Tips zitakazokusaidia kutunza gari lako likadumu muda mrefu zaidi

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
19,089
49,833
Wakuu.
Najua wengi uwa tunajiuliza, inakuaje gari la mwaka 2015 linatoka Japan likiwa na Kilometa 100,000 linafika Tanzania baada ya mwaka mmoja linaonekana chakavu ova limekaa miaka 20 mbele?

Ni kweli tatizo linaweza kua gari lenyewe, miundombinu yetu, mmiliki/dereva, hali ya hewa na sababu zingine kadhaa.

Sasa leo tukuongelee wewe mmiliki/dereva, ni vipi unaweza kuchukua taadhali ili gari lako likadumu muda mrefu zaidi.

1. Kufanya "preventive maintenance" ndani ya muda ulioshauriwa.

Wataalamu wanasema Kinga ni Bora kuliko Tiba. Basi na ww ni bora ukabadirisha engine oil, gearbox oil, na vimiminika vingine ndani ya muda au kilometa sahihi kama walivyo recommend kwenye user manual.
images (2).jpeg

Kwenye issue ya vimiminika jitahidi pia utumie vimimika sahihi vilivyoshauriwa na watengeneza gari. Mfano Oil na ATF sahihi.

2. Endesha gari taratibu

Huna haja kuioverstress gari kwa kuendesha kwa nguvu kama Vin Diesel, kwa kuaccerelate haraka na kubrake haraka.
images (6).jpeg

Kama unataka kufika mahala mapema bora ukaondoka dakika kadhaa kabla kuliko kujichelewesha ili njiani ukiwashe. Ni hatari kwa gari lako, wewe na watumiaji wengine wa barabara.

3. Baada ya kutotumia gari masaa mengi, iache ipate moto kidogo kabla hujaanza kuiendesha kwa nguvu.

Magari ya siku hizi yame advance, sio kwamba uiache iungurume nusu saa kama mabasi ya mikoani ila ukiwasha, ule muda unafungua geti, unaonganisha cm Bluetooth, kama sekunde 30 zinatosha gari kuwarm up, na oil inakua imezunguka vizuri.

Ukitoka safari mdefu, mfano umeendesha masaa 6 nonstop, iache pia ata dakika chache.

4. Sio kila mahala lazima uende na gari, jifunze kutumia usafiri mwingine.

Kuna mahali unaweza kuitwa na mshikaji au demu ila njia ni mbaya, ruksa kumwambia chukua boda tukutane barabarani hapa. Au kama vipi park gari mahala ww kisha nenda na boda.
e620587f-96c3-43a5-b7c4-1ce76c3242ce.__CR0,0,970,600_PT0_SX970_V1___.jpg

Magari yenye ground clearance ndogo ukiforce mahali utakwangua bampa hasara yake ni kubwa na ata ukienda kutengeza bado itaacha kovu.

Pia, Jitahidi kupunguza short trips.

5. Usile (vyakula vyote ulivyoelewa), ndani ya gari.
images (7).jpeg

Just dont.

6. Lifanyie usafi gari mara kwa mara.

Kama unapeleka car wash za bei ndogo it's okay, ila angalau mara moja peleka car wash yenye vacuum cleaner na pressure washer itasaidia.

7. Park pahala penye kivuli muda wa jua kali, au nunua car cover kama unapark kwa muda mrefu.
images (8).jpeg

Ila jitahidi usipark chini ya miti mara kwa mara, tumeona mars nyingi miti kuanguka au majani kuingia sehemu za uwazi kisha kuleta madhara mbeleni.

Okay nimeona tukumbushane izo tu, na nyingine wataongeza wadau.

Pamoja.
 
Wakuu.
Najua wengi uwa tunajiuliza, inakuaje gari la mwaka 2015 linatoka Japan likiwa na Kilometa 100,000 linafika Tanzania baada ya mwaka mmoja linaonekana chakavu ova limekaa miaka 20 mbele?

Ni kweli tatizo linaweza kua gari lenyewe, miundombinu yetu, mmiliki/dereva, hali ya hewa na sababu zingine kadhaa.

Sasa leo tukuongelee wewe mmiliki/dereva, ni vipi unaweza kuchukua taadhali ili gari lako likadumu muda mrefu zaidi.

1. Kufanya "preventive maintenance" ndani ya muda ulioshauriwa.

Wataalamu wanasema Kinga ni Bora kuliko Tiba. Basi na ww ni bora ukabadirisha engine oil, gearbox oil, na vimiminika vingine ndani ya muda au kilometa sahihi kama walivyo recommend kwenye user manual.
View attachment 2945418

Kwenye issue ya vimiminika jitahidi pia utumie vimimika sahihi vilivyoshauriwa na watengeneza gari. Mfano Oil na ATF sahihi.

2. Endesha gari taratibu

Huna haja kuioverstress gari kwa kuendesha kwa nguvu kama Vin Diesel, kwa kuaccerelate haraka na kubrake haraka.
View attachment 2945419
Kama unataka kufika mahala mapema bora ukaondoka dakika kadhaa kabla kuliko kujichelewesha ili njiani ukiwashe. Ni hatari kwa gari lako, wewe na watumiaji wengine wa barabara.

3. Baada ya kutotumia gari masaa mengi, iache ipate moto kidogo kabla hujaanza kuiendesha kwa nguvu.

Magari ya siku hizi yame advance, sio kwamba uiache iungurume nusu saa kama mabasi ya mikoani ila ukiwasha, ule muda unafungua geti, unaonganisha cm Bluetooth, kama sekunde 30 zinatosha gari kuwarm up, na oil inakua imezunguka vizuri.

Ukitoka safari mdefu, mfano umeendesha masaa 6 nonstop, iache pia ata dakika chache.

4. Sio kila mahala lazima uende na gari, jifunze kutumia usafiri mwingine.

Kuna mahali unaweza kuitwa na mshikaji au demu ila njia ni mbaya, ruksa kumwambia chukua boda tukutane barabarani hapa. Au kama vipi park gari mahala ww kisha nenda na boda.
View attachment 2945420
Magari yenye ground clearance ndogo ukiforce mahali utakwangua bampa hasara yake ni kubwa na ata ukienda kutengeza bado itaacha kovu.

Pia, Jitahidi kupunguza short trips.

5. Usile (vyakula vyote ulivyoelewa), ndani ya gari.
View attachment 2945421
Just dont.

6. Lifanyie usafi gari mara kwa mara.

Kama unapeleka car wash za bei ndogo it's okay, ila angalau mara moja peleka car wash yenye vacuum cleaner na pressure washer itasaidia.

7. Park pahala penye kivuli muda wa jua kali, au nunua car cover kama unapark kwa muda mrefu.
View attachment 2945422
Ila jitahidi usipark chini ya miti mara kwa mara, tumeona mars nyingi miti kuanguka au majani kuingia sehemu za uwazi kisha kuleta madhara mbeleni.

Okay nimeona tukumbushane izo tu, na nyingine wataongeza wadau.

Pamoja.
NIKINUNUA NDINGA NITAFUATA HIZI TIPS..

We unaeendesha gari langu huko japan siku zako zinahesabika, jiandae
 
Hiyo namba 4 imenisaidia Sana kwenye kutunza gari yangu.... Ukiachana na mambo ya kufanya service Kwa wakati Jambo kubwa Kwa wamiliki wa magari ni kutoazimisha gari.

Kipindi kama hiki cha mvua huwa napaki gari ndani au huwa napaki gari chamazi shelli alafu nachukua bodaboda Hadi home
 
Asante kwa hizi tips;

Nyongeza- Usipeleke gari yake kwenye gereji za uchochoroni kwa sababu zifuatazo
1. Hawana vifaa vya kitaalamu
2. Hawana mafundi wa uhakika; wengi wamejifunza au bado wapo kwenye mafunzo
3. Kuibiwa kwa mtindo wa kuchomoa baadhi ya vifaa ni suala la kawaida kabisa.
 
Back
Top Bottom