Tutorial Assistant: Nafasi bora ya kazi isiyojadiliwa

Vyuo vikuu viko katika makundi mawili, ambavyo viko chini ya TCU na ambavyo vinasimamiwa na NACTE. IFM ni moja ya vile ambavyo viko chini ya NACTE na kwa kweli, hivi ni vyuo vikuu hapa ndani ila nje havitambukiki. Hata katika orodha ya vyuo vikuu Tanzania kwa mujibu wa TCU hutavikuta. Hivi vyuo, vina vigezo tofauti vya kiajira, kuanzia intaeview zake mpaka masharti na sifa. Hapa GPA ya 3.5 ya degree ya awali utapata kazi na zoezi zima la ajira huendeshwa na tume ya ajira.
Kundi la pili la vyuo ni vyuo vikuu ambavyo vinatambulika na kusimamiwa na TCU. Hivi ni vyuo ambavyo vina hadhi ya kimataifa na vingi viko accredited kimataifa. Sifa ya kupata hapa lazima uwe na GPA ya 3.8 kwa degree ya awali. Ajira zake pia kwa upande wa wafanyakazi wataaluma huendeshwa na kamati za ajira za vyuo. Hapa tume ya ajira huja kama observers tu kuona kama taratibu zote za kiajira zinafuatwa lakini wao sio custodian wa zoezi la ajira hizi.
Tutorial Assistant wa DIT, IFM, TIA...na wengine wanaofanana na hawa ni tofauti na TA wa Udsm, UDOM, SAUT, TUMAINI, SUA..na wengine wanaofanana.
Mishashara katika makundi haya ya vyuo haitofautiani sana isipokuwa hutofautiana katika maslahi mengine kama fursa kusoma.

Karibu kwenye ulingo, uwanoe vijana vichwa.
Mkuu kwa hakika unauzoefu,na naona ukijipanga unachukua hizi kazi MTU yeyote bila koneksheni
 
- Hata Kama kafeli interview? Hivi unajua Kuwa Kanuni za Uendeshaji wa sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma zinasema Kwa Kada ya Ufundishaji wa Vyuoni unatakiwa upate 70% kwenda Juu, Sasa Kama Kakosa hiyo 70% Maana yake hafai.
70% ktk oral au written?
 
Topic unachagua mwenyewe..tuliomba direct chuo na utumishi walokuwapo kusimamia tu ila oral wanakua wale doctors ndo wanauliza maswali..hr na secretary pia academic wa chuo husika anakuwapo.Panel ilikua na watu 7 na tuliitwa watano tu.Walianza na maswali general after that nkaona umeletwa ubao..Mark pen..ufutio nmeambiwa haya chagua topic yoyote utufundishe kwa nusu saa.

Hahaha hapa kama wewe kimeo lazima uombe maji ya kunywa kwanza
 
Vyuo vikuu viko katika makundi mawili, ambavyo viko chini ya TCU na ambavyo vinasimamiwa na NACTE. IFM ni moja ya vile ambavyo viko chini ya NACTE na kwa kweli, hivi ni vyuo vikuu hapa ndani ila nje havitambukiki. Hata katika orodha ya vyuo vikuu Tanzania kwa mujibu wa TCU hutavikuta. Hivi vyuo, vina vigezo tofauti vya kiajira, kuanzia intaeview zake mpaka masharti na sifa. Hapa GPA ya 3.5 ya degree ya awali utapata kazi na zoezi zima la ajira huendeshwa na tume ya ajira.
Kundi la pili la vyuo ni vyuo vikuu ambavyo vinatambulika na kusimamiwa na TCU. Hivi ni vyuo ambavyo vina hadhi ya kimataifa na vingi viko accredited kimataifa. Sifa ya kupata hapa lazima uwe na GPA ya 3.8 kwa degree ya awali. Ajira zake pia kwa upande wa wafanyakazi wataaluma huendeshwa na kamati za ajira za vyuo. Hapa tume ya ajira huja kama observers tu kuona kama taratibu zote za kiajira zinafuatwa lakini wao sio custodian wa zoezi la ajira hizi.
Tutorial Assistant wa DIT, IFM, TIA...na wengine wanaofanana na hawa ni tofauti na TA wa Udsm, UDOM, SAUT, TUMAINI, SUA..na wengine wanaofanana.
Mishashara katika makundi haya ya vyuo haitofautiani sana isipokuwa hutofautiana katika maslahi mengine kama fursa kusoma.

Karibu kwenye ulingo, uwanoe vijana vichwa.

Sorry

Sijaelea hapo IFM,TIA nje havitambuliki kwahiyo mtu akitaka kusoma Masters nje inakuwaje wakati ana bachelor kutoka hizo taasisi?
 
Kuna changamoto kiasi chake, moja ni pale itakapohitaji uthibitisho ama tafsiri ya matokeo yako toka kwenye mamlaka ya vyuo vikuu ya nchi. Kwa msingi huo anayetakiwa kufanya hivyo ni TCU ambaye sio msimamizi wa hivi vyuo vya kati. Sio kwamba haiwezekani bali kumekuwepo na changamoto kadhaa.

oh sawa.
 
Si kweli mkuu, TCU walisha harmonize hiyo kitu, ikapandishwa toka 3.5 hadi 3.8. Nina uhakika na ninachokwambia na nimekuwa kwenye panel kadhaa kwa miaka sita iliyopita
Uko unaishi zamani.
Muongozo niliouona hauzidi miaka mitatu tangu utolewe.!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom