Udhaifu katika miundombinu yetu vipindi vya Mvua, aibu kwetu na ugeni huu mkubwa wa Makamu wa Rais Marekani

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,193
6,381
Vipindi vya mvua ( Masika) Miaka yote kumekuwa kukionekana udhaifu wa miundominu yetu hasa barabara kuhimili hali hiyo ya hewa

Sura za kujaa kwa maji barabara zetu, kupelekea foleni kubwa, vyombo vya moto kuharibika njiani na uharibifu vyombo hivyo na mali

Hata miundombinu mipya kama vile eneo la Daraja la mfugale hugeuka dimbiwi kubwa la maji kiasi barabara kutopitika

Mvua ya leo haijaicha tena bila changamoto barabara ya Nyerere ambayo ndio njia kuu ya wageni wengi wanaingia na kuondoka nchini kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere

Huku tukitarajia ugeni mkubwa wa Makamu wa Rais wa Marekani Bibi Kamala Harris, taswira ya barabara yetu ya Nyerere inatia aibu hasa kipande kuanzia viungunguti kuipita Tazara/Daraja la mfugale

Kwanza upande wa wanaotokea Uwanja wa ndege kuna kipande kimejaa maji, na kutokana na ujenzi unaondelea kumeja maji machafu kwa muonekano au yenye tope, barabara pia inayoendelea kujengwa inaongezq pia muonekana matope, lakini pia kuna mbao,vibanda vya mbao, turubaki ambayo havijakaa katika hali ya mpangilio, kuna dalalada imedondola mpaka muda wa jioni ilikuwa bado haijtolewa pale makutano ya mataa Tazara. Na hapo bado mvua zinadalili ya kuendelea na barabara kuja maji zaidi.

Labda kama ugeni utapanda pangaboi kutokea uwanja wa ndege kufikia walipoandaliwa na mwenyeji wake.

Hizi ni kero za miaka yote na kelele zimekuwa zikipigiwa nyingi lakini aibu itakuwa kubwa zaidi pale mbele ya wageni

Sisemi kwamba kwa vile kuna wageni ndio naona shida hii hapana ila ukiwa na utaratibu mzuri wa usafi kwenu hata akija mgeni hauhangaika kuweka mazingira safi.

Kuna haja sasa ya kuangalia upya miundombinu yetu
 
Ni vizuri Mgeni akiyaona haya mapungufu ili waturudishie msaada wa mfuko wa MCC ambao tuliondolewa kwa kiburi cha Magufuli.
 
Back
Top Bottom