UDOM na PhD kwa wanasiasa. Nini chanzo cha mchezo huu katika elimu ya nchi hii?

Walioanza siyo tu UDOM, ni UDSM na OUT. SUA sijawahi kuwasikia wakitoa digrii za kisiasa kwa wanasiasa. Kwa ufupi wanasiasa wanaharibu elimu ya nchi hii kwa kushirikiana na viongozi wa vyuo ambao wanapewa kuviongoza kisiasa.

Cheo cha Vice Chancellor (VC) ni muhimu sana ktk uongozi wa chuo cha kitaaluma, bahati mbaya nafasi hiyo sasa wanapewa kutokana na uhusiano wao na wanasiasa. Hii ni kwa vyuo vyote vya serikali; ARDHI, UDSM, SUA, MUHAS, NM-AIST, Mzumbe pamoja na colleges zote! Nasema zote!

Watu wanateuliwa hata bila uwezo na kupewa kwa sababu ya kupendana na wanasiasa. wengine hata uhusiano wao na wananchi mitaani ni kama 'wahuni' anaowasma ndg. Polepole. Cheo cha juu ni Chancellor ambacho pia kinashikiliwa na wanasiasa kwa vyuo vyote;

UD - Jakaya Kikwete
SUA - Sinde Warioba
Mzumbe -Mohammed Shein
MUHAS -Ali Hassan Mwinyi
ARDHI -Cleopa Msuya, sasa ni Othman Chande

Sasa wanasiasa wantaka PhD! Vyuo vinawasaidia kwa nguvu zote ili wapate Ph.D. Bahati mbaya sana UDOM imekuwa ni kinara wa kutoa digrii hizi. Nini Sababu kubwa?

Maoni yangu ni kwamba UDOM imekuwa ni chuo cha kufurahisha wanasiasa badala ya taaluma. UDOM ilianza vibaya na sasa inaendelea vibaya. ilianza na viongozi kutoka UD, waliokuwa wameshindikana kuishi na wenzao kijamii, wakapewa nafasi kirafiki, kisiasa. Hata wanafunzi wa digrii ya kwanza wanafundishwa kwa ubora wa matatizo tu, halafu tunashangaa kusikia wakiwa bize na ngono na waalimu wao. Kwa Ph.D Wanakiuka hata sheria zao za ki-taaluma.

Jafo na Biteko wamepewa Ph.D bila kutimiza vigezo vya kitaaluma. Hawajafanya tafiti za kuwawezesha kupata Ph.D. pia hawajatoa machapisho kutokana na tafiti zao kama zilivyo taratibu za chuo. Mbaya zaidi, Ph.D zao zimeandikwa na wanataaluma hao hao wanaotakiwa kuwasimamia na wataandika machapisho kwamba ni ya wanafunzi wao wanasiasa, kumbe ni wao wenyewe waalimu. Hii ni aibu ya kitaaluma na ni aibu ya kisiasa.
Wapo hata huku Vingunguti wanauza supu za mapupu na makongoro
 
Back
Top Bottom