UDSM kwa sasa ni cha kata, imebaki historia tu

UDSM kwa sasa ni cha kata, imebaki historia tu

Weka ushahidi wa division 3 kuwepo udsm.
Mbona wapo nina wanangu wawili mmoja alisoma Civil na mwingine electro mechanical engineering 2009 wote walikuwa na three ya 13.

Ila katika dunia ya sasa tuendayo hasa field hizi za IT,mtu anaweza soma chuo cha kawaida ila akawa anajiongeza kujisomea online courses mkikutana field huko lazima awakimbize haijalishi umesoma chuo gani.
 
Dah naona huu mjadala sasa nikama battle ya udsm na udom na sijui nini huwa kinasababisha huu uadui
Ipo hivi nimebahatika kusoma hivi vyuo vyote viwili udsm undergraduate na udom master lakini pia nimefanya kazi udom
Mtazamo wangu hii vyuo vyote ni bora kwa kozi fulani
Mfano leo nikiwa natafuta mwl au mtaalamu wa IT binafsi nitaenda udom maan hawa vijana wamepikwa kwel na wameiva tuna kutana nao field wapo vizuri sana na kwa IT vijana wa udom wanaenda sambamba na teknologia lakini pia nikiwa na tafuta wanasheria na mhandisi nitaenda udsm hawa vijana wapo vizuri sana kwanza wana workshop za kutosha na wana walimu wabobezi kwenye mambo hayo
Lakini kwa kozi zilizobaki vyuo vyote naona havipishani sana
Kingine mnaposema vijana wa udsm wapo empty ata basic za computer tu hawawez jaman hivi vyuo udaili watu zaid ya 30 elfu hivi unadhan hao wote watakuwa smart. Hizo case hazipo udsm tu nikaribu vyuo vyote
Kumaliza huu mjadala jaman hamna chuo cha hovyo hapa bongo vyuo vyote vinajitahid kwa nafasi yake
Udsm watabaki kuwa na heshima yao ya kuwa chuo kikongwe hapa nchini
Udsm inamiaka 60 udom mwaka huu ndo yalikuwa mahafali ya 13
Najivunia kusoma vyuo hivi vikuu vikubwa hapa nchini udsm na udom

Mwisho vyuo vyote ni bora
Sifurahishwi na hii battle na mbaya zaidi imeingia hadi kwa watendaji wa serikali, huko mbeleni haitakuwa na matokeo mazuri.
 
Hakuna kitu kibaya Kama inferiority complex.

UDSM kinatoa elimu ya kawaida tuu Kama vilivyo vyuo vingine Duniani.

Ishu kubwa kwenye Jambo lolote ni Brand.

Ukishajenga Brand umejenga kila kitu.

Hiyo IPO hata kwenye biashara,

Au kazi.

Kwa mfano wanajeshi wame-brandiwa kuwa wanauwezo mkubwa wamapigano Hali inayofanya jamii kuwaheshimu na kuwaogopa.
Lakini haimaanishi kuwa ndani ya jamii hakuna watu wasiowanajeshi wanaoshindwa kuwapiga hao wanajeshi.

Ishu hapo ni Brand.

Udsm imeshajitengenezea jina na hiyo ni sifa mojawapo ya kuwa kinajielewa.
 
Udsm ni chuo kilichokuwa kimejipambanua miaka hiyo kama chuo bora kabisa katika ukanda huu wa maziwa makuu na afrika kwa ujumla kwa kuzalisha viongozi na wasomi mahili katika nyanja ya siasa,uchumi,na sheria.

Sifa hiyo ilikijengea chuo uimara na kukifanya kiwe chuo bora afrika mashariki na kati kwa wakati ule huku kikiwa nguzo imara na tunu ya elima ya juu ya Tanzania miaka ile na siyo sasa.

Huku systems zote za nchi zikiwa zinasimamiwa na kuongozwa na wasomi na viongozi kutoka UDSM, ambao hata hvyo hawajaweza kulinufaisha taifa kimaendeleo bali wakijikita kwenye utunganji wa sera za hovyo na kusaini mikataba mibovu ya kulikwamisha taifa kimaendeleo.

Kwa sasa siyo tu kwamba elimu inayotolewa na udsm ni mbovu bali hata mifumo na sera za uendeshaji wa chuo hiki zimeparaganyika hasa kuanzia mwaka 2010, hivyo kupeleka kuzalisha wasomi wenye uelewa mdogo wa mambo na wasioweza kushindana tena katika soko la ajira kama zamani.

Hali hii imepelekea chuo hiki kujikuta kwenye ushindani mkubwa kutoka vyuo vingine kama SUA ambacho naweza sema ndicho chuo pekee kinachofanya tafiti za kweli na zenye tija hapa Tanzania ,MUHAS, MZUMBE,UDOM,NELSON MANDELA na ARDHI.

Kutokana na sababu hizo chuo hiki kimebaki kutembelea historia kwenye nyanja zote na kujikita kwenye siasa ya elimu, kutokana na wigo mpana wa kuwa na wasomi wengi waliotapakaa kila idara za serikali, wasomi hawa muda wote wamejikuta kwenye propaganda za kushindanisha ubora wa elimu ya UDSM na vyuo vingine hasa UDOM, Kikifika mbali hadi kuanzisha course zisizotambuliwa na serikali mfano molecular biology and Biotechnology, hiki ni kiashiria tosha kwamba chuo kimeshuka ubora kwani kushindana na chuo chenye miaka 12 tu kwenye taaluma huku chenyewe kikiwa na miaka zaidi ya 40 haileti afya kwenye taaluma.

Katika jambo la kushangaza muhitimu bora wa chuo hichi mwaka huu aliyefanyiwa branding ya kutosha na kupewa airtime ya kutosha kwenye vyombo vya habari alisikika akisema "hakupata mkopo, alipewa boom tu", hii ni aibu kubwa kwa muhusika na chuo pia, na kama aliyesema hivyo angekuwa muhitimu wa chuo kingine hasa UDOM mitandaoni kusingekalika, kwa wasomi wa udsm kuhoji ubora wa muhitimu, GPA na chuo husika.

Mwaka huu ndugu yangu alihitimu shahada ya kemia Udsm akiwa na GPA ya 3.9, lakini hajuhi chochote kuhusu carbon NMR spectrum, IR spectrum, GC-MS,LC-MS, TGA vitu ambavyo ni basics kwenye instrumental analysis, hiki ni kiashiria kwamba ubora wa elimu ya udsm umeshuka.

Mwaka huu nilikuta muhitimu wa zoology stationery akiwa na cheti safi kabisa chenye GPA 4.2 kutoka Udsm, jambo la kushangaza muhitimu huyo hata basics za computer applications hajuhi, yaani alishindwa kabisa kutumia copy, cut, paste vitu ambavyo ni vya kawaida sana, je project alifanyaje?, anajua mwenyewe, hii yote inaonyesha jinsi gani ubora wa Udsm umeshuka.

Mwisho kabisa katika elimu hakunaga umungu mtu, ukijisahau kidogo tu wenzako wanakuongoza, hivyo udsm ijitafakari upya, udsm siyo ya kushindana na Udom nyakati hizi labda miaka ijayo , udsm mnatakiwa mshindane na NAIROBI,MAKERERE,PRETORIA universities kutokana na ukongwe wenu kwenye taaluma.
Mbona wewe umeandika "hajuhi' tena mara mbili?
 
Wewe mwanafunzi wa udsm, naomba unitajie tafiti tatu tu ambazo zitalisaidia taifa zilizofanywa na udsm 2021.
Nawe toa tafiti hizo 3 kutoka vyuo vyako ulivovitaja amabazo zitalisaidia Taifa,
Unahemkwa kwa kukosa nafas ya kusoma UD, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Namba hazi danganyi.. haya tumia akili hapa..

Wakati udsm ikiwa top 10 SUA ilikua nafasi za 80.

Leo udsm imeshuka toka top 10 mpaka nafasi ya 42 na SUA imepanda toka nafasi za 80 mpaka 51!

Ukitumia akili, je SUA na udsm ni chuo kipi kinapanda kielimu?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] SUA bado sana kuja kufikia UDSM, hebu kunyweni maji na m relaaaax.
 
Ninapowaambia ubora wa chuo umeshuka, profs, Dr,wahitimu wa udsm waliojaa humu wanaishia kwenye upepo wa chuo ni bora, chuo kinazidi kuporomoka kila siku, hii ni alarm mbaya kwa chuo kama udsm, lazima wajitafakari
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hizi hasira zako hapana, mweeeeh
 
" Mwaka huu nilimkuta muhitimu wa zoology stationary akiwa na cheti safi......". Kuna Stationary (imara) na Stationery (vifaa vya (kuandikia) ofisini na mashuleni, Duka au sehemu au mahali vifaa vya mashuleni au ofisini vinapouzwa). Nikusaidie tu njia rahisi ya kutofautisha maneno haya Stationary ( 'a' stands for stand) na Stationery ( 'e' stands for envelops).
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mpe za uso huyo.
 
Umenikumbusha mhitimu wa UD ualimu Physics & Chemistry aliletwa shuleni kwetu hajui hata kuandaa prac za Chemistry olevel. Alikuwa anamwita teacher wetu wa Dip anamuandalia fresh.
Uongo mkubwa huu, khaaaaah
 
Daaa, 'ma-left overs' & 'manunga-liyembe' ya UDOM pole sana, hata siku moja huwezi msikia graduate wa UDSM akianzisha uzi wa kipumbavu kama huu wa kulia lia eti wahitimu wa chuo flani sijui wanapendelewa etc.

Yaani nilivyo angalia paragraph mbili tuu za mwanzo za huu uzi moja kwa moja nikabaini mleta uzi ni 'li left over' la UDOM, na kwa kweli serikali isifanya jitihada za kukinusuru na kukiwezesha hiki chuo , elimu itaingia majaribuni. wapo baadhi wa hatimu wa UDOM ambao wapo vizuri, ila shida ni hii type ya mleta huyu crapist , kwanza wanajaza server za JF kwa mi- crap, Mods ebu futilieni mbali huu uchafuu..
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dah naona huu mjadala sasa nikama battle ya udsm na udom na sijui nini huwa kinasababisha huu uadui
Ipo hivi nimebahatika kusoma hivi vyuo vyote viwili udsm undergraduate na udom master lakini pia nimefanya kazi udom
Mtazamo wangu hii vyuo vyote ni bora kwa kozi fulani
Mfano leo nikiwa natafuta mwl au mtaalamu wa IT binafsi nitaenda udom maan hawa vijana wamepikwa kwel na wameiva tuna kutana nao field wapo vizuri sana na kwa IT vijana wa udom wanaenda sambamba na teknologia lakini pia nikiwa na tafuta wanasheria na mhandisi nitaenda udsm hawa vijana wapo vizuri sana kwanza wana workshop za kutosha na wana walimu wabobezi kwenye mambo hayo
Lakini kwa kozi zilizobaki vyuo vyote naona havipishani sana
Kingine mnaposema vijana wa udsm wapo empty ata basic za computer tu hawawez jaman hivi vyuo udaili watu zaid ya 30 elfu hivi unadhan hao wote watakuwa smart. Hizo case hazipo udsm tu nikaribu vyuo vyote
Kumaliza huu mjadala jaman hamna chuo cha hovyo hapa bongo vyuo vyote vinajitahid kwa nafasi yake
Udsm watabaki kuwa na heshima yao ya kuwa chuo kikongwe hapa nchini
Udsm inamiaka 60 udom mwaka huu ndo yalikuwa mahafali ya 13
Najivunia kusoma vyuo hivi vikuu vikubwa hapa nchini udsm na udom

Mwisho vyuo vyote ni bora
Kwanini masters hukusoma pia UDSM? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbona wapo nina wanangu wawili mmoja alisoma Civil na mwingine electro mechanical engineering 2009 wote walikuwa na three ya 13.

Ila katika dunia ya sasa tuendayo hasa field hizi za IT,mtu anaweza soma chuo cha kawaida ila akawa anajiongeza kujisomea online courses mkikutana field huko lazima awakimbize haijalishi umesoma chuo gani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] three ya 13 akapata nafas UD coet? Jaman hamuoni hata aibu kudanganya wazi wazi lol.
 
Back
Top Bottom