Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 71,352
- 95,134
Hadi hapa nishaelewa kwa nini umeleta huu uzi, asante...
Jimbo limemshindaje Josephat Gwajima ndugu Watu8?
Kama serikali haitaki au haipeleki fedha za kujenga barabara au maji au huduma yote ya kijamii jimboni kwake, hilo litakuwaje tatizo la Gwajima?
Kama huduma za jamii kwa ujumla wake i .e maji, umeme, barabara, makazi, mipango miji, usafiri na usafirishaji, kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi nk nk. Ni kwa vipi hii imuhusu Josephat Gwajima?
Hebu nieleze bwana labda nitakuelewa....
Nani mwenye jukumu la kukusanya kodi na kupanga matumizi yake? Gwajima au serikali?
Gwajima ni mbunge na kazi ya mbunge generally ni kusema kwa niaba ya wananchi anaowakilisha bungeni. Kusema juu ya mahitaji yao ya kimaendeleo kijamii na kiuchumi ili serikali kupitia mifumo yake ifanye. Kama serikali haijafanya nani alaumiwe?
Mimi nadhani hapa wa kulaumiwa ni Rais Hayati John P. Magufuli na sasa Samia Suluhu Hassan na chama chenye dhamana ya serikali yaani CCM kuwa wamefeli kuleta maendeleo jimboni Kawe kwa Gwajima...!;