Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Hii ndio dhambi ya kudhani hapa JF ni jamvi la kujadili mambo negative tu!!!
Kwa hiyo kila mtoa hoja anajaribu kuleta lenye negative!!! angalia asilimia 75% ilivyopatikana.

1. Mwenyekiti, Katibu, Makamu wa Kwanza, Makamu wa Pili!

Data Sample =4 people,
sasa 3 are muislam, hence 3/4 x 100 = 75% conclusion CCM 75% ni waislamu.

Takwimu hizo, kila mtu anatumia atakavyo,,, bila kujali kwamba makamu wa pili wa CCM lazima awe Mzanzibar na Wanzanibar ni waislamu by >95%

Upuuzi Mtupu...

Kilitime,

Mimi nimekuwa napinga sana suala la udini hapa na utakumbuka ugomvi wangu na Mchambuzi kuhusu mgombea wa ccm kuwa mkristo.

The same standard imekuwa inatakiwa kutumika kwa wanaccm hapa ambao wamekuwa wanakiita chama cha CUF kama cha kidini na cha waislam. Ni juzi tu hapa wanasisiemu tena wameanza issue kuwa chama cha CHADEMA ni cha watu wa kaskazini na cha kikabila.

Hii generalization ilikuwa tamu kwenu wanaccm na hata wewe you never said a thing about it. Leo kwa sababu ni ccm ndio inasemwa then unaiita upuuzi.

Haijalishi formula gani imetumika, ukweli ni kwamba members wa CC na NEC ya ccm ni asilimia 75 au zaidi waislam. Kubishana kuhusu formula sio tatizo wala solution.

Issue iwe kwamba, udini iwe kwa CUF au CCM usitumike kugeneralize mambo. Mimi nauona huo ukweli kuwa viongozi wengi wa ccm sasa ni waislam lakini ugomvi wangu hauko dhidi ya dini zao au mambo yao ya kikubwa. Ugomvi wangu ni juu wa wizi na ufisadi. The same standard from you guys should be used wakati mnapotumia mbinu chafu dhidi ya upinzani!
 
sumu ya ubaguzi huwa haikomi.. ikishaingia kwenye kundi fulani basi kundi hilo huanza wa kubagua. Likimaliza kubagua linatafuta kipimo kingine cha kutumia kubagua. Ukishabagua makabila na kuamua kabila fulani ni duni halistahili, basi unaenda kwenye kipimo kingine; dini. Ukishawabagua watu kwa dini, ukimaliza utajiuliza "hivi wengi ni dhehebu gani?" hivyo utaanza kuwatenganisha Sunni na Shia, Wakatoliki na Waprotestanti n.k mwisho unaweza kujikuta unaanza kubagua watu kwa kuwaanangalia (nani anafanana na Mtutsi)..

La maana ni lazima tuukatae ubaguzi mapema unapojitokeza. Ratio ya CC inasema wajumbe saba kutoka pande zote mbili za Muungano (which is absurdy in itself) hiyo kutoka Zanzibar you'll probably get all seven wakiwa ni Waislamu. Halafu ukija bara wale saba hata wakristu wakiwa wanne bado kwenye general membership utakuta waislamu 10.. Sasa ukija na nafasi za viongozi wanaoingia kwa nyadhifa zao Kikwete, Shein, Karume, Makamba bado namba ya Waislamu inaongezeka. So, hilo ni jambo la mantiki, utaweza kuepuka vipi isipokuwa useme "Zanzibar ichague wakristu, au Bara ilete wagombea wakristu tu" .. na ukishafanya hivyo.. ile sumu itakuwa imekuingia!!

Lakini jamani kwani tatizo letu ni namba ya waislamu kuzidi kuongezeka? Kwani katika hiyo kamati unayotaja, kuna mwongozo unaosema iwe na waislamu wangapi? Maana mwongozo kama huo ungekuwapo, basi ingekuwapo pia njia (methodology) ya kuhakikisha kwamba ratio inakuwa hivyo. Mimi nadhani suala la kuanza kuhesabu kuna waislamu wangapi na wakristo wangapi katika chama au serikali ni paranoia. Upuuzi mtupu. Watu wanachaguliwa kwa mujibu wa sifa zilizowekwa katika katiba. Zinapofuatwa sifa hizo na kanuni zilizopo kuna uwezekano wa kupata kiongozi mwanaume au mwanamke, mwenye dini au asiye na dini, mweusi au aso mweusi, kabila hili au lile, alimradi wote walishiriki katika mchakato wa kupata kiongozi. Sasa hapo tatizo liko wapi?
 
Kithuku soma tena hiki alichoandika Mwanakijiji katika hiyo quote ulotumia hapo juu:

Mzee Mwanakijiji said:
sumu ya ubaguzi huwa haikomi.. ikishaingia kwenye kundi fulani basi kundi hilo huanza wa kubagua. Likimaliza kubagua linatafuta kipimo kingine cha kutumia kubagua. Ukishabagua makabila na kuamua kabila fulani ni duni halistahili, basi unaenda kwenye kipimo kingine; dini. Ukishawabagua watu kwa dini, ukimaliza utajiuliza "hivi wengi ni dhehebu gani?" hivyo utaanza kuwatenganisha Sunni na Shia, Wakatoliki na Waprotestanti n.k mwisho unaweza kujikuta unaanza kubagua watu kwa kuwaanangalia (nani anafanana na Mtutsi)..

La maana ni lazima tuukatae ubaguzi mapema unapojitokeza. Ratio ya CC inasema wajumbe saba kutoka pande zote mbili za Muungano (which is absurdy in itself) hiyo kutoka Zanzibar you'll probably get all seven wakiwa ni Waislamu. Halafu ukija bara wale saba hata wakristu wakiwa wanne bado kwenye general membership utakuta waislamu 10.. Sasa ukija na nafasi za viongozi wanaoingia kwa nyadhifa zao Kikwete, Shein, Karume, Makamba bado namba ya Waislamu inaongezeka. So, hilo ni jambo la mantiki, utaweza kuepuka vipi isipokuwa useme "Zanzibar ichague wakristu, au Bara ilete wagombea wakristu tu" .. na ukishafanya hivyo.. ile sumu itakuwa imekuingia!!

Kinachokataliwa hapa ni ubaguzi wa aina yoyote maana ukishatumika utaendelea bila kukoma. The same standard inayotumiwa na ccm kusema kuwa cuf ni chama cha kidini (kwa sababu tu viongozi wake wengi ni waislam) inabidi iachwe kabisa kwa sababu ikiendelea matokeo yake ndiyo yanakuwa haya ya kuona nani ni nani hata ndani ya hiyo ccm yenyewe!
 
naona watanzania tunababaika sana na majina ya watu!

dini ya mtu haitakiwi kufuatiliwa kwa jina la mtu au maneno yake. dini ya mtu ni vitendo. sasa hata kama watakuwa majina ya kiislam 100% as long as hawatendei haki watu, wanaiba, ni mafisadi, hawawahurumii wanyonge, wabadhirifu wa mali ya umma, hatuwezi kuwahukumu kama waislam ( kwa kuwa wanaenda kinyuma na dini yao inavyoamrisha)

Nakushukuru gaijin kwa kulileta hili. Shule ya sekondari nilikosomea kulikuwa na jumuiya za wakristo na waislam. Kuna wakati Jumuiya ya waislam ilikuwa na kiongozi anaitwa Peter. Na darasani kwangu nilikuwa nasoma na Anthony na Jacob ambao walikuwa waislam. Jacob alikuwa na jina lingine akiitwa Yunus, lakini hakuwahi kulitumia katika taarifa zake. Hadi leo nawasiliana nao na hawajabadilisha majina yao. Kiongozi wa kwaya ya UKWATA (wakristo) alikuwa anaitwa Hussein Alli, na hadi leo ameongeza tu jina la ukoo wake, lakini bado anaitwa Hussein Alli. Bwenini kwetu kiongozi wa wakatoliki ambaye ndiye alikuwa anahimiza wanafunzi wapya (form one) kujua chumba cha sala kilipo alikuwa msambaa anaitwa Hassani Saidi, na ndiye pia alikuwa mwalimu wa mafundisho (kama katekista) kwa ajili ya wale waliokuwa hawajapata ekaristi na kipaimara. Nadhani kama kuna members hapa ambao tulikuwa shule moja wameshaanza kukumbuka mengi. Na je mwafahamu ya kuwa yule aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na naibu waziri mkuu katika serikali ya Saddam Hussein, akiitwa Tariq Aziz, mwafahamu ya kuwa alikuwa mkristo wa dhehebu la Koptic? Kwa hiyo ndugu zangu msihukumu kwa majina, lakini kubwa zaidi, msihukumu kwa dini.
 
Siye wa TZ ni watu wa ajabu sana, hizi topiki za udini zinapamba moto kama moto wa vifuu, nawauliza je tutafika kweli?

Kutoaka na nionavyo mimi nikuwa wengi wetu ni wadini na wakabila wa kutupwa, ila tunajifanya hatujali, ndiyo maana hizi topiki zinapendwa sana na tunazishabikia.

Mimi napinga ubaguzi wa aina yeyote ile. Na deep down najua ukweli uko wapi, ila sipendi kuongezea petroli hapa na naamua kukaa kimya ili mada kama hizi ziishe mapema lakini wapi.

Nawaomba wote wanaopinga ubaguzi wa aina zote tusichangie hapa, kwani kuna topiki nyingi ambazo tunaweza kuchangia na kusidia taifa zaidi kuliko hii.

Nilikuwepo!
 
Mimi nashangaa sana , kwa nini watu wengi wanashughulika na Imani za viongozi badala ya kushughulikia nini wanatenda kwa jamii?? Tusiwe na upeo mdogo wa kutazama muhimu ni kua kiongozi anawajibika vipi ktk kazi zake (wajibu ) na tukitazama hayo Udini na ukabila hatutoviona na tutamkosoa kiongozi kwa mabaya yake na sio Imani yake nadhani haya ndio maendeleo kinyume tutabaki kila mara kutazama majina (dini) na hakuna maendeleo tutapata ila kuzidisha chuki na hali sote ni nchi yetu na hakuna wa kuondoka ila haki sawa kwa wote
 
Kuna mtu aliwahi kusema hapa kuwa kuna makubaliano ndani ya ccm kuwa na uwakilishi sawa wa dini kubwa nchini za uislam na ukristo. Matokeo ya uchaguzi dodoma yanaonyesha kuwa waislam sasa wana-nafasi asilimia 75 ya uongozi wa ccm.

NOTE: Uongozi (Ukiondoa nafasi ya Mnykt na Katibu mukuu)Katika CCM (nadhani hata vyama vingine itabidi waige hivyo) umegawanywa sawia kati ya Tanganyika na Zenji.

Tanzania = Tanganyika + Zanzibar
.
. . Tanganyika = Zanzibar = 1/2 Tanzania

Muslims(Tanganyika) = 50% (population)

Muslim(Zanzibar)=100% (Population)

Viongozi Muslims(Toka Tanganyika) = 50% (Ya viongozi toka Tanganyika)

Viongozi Muslims(Toka Zanzibar)=100% (Ya viongozi toka zanzibar)

Viongozi MUslim(Tanzania)= 1/2( 100% + 50%) = 75%

A miracle!!! no just! arithmetical computations!!!

NB: Equal sign inawakilisha uwiano unaokaribiana tu, na sio sawasawa kabisa.
 
Jamani tuache kuendekeza mambo ya UDINI!!!! Tuhoji tu tutapoona mtu anachaguliwa kwa dini yake na si vigezo vingine vya kiuongozi.

Ni ujinga na uzuzu mtupu mtu kusema eti chama fulani ni cha kidini kwasababu viongoziwe wengi ni wa dini fulani bila kuangalia sababu za msingi kwanza!! eti serikali ni ya kikristu etu tu kwasababu viongozi wengi ni wakristu !! Chaa! hamuoni kuwa wengi wao wameenda shule??!!

Kuendekeza mambo hayo mwishowe mtakuwa si watu wa DINI tena bali watu DUNI!!!
 
Mimi nashangaa sana , kwa nini watu wengi wanashughulika na Imani za viongozi badala ya kushughulikia nini wanatenda kwa jamii?? Tusiwe na upeo mdogo wa kutazama muhimu ni kua kiongozi anawajibika vipi ktk kazi zake (wajibu ) na tukitazama hayo Udini na ukabila hatutoviona na tutamkosoa kiongozi kwa mabaya yake na sio Imani yake nadhani haya ndio maendeleo kinyume tutabaki kila mara kutazama majina (dini) na hakuna maendeleo tutapata ila kuzidisha chuki na hali sote ni nchi yetu na hakuna wa kuondoka ila haki sawa kwa wote

babu, we have a long way to go !

vizuri sana uliposema kwa nini hatuangalii utendaji wa kazi na sio dini zao, vil vile kama nilivyosema kwa nini tusiangalie maendeleo ya nchi bila kujali viongozi wametoka chama gani, lakini watu wakaniona ovyo !
 
Jamani tuache kuendekeza mambo ya UDINI!!!! Tuhoji tu tutapoona mtu anachaguliwa kwa dini yake na si vigezo vingine vya kiuongozi.

Ni ujinga na uzuzu mtupu mtu kusema eti chama fulani ni cha kidini kwasababu viongoziwe wengi ni wa dini fulani bila kuangalia sababu za msingi kwanza!! eti serikali ni ya kikristu etu tu kwasababu viongozi wengi ni wakristu !! Chaa! hamuoni kuwa wengi wao wameenda shule??!!

Kuendekeza mambo hayo mwishowe mtakuwa si watu wa DINI tena bali watu DUNI!!!

kula 5 bokassa !
 
Mimi nashangaa sana , kwa nini watu wengi wanashughulika na Imani za viongozi badala ya kushughulikia nini wanatenda kwa jamii?? Tusiwe na upeo mdogo wa kutazama muhimu ni kua kiongozi anawajibika vipi ktk kazi zake (wajibu ) na tukitazama hayo Udini na ukabila hatutoviona na tutamkosoa kiongozi kwa mabaya yake na sio Imani yake nadhani haya ndio maendeleo kinyume tutabaki kila mara kutazama majina (dini) na hakuna maendeleo tutapata ila kuzidisha chuki na hali sote ni nchi yetu na hakuna wa kuondoka ila haki sawa kwa wote

UNCLE USISAHAHU HILI VUGUVUGU LA MJADALA HUU LIMEKUWA DERIVED FROM THE CURRENT SITUATION BONGO YA MAHAKAMA YA KADHI!SO, KAMA VIONGOZI WOTE NI WAISLAM JE WATASIKILIZA HOJA AMBAYO NI YA TOAUTI NA INAYOKUBALIANA NA MAHAKAMA YA KADHI?MAYBE LAKINI POSSIBILITY NI NDOGO SANA!USISAHAU MVUTIA KAMBA....
 
naona watanzania tunababaika sana na majina ya watu!

Nakushukuru gaijin kwa kulileta hili. Shule ya sekondari nilikosomea kulikuwa na jumuiya za wakristo na waislam. Kuna wakati Jumuiya ya waislam ilikuwa na kiongozi anaitwa Peter. Na darasani kwangu nilikuwa nasoma na Anthony na Jacob ambao walikuwa waislam. Jacob alikuwa na jina lingine akiitwa Yunus, lakini hakuwahi kulitumia katika taarifa zake. Hadi leo nawasiliana nao na hawajabadilisha majina yao. Kiongozi wa kwaya ya UKWATA (wakristo) alikuwa anaitwa Hussein Alli, na hadi leo ameongeza tu jina la ukoo wake, lakini bado anaitwa Hussein Alli. Bwenini kwetu kiongozi wa wakatoliki ambaye ndiye alikuwa anahimiza wanafunzi wapya (form one) kujua chumba cha sala kilipo alikuwa msambaa anaitwa Hassani Saidi, na ndiye pia alikuwa mwalimu wa mafundisho (kama katekista) kwa ajili ya wale waliokuwa hawajapata ekaristi na kipaimara. Nadhani kama kuna members hapa ambao tulikuwa shule moja wameshaanza kukumbuka mengi. Na je mwafahamu ya kuwa yule aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na naibu waziri mkuu katika serikali ya Saddam Hussein, akiitwa Tariq Aziz, mwafahamu ya kuwa alikuwa mkristo wa dhehebu la Koptic? Kwa hiyo ndugu zangu msihukumu kwa majina, lakini kubwa zaidi, msihukumu kwa dini.

Jamani,

Hivi tariq Aziz yupo wapi ?

Nawe Kithuku kila kiongozi wa dini alikuwa na jina la upande mwingine kwi kwi kwii

What a coincedence?!?
 
NOTE: Uongozi (Ukiondoa nafasi ya Mnykt na Katibu mukuu)Katika CCM (nadhani hata vyama vingine itabidi waige hivyo) umegawanywa sawia kati ya Tanganyika na Zenji.

Tanzania = Tanganyika + Zanzibar
.
. . Tanganyika = Zanzibar = 1/2 Tanzania

Muslims(Tanganyika) = 50% (population)

Muslim(Zanzibar)=100% (Population)

Viongozi Muslims(Toka Tanganyika) = 50% (Ya viongozi toka Tanganyika)

Viongozi Muslims(Toka Zanzibar)=100% (Ya viongozi toka zanzibar)

Viongozi MUslim(Tanzania)= 1/2( 100% + 50%) = 75%

A miracle!!! no just! arithmetical computations!!!

NB: Equal sign inawakilisha uwiano unaokaribiana tu, na sio sawasawa kabisa.

Yani hapa ndio nimechoka kabisaaaaa.

Population ya bara na zanzibar ni tofauti kabisa lakini tunapata nafasi sawa? niite mdini lakini mimi nitakiita ccm kama chama cha waislam kama wao walivyokiita cuf kwa muda wote huu.
 
Jamani,

Hivi tariq Aziz yupo wapi ?

Nawe Kithuku kila kiongozi wa dini alikuwa na jina la upande mwingine kwi kwi kwii

What a coincedence?!?

Hapana, viongozi walikuwa wengi, nimetaja tu wale ambao kwa majina yao usingeweza kutambua ni wa dini hiyo. Lakini walikuwepo wengine pia wenye majina yanayoendana na yaliyozoeleka kwenye dini zao.

Huyo Tariq Aziz bado yuko mahabusu na kesi yake inaendelea huko Iraq.
 
Halafu Jamani HUYU MTU ANAEITWA KADA kwa nini aruhusiwe kujisajili mara mbili? Admin. tafadhali hebu liangalie hili na Kada uje ueleze huu utovu wako wa nidhamu unakusaidia nini hapa jamvini
Ben,usiseme Kada tu hata wewe yawezekana umejisajili nick zaidi ya moja.Hapa wapo kibao tu wamejisajili majina zaidi ya moja.

je ni kosa kujisajili hivyo?

Hata moderators na may be Adm mwenyewe anaweza kuwa kajisajili zaidi ya mara moja
 
katika dini ambayo haina mgogoro ni dini ya Pagan.Karibuni mjumuike nami.Hizo dini zisiwatishe ni kama Chama Cha Siasa tu
 
Ben,usiseme Kada tu hata wewe yawezekana umejisajili nick zaidi ya moja.Hapa wapo kibao tu wamejisajili majina zaidi ya moja.

je ni kosa kujisajili hivyo?

Hata moderators na may be Adm mwenyewe anaweza kuwa kajisajili zaidi ya mara moja

mtu huyu shalow naona anakuja na kuchungulia hapa, halafu anamchokonoa kada sijui kwa nini ! yaani he is used to it !
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom