Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

Kwa nini hawaendi kukamata wamiliki wa mabaa sehemu mbalimbali nchini wanaofungua mabaa muda wa kazi badala yake wanakimbilia vilabuni tu?
 
wanashindwa kupambana na boko halamu na majambazi walio na mafunzo kama wao ili wapime ubavu wao, eti wanapambana na wananchi tena akina mama na watoto.
 
Mtoa mada sijui kama umezaliwa kijjini na unaelewa vizuri shughuli za watu wanaoishi huko,kwa wanaojua, huko kwetu Iringa wanavijiji huwa wanaamka mapema sana saa kumi asubuhi wanakwenda mashambani, wanafanya hivyo ili wawahi kabla jua halijawa kali, kwa hiyo saa nne au tano wengi wamesharudi wanaendesha shughuli nyingine za kujipatia fedha, kumbuka wanapokuwa shambani hawazalishi pesa kule, ili wapate pesa za kukidhi mahitaji yao mengine ni lazima wapange muda wao wa kazi, muda gani waende mashambani na ni muda gani wafungue maduka na biashara nyingine, huo utaratibu hata viongozi wa vijiji wanaujua na hata wao ndivyo wanavyoishi!!, sasa polisi kwa nini wasiwasiliane na uongozi wa kijiji? hii nchi sheria nyingi tu haziendani na hali halisi ya maisha yetu (non applicable) na ndiyo maana tunahitaji changes ili tuwe na taratibu zitakazoendana na mazingira yetu, ebu fikiri kidogo tu, mama mwenye watoto hana mume, akienda shambani saa mbili asubuhi kama ndiyo muda kisheria wa kuanza kazi atoke saa kumi, hana mshahara, hajui shilingi moja, anahitaji ada na michango ya watoto shule, anahitaji sabuni, sukari, chumvi mafuta ya kula nk, atapata muda gani wa kutafuta hizo pesa kwa ajiliya mahitaji hayo? je asubiri hadi avune mwezi wa saba? au atumia akiba ya mahindi ya mwaka jana kidogo atengeneze pombe auze ili apate mtaji wa elfu nane aweze kuanza kununua debe moja kila siku ili akitoka shambani auze apate elfu tatu imsukume nabakishe ile capital kwa ajili ya kesho? Kama si kuwahi shambani usiku atajipangaje kwa shughuli hizo nyingine? Mtoa mada fikiria kwa umakini, sheria ziko mijini tu na baadhi vijijini but otherwise watu wanaishi kwa taratibu zao, hakuna mjomba kijijini.
 
Nafikiri kuna haja ya kubadili mafunzo ya polisi pale CCP, Polisi wa Tanzania wao hufundishwa kupiga na sio kulinda raia na ndio maana kila ikitokea sintofahamu wao hufuka na kurusha mabomu ya machozi virungu na wakati mwingine risasi za moto hutumika. Hebu tujiulize hizo nchi ulizotaja umeshawahi sikia polisi wao wakipiga hovyo raia? Umeitaja nchi ya Russia, Unajua kuwa katika wazungu wanywaji wa pombe kali wao ndio namba moja? Hebu tuangalie nchi ambazo ni mifano kwetu Kama Nchi za ulaya na Marekani, Ghasi ahutoke mara kwa mara na tunaona wanavyodhibiti hizo ghasia bila virungu wala mabomu ya machozi.

Kwa mtazamo wangu, Polisi wa Tanzania wao hawafundishwi kulinda raia, bali mafunzo yao ni kupambana na yeyote atakayeipinga serikali na ndio maana kuna neo jeshi, kwa kawaida katika nchi zote zilizostaarabika hawana jeshi la polisi bali wana idara za polisi ambazo ni za kiraia zaidi na hupata mafunzo ya kulinda usalama wa kila raia wao.
 
Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.

kwani kusimamia sheria ndo umpige raia na kusababisha mpaka vifo.Tatizo la polisi wetu ni form four failure kwahiyo wanaona kama bahati kwa kazi walionayo.
 
Sheria ni msumeno hukata kila upande. Kama polisi wangekuwa na weledi basi washughulikie kila crime badala ya kujikita kwa soft targets kama waandamanaji, wanywa pombe, wanafunzi, vyama vya upinzani, watoto wa chekechea nk. Mbona escrow, EPA, MEREMETA, DEEP GREEN, wezi wa makaratasini, wahujumu uchumi, wezi migodini, twiga wanaopanda ndege, meno ya ndovu, nk. hawagusi?Polisi wameonyesha udhaifu mkubwa, upungufu wa weledi, wala rushwa wakubwa, waonevu, kwa kifupi wamepungukiwa na ubinadamu. Wanafanya kazi kama robot, hawana uwezo wa kuchambua ni cha kufanya na kifanywe vipi, wakubwa wao halikadhalika ni vilaza pia. Ni lazima tutaendelea kuwalaumu mpaka watakapojifunza kufanya kazi kwa weledi. Mifano ya China usiyuletee hapa kwa sababu wale wameweka viwango. Umetumwa Tanzania kujenga uwanja wa taifa kwa kiwango fulani, usipotekeleza kama ulivyoagizwa kichwa chako ni halali yao bila kujali cheo chako. Rais akihusishwa kwenye ufisadi wanakukata kichwa nk. Hayo hayawezekani Tz. Chenge fisadi mkubwa anatanua barabarani na anapewa kazi ya kutunga katiba. Only in Tanzania uwezi kuona sehemu nyingine. Hata Rwanda kanchi kadogo tu kametushinda. Halafu unatoa mishipa hapa kutetea utendaji wa pilisi we vipi?
 
achana na huyo... ni fal@ fulani alishakua hapa akapaparikia u-system, wakamfiz, akajaribu kupiga mikwara akina MMM, naona sasa kaishia kuwa shoga mboga tu, na frustrations kibao
Hivi ni nani halisi huyu jinga? ukiacha hayo ya mmm analiharibu pia jina la tumutemeke sanga
 
M najuaga hzo ni kazi za Askar Mgambo wakishimdwa ndo wanaomba msaaada siyo from nowhere una agiza polis wanakuja na SMG jaman umeambiwa SOMALI hapaa
 
Kuwa na uchungu wa maisha ya binadamu wenzako kama ambavyo nawe ungependa kuishi
Swala la kuuza gongo haliondoi dhamani ya ubinaadamu wake kabisa
Kama tatizo ni kuuza gongo basi ungefuatwa utaratibu wa adhabu zilizoko kisheria
Na mimi nadhani tufike mahala tuheshimiane kama binadamu hata kama nafanya kazi isiyokupendeza, ila kumbuka hali ngumu ya maisha ndo imemfanya mama huyu kujitafutia riziki kwa njia hiyo ndugu.
Natumaini utanielewa vizuri tu.

Nimekuelewa, lakini na muuza gongo anasababisha vifo kwa watu kuungua maini.
 
Bahati mbaya hiyo sheria watu hawaiweki hapa tuisome.Lakini mimi niliwahi kufanya biashara ya baa.
Sheria inasema sehemu za vivywaji kunaruhusiwa kufunguliwa asubuhi hadi saa nane. Halafu SAA kumi na mbili jioni kunafunguliwa tena hadi SAA tano usiku kwa siku za kazi.
Siku za wikendi kufunga ni SAA sita usiku.
Tukio limetokea kati ya SAA tano na sita mchana.Kwa hiyo,hawa wauza pombe wameonewa.
 
Wewe ndo ndondocha, hujui wanasiasa unao wazungumzia ndo huwa wanawatuma polisi kuua wananchi wanao andamana na mikutano ya vyama pinzani? Mkumbukeni Daudi Mwandosi polisi walivyo Muua, mbona hamkuja humu jamvini kulaani mauaji ya Mwandishi yule mahiri wa habari? Acheni unafiki, mbona yanapotokea mauaji hamzungumzii watu wanao poteza uhai? Sins Imani wala A mani na Polisi. Natamani ningekuwepo Nipate kesi

We ulishawahi kuja humu jamvini kulaani dhidi ya walioua polisi Ushirombo na Ikwiriri?
 
Mtoa post ni moja ya wasaliti wazuri sana,,,,hii anapost toka lumumba project!!
 
Ooh my God Poor you!!Policcm hawajaanza kufanya Mauaji leo!!
Amri inapotoka mamlaka ya Juu wao ni kama vibaraka(misukule) na wanafanya utekelezaji wa kile wanachoambiwa!!
polisi wanatesa ,,wanapiga raia wasio na hatia!!
Na mbaya zaidi kuongozi mkubwa serikalini alisema raia WAPIGWEE TU!!!
Kwa sasa hivi Kuna chuki imeshajengeka kati ya wananchi Vs Policcm
Wao hutumwaa tu kufanya mauaji ya Raia!!
Walipiga risasi raia kule Arusha kwenye maandamani ya Chadema !!wamempiga bom daud mwangosi R.I.P,,,juzi wamepiga na kuvunja miguu wanafunzi wa Udom walikua wakifanya madai ya msingi,,Juzi wamempiga Lipumba na wafuasi wake wa CUF hata UDSM chuo kikuu mlimani walkuja saana kutupiga wanafunzi pale binafsi nawachukiaa polisi kama nn sijui!!yaani I HATE polisi wa Tanzania
Wacha kuwateteeaa ww kwa mambo yao ya Kipumbafu uyo mama aliekufa Iringa kama ana wanae wanamtegemea ??na ndio alkua kwenye Uzalishaji wa mali !!!watoto wake ww ndo utawasomesha???
Hao wezi wa mabilioni kina Chenge na kina Tibaijuka hujawaona?? Wao si wahalifu??mbona polisi hawakutumwa kuenda kuwakamata??
Yaani watu wanafisadi nchi lakini mpka dakika hii naandika hii comment wapo huru na mihela waliochota!!Alafu leo hii mama wa watu anajitaftiaa Riziki unaenda kumpiga anakufa??
Hivi inakuingia akilini ww mtoa post???
Yaani Tanzania kuna watu wapuuuzi kama ww wanaotuchelewesha mapinduzi yaani Fujooo zoote na Mauaji leo bado unaitetea polisi????
Unataka kupewa wilaya ww sio bure!!!!
Elimu yako isiishie kwenye kukariri vifungu vya sheria ila iwe ya 1 kukubadilisha fikra zako na kufanya upembuzi wa mambo kiundani!!!
Amka toka usingizini ww!!!!
 
huna akili timamu nyau we, kuna siku uliambiwa utekelezaji wa sheria lazima ushirikishe wanasiasa ili polisi wawajibike ktk majukumu yao? hao hao wenyeviti wa vijiji ndo wapika gongo wakuu, fikiri vizuri.

Kama kuna mjinga au mtu aliyechangia ujinga katika uzi huu ni wewe!

Bila shaka ujinga wako umechangiwa na elimu uliyoikimbia shuleni!
 
Haukuwa wakati muafaka wa kifanya hivyo. By the way,dhana inafahamika kwamba kulikuwa na wauzaji & wanywaji wa pombe wakati ambao ulikuwa sio mujjarab.

kwa nini polis wawaandame wauza vilabu vya pombe za kienyeji tu wakati wenye bar wanauza masaa 24? Au bar hawazioni? Hakika polisi wasipotenda haki watafanya kaz ktk mazingira magumu sana. Na kila mtu ataachukia.
 
Back
Top Bottom