UDSM kwa sasa ni cha kata, imebaki historia tu

UDSM kwa sasa ni cha kata, imebaki historia tu

Elimu inayotolewa vyuoni inaweza kuwa ni ile ile tu kwa vyuo vingi maana hata waalimu wa vyuo vingine wengi wanatokea udsm.

Ishu kubwa katika hivi vyuo ni uzito wa jina la chuo, baaasi??

Mtu anaweza kuwa na gpa ya 4.3 kutoka vyuo vingine lakini mtu wa Udsm mwenye gpa ya 2.9 akapewa uzito kwasababu tu kasoma udsm.

Ukiangalia vizuri unakuja kugundua vyeo vingi sana vya serikalini vya juu juu wengi ni wahitimu wa udsm, ni kama vile wanabebana kifamilia.

Kupata nafasi tu ya kusoma udsm ni heshima kubwa sana, mtu anaweza kawa kapata divisioni 3 form 4, division 3 form 6 lakini akiinga tu udsm ana uwanja mpana sana kuliko kipanga aliepiga division 1 kali form 4 na 6 ila akaishia kusomea vyuo vingine.

Kwa lugha nyepesi, UDSM NI BABA LAO!!
Hapo kwenye baba lao, ndo ulichokosea mkuu
 
Mie sina ufahamu mkubwa sana wa mambo. Ila nilishangaa sana mhitimu wa degree wa UDSM hajui kutuma email. Yaani hajui subject inamanisha nini na kwenye email content iweje. Hajui hata maneno ya kuanzia yanakuwaje na akituma email eti anatuma ikiwa haina subject. Nilishangaa sana.
 
Kulikuwa na post yenye kuonyesha mapungufu makubwa ya maonyesho ya UDSM.
Ikiwezekana, iletwe please
 
Sijabahatika kufika elimu ya chuo ila hapo ni sawa na kumuelewesha kijana kitanzania wa kisasa kwamba Hata android wana aina ya simu kali kuliko Iphone.
 
Dah! Jamaa umeandika sana. Kiufupi umejaribu kuonesha mapungufu yaliyopo kwa wahitimu wa UDSM ambao wewe binafsi unadai kuwafahamu. Sasa katika kuendelea na utafiti wako hebu tafuta waajiri au wakuu wa vitengo katika sehemu tofauti tofauti uwaulize utendaji kazi wa wahitimu wa UDSM na vyuo vingine upoje na wakwaambie wao wanaona wahitimu gani ni afadhari. Binafai nimehitimu UDSM na kazini nipo na wahitimu kutoka vyuo tofauti tofauti, wengi wao Wana chuki na UD kwa sababu tu walikosa nafasi pale. Kiutendaji huwa tupo tofauti sana!! Vyuo vingine vijifunze UDSM na sio kuwatuma wahitimu wake kupondea
 
Unataka vigezo gani wewe, jadili hoja usilete maneno tu nitajie tafiti hata tano mwaka 2021 zilizofanywa na Udsm kama ni chuo bora kweli kama kinavyojipambanua ambazo zimeleta au zinaendelea kuleta matokeo chanya kwenye sekta yeyote.
Hili swali gumu sana. najua hapa umemshika pabaya
 
Mie sina ufahamu mkubwa sana wa mambo. Ila nilishangaa sana mhitimu wa degree wa UDSM hajui kutuma email. Yaani hajui subject inamanisha nini na kwenye email content iweje. Hajui hata maneno ya kuanzia yanakuwaje na akituma email eti anatuma ikiwa haina subject. Nilishangaa sana.
Badala ya kushangaa mueleweshe!
 
UDSM ni chuo bora Tanzania, No doubts
Pengine ni bora kwa sababu vyuo vingine Tz ni HOVYO kabisa LABDA!
 
Back
Top Bottom