Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania: Uwezekano wa kupata Corona Dar ni mkubwa

In the daily update today 1500 samples were tested. Kenya now has 22 more confirmed cases. 25 truck drivers waiting to enter Kenya via Namanga border have all tested positive for Covid19. 24 are Tanzanians, 1 Rwandan.
The GOK has rightly notified GOT of the truck driver cases and denied them entry into Kenya.
 
Hivi Marekani inaweza kushindwa ku-organize repatriation ya watu wake? Kama Kunyaland imesomba watu wake J3? The issue here is the US is by far worse than Tanzania!
 
Msanii wa Tanzania

Haki miliki ya pichaERICKY BONIPHACE

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umewaonya raia wake waishio nchini humo kuchukua tahadhari juu ya hatari ya maambukizo ya corona.

Mapema leo Jumatano, barua pepe kutoka ubalozi huo wa jijini Dar es Salaam kwenda kwa raia wa Marekani waliopo Tanzania kuhusu hali ya virusi vya corona ilisambaa mitandaoni.
Ubalozi huo tayari umechapisha taarifa hiyo kwenye mitandao yake ya kijamii pamoja na tovuti yake.

"Hatari ya kupata maambukizi ya Corona jijini Dar es Salaam ni kubwa sana. Licha ya kwamba taarifa hazitolewi mara kwa mara.

Ushaidi wote unaonyesha kuwa kuna mlipuko mkubwa wa maambukizi ya corona jijini Dar es Salaam na meneo mengine ya Tanzania. Ubalozi wa Tanzania unawataka raia wa Marekani pamoja na familia zao kubaki nyumbani na kutoka kwa ajili ya mahuitaji muhimu tu kama chakula, na kuzuia kukaribisha wageni katika nyumba zao".

Taarifa hiyo iliongeza kusema hospitali nyingi Dar es Salaam zimejaa kipindi hiki. Huku uwezo wa hospitali zilizopo Tanzania ni mdogo na hii inaweza kupelekea huduma za afya kuchelewa zikiwemo huduma za afya za kukabiliana na corona.

Aidha serikali ya Tanzania haijatoa ripoti kuhusu takwimu mpya ya wagonjwa wa corona tangu Aprili 29.

Mpaka sasa taarifa rasmi za maambukizi ya wagonjwa wa corona Tanzania ni 509, waliopona 183 na vifo 21.
Kunawa mikono

Haki miliki ya pichaERICKY BONIPHACE

Hatahivyo ubalozi wa Marekani nchini Tanzania uliongeza kusema kuwa inawawia vigumu kuwaondoa raia wake nchini humo kwa sababu serikali ya Tanzania imesitisha safari zote za kimataifa tangu Aprili, 11 na hakuna hata ndege za kibiashara zinazofanya kazi.

"Raia wa Marekani waliopo Tanzania wametakiwa kujiandaa kubaki nchini humo kwa muda usiojulikana.

Raia wa Marekani waliopo Tanzania wametakiwa kujiandaa kubaki nchini humo kwa muda usiojulikana.

Serikali ya Marekani haina mpango wa kuleta ndege nchini humu siku kwa sasa lakini ikitokea fursa hiyo watawajulisha hivyo ni vyema wakatuma taarifa zao kama familia, kundi au yeyote ambaye ni mkazi wa kudumu wa Marekani atume taarifa zake ubalozini".

Tanzania kukosolewa
Kumekuwa na ukosolewaji wa ndani na nje ya Tanzania juu ya hatua zinazochulukiwa na serikali ya nchi hiyo katika mapambano dhidi ya virusi vya corona.

Wakati nchi mbalimbali duniani n ahata majirani wakichukua hatua kali kama za kupiga marufuku watu kutoka nje ama 'lockdown' Tanzania imeamua kutoa tahadhari zaidi kwa raia wake.

Rais John Magufuli wa Taifa hilo pia amesema katu haitatangaza lockdown.
Mwezi uliopita, Shirika la Afya Duniani- WHO liliikosoa Tanzania kwa kuchelewa kuchukua hatua za mapema kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Mkuu wa WHO wa bara la Afrika Bi Matshidiso Moeti alisema kumekuwa na hofu juu ya kukua kwa kasi ya maambukizi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

"Kwa hakika tumeona kuwa watu kuacha kutangamana, pamoja na kupiga marufuku kwa mikusanyiko ya watu wengi kumechukua muda mrefu kufanyika na tunaamini kuwa hayo yanaweza kuwa ni moja ya mambo yaliyosababisha ongezeko la kasi la wagonjwa wa corona," alisema Dkt Moeti katika mkutano na wanahabari.

Tanzania pia imekosolewa kwa msimamo wa rais Magufuli wa kuendelea kuruhusu nyumba za ibada kuwa wazi. Hata hivyo baadhi ya viongozi wa dini nchini humo wamechukua hatua binafsi za kufunga maeneo yao ya ibada kwa hofu ya kusambaza maambukizi ya corona.
Hivi karibuni, rais Magufuli alitilia shaka ubora wa vifaa vinavyotumika katika kupima corona kwenye maambara kuu ya nchi hiyo. Hilo lilitokana na uchunguzi wa siri aliouagiza kwa kutumia sampuli za Wanyama na matunda na baadhi yake kukutwa na virusi.

Maafisa wawili waandamizi wa maabara hiyo wamesimamishwa kazi huku uchunguzi ukifanyika.

Hata hivyo, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (CDC) pamoja na WHO wamesema kwamba vifaa vya kupimia virusi vya corona nchini Tanzania havina shida yeyote.

Kituo hicho cha Africa CDC pamoja na wakfu wa Jack Ma, Shirika la msaada la bilionea wa China, ndio walisambaza vifaa hivyo.

Tanzania pia inakosolewa kwa kutokutoa takwimu za mara kwa mara za mwenendo wa ugonjwa huo. Mara ya mwisho kwa takwimu kutolewa ilikuwa wiki mbili zilizopita.
 
Back
Top Bottom