sumu ya ubaguzi huwa haikomi.. ikishaingia kwenye kundi fulani basi kundi hilo huanza wa kubagua. Likimaliza kubagua linatafuta kipimo kingine cha kutumia kubagua. Ukishabagua makabila na kuamua kabila fulani ni duni halistahili, basi unaenda kwenye kipimo kingine; dini. Ukishawabagua watu kwa dini, ukimaliza utajiuliza "hivi wengi ni dhehebu gani?" hivyo utaanza kuwatenganisha Sunni na Shia, Wakatoliki na Waprotestanti n.k mwisho unaweza kujikuta unaanza kubagua watu kwa kuwaanangalia (nani anafanana na Mtutsi)..
La maana ni lazima tuukatae ubaguzi mapema unapojitokeza. Ratio ya CC inasema wajumbe saba kutoka pande zote mbili za Muungano (which is absurdy in itself) hiyo kutoka Zanzibar you'll probably get all seven wakiwa ni Waislamu. Halafu ukija bara wale saba hata wakristu wakiwa wanne bado kwenye general membership utakuta waislamu 10.. Sasa ukija na nafasi za viongozi wanaoingia kwa nyadhifa zao Kikwete, Shein, Karume, Makamba bado namba ya Waislamu inaongezeka. So, hilo ni jambo la mantiki, utaweza kuepuka vipi isipokuwa useme "Zanzibar ichague wakristu, au Bara ilete wagombea wakristu tu" .. na ukishafanya hivyo.. ile sumu itakuwa imekuingia!!