Ubepari unaporomoka, What's Next?

Kaka tafadhali sana jitunzie heshima yako huyo unayejibizana naye ni tofyo kabisa hapo hana theory yoyote ya uchumi anachojua ni ubepari na ujamaa tu hajui kama hizi kitu zinaweza kuwa modified ili ziapply hapa Africa ye anawaza ujamaa ukija utakua kama wa enzi za mwalimu na ndo utakua mwisho wake Kupiga picha na magari ya Kina Mosha..
Any way endelea kutupa darasa kuhusu Islamic Economy na pia African Modified Socialim achana na Viazi hao

Mkuu,

Economics key fundamental definition is how we managed our resources. This is why economics is called the father of all social science subjects. Sasa kwakuwa tunajiuliza vipi tunazitawala resources zetu basi ndio akina Karl Max, Smith, Ricardo and others wakaja na mifumo mbali mbali mikuu inayotambulika ni ubepari kwa maana ya kutoa fursa zaidi kwa sekta binafsi kusimamia utawala wa rasilimali zetu na ujamaa unaosema ni serikali na vyombo vinavyosimamiwa na serikali ndio vina mamlaka ya kusimamia rasilimali zetu.

Changamoto zilizojitokeza kwa muda wa karne mbili ni kwamba mifumo hii imeonekana inachangamoto zake. Ila kubwa ni kwamba mifumo yote inaendeshwa kwa misingi ya kutokuwa na utu na usawa pamoja na uwazi kwa maana ya Transparency. Na hapo ndio wasomi wengine akina Lloyd Metzer, Mohsin Khan walipendekeza kuwepo na economic model nyengine ambayo inao uwezo wa kuzuia mapungufu yanayotokana na mfumo wa ubepari na kijamaa.

Na hawa hawakupata msingi isipokuwa walifuata nyayo za akina Joseph Spengler, na Joseph Schumpeter. Nao hawa walitoa mawazo kutoka kwa akina Ibn Taymiyaah, Ibn Miskawayh, Imam Al-Ghazal, Imam Nawawi, na wengineo wengi. Na hawa walitoa kutoka kwa wanazuoni kama Imam Abu Hanifa, Imam Maliki na Imam Shafii (Mmungu awarehemu na awalipe kwa jitihada zao na sisi pia atupe).

Sasa kwanini nasema Islamic Economics na sio Modified Socialism or Capitalism. Hii ni kwasababu any model iliyopo inategemeana sana na utility ya model kufikia malengo husika. Changamoto iliyonayo mfano Capitalism ni kwamba msingi wake mkuu ni kuhamasisha sekta binafsi. Sasa kama unahamasisha sekta binafsi ni lazima uweke mazingira ya kuwawezesha sekta binafsi na hapo ndio unaanza kuingia katika matatizo. Mfano sekta binafsi watataka fursa za pesa za kibenki. Lakini, benki nazo zinatakiwa zipate faida na hivyo basi itabidi sekta za binafsi zipewe fursa kwa mujibu wa taratibu za kibenki. Ikiwa itakuwa ngumu inamaana serikali itabidi iwe inatoa msaada kidogo kuwasaidia sekta binafsi zikue na hivyo basi itabidi iwakamue wanyonge kuchangia katika fuko la nchi. Na kwa maana hivyo utakuwa unawanufaisha wachache kwa kuwakamua wengi wanyonge.

Tukija kwenye mfumo wa ujamaa nao pia una changamoto zake. Mojawapo ni mzigo mkubwa wa matumizi ya serikali. China wamejaribu kuweko mfumo wao wa kibepari na ujamaa. Imewasaidia kuweza kubalance baina ya sekta binafsi na jukumu la serikali kuhudumia jamii. Ila China changamoto waliyonayo ni kuwa ndani ya mfumo huo wa kijamaa umetengeneza tabaka la watawala ambao wamekuwa wakitumia sekta binafsi kutafuna hela za serikali na kuzitorosha nje ya nchi. Kama mtakumbuka kuna kesi mmoja inamhusisha jamaa mmoja mwingereza na mama wa kichina. Jamaa aliuwawa Beijing ikasemekana alijua kumbe walirushana hela kati ya mwanamke na yule bwana. Ilipokuja kuchunguzwa iligundulika yule dada alikuwa mke wa kigogo au waziri fulani kule china na matokeo yake akawa amesimamishwa na kufunguliwa kesi.


Sasa utakuta kuwa Islamic Economics imebakia katika mfumo wa kiuchumi ambayo ni ngumu kutekelezeka but ndio solution katika mfumo wa kiuchumi wa dunia hii. Islamic Economics inagusa kote katika ubepari na ujamaa ila kuna la ziada nalo uwazi, jukumu la pamoja na kufanya kazi kwa kufuata misingi fulani ya kiungu. Naomba ieleweke hapa simaanishi watu wakasali msikitini bali la hasha. Ninachomaanisha mfumo wa kiuchumi umeundwa na kitabu kitakatifu cha quran inamaana unachokifanya lazima kiendane na mifumo ya msingi iliyojengwa na Quran pamoja Sunna za bwana mtume SAW.


Jamani nimetumia muda wa kutosha kwa leo Nilikuwapo!
 
W. J. Malecela ukisoma vizuri nilichoandika nimesema ni "dalili" ya kuanguka kwa ubepari wala sijasema ubepari "unakufa". Mdondoaji hoja zako zina mashiko ila jipange vizuri ili wale wenye hofu ya kutengwa na mfumo wa "Islamic Economy" kwa kutokuwa waislamu waone ni kwa jinsi gani watashiriki.

kwa mfano, ni vipi Muislamu na asiye muislamu wakihitaji huduma moja kwa wakati mmoja hakutakuwa na kubaguana mbele ya mtoa huduma? Wasio waislamu wataruhusiwa kukopa kwenye benki zisizotoza riba halafu wao wakaruhusiwa kuzitumia fedha walizokopa kwa shughuli zinazohusiana na utozaji wa riba??
 
W. J. Malecela ukisoma vizuri nilichoandika nimesema ni "dalili" ya kuanguka kwa ubepari wala sijasema ubepari "unakufa". Mdondoaji hoja zako zina mashiko ila jipange vizuri ili wale wenye hofu ya kutengwa na mfumo wa "Islamic Economy" kwa kutokuwa waislamu waone ni kwa jinsi gani watashiriki.

kwa mfano, ni vipi Muislamu na asiye muislamu wakihitaji huduma moja kwa wakati mmoja hakutakuwa na kubaguana mbele ya mtoa huduma? Wasio waislamu wataruhusiwa kukopa kwenye benki zisizotoza riba halafu wao wakaruhusiwa kuzitumia fedha walizokopa kwa shughuli zinazohusiana na utozaji wa riba??

Mkuu,

Uingereza na Ujerumani na Marekani huduma za kibenki zinazofuata sharia hutolewa kwa waislamu na wasiokuwa waislamu. Makampuni ya Ujerumani na Uingereza wameona kuna unafuu kukopa katika masoko ya mitaji inayotumia sharia za kiislamu. Wiki iliyopita South Africa wameamua kukopa katika masoko ya mitaji inayofuata sharia za kiislamu. Leo Benki Kuu ya Ulaya wameshusha interest hadi karibu 0 (0.05% au 0.0005). Sasa unahitaji kuwa convince kivipi Kigarama. Anyway, mie sina haja ya kumshawishi mtu ni yeye mwenyewe ndio atashawishika kuja au la.
 
Back
Top Bottom