UDOM na PhD kwa wanasiasa. Nini chanzo cha mchezo huu katika elimu ya nchi hii?

Mi binafsi kama mwanazuoni wa chuoni nasema kama vyuo hivyo vimeamua kuwazawadia PhD wanasiasa kama njugu zinavyogawiwa acha wagawiwe tu.

Sometimes kipofu akiamua kumuongoza kipofu mwenzake acha wote wadumbukie shimoni. Mi sinaga huruma na mtu au taasisi ya kipumbavu. Kwani chuo kikuu cha Dar es Salaam kilikuwa nafasi ya ngapi kwa ubora Afrika miaka ya 90 na leo hii kipo nafasi ya ngapi? Leo hii VC wa UD na genge lake wanahangaika kuiokoa UD isiendelee kuporomoka lakini wapi....ukifanya upumbavu mmoja wa msingi utakugharimu milele.

UD walianza hivi hivi, kudharau mambo ya misingi: mfano degree zilizopaswa kuwa miaka minne kuzifast track kuwa miaka mitatu ili kukidhi matakwa ya wanasiasa, kutoboresha miundombinu ya kufanyia tafiti, n.k. Madhara yake wamekuja kuyaona miaka 20 baadaye, I swear elimu inayotolewa UD leo hii yaani ni bora mtoto akaende straight veta after form six.

Ni suala muda tu hivi vyuo vyetu kupuuzwa kabisa kabisa na jamii.
 
Biteko na Jaffo kutwa wako kwenye kazi za uwaziri, na kwa kipindi cha Mwendazake wizara zao(madini na TAMISEMI) pamoja na ya Nishati zilikuwa ndiyo mawaziri wako "on the move 24/7". Wanapata wapi muda wa kufanya utafiti chini ya Magufuli?

Labda kwa vile Magufuli naye PhD yake ilikuwa ya hivyo hivyo pengine alibariki UHUNI huu wa PHD mchongo. Wananunua tu, hamna namna wanaweza kufanikisha kwa miaka 4.

Ni bora usome Master's degrees hata 2 kwa sasa kuliko PhD kwa watu wasio vyuoni au kwenye tafiti. Hizi PhD zimepoteza hadhi na ndiyo maana hata yule mjinga wa darasa la Saba kutoka Geita ameagiza ya kwake kwa USD 500 na kapewa.

Nashauri ikiwezekana TCU ifanye academic audit ya haya matakataka ya UDOM na ikikuta kuna mianya iwachukulie hatua stahiki
 
Muhas nani aende shule serious kiasi hicho, au aende SUA, shule haitaki mbwembwe, zamani walikuwa wanaendaga Open university Sasa hivi wanakimbilia Udom, kwenye mtelezo wa Ganda la ndizi.
 
Sio PHD tu hadi master wanapewa kuna jamaa alisomaga hapo alishangaa siku ya graduation eti wapo na simbachawene naye amegraduate wakati hakuwahi kumuona hata siku moja class.
Akawauliza jamaa wa evening program wakasema hawajawahi kumuona.
Wakati huo simbachawene naibu waziri wa nishati muda mwingi alikuwa dsm
 
Walioanza siyo tu UDOM, ni UDSM na OUT. SUA sijawahi kuwasikia wakitoa digrii za kisiasa kwa wanasiasa. Kwa ufupi wanasiasa wanaharibu elimu ya nchi hii kwa kushirikiana na viongozi wa vyuo ambao wanapewa kuviongoza kisiasa. Cheo cha Vice Chancellor (VC) ni muhimu sana ktk uongozi wa chuo cha kitaaluma, bahati mbaya nafasi hiyo sasa wanapewa kutokana na uhusiano wao na wanasiasa. Hii ni kwa vyuo vyote vya serikali; ARDHI, UDSM, SUA, MUHAS, NM-AIST, Mzumbe pamoja na colleges zote! Nasema zote! Watu wanateuliwa hata bila uwezo na kupewa kwa sababu ya kupendana na wanasiasa. wengine hata uhusiano wao na wananchi mitaani ni kama 'wahuni' anaowasma ndg. Polepole. Cheo cha juu ni Chancellor ambacho pia kinashikiliwa na wanasiasa kwa vyuo vyote;
UD - Jakaya Kikwete
SUA - Sinde Warioba
Mzumbe -Mohammed Shein
MUHAS -Ali Hassan Mwinyi
ARDHI -Cleopa Msuya, sasa ni Othman Chande

Sasa wanasiasa wantaka PhD! Vyuo vinawasaidia kwa nguvu zote ili wapate Ph.D. Bahati mbaya sana UDOM imekuwa ni kinara wa kutoa digrii hizi. Nini Sababu kubwa?

Maoni yangu ni kwamba UDOM imekuwa ni chuo cha kufurahisha wanasiasa badala ya taaluma. UDOM ilianza vibaya na sasa inaendelea vibaya. ilianza na viongozi kutoka UD, waliokuwa wameshindikana kuishi na wenzao kijamii, wakapewa nafasi kirafiki, kisiasa. Hata wanafunzi wa digrii ya kwanza wanafundishwa kwa ubora wa matatizo tu, halafu tunashangaa kusikia wakiwa bize na ngono na waalimu wao. Kwa Ph.D Wanakiuka hata sheraia zao za ki-taaluma.

Jafo na Biteko wamepewa Ph.D bila kutimiza vigezo vya kitaaluma. Hawajafanya tafiti za kuwawezesha kupata Ph.D. pia hawajatoa machapisho kutokana na tafiti zao kama zilivyo taratibu za chuo. Mbaya zaidi, Ph.D zao zimeandikwa na wanataaluma hao hao wanaotakiwa kuwasimamia na wataandika machapisho kwamba ni ya wanafunzi wao wanasiasa, kumbe ni wao wenyewe waalimu. Hii ni aibu ya kitaaluma na ni aibu ya kisiasa.
Akina Shabani Mlacha sijui yuko wapi siku hizi yule mpuuzi.
 
Dr. Nchimbi, sikumbuki vzr kama Master yake au Udr yenye utata. Lkn alitunukiwa SUA
 
Tanzania ni nchi huru na ina viwango vyake vya Phd ambavyo ni bora na tofauti na vile vya mabeberu, kigezo ni lazima uwe mwanaccm.
Mwandosya huyo
IMG-20211218-WA0005.jpg
 
Back
Top Bottom