Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,518
- 34,322
Kwa Sasa CCM siyo tena chama cha Siasa bali ni kundi kubwa la watu linalotumia Siasa kujitajirisha.
Wakati wa enzi za Ali Hassan Mwinyi akiwa Mwenyekiti (1993-1994) wa chama hicho, mmojawapo wa waasisi wa chama hicho, Mwalimu Julius Nyerere alisema " CCM imegeuka kuwa kama kokoro, inabeba kila kitu"
Leo miaka 30 baadae CCM itakuwa imebeba mauchafu mangapi? Kama wakati ule Mwalimu aliona kuwa imegeuka kokoro, leo hii CCM ikoje?
Kabla ya uchaguzi 2025 CCM itagawanyika kutokana na makundi maslahi yaliyo ndani ya chama hicho.
Kundi la kwanza ni lile ambalo lilikuwa linaamini kuwa Magufuli atatawala milele. Kundi hili lilikuwa halijajitayarisha kuishi nje ya mfumo wa Magufuli.
Kundi la pili ni lile lililokuwa linaamini kuwa ikifika mwaka 2025 Magufuli atatoka madarakani na wao kuweka mtu wao.
Kundi hili la pili halikuwahi kuwaza kuwa Samia Suluhu Hassan atakuwa Mgombea wao kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.
Kundi la tatu ni la wafuasi wa Samia Suluhu Hassan. Hawa ni wafuasi walioibukia kutoka kusiko julikana.
Kabla ya Samia kuwa Rais, kundi hili la watu walikuwa hawajawahi kuamini kuwa Samia anafaa kuwa Rais.
Lakini Samia alipoupata urais kundi hili likagundua kuwa halikubaliki na kundi la kwanza wala na la pili, hivyo likajibanza kwa Samia.
Kwa kuwa ndani ya CCM hivi Sasa hakuna mtu anayeheshimika na makundi yote hayo matatu, bila ya shaka mgawanyiko ndani ya chama hicho ni Lazima kutokea!!