Uchaguzi Serikali za Mitaa: Ni huzuni, aibu, fedheha na si afya kwa Chama cha Mapinduzi(CCM)

Mkuu kwanza nikupongeze kwa mpangilio wako wa hoja, naomba niweke wazi bila kukipendelea chama changu ccm

Mosi mimi kama kiongoz wa chama ngazi ya kata naomba nikuwekee machache ambayo wenzetu walikosea na sisi tukaona gep na tukalitumia vizuri,
Viongoz wa ccm kabla ya kuchukua form tulikaa vikao na kuanza kuzipia kanuni ambazo tayali vyama vyote vilipewa, na baada tarehe ya form kufika wagombea wetu walichukua tukakaa kuwaelimisha namna ya ujazaji wahizo form kwa kupitia kipengere kimoja hadi kingine kwa umakin mkubwa,
Baada zoezi la kuchukua na kurudisha kuisha na zikabandikwa kwenye mbao tulienda pia ili kuangalia kama wenzetu walikidhi vigezo,
Nakili kabisa kua walicho kifanya wenzetu ni vituko. Form zao nyingi zilikua na kasoro na ndo maana tukawawekea mapingamizi
Ingawa pia kwetu yalikuwepo makosa madogo madogo, lkn Hayo yote wao hawakufuatilia

Uko sahihi kwa utetezi wako, sasa twende pamoja, lengo la kujaza fomu ni ili kupata wagombea kwenye uchaguzi na sio umahiri wa kujaza fomu. Sehemu zote zenye nia njema unapojaza fomu kisha ukakosea, hupewa nyingine ujaze kwa usahihi na sio kuenguliwa kwani hapo haukuwa mtihani wa kujaza fomu bali lengo ni uchaguzi. Makosa ya ujazaji fomu yako kuanzia bank, fomu za NIDA, nk, lakini kote huko hakuna aliyefukuzwa kwa kukosea kujaza, bali hupewa fomu nyingine ili kujaza kwa usahihi kwani lengo sio kukomoa bali kupata huduma husika.

Hilo hapo juu ni moja, huenda kweli walikosea kujaza kama mnavyolazimisha japo ni jambo lisilowezekana kwa idadi hiyo. Je ni kipi kilikuwa kinafanya hao wasimamizi wagome kutoa ushirikiano kwa wagombea wa upinzani na hujuma nyingine za wazi kwenye huo mchakato? Ni dhahiri hapa rais ndio anayeagiza huo ubakaji wa box la kura, hasa ukizingatia kile kinachoendelea kwenye huo mchakato.
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa mpangilio wako wa hoja, naomba niweke wazi bila kukipendelea chama changu ccm

Mosi mimi kama kiongoz wa chama ngazi ya kata naomba nikuwekee machache ambayo wenzetu walikosea na sisi tukaona gep na tukalitumia vizuri,
Viongoz wa ccm kabla ya kuchukua form tulikaa vikao na kuanza kuzipia kanuni ambazo tayali vyama vyote vilipewa, na baada tarehe ya form kufika wagombea wetu walichukua tukakaa kuwaelimisha namna ya ujazaji wahizo form kwa kupitia kipengere kimoja hadi kingine kwa umakin mkubwa,
Baada zoezi la kuchukua na kurudisha kuisha na zikabandikwa kwenye mbao tulienda pia ili kuangalia kama wenzetu walikidhi vigezo,
Nakili kabisa kua walicho kifanya wenzetu ni vituko. Form zao nyingi zilikua na kasoro na ndo maana tukawawekea mapingamizi
Ingawa pia kwetu yalikuwepo makosa madogo madogo, lkn Hayo yote wao hawakufuatilia
Unaposema form za wagombea wa CCM zilikuwa na kasoro ndogo lakini wao hawakufuatilia. Ni nani hao ambao hawakufuatilia? Ebu fafanua hapo.
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa mpangilio wako wa hoja, naomba niweke wazi bila kukipendelea chama changu ccm

Mosi mimi kama kiongoz wa chama ngazi ya kata naomba nikuwekee machache ambayo wenzetu walikosea na sisi tukaona gep na tukalitumia vizuri,
Viongoz wa ccm kabla ya kuchukua form tulikaa vikao na kuanza kuzipia kanuni ambazo tayali vyama vyote vilipewa, na baada tarehe ya form kufika wagombea wetu walichukua tukakaa kuwaelimisha namna ya ujazaji wahizo form kwa kupitia kipengere kimoja hadi kingine kwa umakin mkubwa,
Baada zoezi la kuchukua na kurudisha kuisha na zikabandikwa kwenye mbao tulienda pia ili kuangalia kama wenzetu walikidhi vigezo,
Nakili kabisa kua walicho kifanya wenzetu ni vituko. Form zao nyingi zilikua na kasoro na ndo maana tukawawekea mapingamizi
Ingawa pia kwetu yalikuwepo makosa madogo madogo, lkn Hayo yote wao hawakufuatilia
Hata mtoto wangu Wa darasa la pili hawezi kukuamini,wagombea wote Wa upinzani hawajui kujaza form,hii inatokea mwaka huu,tulijua hamwezi kukosa sababu,sasa basi malengo yenu yametimia kama mlivyotaka,fanyeni sherehe kwa kushinda kwa kishindo,pili ninaamini wapinzani ndo walikuwa wanawaletea watz umaskini kwa sasa uchumi utapaa kwa double digit,huduma za jamii asilimia 100 maisha bora kwa kila mtanzania
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha ! Machafuko huanza kwanza kwa kudharau mambo madogo kama haya but mwisho wa siku watakaoumia ni wapiga kura na ambao hawapigi kura
Tamko la kimaslahi, mimi ni nwanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo ni takayo yawasilisha hapa ni kwa manufaa ya ustawi wa chama changu CCM na Taifa letu kwa ujumla.

Nimefatilia kwa umakini mchakato mzima wa uchaguzi wa viongozi wetu katika ngazi ya Serika za Mitaa. Hakika kinachoendelea huko hakina afya na pia ni hatari zaidi kwa CCM. Binafsi naamini hizi vurugu mpaka kufikia hatua baadhi ya vyama kujitoa ni aibu kubwa katika utawala wa kidemokrasia ambao kimsingi CCM ndiye mwasisi wake.

CCM imekuwa ikijipambanua kama chama bora na zaidi ni kutokana na utendaji makini wa Rais Magufuli katika kipindi hiki cha awamu ya tano. Katika uongozi wa Rais wetu mambo mengi yamefanyika ambayo sina sababu ya kuyataja hapa. Hii ilikuwa karata tosha ya kutupa ushindi wa kishindo bila ya hofu wala figisufigisu zinazotokana na Watendaji wetu huku chini.

Kimsingi watendaji hawa wa Serikali chini ya TAMISEMI, tuseme ukweli wametutia aibu. Serikali iko uchi na chama changu chenye dhamana ya Serikali na mdau mkubwa wa uchaguzi huu pia kiko uchi

Ebu tujiulize maswali machache katika sintofahamu hii na mwisho ni malizie kwa ushauri.

A. TAMISEMI
1. Je, kwa kutumia mantiki (logic) ndogo tu, TAMISEMI inaamini idadi kubwa ya wagombea wa Upinzani walioenguliwa hawana sifa?

2. Je, nini sababu hasa ya Wagombea wengi wa upinzani kushindwa kujaza fomu zao kwa ukamilfu?

3. Iwapo fomu hizo zilikuwa na ugumu wa kuzijaza, ni kwanini TAMISEMI haikuona umuhimu wa kuwa na Semina elekezi kwa wagombea?

4. Kwakuwa wasimamizi wa uchaguzi wanasimamiwa na TAMISEMI kupitia Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye ana maslahi uchaguzi huu, Je, msimamizi huyu wa chini anakwepaje kubinya haki?

5. Tukiacha uchaguzi huu uendelee bila kujali sintofahamu iliyopo, itakuwa ni kwa manufaa ya nani?

B. CHAMA CHA MAPINDUZI
1. Chama changu kitanufaika vipi na ushindi utaotokana na ukiukwaji wa wazi wa haki?

2. Hivi ni kweli uimara wa chama changu unatokana na ulegelege ama udhaifu wa vyama pinzani?

3. Kwanini chama changu kupitia Msemaji wetu tumekuwa na papara ya kuisemea TAMISEMI juu ya uchaguzi huu?

4. Je! Ni kweli tetesi zinazozagaa huku mtaani kuwa yanayotokea sasa yalipangwa makusudi na Chama Changu?

5. Je! Ni kweli kabisa Wagombea wetu ndani ya CCM wana weledi wa kutosha hivyo kufikia hatua ya kujaza fomu pasipo kukosea?

Iwapo tutaruhusu haya yaendelee, nina wasiwasi ushindi wa kishindo wa CCM katika uchaguzi huu utakuwa ni ushindi wa mkopo ambao bila shaka malipo yake yatakuwa ya gharama kubwa baadae. Chama bora kinapaswa kukuzwa katika ushindani usio na shaka. Hatuna sababu ya kujisifia kupitia njia mbovu zinazopangwa na kutekelezwa na watendaji wetu waliopo chini ili kupata sifa na kupendwa na Mamlaka teuzi.

Nasikitika kuwa ni bahati mbaya sana leo hii nchi imekosa wa kuisemea katika ngazi ya viongozi wetu wakuu wastaafu. Yanayoendelea leo, ingekuwa enzi za uhai wa Mwalimu Nyerere, angekuwa ameishatoka na kusema jambo. Mwalimu hakuwa mtu wa kusubiri maovu yatokee ndipo baadae aingilie. Sifa bora ya viongozi wote makini duniani ni kuwa pro-active, na hii ilikuwa sifa kuu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika enzi zote za uhai wake.

Hakika hatupaswi kutoa mwanya wa Chama changu CCM kushiriki uchaguzi wenye dosari kubwa namna hii. Kwa busara na kwa manufaa ya Nchi, nashauri viongozi wakuu wa Chama changu waishauri Serikali kuhairisha uchaguzi na kutatua kwanza dosari zilizopo kwa njia ya maridhiano kisha tusonge mbele tukiwa salama na wamoja. Hatuwezi kuligawa Taifa katika misingi yenye kunyima haki kwa manufaa ya muda mfupi ya kisiasa.

Nikipata wasaa, nitakuja kuelezea athari katika USTAWI WA CHAMA CHA MAPINDUZI kutokana na sintofahamu hii iwapo mamlaka zenye dhamana katika uchaguzi huu, zitakosa kabisa utashi wa kutatua na kuacha CCM itumbukie katika uchaguzi huu wa hovyo kabisa katika historia ya nchi yetu.
 
Jamani eeeee!!!!!!! Katafute riziki,mambo ya siasa ya nchi hii muda mwingine inabidi kuziba pua.
 
Tukubali kushindwa kama hatukujipanga kwa wakati huu

Demokrasia ina mambo mengi ukizidiwa mbinu unarudi nyuma kusahihisha makosa
ahsante kwa kuunga mkono siasa za hila zinazolindwa kwa nguvu zote!!!!!!!
Anyway ushindi ni ushindi kaza mwendo mkuu
 
Tukubali kushindwa kama hatukujipanga kwa wakati huu

Demokrasia ina mambo mengi ukizidiwa mbinu unarudi nyuma kusahihisha makosa
Tuelezee aina za demokrasia unazozifahamu ili tujue hii imeangukia wapi? Hiki kituko ulishakisikia wapi duniani kama siyo hapa Tanzania? Tumejitahidi kuitangaza nchi yetu lakini sasa inafika wakati tutasema sisi siyo watanzania bali ni wakenya kwa kuogopa kashfa. Hata wakati wa mwalimu tulikuwa tunapigia jembe na nyumba au ndiyo na hapana na hakuna mtu alikuwa anakuwa disqualified sababu kulikuwa na wasaidizi kukuongoza kukosoa ulipokosea.
 
Tukubali kushindwa kama hatukujipanga kwa wakati huu

Demokrasia ina mambo mengi ukizidiwa mbinu unarudi nyuma kusahihisha makosa

Tumekuwa na nakisi kubwa ya uongozi katika zama hizi. Watu mbilikimo katika uongozi hawawezi kujua umuhimu wa seriali za mitaa. Kumbe huu ndio uongozi muhimu kabisa kuna unakuwa maisha ya kila siku ya wananchì. Ifahamike kuwa katika ngazi hizi za chini kabisa wananchì huwa hawachagui vyama vya siasa bali "individuals" wanaokidhi vigezo vinavyotumika kwenye jamii husika kumtambulisha mtu mwenye karama ya uongozi; siyo chama. Hata kama ingekuwa kweli kuwa wagombea wa vyama shindani wamefanya makosa kwenye fomu za kugombea bado busara ingetumika kuona kuwa hayo makosa hayaathiri uchaguzi wenye ushindani. Ukiona tu zaidi ya nusu wagombea wanakwenda kuenguliwa ujue tayari uchaguzi umevurugika na siyo busara kuendelea. Kwa hili la uchaguzi wa serikali za mitaa nchi ya Nyerere imenajisiwa kupita maelezo. Itoshe tu kusema: com, the ball is in your court.
 
Jafo umechemka sana bro.; kuna watu eti walikuwa wanatoa chepuo kwamba unafaa URAIS 2025, sasa uchaguzi huu mdogo umekushinda huo urais upi utaweza, labda kuongeza wake hadi wafike 4 hilo sipingi.
 
Ati ccm members wao walijaza 100% perfectly huu ushenzi anaweza kuuamini Jaffo tu.
Tamko la kimaslahi, mimi ni nwanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo ni takayo yawasilisha hapa ni kwa manufaa ya ustawi wa chama changu CCM na Taifa letu kwa ujumla.

Nimefatilia kwa umakini mchakato mzima wa uchaguzi wa viongozi wetu katika ngazi ya Serika za Mitaa. Hakika kinachoendelea huko hakina afya na pia ni hatari zaidi kwa CCM. Binafsi naamini hizi vurugu mpaka kufikia hatua baadhi ya vyama kujitoa ni aibu kubwa katika utawala wa kidemokrasia ambao kimsingi CCM ndiye mwasisi wake.

CCM imekuwa ikijipambanua kama chama bora na zaidi ni kutokana na utendaji makini wa Rais Magufuli katika kipindi hiki cha awamu ya tano. Katika uongozi wa Rais wetu mambo mengi yamefanyika ambayo sina sababu ya kuyataja hapa. Hii ilikuwa karata tosha ya kutupa ushindi wa kishindo bila ya hofu wala figisufigisu zinazotokana na Watendaji wetu huku chini.

Kimsingi watendaji hawa wa Serikali chini ya TAMISEMI, tuseme ukweli wametutia aibu. Serikali iko uchi na chama changu chenye dhamana ya Serikali na mdau mkubwa wa uchaguzi huu pia kiko uchi

Ebu tujiulize maswali machache katika sintofahamu hii na mwisho ni malizie kwa ushauri.

A. TAMISEMI
1. Je, kwa kutumia mantiki (logic) ndogo tu, TAMISEMI inaamini idadi kubwa ya wagombea wa Upinzani walioenguliwa hawana sifa?

2. Je, nini sababu hasa ya Wagombea wengi wa upinzani kushindwa kujaza fomu zao kwa ukamilfu?

3. Iwapo fomu hizo zilikuwa na ugumu wa kuzijaza, ni kwanini TAMISEMI haikuona umuhimu wa kuwa na Semina elekezi kwa wagombea?

4. Kwakuwa wasimamizi wa uchaguzi wanasimamiwa na TAMISEMI kupitia Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye ana maslahi uchaguzi huu, Je, msimamizi huyu wa chini anakwepaje kubinya haki?

5. Tukiacha uchaguzi huu uendelee bila kujali sintofahamu iliyopo, itakuwa ni kwa manufaa ya nani?

B. CHAMA CHA MAPINDUZI
1. Chama changu kitanufaika vipi na ushindi utaotokana na ukiukwaji wa wazi wa haki?

2. Hivi ni kweli uimara wa chama changu unatokana na ulegelege ama udhaifu wa vyama pinzani?

3. Kwanini chama changu kupitia Msemaji wetu tumekuwa na papara ya kuisemea TAMISEMI juu ya uchaguzi huu?

4. Je! Ni kweli tetesi zinazozagaa huku mtaani kuwa yanayotokea sasa yalipangwa makusudi na Chama Changu?

5. Je! Ni kweli kabisa Wagombea wetu ndani ya CCM wana weledi wa kutosha hivyo kufikia hatua ya kujaza fomu pasipo kukosea?

Iwapo tutaruhusu haya yaendelee, nina wasiwasi ushindi wa kishindo wa CCM katika uchaguzi huu utakuwa ni ushindi wa mkopo ambao bila shaka malipo yake yatakuwa ya gharama kubwa baadae. Chama bora kinapaswa kukuzwa katika ushindani usio na shaka. Hatuna sababu ya kujisifia kupitia njia mbovu zinazopangwa na kutekelezwa na watendaji wetu waliopo chini ili kupata sifa na kupendwa na Mamlaka teuzi.

Nasikitika kuwa ni bahati mbaya sana leo hii nchi imekosa wa kuisemea katika ngazi ya viongozi wetu wakuu wastaafu. Yanayoendelea leo, ingekuwa enzi za uhai wa Mwalimu Nyerere, angekuwa ameishatoka na kusema jambo. Mwalimu hakuwa mtu wa kusubiri maovu yatokee ndipo baadae aingilie. Sifa bora ya viongozi wote makini duniani ni kuwa pro-active, na hii ilikuwa sifa kuu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika enzi zote za uhai wake.

Hakika hatupaswi kutoa mwanya wa Chama changu CCM kushiriki uchaguzi wenye dosari kubwa namna hii. Kwa busara na kwa manufaa ya Nchi, nashauri viongozi wakuu wa Chama changu waishauri Serikali kuhairisha uchaguzi na kutatua kwanza dosari zilizopo kwa njia ya maridhiano kisha tusonge mbele tukiwa salama na wamoja. Hatuwezi kuligawa Taifa katika misingi yenye kunyima haki kwa manufaa ya muda mfupi ya kisiasa.

Nikipata wasaa, nitakuja kuelezea athari katika USTAWI WA CHAMA CHA MAPINDUZI kutokana na sintofahamu hii iwapo mamlaka zenye dhamana katika uchaguzi huu, zitakosa kabisa utashi wa kutatua na kuacha CCM itumbukie katika uchaguzi huu wa hovyo kabisa katika historia ya nchi yetu.
 
Wapinzani hawakufuatilia ili kuwawekea pingamizi kama walivyo wenzao was ccm
Bado sijaelewa labda mimi ni kilaza nivumilie tu. Ninachotaka kijua hapa ni hivi, kila ngombea alijaza form yake na baada ya kujaza inapelekwa kwa hao watendaji. Sasa hizo form kila mgombea alikuwa na uhuru wa kukagua form za wenzake upande wa upinzani ajue kama kakosea kujaza? Au niweke swali langu hivi, hao wagombea wa CCM walijuaje kwamba wapinzani wao wamekosea kujaza form? Au form baada ya kujazwa zilibandikwa kwenye ubao/ukutani?
 
Viongoz wa ccm kabla ya kuchukua form tulikaa vikao na kuanza kuzipia kanuni ambazo tayali vyama vyote vilipewa, na baada tarehe ya form kufika wagombea wetu walichukua tukakaa kuwaelimisha namna ya ujazaji wahizo form kwa kupitia kipengere kimoja hadi kingine kwa umakin mkubwa,
Baada zoezi la kuchukua na kurudisha kuisha na zikabandikwa kwenye mbao tulienda pia ili kuangalia kama wenzetu walikidhi vigezo,
Wewe kweli kiongozi mzuri. Sasa kama hizo fomu zilitakiwa umakini mkubwa, waliotakiwa kuwafunza namna ya kujaza ni viongozi wa vyama au huyo huyo mwenye kuziandaa?? Kutakuwa na kosa gani kusema kuwa; Jafo ni CCM, akaandaa fomo (CCM), akaweka kamtego kadogo kumpata kosa mjazaji, halafu akauonesha mtego kwa wanaye (CCM) huku akiuficha mtego wake kwa wasio wana(Wapinzani) ili tu washindwe??
Mshauri Jafo kuwa; Asituteulie viongozi halafu aseme tuwachague aliokwisha wateua. Huo ni uhuni na hatutaki kuitwa wahuni.
Ushauri; Asogeze mbele uchaguzi tuletewe wapinzani wa kutupinga ili watu wanaotupenda ambao kwa kweli ni wengi watuchague.
 
Ngoja tuendelee kusifu na kuabudu

Binafsi naishukuru sana sana serikali ya awamu ya tano kwa kututengenezea ardhi, mito(rivers), maziwa(lakes), wanyamapori, misitu ya asili, Bahari pamoja na mlima Kilimanjaro. Lakini pia naishukuru serikali kwa kutuondolea joto na kutuletea mawingu na mvua katika jiji letu la Dar kwa siku ya leo.

mungu ibariki serikali yetu ya awamu ya tano
 
Back
Top Bottom