Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.

Unaeleweka lakini tatizo sio Kusimamia by laws tatizo ni kitendo cha Polisi kujeuza VIJIWE Vya Pombe Za kienyeji ni miradi ya kuchuma ..Hilo likemewe Kwani wauza wengi hata watu walioojiwa wamesema Imekuwa kawaida Sasa kwa Polisi kupita na kupanya pesa Za kinamama na Mara nyingine hadi walevi wanaokutwa

Kama wangekuwa wanapita wanafunga Vilabu na hawachukui CHOCHOTE kungekuwako na kuheshimiana ...lakini ukizoea kuchukua pesa Siku ukikuta hawana Ndio Hiyo mnakimbizana
 
Huyu TuntemekeSanga kila uzi anaoweka hapa jamvini UNANIBOA sijui kwanini napata hali hii.
 
Last edited by a moderator:
Haukuwa wakati muafaka wa kifanya hivyo. By the way,dhana inafahamika kwamba kulikuwa na wauzaji & wanywaji wa pombe wakati ambao ulikuwa sio mujjarab.

Wakati muafaka wa kunywa ni upi? Hasa kwa mtu ambaye kazini anaingia usiku,lets say saa nane hadi saa sita usiku? Mtu huyu.muda wake wa kunywa ni upi?
 
Ccm inahusikaje hapo!!!! We ---- sana wewe!!!endelea ns mjadala uliyopo na si kuhusisha vyama vya siasa!!mbwa we!!!
we #Mtoto Wa Longido ndio maana mzee ruksa aliwauza uarabuni.Nimesema chuki za watu zinajengeka hatuahatua kwa hatua.Upendeleo wa polisi kwa chama tawala ni chanzo kimojawapo cha chuki.Kama polisi wanapiga watu wasio wana ccm ovyo,kuwajeruhi nk watasikilizwa na ndugu au jamaa wa waathirika?
Polisi wanapaswa kuacha upendeleo wa kisiasa.Nchi hii sio yao au ya ccm peke yao.
Wafanye haki kwa watu wote nao wataheshimiwa na kusikilizwa.
Mambo mengine yanahitaji diplomasia tu,sio kutumia nguvu.
Hivi wewe Mtoto Wa Longido unafikiri watu wa Iringa wamesahau polisi haohao walivyomuua Mwangosi? Au mnafikiri mkiua halafu watu wakanyamaza ndio yameisha?
 
Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.
ulikuwepo eneo la tukio?
 
TuntemekeSanga inawezekana unalosema lina mantinki. Na naona kuna maan fulani. Sida ni uhusiano kati ya raia na jeshi umeharibika vibaya sana. Polisi wame amuka kuwa c****m za watawala, bila kujali kuwa wana wajibu wa kulinda raia na mali zao. Raia wamebaki wapweke bila chombo kwa ajili yao. Uhusuiano umeharibika na hawataki kuurudisha, maana polisi inategemea raia kupata intel kuzuia uhalifu.

Tunayoyaona ni matokeo ya jeshi hili kuamua kutumikia mabwanyenye, watu wameamua kuishi kivyao; na sasa tunayaona madogo, yataendelea kukua tu, maana vijana wenye nguvu wasio kuwa na ajira wamejaa tele mitaani na vijijini kwetu.

Ni wakati wa kurudi kwenye meza na kuchora mipango mikakataki kurudisha hali njema kati ya jeshi hili na wananchi... otherwise, zitaendelea kuwa nyimbo tu za ngonjera. Wao si walisema "wapigwe tu..." sasa tutashuhudia wanapigwa wao...
 
Last edited by a moderator:
Daaaah!!! kumbe mama aliyeuwawa alikuwa ni muuza chakula na sio muuza pombe???? Kwani sheria pia imekataza kuuza chakula mchana mpaka wamchote mtama mama wa watu???!! Pooor Tanzania walichofanya wananchi mi naona sawasawa tuu.
 
Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.

Mimi nina tatizo na by-laws zinazotungwa ambazo kwa upande wangu naona zinaingilia uhuru wa mwananchi. Mie nikinywa pomba asubuhi, kuna tatizo gani? Unajuaje kuwa usiku naenda kuvua samaki? Waache watu waishi wanavyopenda, wanajua watapata kipato wapi cha kufanya waishi as long as hawajiingizi katika vitendo viovu! Kwa nini sehemu moja ya nchi iwe si halali kufanya kitu fulani na sehemu ingine iwe halali? Unywaji holela maana yake nini?
 
Haukuwa wakati muafaka wa kifanya hivyo. By the way,dhana inafahamika kwamba kulikuwa na wauzaji & wanywaji wa pombe wakati ambao ulikuwa sio mujjarab.

Mbona polisi hawatufati sie huku bar asubuhi tunapata supu na bia kadhaa
 
Angekuwa ni mama yako au mkeo amekufa sijui ungekuja na comment gani hapa? Shame to you. Anyway, what goes around comes around. Its matter of time. Hata Ghadafi alikuwa hivyo hivyo
 
Angekuwa ni mama yako au mkeo amekufa sijui ungekuja na comment gani hapa? Shame to you. Anyway, what goes around comes around. Its matter of time. Hata Ghadafi alikuwa hivyo hivyo

Unajua kuna watu utafikiri wanaishi Mars wamesahau kuwa hawa MAWAZIRI na watu wakubwa wengi tu Leo ..mama Zao waliuza Pombe Za kienyeji ili wao wasome ...hakuna watu wa kuheshimu Kama wamama wauza Pombe au mam ntilie
 
Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.
ulikuwepo eneo la tukio?

Wewe kama ulikuwepo rush a video hapa, msiongee lugha laini kwenye jambo gumu mkuu. Umetumwa?
 
Kamua nan mama kama c polisi ,polisi kazi yao ckuhukumu ila kufikisha watuhumiwa kwenye vyombo vya sheria
 
unabikumbusha shoga mmoja anaitwa dibibi... Ukimuona kama mtu kumbe anafirwa hovyohovyo....

Mkuu nilikuwa natafuta cha kumuambia huyo Jamaa ila kwa hili ulilompa ngoja nikae kimya Ili ukipigwa Naweza kukupa I'd yangu na password ukavitumia kwa muda......Jamaa amechangia upuuzi sijapata kuona tangu nianze kuingia JF.
 
Nina uhakika 100% huyo aliyefariki angekuwa mama yako aliyeuza hizo pombe ili uishi, usome na ule usingekuwa na kiherehere cha kuandika hayo yote. Naomba mungu nawe yakukute siku moja.

Kama ntakiuka utaratibu na sheria,lazima yatanikuta. You know, watu mko na ushabiki sana usiokuwa na maana.

Hope nimezingatia vigezo vyote vya misingi na utaratibu ktk post yangu hii. Hainamaana kuendelea kuangaliwa tu ilhali taratibu zinavunjwa.

Sometimes,sheria inapaswa kuchkua mkondo wake. That's why vyombo vya dola vipo. Ukikiuka unafuatiliwa.
 
Waliochoka kuona polisi wote ni criminals

Mkuu Ghosryder , nashukuru kwa mchango wako mahsusi. Kukosoa tukosoe. Lakini pia tukubali kukosolewa kama wananchi pale tunapokiuka utaratibu.

Watu wanachangia kwa ushabiki wa ovyo tu. They have been Fooling themselves wakidhani kuna Serikali itakayokuja ifumbie macho Ukiukwaji washeria na Taratibu za nchi.

Watu hawajiongezi. Wamekalia ujima,ushabiki,ukereketwa na Siasa majitaka tu.

Thanks a Millions!
 
Last edited by a moderator:
Mimi naona kila amaeandila hajui uchungu wa kuondokewa na mpendwa wako ktk mazingira yale,hebu chukulia mkeo,mama yako,mtoto wako yupo kijijini baada ya kutafuta kazi kwa miaka mingi akakosa,katafuta mtaji wa biashara kakosa alafu akaambiwa biashara ya mtaji mdogo ni pombe ambayo inaweza kukuletea chakula,kusomesha watoto,kulipa pango alafu mpendwa hiyo anakufa kwa staili yoyote ile inayosababishwa na polisi ktk kudhibiti asifanye biashara ile,unazani utafanyaje?wanaotetea ujinga wa kuua nazani na wao siku moja wapenwa wao wauliwe tuone

Mkuu, hakuna asiyejua uchungu huo. Hata Mama wa Jambazi(mfano) hulia pale mwanae anapouawa kwa tukio la uhalifu.

Wakati fulani, haiwezekani mtu kukiuka utaratibu halafu akaachwa hivihivi. Dhana ya Mamlaka na Utawala bora itakuwa imekufa asilani.

Tuwe tayari kuupokea ukweli. Bahati nzuri mama-muza hakuuawa kwa kipigo wala kuteswa.
 
Tuntemeke Sanga alikua hero wetu, he challenged the status quo and he had right questions to the situation

Wewe na yule shogamboga Mtela, mnalitumia vibaya hili jina??

Kwa wahehe, wabena na wakinga, Mzee Tuntemeke was beyond normal person

Mnakosea sana, na mnatuumiza sana

Pole sana dogo!
 
Back
Top Bottom