Tutaajiri Makatibu CHADEMA nchi nzima-Dr Slaa

By Molemo
Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amesema chama chake kimeamua kupanga mikakati madhubuti ya kujiimarisha ndani ya chama.

Kiongozi huyo mashuhuri nchini aliyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa baraza la Ushauri Mkoa wa Kagera lililofanyika Karagwe na kuhudhuriwa na viongozi wa majimbo yote ya mkoa wa Kagera.

Dr Slaa alisema moja ya mikakati ya chama chake ni kuajiri Makatibu wa Chama kote nchini.Pia Kiongozi huyo makini nchini alisema mikakati mingine ni kugawa Pikipiki kila Kata kwa ajili ya shughuli za chama na pia kujenga ofisi za kudumu kote nchini na zenye hadhi.

Kiongozi huyo anayetenda kwa mujibu wa maneno yake amewahakikishia viongozi hao wa chama kwamba atahakikisha mambo yote hayo yatasimamiwa kwa ukamilifu.

Source:Tanzania Daima

- Yaaani huyu Mzee huwa ananishangaza sana, yaani Chama hakina wanachama kabisa Zanzibar wala Songea, lakini yeye anakimbilia kufungua matawi Ughaibuni na sasa eti atawaajiri Makatibu kila Mkoa, yaani hawa Chadema na huyu Mzeee hawana jipya lao, kila siku kuiga toka CCM, sasa nimeamini kwamba kinyago ulichokichonga mwenyewe hakiwezi kukutisha!!

Le Mutuz!!
kweli wivu mbaya!!!
ona unavyomwaga puumba hata hujistukii!
sasa nnaanza kuelewa kwa nini walikupeleka ukasome ughaibuni, kama ungebaki bongo disco ilikuwa inakuhusu.
 
- Look here mimi nimegombea na kushinda so sasa ni kiongozi wa Taifa in just miezi kumi tu, nyie Chadema miaka 25 kila mkigombea mnapigwa chini Urais na wananchi, sasa hata udiwani nao mnapigwa chini tena kwa kipigo cha mbwa, sasa wananchi wa Tanzania tuwasaidaje? si mjipime tu muwache siasa maana zina wenyewe hizo!! nyie hamziwezi tena!! ha! ha!

Le Mutuz!!

Acha propaganda sipendi kukujibu ila leo nitakujibu vyama vingi vimeanza mwaka 1992 ni maana mpaka sasa vina miaka 20 tu ya uhai.

Mara ya kwanza chadema kuweka mgombea uraisi ni mwaka 2005 mbowe alipogombea na ya pili 2010 dr slaa alipogombea.

1995 na 2000 hatukusimamisha mgombea.sasa unasema mmetushinda kwa miaka 25 inatoka wapi wewe jamaa.

Tumesimamisha wagombea uraisi kwa mwaka 2005 na 2010 utacheki chama kinavyokua kwa kasi.

Naona chadema kinakunyima usingizi kwa ukongwe wenu kwenye siasa kunyima usingizi na chadema kweli speed yetu inawatisha.

Tekelezeni ahadi propaganda kwenye mitandao bila kusimamia hoja won't help ccm.

Tuleteeni maisha bora wananchi wameyakosa sasa wanayafuata chadema.

Wamekosa elimu bure wataifuata chadema.
 
kweli wivu mbaya!!!
ona unavyomwaga puumba hata hujistukii!
sasa nnaanza kuelewa kwa nini walikupeleka ukasome ughaibuni, kama ungebaki bongo disco ilikuwa inakuhusu.

huyu alipelekwa exile .... lakini haikumsaidia
 
Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amesema chama chake kimeamua kupanga mikakati madhubuti ya kujiimarisha ndani ya chama.

Kiongozi huyo mashuhuri nchini aliyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa baraza la Ushauri Mkoa wa Kagera lililofanyika Karagwe na kuhudhuriwa na viongozi wa majimbo yote ya mkoa wa Kagera.

Dr Slaa alisema moja ya mikakati ya chama chake ni kuajiri Makatibu wa Chama kote nchini.Pia Kiongozi huyo makini nchini alisema mikakati mingine ni kugawa Pikipiki kila Kata kwa ajili ya shughuli za chama na pia kujenga ofisi za kudumu kote nchini na zenye hadhi.

Kiongozi huyo anayetenda kwa mujibu wa maneno yake amewahakikishia viongozi hao wa chama kwamba atahakikisha mambo yote hayo yatasimamiwa kwa ukamilifu.

Source:Tanzania Daima

selection katika recruitment ifanyike kwa umakini sana. Mimi nita-apply!!
 
Dr ni mtu mwenye mipango na mikakati dhabiti. Kuajiri makatibu wa wilaya na mikoa kwanza ni kuongeza ajira kwa watanzania hasa wanachama wa chadema lakini la pili ni kujenga heshima na kukubalika zaidi kwa watanzania kwani kunapokuwepo na ofisi rasmi na watendaji wa chama inawafanya wananchi wajisikie kuwa chama kipo katika jamii yao
 
- Yaaani huyu Mzee huwa ananishangaza sana, yaani Chama hakina wanachama kabisa Zanzibar wala Songea, lakini yeye anakimbilia kufungua matawi Ughaibuni na sasa eti atawaajiri Makatibu kila Mkoa, yaani hawa Chadema na huyu Mzeee hawana jipya lao, kila siku kuiga toka CCM, sasa nimeamini kwamba kinyago ulichokichonga mwenyewe hakiwezi kukutisha!!

Le Mutuz!!
Baba yako na mama yako wa kambo walifanya nini la maana zaidi ya kushindwa na watu dhaifu kama Lusinde
 
Nilikuwa nafikiri tayari Chadema wana makatibu wa wilaya na mikoa, kumbe muda wote huo na maandamano kila siku kumbe hata katibu wa wilaya hakuna?. Sasa kadi za chama zinauzwaje huko wilayani na mikoani kama hata ofisi hakuna?. Kuna ofisi za Chadema UK na NY, kumbe hakuna ofisi za chadema Chalinze?, lazima kuna tatizo ndani ya Chadema.
Makatibu walikuwepo, lakini mpaka sasa wanafanya kazi kwa kujitolea bila malipo. Efficiency ya mtu anayefanya kazi kwa kujitolea haiwezi kuwa sawa na yule aliyeajiriwa kwani huyu wa kujitolea itabidi muda mwingine autumie kufanya kazi ya kipato ili aweze kujikimu. Bila shaka wanaposema wataajiri, ni kuwawezesha makatibu hawa kufanya kazi full time hivyo kuongeza ufanisi. Kama kulikuwa na tatizo CDM, bila shaka ni matokeo ya ruzuku kiduchu ya 60m waliyokuwa wanapata hadi mwishoni mwa 2010. Baada ya ruzuku kuongezeka, matunda yanaanza kuonekana. Wapeni muda, 2015 mtashangaa.
 
Viva cdm ile mikakati niliyokuwa naiwaza ndio imeanza. Watakao ajiriwa wawe wanacdm damu damu. Ofisi wanachama wachangie kwa nguvu zote. Ramani iwe moja nchi nzima ili wanachama wazitambue ofisi hizo kirahisi ila ukubwa waweza kuwa tofauti kutokana na mahitaji.
 
Cdm ikiimarisha ofsi za tawi mpaka mkoa nch nzima magamba hawato kua nakitu 2014 selikali za mitaa huku magamba hawana ujanja na tunawasubir kwa ham tuwaonyeshe.cdm imalishen chama mnakubalika tz nzima
 
- Lets say wewe na Chadema mnajitambua then howcome mmeshindwa tena kwa kipigo cha mbwa mwizi kwenye uchaguzi wa Udiwani, viti 22 kwa viti 5 tu aibu kwa chama cha ukombozi!! ha! ha! ha!, haya sasa subirini maandamano nashangaa sana vipi safari hii hamkuibiwa kura kwenye kuhesabu kura si unaujua ule muziki wenu!

Le Mutuz!!
Eti na hili lila burger linataka lishindane na watoto wa Mwinyi !!!! ha! ha! ha! watoto wa mwinyi walisoma na waliitumia nafasi vizuri siyo wewe kazi ilikuwa ni kujirusha kwenye club na kuishia kupata videgree vya kuunga unga ya kwenye vyuo vya buguruni ya huko USA
 
- Yaaani huyu Mzee huwa ananishangaza sana, yaani Chama hakina wanachama kabisa Zanzibar wala Songea, lakini yeye anakimbilia kufungua matawi Ughaibuni na sasa eti atawaajiri Makatibu kila Mkoa, yaani hawa Chadema na huyu Mzeee hawana jipya lao, kila siku kuiga toka CCM, sasa nimeamini kwamba kinyago ulichokichonga mwenyewe hakiwezi kukutisha!!

Le Mutuz!!

Too low for malecela's sijui hii familia mmekumbwa na maswahiba gani.nadhani ccm imegundua madhaifu yenu na umeamua kuwatosa.

By the way pole kwa msiba wa ndugu yako uliotokea hivi karibuni.
 
Nilikuwa nafikiri tayari Chadema wana makatibu wa wilaya na mikoa, kumbe muda wote huo na maandamano kila siku kumbe hata katibu wa wilaya hakuna?. Sasa kadi za chama zinauzwaje huko wilayani na mikoani kama hata ofisi hakuna?. Kuna ofisi za Chadema UK na NY, kumbe hakuna ofisi za chadema Chalinze?, lazima kuna tatizo ndani ya Chadema.
Makatibu wapo ila ni kazi ya kujitolea mpaka sasa. Mpango mpya ni kutoa ajira ya kudumu ili kuwa na Makatibu wafanyao kazi fulltime
 
Dr ni mtu mwenye mipango na mikakati dhabiti. Kuajiri makatibu wa wilaya na mikoa kwanza ni kuongeza ajira kwa watanzania hasa wanachama wa chadema lakini la pili ni kujenga heshima na kukubalika zaidi kwa watanzania kwani kunapokuwepo na ofisi rasmi na watendaji wa chama inawafanya wananchi wajisikie kuwa chama kipo katika jamii yao
Not only that. Hata wangeajiriwa kwa mshahara wa kima cha chini kisichokatwa PAYE, bado serikali ingekusanya kodi ya Skills Dev Levy 6% mishahara ya makatibu wote nchini.And the circle continues, watakuwa na uwezo wa kununua kitanda, hivyo kumpa ajira seremala. Watahitaji kitumbua asubuhi, hivyo kumpa ajira mpika nitumbua nk. Nina hakika waziri Mgimwa akipata taarifa hizi atamsaidia Dr Slaa namna ya kufanikisha zoezi hili haraka.
 
- Yaaani huyu Mzee huwa ananishangaza sana, yaani Chama hakina wanachama kabisa Zanzibar wala Songea, lakini yeye anakimbilia kufungua matawi Ughaibuni na sasa eti atawaajiri Makatibu kila Mkoa, yaani hawa Chadema na huyu Mzeee hawana jipya lao, kila siku kuiga toka CCM, sasa nimeamini kwamba kinyago ulichokichonga mwenyewe hakiwezi kukutisha!!

Le Mutuz!!

Mzee ni Baba yako!!!!!! kwenda zako uko na liccm lako lakizee. Ngoja 2015 tutawaonyesha kazi. Peoplezzzzzzzzzzzzzzz!!!!!!!
 
- Yaaani huyu Mzee huwa ananishangaza sana, yaani Chama hakina wanachama kabisa Zanzibar wala Songea, lakini yeye anakimbilia kufungua matawi Ughaibuni na sasa eti atawaajiri Makatibu kila Mkoa, yaani hawa Chadema na huyu Mzeee hawana jipya lao, kila siku kuiga toka CCM, sasa nimeamini kwamba kinyago ulichokichonga mwenyewe hakiwezi kukutisha!!

Le Mutuz!!

wewe nawe mbona ni mzee pia au unajidanganya kuwa ww ni kijana?
 
Too low for malecela's sijui hii familia mmekumbwa na maswahiba gani.nadhani ccm imegundua madhaifu yenu na umeamua kuwatosa.

By the way pole kwa msiba wa ndugu yako uliotokea hivi karibuni.
Mkuu najua sio vizuri kuingilia nasaba za koo za watu ila kwa vile huyu katuchosha na anamwaibisha JSM hebu tujiulize;
Akina Mwale ukiwaangalia wana akili na hekima za kufanana na mzee wao kulikoni huyu bonge?
Au ndiyo yale ya wahenga kuwa kitanda hakizai haramu? Maana wakati mwingine wazee wetu wanakuwa busy sana na safari nyingi kisha mashamba boys wakati mwingine wanapata bahati ya mwaliko wa kutandika kitanda. He he he! Utakuwa umenielewa mkuu
 
Too low for malecela's sijui hii familia mmekumbwa na maswahiba gani.nadhani ccm imegundua madhaifu yenu na umeamua kuwatosa.

By the way pole kwa msiba wa ndugu yako uliotokea hivi karibuni.

Yaani mtu akikuambia huyu mtu amezaliwa tumbo moja na yule Dr Mwele huwezi kuamini.Dr Mwele ni jembe na ana hekima ya hali ya juu lakini huyu kaka yake nina shaka huenda anakunywa gongo.
 
Back
Top Bottom