Rais Samia Atoa Helkopta kwa Mawaziri Kutafuta Ufumbuzi wa Miundombinu ya Barabara ya Liwale - Lindi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

RAIS SAMIA ATOA HELIKOPTA KWA MAWAZIRI KUTAFUTA UFUMBUZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA YA LIWALE - LINDI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Helikopta kwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Deo Ndejembi kufika Wilaya ya Liwale kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya miundombinu ya barabara na madaraja kutokana na mvua kubwa kunyesha na kusababisha barabara kufungwa.

Mawaziri hao wamewasili Wilayani Liwale Mkoani Lindi leo tarehe 05 Machi 2024 wakiwa wameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack na Wataalam kutoka Wakala ya Barabara (TANROADS) na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya miundombinu ya barabara na madaraja yanayounganisha Wilaya hiyo na sehemu nyingine kujaa maji.
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.02.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.02.jpeg
    448.8 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.03.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.03.jpeg
    520.3 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.04.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.04.jpeg
    622 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.05.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.05.jpeg
    683.8 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.05(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.05(1).jpeg
    378.3 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.06.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-05 at 18.49.06.jpeg
    458.9 KB · Views: 6
Ni jambo zuri sana kuona namna viongozi wetu wanvyoonesha kuwajai wananchi ila binafsi haya ni maoni yangu tu!
Kwanini Innocent Bashungwa na Deo Ndejembi pamoja na msafara wao usitumie barabara ili kwenda kutafuta ufumbuzi huo. Watumie barabara ili wapate kuona wananchi wanavyoteseka, ifike sehemu gari likwame kwenye tope, baadaye wakutane na mvua kubwa na barabara ikatike kiasi kwamba wachukue siku tatu kufika Liwale! Haina maana kwenda kwa wananchi kuongea nao mkiwa mmeshuka kwenye ndege!​
 
RAIS SAMIA ATOA HELIKOPTA KWA MAWAZIRI KUTAFUTA UFUMBUZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA YA LIWALE - LINDI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Helikopta kwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Deo Ndejembi kufika Wilaya ya Liwale kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya miundombinu ya barabara na madaraja kutokana na mvua kubwa kunyesha na kusababisha barabara kufungwa.

Mawaziri hao wamewasili Wilayani Liwale Mkoani Lindi leo tarehe 05 Machi 2024 wakiwa wameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack na Wataalam kutoka Wakala ya Barabara (TANROADS) na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya miundombinu ya barabara na madaraja yanayounganisha Wilaya hiyo na sehemu nyingine kujaa maji.
Kumbe CCM inazo chopa! Hongera.
 
Hivi hata kuwapa mawaziri chopa ni hadi wapewe na Rais???

Hii nchi uchawa umefika stage kubwa sana. Chopa ya jeshi mawaziri kwenda site unasema wamepewa na Rais.

Badala mpeleke mainjinia hata hivyo mnampeleka Ndejembi. Ujinga mtupu..
 
Mamlaka za mkoa wilaya tarafa kata Kijiji zote zimeshindwa kung'amua hayo maeneo na kuwasilisha andiko kabla au ni waziri pekee ndie anaeaminika!?
Halafu jamaa huwa wanafatana kama kumbikumbi kwa Nini mwingine asiende ulanga mwingine tegeta n.k
 
Back
Top Bottom