Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Mugongo Mugongo yupo kwa jina lingine. Kwani ulifikiri kapotea?
Murangira yupo wapi? jibu yupo.
Chief Ihunyo yupo wapi? jibu yupo.

Jamani wananchi, kwanza naomba mtuletee maandiko tuliyosema KHAF ni chama cha kidini, isije ikwa maneno ya mtaani mnayaleta hapa!

Kitila umenichekesha kweli, Kama kweli CCM imemteua Kada (utani km ulivyosema) kuwa msemaji wao kwenye NET, basi ningemshauri Tendwa akifutilie mbali maana kitakuwa kimekosa dira na mwelekeo!
 
Kwa msingi huu, kama wanaccm hapa walikiita chama cha cuf cha kidini kwa sababu ya viongozi wake. Nadhani sasa inabidi ccm pia kiitwe chama cha waislam.

Kuanzia sasa kwa mtizamo wangu na imani yangu ya jino kwa jino dhidi ya ccm kwa kuiita cuf chama cha kidini. Kuanzia leo ccm inabadilishiwa jina hapa kutoka CCM kwenda CCW.

CCW inamaanisha Chama Cha Waislam

Mgaya,

I am sure you can do better than this, Try to come up with something positive, or even some strong points/basis of your conclusion. NOT THAT ONE. Please!
 
naona watanzania tunababaika sana na majina ya watu!
tunamhukumu mtu dini yake kwa kuwa yeye ana jina la kiislam au la kikristo, au huwa anasali mara moja moja kanisa fulani au msikiti fulani.

dini ya mtu haitakiwi kufuatiliwa kwa jina la mtu au maneno yake. dini ya mtu ni vitendo. sasa hata kama watakuwa majina ya kiislam 100% as long as hawatendei haki watu, wanaiba, ni mafisadi, hawawahurumii wanyonge, wabadhirifu wa mali ya umma, hatuwezi kuwahukumu kama waislam ( kwa kuwa wanaenda kinyuma na dini yao inavyoamrisha)

nafikiri kwa waislam wanalijua hilo kwani the prophet SAW amesema " taqwa( uchamungu) haupo kwenye mdomo, upo moyoni"

nawasilisha
 
Mugongomugongo unatumia jina gani tafadhali jitokeze tu acha woga mi nilidhani wewe jasiri sana(kidding).
Halafu Jamani HUYU MTU ANAEITWA KADA kwa nini aruhusiwe kujisajili mara mbili? Admin. tafadhali hebu liangalie hili na Kada uje ueleze huu utovu wako wa nidhamu unakusaidia nini hapa jamvini
 
Nashukuru,
Nadhani kila mtu anaweza ongea anayo weza lakini lamsingi awe na supporting arguement pamoja na evidence.Kama unaweza toa scholarly argument tusiangalie hapa tulipo tu,tuangalie nyuma ,hapa na tuweze kufikiria mbele.
Nani asiyejua asili ya ccm ni TAA,na TAA ilikuwa asilimia tisina nane ni watu wamsikitini kama anavyosema Mchungaji Kishoka.Tumeingia ktk CCM ukweli ni kuwa waislamu wanaonekana wengi kutokana na Zanzibar.Zanzibar wakristo ni wachache,lakini yuko mkristo ameingia kwa tiketi ya Zanzibar na bado ni waziri kule Zanzibar sio tatizo.
Tunaposema leo kuwa ccm imeundwa na waislamu tukasahau miaka minne iliyopita katibu alikuwa Mangula mtu wa kanisa,mwenyekiti Mkapa mtu wa kanisa,makamu Malecela mtu wa kanisa.
Nadhani hivyo si vigezo vilivyo safi katika kutoa hoja.Vile vile tusijione sisi wakristo ndio tunaakili sana,wako viongozi wakristo na waislamu wamefanya mabaya na wengine wamefanya mema.Lamsingi ni tabia ya mtu,uwezo wa mtu na ari aliyonayo.
Aristotle alikuwa anasema jambo linakuwa zuri kulingana na mtu mwenyewe,Jerremy Bentham na John Stuart Mill wao wanaamini jambo jema ni lile litakalokuwa na matokeo mazuri,Immanuel Kant yeye anasema kitendo ndicho kiwe chema na si kuangalia matokeeo.Wote wanaweza wakawa sawa.Lamsingi tuangalie mazingira,wakati,matokeo,na matendo yetu.
Naomba kuwasilisha.
 
WaTanzania wenzangu, sio Dhambi JF kukosa Thread Mpya hata kwa Mwezi Mzima especially kukiwa hakuna la Kujadili! Sasa hili lililoletwa hapa du! Nadhani mtoa hoja amekosa la kuleta lakini akapenda awe na kitu cha kujadili,,, na akaamua kuleta hili hapa!

Imani yangu ni kwamba hata wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM ulipita hawakuwahi kufikiria kuhusu hili la dini, at least la unatoka mkoa gani? hilo naweza kuliona kwa mbali.

Suala la ubaguzi wa DINI Tanzania halitafanikiwa hata kidogo...Ni suala la kufikirika tu... halipo.

Kuna jamaa yangu mmoja tulionana jana tukiwa tunaongea mambo fulani fulani ya kiimani, akaniambia amesitushwa na muongezeko wa idadi ya ndoa za bomani zinazofungwa siku hizi... hope hili linajieleza lenyewe...

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Waumbue Wabaguzi wa Aina Zote,,,
Ahsanteni Kwa kunisoma...
 
...............hiyo Mahakama Ya Kadhi Kamwe Haitakuja Tanzania Hata Waipiganie Vipi...kwamwe Hawataweza Kuianzisha Hapa....haitakiwi!!!!..wale Wahashimiwa Mashehe Wetu Wanaoipigania..labda Hawana Kazi Ya Kufanya....hatutaki..serikali Haina Dini!!!!na Mahakama Zetu Zinatosha ...mtu Akitaka Kwenda Kupatanishwa Kanisani Au Msikitini Ni Ruksa..lakini Kamwe Hatuwezi Kuwapa Seal Ya United Republic Mahakama Za Kadhi!!!
 
Exactly!! Thank you! I mean its a very slow economic growing country halafu wananci wenyewe are so poor! So why bother with 'Udini' while each individual has their own mind with his/her God?As long as kiongozi wangu anafanya shughuli vyema,leading the country...you know wot I mean?
 
Who cares if 75% of leadership belongs to Masjid? the question is not their religion but their organizational skills, efficiency, capability to lead and standing tall to deliver.

Naona watu wameshidwa kumuelewa Rev. Yeye hajali Uisilam au Ukristo yeye anataka watu watakaochaguliwa wawe na skills, wawe efficiency, uwezo na mimi naongeza wawe committed kwa wananchi waliowachagua na sio kwenye familia zao peke yake. Wawe na uzalendo wa kweli sio ule wa kutudanganya kwenye majukwaa ya siasa kumbe kwenye mioyo yao ni tofauti kabisa
 
So poor, Jambazi ni jambazi tu whether Christian, Moslem, Pagan or whatever. Can some one tell me whether Andrew Chenge, Basil Mramba, Balali, etc and Muslims, and whether Mr So and so who are in list of shame are christians. Lakaini wote hao wako kwenye CCM. We have to use our brains guys, religion is just being used by those who are coward to wage the war against corruption, the best way is to target corruption not religions.
 
Jamani mimi nadhani kua matatizo sio udini ila kiongozi kutokua kua muadilifu kwani hata kama mtu muislam au mkristo lakini anastahili kua kiongozi kwa Elimu yake basi hakuna matatizo na kama mtu atatumia Imani yake kutokua muadilifu ktk wadhifa wake basi hafai
Kwa hiyo maoni yangu ni kua muhimu sio kutazamwa mtu Imani yake ila uuadilifu wake kikazi kwani ktk kumchagua kiongozi hatazamwi Imani yake ila uwezo wake na pia Tz ni ya wote sio ya kabila, Imani au sehemu fulani.
 
sure hiii issue haipo kwenye nec na cc tu bali kwenye nyanja zote za uongozi wakuu wa wilaya , wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa mashirika ya umma n.k asilimia kubwa ni waislamu lakini jambo la muhimu ni kufunika kombe maana ....
 

...ilianzia 'ma-shushushu -NCCR-MAGEUZI,

...halafu ikaja Ubara -CCM na Upemba -CUF,

...tena ikaja CHADEMA -Ukaskazini! ...sasa ishakuwa -CCM waislamu?

...baada ya hapo 'tutaenda' 75% ya jeshi ni Wakurya na polisi, au (ashakum si matusi ) 75% ya 'omba omba' mjini Dar ni wagogo, 75% ya 'watu wa pwani'...




“Dhambi ya ubaguzi ni sawa na dhambi ya kula nyama ya mtu. Ukishaonja nyama ya mtu utaendelea kuila tu!” -Nyerere
 
Suala la kwamba suala la dini halina nafasi ktk safu za uongozi wa vyama na serikali ni kujidanganya.. Hata hapa JF kuchangiwa kwa wingi kwa thread hii kunaonyesha nyoyo nyingi zinaguswa na suala hili, kujifanya huumii huku umekalia msumari si busara hata kidogo!!

Karibu duniani kote jitihada kubwa inafanyika kuhakikisha kuna uwiano mzuri wa uwakilishi ktk mambo karibu yote ya uongozi kuhusu makundi mbalimbali ya kijamii..Kuna watu wanajifanya waliberali eti who cares if 100%..tusidanganyane bwana..Hivi viongozi wote wawe waislam, ina maana hakuna wakristo wenye kustahili hizo nafasi? Wakristo waende wapi sasa? Unataka wakristo wajisikieje? Nani atawakilisha maslahi yao? (Vice versa is also true, for moslems)

Mi nashauri busara itumike ili kwamba kila kundi ktk jamii lijihisi kuwa muhimu ndani ya vyama na serikali kwa kupata uwiano mzuri wa uwakilishi.Nchi ni yetu sote..tuzingatie hili...
 
Hii ndio dhambi ya kudhani hapa JF ni jamvi la kujadili mambo negative tu!!!
Kwa hiyo kila mtoa hoja anajaribu kuleta lenye negative!!! angalia asilimia 75% ilivyopatikana.

1. Mwenyekiti, Katibu, Makamu wa Kwanza, Makamu wa Pili!

Data Sample =4 people,
sasa 3 are muislam, hence 3/4 x 100 = 75% conclusion CCM 75% ni waislamu.

Takwimu hizo, kila mtu anatumia atakavyo,,, bila kujali kwamba makamu wa pili wa CCM lazima awe Mzanzibar na Wanzanibar ni waislamu by >95%

Upuuzi Mtupu...
 
Kuna mtu aliwahi kusema hapa kuwa kuna makubaliano ndani ya ccm kuwa na uwakilishi sawa wa dini kubwa nchini za uislam na ukristo. Matokeo ya uchaguzi dodoma yanaonyesha kuwa waislam sasa wana-nafasi asilimia 75 ya uongozi wa ccm.

Ilivyokuwa CUF na viongozi wengi waislam watu waliita cuf, chama cha waislam. Sijui kama ccm itaitwa the same name? Viongozi wakuu wanne, Kikwete, Karume, Msekwa, na Makamba; ratio inaonekana tayari. Kwa kamati kuu (cc), ratio ipo wazi, cha ajabu hata NEC, ni the same trend.

Haya ni makubaliano ndani ya ccm au ni mabadiliko ya yale makubaliano ya awali? Naomba kuwasilisha

Mwaka 1997 viongozi wakuu wa CCM walikuwa Ben Mkapa, John Malecela, Phillip Mangula na Salmin Amour. Huu pia ulikuwa udini au?
 
Mada hii ni nzuri lakini mwenendo wa mjadala wake unaweza usiwe mzuri.Watu wanaweza kuanza kumjadili mtu na ni sio Chama,kujibizana wana JF wenyewe kwa wenyewe na hivyo kupoteza maana halisi ya mtoa hoja.

Nashauri mada hii iachwe au iahairishwe kama inawezekana.Kwakuwa kuendelea kuijadili mada hii sidhani kama kutatuongezea uwezo wa kufikiria hoja zenye msisimuko wa maendeleo na mapambano dhidi ya wanaotafuna nchi yetu.

Nawasilisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom