauti na ukienda nchi za wenzetu mfano Afrika Kusini, Kenya au Rwanda, Watu wanaendesha Matoleo mapya ya Magari kwasababu Serikali zao zimeweka kodi rafiki za uagizaji Magari ili kuepuka kuwa dampo la Magari chakavu.
Hapa kwetu Tanzania kuwa na gari jipya ni kama anasa au unaonekana fisadi. Wakati ni jambo la kawaida kwa wenzetu. Ifike hatua nchi iwe na mipango ya maana kwa raia wake. Iweke kodi rafiki ili kuvutia Watu kumiliki Magari mapya sio vyuma chakavu.
Lakini pia, kodi rafiki zitavutia hata Watu kununua magari kutoka nchi nyingine kwa wingi sio Tanzania inaonekana soko la magari ya Japan tu tena hasa Toyota.