Ubepari unaporomoka, What's Next?

All is well
tatizo ni kwamba sioni some one anajenga hoja zake for the the benefit of Tanzanians interests,
Jana kuna mtu karusha topic hapa akionyesha namna gani wakulima wa kutoka Marekani (Jimbo la Iowa)
walivyonunua ardhi kubwa sana ya Tanzania kwa Malengo ya kuja kuendesha kilimo cha kisasa, na
kuwatrain watanzania kuendesha kilimo cha kisasa, for whose benefits, I do not know?

Wakulima hawa hawa wa IOWA ndio nasikia wanaongoza kule marekani kwa kupewa subsidy,
subsidy ni socilist practice ambayo bado inakumbatiwa na mabepari in favour of their
agriculturalisits, surprisingly, wakulima hawa hawa wa IOWA two days ago wamemshutumu
Obama on his face kwamba agenda yake ya health insurance ni socialistic and they do not want it?
very contradicting?. they love both socialism and capitalism at a go.

Back to Tanzania, tunacopy economic strategies na kuziimplement bila ya kuziblend zisuit our,
situation, Hakuna ecomomic model ambayo ni mbaya, wala nzuri kuliko nyingine, zote ziko okay,
inategemeana na trend kwenye ecomonies zingine, socialism ikiwa blended inteligently huku ikipewa
pilitical back up yenye masilahi ya uma it can work out anywhere.

yes socialism can be very well practised in capitalistic environment and vise versa, issue ni dhamila
ya kuzitekeleza agenda hizo kwa dhati kabisa, yaani serikali yetu na nyinge yoyote ile inatakiwa
kuangalia interests za majority katika any model. it will work it out. given, ujinga hasa wa rushwa, ubaguzi,
wizi na uovu mwingine unakuwa on check seriously all the time.

Hii mambo amefanya Mwinyi na Mkapa ya kuabandon socialism ya nyerere kabisa kabisa (badala ya kuiblend)
na all of a sudden, tena bila maelezo ya kutosha wakatuletea ubepari, haina tofauti na kuweka barafu
kwenye glass then ghafla unaitoa na kuweka maji ya moto a thousand of centgrade degrees and you brake the glass.
Ndio inatufanya kuhangaika kutafuta the best economic model

All models are okay for some time, it depends how you play them out.
 
Ubepari maana yake nini Kigarama? Uchambuzi wako juu ya kuporomoka kwa ubepari ni rahisi mno (too simplistic). Vitu unavyorejea kama ushahidi wa kuporomoka havitoshi kuashiria kuporomoka kwa ubepari bali ulafi wa baadhi ya wahodhi mali hasa Marekani, kama vile kutoa mikopo ya kununua nyumba kwa watu ambao wakuwa na uwezo wa kulipa madeni yao, vita mbili za Iraq na Afghanistan ambazo zilinakula madhuhuli ya walipa kodi hapa Marekani. Sera za kibepari za masoko huru na ushindani ndizo zilizoifanya China ifike hapa ilipo. Ubepari bado upo hai na utakuwa kama mfumo kwa muda mrefu sana.
Mimi nadhani mwanakijiji ameelewa vizuri sana kuhusu hii mada. Mimi sizungumzii 'matendo" ya ubepari bali nazungumzia dhana ya ubepari . Uwekezaji ni uwekezaji kama ilivyo kwa kiwanda ni kiwanda kiwe kinamilikiwa na bepari au mjamaa. Tofauti ya mifumo inaletwa na tafsiri ya watu juu ya kile kinachokusudiwa kufanya na matokeo yake. Hebu jiulize kwa nini mafundisho ya kuhusu mungu shina lake ni moja lakini Imani zinatofuatiana?
 
Mfano wa talanta ni mfano (parable) tu ya mifumo hasi ya Kibepari/Kibeberu. Ila Ukristo wenyewe hasa ambao haujachakachuliwa ni Ujamaa. Cheki:

"All the believers were together and had everything in common. They sold property and possessions to give to anyone who had need. Every day they continued to meet together in the temple courts. They broke bread in their homes and ate together with glad and sincere hearts" - Acts 44 - 46

Kwanini unatuhumu kitu ambacho wewe mwenyewe unatenda? Nani alikudanganya Ukristo ni ujamaa? Check your facts dude
 
Ujamaa ndio utakuja kuu-replace ubepari,

Mara nyingi hizi system huwa zinakuja automaticaly, lakini ujamaa tuliokuwa nao na ukomunisti wa urusi ulikuja by force (Mapinduzi, vita, nk), haukuja kwenye muda muafaka, hizi ni stage zinazomuhusu binadamu na yeye ndio muamuzi wa kuamua, Upepari ulikuja kwa kufuata stages na unaisha kwa kufuata stages na ujamaa wa kweli ndio utaingia kwa kufuata matakwa ya kibinadamu na walasio kwa mapinduzi nao utadumu mpaka mwisho wake ili stage nyingine iingie

Try to factuate that mankind did sin in a perfect scene possible i.e. Eden garden. Try to imagine that such falliable creature devised a mechanism thru a mixed ends. I concur that histicorically we are in for it whether we like or not.....capitalism and ujamaa (socialism not communism) will be mainstays production ideologies only subject modification.


I prefer to circumvent the question, even to rephrasing it. What best available and can be drawn from those two main production lanes which can be suitable to suite y/our environment and national needs. Not to choose one above the other as the best because none is.

For a start, I will practice economy policies on capitalism and political ones on socialism (I do not include communism).
 
Hauporomoki, unaporomoshwa.Tuko kwenye transition period.Tunaelekea towards the NWO.Mfumo huu utakua kama ule wa Mao au Lenin.Bado haija amuliwa.Haya ya Urusi na China ya Mao yalikuwa majaribio.Africa tulikuwa na jaribio la African Socialism.
Kwa zaidi ya Miongo miwili sasa (2 decade ) nchi zinazoendelea na maskini sana duniani ziliaminishwa kwamba kwa kufuata mfumo wa kibepari nchi hizo zitaokoka katika janga la kuangamia kiuchumi kwenye "dunia kijiji" au al maarufu Global village.

Lakini sasa mfumo huo wa Kibepari unaporomoka kama ulivyoporomoka mfumo wa kikomunisti Urusi. Kama mbadala wa Ukomunisti na Ushoshalisti ulikuwa ni ubepari na ubepari sasa unaporomoka ni nini kitaziba ombwe litakalosababishwa na kuporomoka kwa ubepari? Tulikuwa tunaambiwa hata humu ndani tuliambiwa pia. "ujamaa ulituchelewesha kuendelea" Je sasa tuna haja ya kujivunia ubepari?

Maneno kama vile "Austerity" "Slump" au "Crunch" pia "Recession" tumekutana na " Budget talks stalemate in US" kuna hili pia "china hold 45% of US bond" na mengineyo mengi ni dalili za kuanguka kwa mfumo wa kibepari.

Ni mawazo tu usikasirike.
 
Unajua soko kubwa la bidhaa za China liko wapi?
Mkuu wangu sibishani na wewe isipokuwa ni mtazamo wangu naomba tu unielewe hapo..Amerika ndio soko kubwa la China!.... kwa lugha yangu nasema - Hapana America sii soko kuu la China ila USA ni mhitaji mkubwa wa mali za China... hakuna nchi inayoweza kuchukua nafasi ya China ku manufacture na kusupply to America at that cost - HAKUNA..Tunarudi paleplae kwamba Demand ndio huongoza Supply na mhitaji ni Amerika - Hii ndio theory yangu.

Ni hivi USA wasiponunua mali ya China nchi nyingine Duniani zitanunua hasa Afrika na Asia ambao tunakuja juu na tunapenda bure ghali. Uchumi wa China unaweza kweli kushuka kidogo sana lakini sii sawa na Amerika wakiacha kununua mali za China ambazo ni cheap kulingana na maisha ya Wamarekani wengi.. American can't afford European goods, even those made in USA tena sawa na sisi tunavyoshindwa kuondokana na mitumba.

Europe sii wanunuzi wakubwa wa mali za China tena nchi nyingi wamepiga marufuku ndio maana hakuna soko kubwa la mali za China pia wenzetu wanajali sana quality na standard zao sio USA na Canada.. huku tunabambikiwa kila kitu kwa kwenda mbele after all sisi wote ni immigrant tumekuja kuchuma - who cares! - Ubepari ni pamoja na Kanyaboya!.

Kwa hiyo mkuu wangu mahesabu ya nchi kama Marekani kwamba China itakuja anguka kiuchumi ni hadithi za Alinacha kama utatazama hali halisi, watu na Mazingira kwa sababu soko la mali za China ndio linazidi kupanuka mwaka hadi mwaka wanauza kiasi kwamba inafikiriwa watashindwa kukidhi mahitaji ya soko (demand)...American hawana cha kuuza nje isipokuwa silaha na Dollar yao inapoteza nguvu kila kukicha...
 
Wakuu kuna vitu vitatu hapa sijui ni kipi kilichoporomoka!
CAPITALISM, CAPITALIST, CAPITALIZE
Ndugu yangu hakuna kilichoporomoka bali Capitalism ndiyo inaporomoka. kumbuka huwezi kuwa na Capitalism bila ya Capitalist ambao wana Capitalize uchumi.
Ujerumani imeshatangaza kwamb mategemeo ya uchumi kukua kwa asilimia 0.5 yameshindikana badala yake uchumi wao umekuwa kwa asilimia 0.1. kumbuka Uchumi wa jerumani ndiyo dhamana ya fedha ya Euro, kwa maana nyingine Euro nayo thamani yake imeporomoka.
 
Ndugu yangu hakuna kilichoporomoka bali Capitalism ndiyo inaporomoka. kumbuka huwezi kuwa na Capitalism bila ya Capitalist ambao wana Capitalize uchumi.
Ujerumani imeshatangaza kwamb mategemeo ya uchumi kukua kwa asilimia 0.5 yameshindikana badala yake uchumi wao umekuwa kwa asilimia 0.1. kumbuka Uchumi wa jerumani ndiyo dhamana ya fedha ya Euro, kwa maana nyingine Euro nayo thamani yake imeporomoka.
Kwa hiyo Ubepari hauwezi kufa isipokuwa tupo ktk kubadilishana mikono - kuna wasiwasi ya China, India, Brazil, na pengine Russia ndio watakuwa vinara wa Ubepari..
 
Kwa hiyo Ubepari hauwezi kufa isipokuwa tupo ktk kubadilishana mikono - kuna wasiwasi ya China, India, Brazil, na pengine Russia ndio watakuwa vinara wa Ubepari..
Nadhani sijasema kwamba ubepari umekufa bali unaporomoka na kuporomoka huku kwa ubepari ni lazima kutatengeneza ombwe ambalo ni lazima lizibwe. Kwa bahati mbaya ubepari wa Uchina,Brazil au india hauwezi kuwa sawa na wa kimarekani.
Swali langu baada ya kuporomoka kwa ubepari ni nini kitafuatia kwa sisi vinchi ambavyo kama kasuku tuliimba sera za kibepari na kama mazuzu tulitekeleza maelekezo yoote ya IMF bila ya kuuliza uliza.
 
..hivi China kwenye Ujamaa kuna un-employment checks, social security program, au food stamps?
 
hata sijui nyerere anaingia vipi hapa....
au ni kwa kuwa mko in love na nyerere????????

hiyo china aliyokuwa anaiga nyerere iko wapi leo hii?

hivi kuna mtu anaweza kutufafanulia sweden,denmark,finland wanatumia model ipi ya uchumi??????/
Kwa mtazamo wa Nyerere, ubepari na hata ukomunist ulikuwa hauna mpango.In short mimi binafsi namuona Nyerere aliona mbali maana hawa viongozi waliomfuatia wamekuwa na bidii kuusifia ubepari na hata kuwa makuwadi wake! Ubepari unavyoporomoka, wao watatuambia nini tena? Story si ndio itakuwa imefika mwisho wake??
 
..hivi China kwenye Ujamaa kuna un-employment checks, social security program, au food stamps?
Mkuu hawa wajamaa wala usifanye mchezo nao..If they can work for 50cents/hrs, unaweza ajili watu wangapi na kwa masaa mangapi.. Kumbuka tu kwamba wao wanatumia work force kukidhi mahitaji ya watu haraka iwezekanavyo na at the lowest cost possible ndani ya system ya Kibepari... Mahala US tunapoajiri mtu mmoja wao wanaweka wanne (wajuzi na wasomi) cheaper kisha wanasimamiwa kibepari.. With 1.5 billioni hata kama una 20% unemployment, nguvu ya ile 80% work force ni sawa na uszalishaji wa Europe nzima. Kulingana na record za kidunia wana kitu kama 4.5% unemployment rate take it as - funika kombe...

Tatizo la kiuchumi ni pale hatutazami vitu ktk real face value. Kwa mfano Guinea Bissau imekuwa ranked kama nchi tajiri Afrika nzima kumbe hakuna kitu kiukweli isipokuwa pato lao na hesabu ya watu ndio imewapa nafasi hiyo. Unemployment ni ndogo kwa sababu hawana watu hata hivyo tena wanahitaji zaidi..Kuna maskini huko kupita maelezo na kimaisha ni bora ya wakazi wa Mwanza au Arusha kuliko kuishi huko... Kwa hiyo hata upande wa China watu wanaitazama hivyo yaani pato lao against Population lakini bila kujua kwamba nguvu ya watu 1bil ktk uzalishaji acha hao over 200,000 diasporas ambao wanafanya kikweli sii tunawaona wanavyoishi huku majuu....China is Untouchables..
 
Ubepari hauporomoki, bali unakuwa kwa kasi sana. Mnapozungumzia Ubepari usiangalie Marekani tu peke yake, angalia pia BRICK countries kama Brazil, China, Russia, na India, uchumi wao unakuwa kwa kasi sana kutokana na Ubepari.

Kitu kinachotokea kwa Marekani sasa hivi ni Comperative Advantage kutoka ktk hizi nchi za BRICK, Brazil, India, Russia, na China. Philosophy ya comperative advantage ndiyo inayotumika sasa hivi ktk hizi nchi, na ndiyo maana China ana Comperative Advantage kubwa kutokana na cheap labor.

In the future, uchumi wa China, na per capita yao itapoanza kukua zaidi, na poverty level itapungua. Hii itasababisha vitu na maisha kupanda China na kuwa same level na nchi za Ulaya, North America. Hapo ndipo utakapoona comperative advantage yao China ya cheap labor inaondoka.

Chukulia Mfano wa Japan, South Korea, nk. Utagundua comperative advantage ya cheap labor ni ya short term. KtK miaka ijayo kama 2050, Africa ndiyo itakuwa ina comperative advantage kubwa ya cheap labor. Ndiyo maana China anawekeza sana Africa, kwa sababu wanajua Afrika ndiyo itakayokuwa inatengeneza vitu vyote.
 
Last Time I checked hata China ni capitalist country....

Majority of countries wana mfumo wa kibepari wenye forms tofauti..., State Capitalism; Corporate Capitalism, kwahiyo they are just labels deep down wote tuna mfumo wa Kibepari
 
Kwa hiyo Ubepari hauwezi kufa isipokuwa tupo ktk kubadilishana mikono - kuna wasiwasi ya China, India, Brazil, na pengine Russia ndio watakuwa vinara wa Ubepari..

Good point. Hizi nchi uchumi wao unakuwa kwa kasi kwa sababu ya Ubepari. Hawa watu wanaosema Ubepari unaporomoka wao wanaangalia Marekani tu. Hizi nchi zina comperative advantage kubwa sana ya cheap labor.

Swali la kujiuliza, je sisi TZ, tutakuwa na vyuo vikuu vingapi ktk 2050, kutoa cheap labor ya Dunia? Kwa sababu haya makampuni (investors) yanaangalia sana elimu ya juu ktk kuwekeza ktk nchi.
 
unajua hili nimewahi kulifikiria sana na ni vizuri kuuliza: Uislamu kama mfumo wa uchumi unakaribiana na ubepari au ujamaa?

Uislaam hauko kwenye ubepari wala ujamaa. Uislaam ni mfumo wa Maisha as a whole unaojitegemea na wala haukaribiani na hiyo mifumo iliyoundwa kibinadam.
 
Ukiangalia Marx's theory of history baada ya ubepari ni ujamaa halafu communism. Na hapa hakuna kuruka stage kama tulivyojaribu sisi kuruka stage ya ubepari!

Umeniacha hoi kwenye nyekundu. Which is which?
 
Good point. Hizi nchi uchumi wao unakuwa kwa kasi kwa sababu ya Ubepari. Hawa watu wanaosema Ubepari unaporomoka wao wanaangalia Marekani tu. Hizi nchi zina comperative advantage kubwa sana ya cheap labor.

Swali la kujiuliza, je sisi TZ, tutakuwa na vyuo vikuu vingapi ktk 2050, kutoa cheap labor ya Dunia? Kwa sababu haya makampuni (investors) yanaangalia sana elimu ya juu ktk kuwekeza ktk nchi.
Sidhani kama hakuna asiyeona hiyo " comparative advantages" ya hizo nchi hizo nyingine zinazojaribu kuujenga mfumo wa kibepari. Lakini ni lazima pia tukubali kwamba kila kitu lazima kiwe na " axis" yake, na kwa ubepari ni lazima uzitaje Marekani, uingereza, na ujerumani

Kumbuka kwamba ni US Dollar, Yen, Pound na Deutch Mark ndizo zinatumika kuweka vigezo vya thamani ya fedha nyingine duniani.
 
Back
Top Bottom