Nilikuwa napata shida sana ni kwanini unakuta watu wanachinjana kwa sababu tu ya tofauti ya dini zao ila sasa nimeanza kuelewa. Hii tabia ya kudharau madrassa imeota mizizi sana hapa JF na isipokemewa na kuisha itatupeleka pabaya sana. Inashangaza sana, yaani watu wanajadili mada tofauti halafu mtu anatoka huko alikotoka anaona jambo la msingi ni kuleta dharau kwa madrassa.Sasa hiyo ndiyo nini? Watu waliyoenda madrassah utawajua tu for their predisposition to rampant copying-and-pasting without feeling the need to explain anything further. Halafu hapo anajiona kachangia kitu cha maana.
Kwa kweli naomba niseme nimejaribu sana kutokujali lakini sasa naona imezidi. Na ninasema hizi dharau taratibu naona zinaanza kuzaa chuki kali sana moyoni mwangu. Tuwe makini sana maana kama tukiacha hali iendelee hivi, nina hakika itafikia mahali pabaya, na ubaya au uzuri mahali hapo mimi sipaogopi hata kidogo.
Tuheshimiane wakuu, msidhani waislamu ni wajinga sana.