UDOM na PhD kwa wanasiasa. Nini chanzo cha mchezo huu katika elimu ya nchi hii?

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
3,981
2,041
Walioanza siyo tu UDOM, ni UDSM na OUT. SUA sijawahi kuwasikia wakitoa digrii za kisiasa kwa wanasiasa. Kwa ufupi wanasiasa wanaharibu elimu ya nchi hii kwa kushirikiana na viongozi wa vyuo ambao wanapewa kuviongoza kisiasa.

Cheo cha Vice Chancellor (VC) ni muhimu sana ktk uongozi wa chuo cha kitaaluma, bahati mbaya nafasi hiyo sasa wanapewa kutokana na uhusiano wao na wanasiasa. Hii ni kwa vyuo vyote vya serikali; ARDHI, UDSM, SUA, MUHAS, NM-AIST, Mzumbe pamoja na colleges zote! Nasema zote!

Watu wanateuliwa hata bila uwezo na kupewa kwa sababu ya kupendana na wanasiasa. wengine hata uhusiano wao na wananchi mitaani ni kama 'wahuni' anaowasma ndg. Polepole. Cheo cha juu ni Chancellor ambacho pia kinashikiliwa na wanasiasa kwa vyuo vyote;

UD - Jakaya Kikwete
SUA - Sinde Warioba
Mzumbe -Mohammed Shein
MUHAS -Ali Hassan Mwinyi
ARDHI -Cleopa Msuya, sasa ni Othman Chande

Sasa wanasiasa wantaka PhD! Vyuo vinawasaidia kwa nguvu zote ili wapate Ph.D. Bahati mbaya sana UDOM imekuwa ni kinara wa kutoa digrii hizi. Nini Sababu kubwa?

Maoni yangu ni kwamba UDOM imekuwa ni chuo cha kufurahisha wanasiasa badala ya taaluma. UDOM ilianza vibaya na sasa inaendelea vibaya. ilianza na viongozi kutoka UD, waliokuwa wameshindikana kuishi na wenzao kijamii, wakapewa nafasi kirafiki, kisiasa. Hata wanafunzi wa digrii ya kwanza wanafundishwa kwa ubora wa matatizo tu, halafu tunashangaa kusikia wakiwa bize na ngono na waalimu wao. Kwa Ph.D Wanakiuka hata sheria zao za ki-taaluma.

Jafo na Biteko wamepewa Ph.D bila kutimiza vigezo vya kitaaluma. Hawajafanya tafiti za kuwawezesha kupata Ph.D. pia hawajatoa machapisho kutokana na tafiti zao kama zilivyo taratibu za chuo. Mbaya zaidi, Ph.D zao zimeandikwa na wanataaluma hao hao wanaotakiwa kuwasimamia na wataandika machapisho kwamba ni ya wanafunzi wao wanasiasa, kumbe ni wao wenyewe waalimu. Hii ni aibu ya kitaaluma na ni aibu ya kisiasa.
 
yusufuj

JF-Expert Member
Sep 23, 2021
295
379
Hivi jamani hawa wastaafu huwa hawachoki? Sinde Warioba, Cleopa Msuya JK na wengine, kwa nini msikatae hizo nafasi? Kwani hakuna maprofesa waliostaafu toka vyuoni kama kina Mwandosya, na wengine wakapewa hizo nafasi jamani? Wanasiasa hawa sijui kama wanasaidia hivi vyuo sana
 
The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,554
7,637
Hivi jamani hawa wastaafu huwa hawachoki? Sinde Warioba, Cleopa Msuya JK na wengine, kwa nini msikatae hizo nafasi? Kwani hakuna maprofesa waliostaafu toka vyuoni kama kina Mwandosya, na wengine wakapewa hizo nafasi jamani?? Wanasiasa hawa sijui kama wanasaidia hivi vyuo sana

Mwandosy alikuwa mwenyekiti wa bodi ya chuo Mwalimu Nyerere memory academy kama sikosei akakosana na mwendazake akafurushwa kwa spidi ya wahuni.
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
3,822
5,683
Sio PHD tu hadi master wanapewa kuna jamaa alisomaga hapo alishangaa siku ya graduation eti wapo na Simbachawene naye amegraduate wakati hakuwahi kumuona hata siku moja class.

Akawauliza jamaa wa evening program wakasema hawajawahi kumuona.

Wakati huo Simbachawene Naibu Waziri wa nishati muda mwingi alikuwa dsm.
 
The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,623
14,058
Hivi jamani hawa wastaafu huwa hawachoki? Sinde Warioba, Cleopa Msuya JK na wengine, kwa nini msikatae hizo nafasi? Kwani hakuna maprofesa waliostaafu toka vyuoni kama kina Mwandosya, na wengine wakapewa hizo nafasi jamani?? Wanasiasa hawa sijui kama wanasaidia hivi vyuo sana
Bado wanawashwa washwa
 
fundimchundo

JF-Expert Member
Jul 23, 2010
548
807
Walioanza siyo tu UDOM, ni UDSM na OUT. SUA sijawahi kuwasikia wakitoa digrii za kisiasa kwa wanasiasa. Kwa ufupi wanasiasa wanaharibu elimu ya nchi hii kwa kushirikiana na viongozi wa vyuo ambao wanapewa kuviongoza kisiasa. Cheo cha Vice Chancellor (VC) ni muhimu sana ktk uongozi wa chuo cha kitaaluma, bahati mbaya nafasi hiyo sasa wanapewa kutokana na uhusiano wao na wanasiasa. Hii ni kwa vyuo vyote vya serikali; ARDHI, UDSM, SUA, MUHAS, NM-AIST, Mzumbe pamoja na colleges zote! Nasema zote! Watu wanateuliwa hata bila uwezo na kupewa kwa sababu ya kupendana na wanasiasa. wengine hata uhusiano wao na wananchi mitaani ni kama 'wahuni' anaowasma ndg. Polepole. Cheo cha juu ni Chancellor ambacho pia kinashikiliwa na wanasiasa kwa vyuo vyote;
UD - Jakaya Kikwete
SUA - Sinde Warioba
Mzumbe -Mohammed Shein
MUHAS -Ali Hassan Mwinyi
ARDHI -Cleopa Msuya, sasa ni Othman Chande

Sasa wanasiasa wantaka PhD! Vyuo vinawasaidia kwa nguvu zote ili wapate Ph.D. Bahati mbaya sana UDOM imekuwa ni kinara wa kutoa digrii hizi. Nini Sababu kubwa?

Maoni yangu ni kwamba UDOM imekuwa ni chuo cha kufurahisha wanasiasa badala ya taaluma. UDOM ilianza vibaya na sasa inaendelea vibaya. ilianza na viongozi kutoka UD, waliokuwa wameshindikana kuishi na wenzao kijamii, wakapewa nafasi kirafiki, kisiasa. Hata wanafunzi wa digrii ya kwanza wanafundishwa kwa ubora wa matatizo tu, halafu tunashangaa kusikia wakiwa bize na ngono na waalimu wao. Kwa Ph.D Wanakiuka hata sheraia zao za ki-taaluma.

Jafo na Biteko wamepewa Ph.D bila kutimiza vigezo vya kitaaluma. Hawajafanya tafiti za kuwawezesha kupata Ph.D. pia hawajatoa machapisho kutokana na tafiti zao kama zilivyo taratibu za chuo. Mbaya zaidi, Ph.D zao zimeandikwa na wanataaluma hao hao wanaotakiwa kuwasimamia na wataandika machapisho kwamba ni ya wanafunzi wao wanasiasa, kumbe ni wao wenyewe waalimu. Hii ni aibu ya kitaaluma na ni aibu ya kisiasa.
Je, ni kweli Wanasiasa Wanafanya PhD kama Wengine?

Nataka nishee mawazo yangu kuhusu Doctor Jafo S.S. kujipatia PhD. ndani ya muda. Kabla ya hapo niseme kwanza haya maneno yanayofuata.

Nimekumbuka wanasiasa wachache waliojipatia PhDs wakiwa mawaziri au vyeo vingine serikalini: Dr. Magufuli J.P.J., Dr. Nchemba, M.L., Dr. Biteko, M.D., et al.

Nianze kwa kukumbusha kwamba kusoma PhD ni kugumu sana, nadhani mtakubaliana nami. Kuanza kuandaa proposal, ifikie viwango vya kuridhisha supavaiza, idara na chuo. Aandae study design iliyonyooka ili apate kibali cha utafiti kutoka chuoni.

Siyo tu kibali, bali ukusanyaji data na uchakataji wake ili ulete maana na matokeo tarajiwa au kinyume.

Baada ya hapo kuna zile progress ambazo mara urudi field, mara udizaini upya study, mara ubadilishe objectives, n.k.

Wakati wote huo ukimeinteini constant communications/meeting with supervisors. Huku ukijitahidi kupablishi kwenye predator journals na conferences ili utimize vigezo vya chuo husika.

Hili tunaliona kwa career academicians ni GUMU sana sana wakati hawana kazi nyingine zaidi ya kusoma tu ili wapate hiyo PhD. Wengine hadi wanafikia kushindwa kumaliza PhD na kulazimika kubadilishia kada ya kazi (au kufukuzwa hapo zamani).

Sasa tujiulize, mtu ni waziri, ana majukumu kede kede nchi nzima. Anazunguka na raisi au waziri mkuu au makamu wa raisi. Wakati huo huo anakimbizana na dharura zinazojitokeza wizarani na nchini pote. Je, mtu huyu anapata wapi muda wa kufanya yote ya hapo juu ili apate PhD?

Najiuliza na sidhani kama nitaweza kujijibu NAOMBA mnisaidie. Hawa wanasiasa wanapataje PhD kirahisirahisi wakati career academicians wanashindwa?

Nafikiri jibu likipatikana litasaidia wengine wengi waweza kufanikisha jambo hili.

Nitoe mifano miwili tu midogo. Nina wanafunzi wa MSc. Eng. wawili. Wanafanya kazi. Imekuwa taabu sana kupata progress ninayoitegemea kwao kutokana na majukumu ya kazini. Kumbuka hawa wanafanya kazi kitengo kimoja tu na siyo nchi nzima. Ninaye mwingine wa PhD., yeye hata proposal bado hajaweza kuikamilisha na mwaka unaisha. Kwanini? Ametingwa na majukumu ya kazini.

Iweje leo mtu anazunguka Tanzania nzima, yupo bungeni, anaenda nchi za nje, ana majukumu lukuki ya kitaifa. Anawezaje kumaliza PhD kwa haraka hivyo?

Nijibuni ili niwasaidie wanafunzi wangu jamani wamalize haraka kwa muda. Sababu kama waziri anaweza kwanini wao washindwe?

Ninachofikiria, inawezekana kuna kamchezo kachafu kanakofanywa na wanasiasa. Labda study wanafanyiwa na CONTRACTORS halafu anamwambia mwanafunzi akariri na kuprezenti. Hili yawezekana linafanyika bila supavaiza kujuwa au anajuwa lakini anaona bora liende tu.

Hili yawezekana hata hawa wanafunzi wengine wanafanya lakini kwa kiwango cha chini. Ndiyo maana wanachelewa kumaliza. Hawa wanasiasa wanafanya kiwango cha juu ndiyo maana wanamaliza mapema.

Nimefikiria tu. Nimefikiria nikaona nirushe hapa ili mnichape bakora.

Lakini nitashukuru mkinielekeza wanachofanya wao ili niweze kuwasaidia wanafunzi wangu.

Ikitokea siku nipate wasaa, nitaongea na Dr. Jafo, Dr. Biteko, Dr. Nchemba, et al. Nitawauliza mliwezaje wezaje? Wengine wanashindwa wakati wana vikazi vidogo vidogo tu.

Asalaam.
Aviti T. Mushi
Aliyechelewa kupata PhD, hivyo anawashangaa wanasiasa wanaowahi kuzipata ndani ya muda.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
20,391
43,878
SUA huwa wako strictly na huwa hawajipendekezi kwa wanasiasa ma orof wamejikita kwenye kuandika miradi na tafiti so hawana njaa ya kujipendekeza kwa wanasiasa Ili wateuliwa, Mimi mwanasiasa aki graduate SUA, nitaamini hyo PhD yake
... SUA, MUHAS, na AU walafi wa PhD hawatii pua pale! Bachelors zenyewe zinasotewa 5 years ndio itakuwa PhD; that's the reason. Wanakimbilia huko kwenye degree laini laini and easy to forge. PhD (Veterinary Medicine), PhD (Medicine), PhD (Architectural Studies) sio mchezo mchezo.
 
katitu

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
2,154
1,735
Je, ni kweli Wanasiasa Wanafanya PhD kama Wengine?

Nataka nishee mawazo yangu kuhusu Doctor Jafo S.S. kujipatia PhD. ndani ya muda. Kabla ya hapo niseme kwanza haya maneno yanayofuata.

Nimekumbuka wanasiasa wachache waliojipatia PhDs wakiwa mawaziri au vyeo vingine serikalini: Dr. Magufuli J.P.J., Dr. Nchemba, M.L., Dr. Biteko, M.D., et al.

Nianze kwa kukumbusha kwamba kusoma PhD ni kugumu sana, nadhani mtakubaliana nami. Kuanza kuandaa proposal, ifikie viwango vya kuridhisha supavaiza, idara na chuo. Aandae study design iliyonyooka ili apate kibali cha utafiti kutoka chuoni.

Siyo tu kibali, bali ukusanyaji data na uchakataji wake ili ulete maana na matokeo tarajiwa au kinyume.

Baada ya hapo kuna zile progress ambazo mara urudi field, mara udizaini upya study, mara ubadilishe objectives, n.k.

Wakati wote huo ukimeinteini constant communications/meeting with supervisors. Huku ukijitahidi kupablishi kwenye predator journals na conferences ili utimize vigezo vya chuo husika.

Hili tunaliona kwa career academicians ni GUMU sana sana wakati hawana kazi nyingine zaidi ya kusoma tu ili wapate hiyo PhD. Wengine hadi wanafikia kushindwa kumaliza PhD na kulazimika kubadilishia kada ya kazi (au kufukuzwa hapo zamani).

Sasa tujiulize, mtu ni waziri, ana majukumu kede kede nchi nzima. Anazunguka na raisi au waziri mkuu au makamu wa raisi. Wakati huo huo anakimbizana na dharura zinazojitokeza wizarani na nchini pote. Je, mtu huyu anapata wapi muda wa kufanya yote ya hapo juu ili apate PhD?

Najiuliza na sidhani kama nitaweza kujijibu NAOMBA mnisaidie. Hawa wanasiasa wanapataje PhD kirahisirahisi wakati career academicians wanashindwa?

Nafikiri jibu likipatikana litasaidia wengine wengi waweza kufanikisha jambo hili.

Nitoe mifano miwili tu midogo. Nina wanafunzi wa MSc. Eng. wawili. Wanafanya kazi. Imekuwa taabu sana kupata progress ninayoitegemea kwao kutokana na majukumu ya kazini. Kumbuka hawa wanafanya kazi kitengo kimoja tu na siyo nchi nzima. Ninaye mwingine wa PhD., yeye hata proposal bado hajaweza kuikamilisha na mwaka unaisha. Kwanini? Ametingwa na majukumu ya kazini.

Iweje leo mtu anazunguka Tanzania nzima, yupo bungeni, anaenda nchi za nje, ana majukumu lukuki ya kitaifa. Anawezaje kumaliza PhD kwa haraka hivyo?

Nijibuni ili niwasaidie wanafunzi wangu jamani wamalize haraka kwa muda. Sababu kama waziri anaweza kwanini wao washindwe?

Ninachofikiria, inawezekana kuna kamchezo kachafu kanakofanywa na wanasiasa. Labda study wanafanyiwa na CONTRACTORS halafu anamwambia mwanafunzi akariri na kuprezenti. Hili yawezekana linafanyika bila supavaiza kujuwa au anajuwa lakini anaona bora liende tu.

Hili yawezekana hata hawa wanafunzi wengine wanafanya lakini kwa kiwango cha chini. Ndiyo maana wanachelewa kumaliza. Hawa wanasiasa wanafanya kiwango cha juu ndiyo maana wanamaliza mapema.

Nimefikiria tu. Nimefikiria nikaona nirushe hapa ili mnichape bakora.

Lakini nitashukuru mkinielekeza wanachofanya wao ili niweze kuwasaidia wanafunzi wangu.

Ikitokea siku nipate wasaa, nitaongea na Dr. Jafo, Dr. Biteko, Dr. Nchemba, et al. Nitawauliza mliwezaje wezaje? Wengine wanashindwa wakati wana vikazi vidogo vidogo tu.

Asalaam.
Aviti T. Mushi
Aliyechelewa kupata PhD, hivyo anawashangaa wanasiasa wanaowahi kuzipata ndani ya muda.
wakuu wa vyuo wanajidhalilisha kwa njaa zao za kupenda teuzi.vyuo vyetu sasa vimeguka majalala ya kutoa Phd feki.nashangaa mkuu wa UDOM alikuwa mwalimu wangu pale chuo cha ushirika moshi enzi hizo na baadaye tukakutana tena enzi ya MUcoBs na alikuwa very smart lkn namshanga kapelekwa UDOM kabadilika kabisa.sijui nn kimempata.
 
NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
5,380
9,634
Tatizo ni Imani iliyoibuka kwamba ili uteuliwe kugombea Uraisi ndani ya chama lazima uwe na Doctorate fulani hv!!hii ndio imefanya wanasiasa kukimbilia hizo Phds!!!
 
24 Reactions
Reply
Top Bottom