Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

Kasumba ya kuwa "dawa ya moto ni moto" inapotosha. Wakati mwingine dawa ya moto ni baridi. Aliyetudanganya kuwa kila inapotokea wananchi wamechachama kwa sababu yeyote tutumie nguvu za ziada hususani mabamu ya machozi, risasi au kuwakamata.. huyu alitupotosha. Uzoefu labda kama lengo ni kujenga hofu ndani ya wananchi, lakini nafikiri tulipofikia, ni vema kutumia busara, psychology na hekima katika kutatua na kudhibiti hali kama hii kila inmapojitokeza. Na tukumbuke kuwa dawa ya moto si kila wakati iwe ni moto.

Mbona wananchi wamekiuka miiko na kuondokana na maadili ya mababu zetu? Polisi au vazi la polisi lilikuwa na heshima yake enzi zetu. Vazi la polisi lilibeba miiko kwa wananchi: palipo na ishara ya polisi ilimaanisha AMANI, UTULIVU, KIMBILIO, HAKUNA GHASIA... hata kama kungelikuwepo na vurugu, kitendo cha kuona mtu aliyevalia kama polisi,... wangelikimbilia huko... iweje siku hizi, wananchi wamechoka kuona "polisi"

Mkuu; Dunia ya leo si ya kale! We people have changed. We have grown a sortie of aggression.

Ushauri wako ni bora na umetoa mchango ulioutukuka ktk mada hii. Bravo!

Hope Polisi na wakubwa wao wangezingatia dhana hiyo. Si kila purukushani hutulizwa na Purukushani. Wanapaswa kuongeza weledi na maarifa zaid.

Pia, ni vyema nasie wananchi kujitahidi kuwa na simile. Kuna matukio au visa tunavifanya sometimes kwa namna ambayo haipendezi. Tujitahidi kuheshimu Mamlaka na kuwa watulivu ktk nyakati fulanifulani za matukio na visa. Sio kuwa aggressive na ushabiki usio na msingi.
 
Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.

Nina uhakika 100% huyo aliyefariki angekuwa mama yako aliyeuza hizo pombe ili uishi, usome na ule usingekuwa na kiherehere cha kuandika hayo yote. Naomba mungu nawe yakukute siku moja.
 
Police wanakamata wahalifu karibia kilasiku mitaani yes!! wanafanya kaziyao. Mimi nadhani niwakati wanapo fanya kazi kinyume na mafunzo yao kwa bahati mbaya,kwa uelewa mdogo, ama kwakutaka sifa za kijingahivi, hapondio panakuwa na tatizo, inaonekana baadhi ya polisi hawatumii kabisa mbinu za kiufundi kudhibiti au kukamata wahalifu kwa kuzingatia aina ya kosa lililo tendwa na aina ya nguvu zinazo hitajija kwa mtuhumiwa wa kosa la aina flani. Hatakama huyo mama R.I.P. alijikwaa,huenda nikutokana na hofu ambayo wao police waliisababisha. Police wanatakiwa kufanya kaziyao kwa ujuzi zaidi kuliko kutumia manguvunguvu na vitisho ambavyo husababisha madhara makubwa ambayo hufanya wananchi kuwachukia.
Mimi nadhani.
Waache kuajiri kindugu, kijamaa, waajiri watu ambao ni qualified kwenye hizo position otherwise lawama hazitaisha na mwisho utakuwa mbaya.
 
Nasikitika sana kusikia kule Ilula wananchi waliwaandamisha POLISI halafu wasiue hata mmoja! Eti wanaishia kuvunja vioo vya magari tu? Wananchi hawa she.nzy type kabisa kwa kushindwa kuitumia vizuri hii fursa adimu kama hiyo!! Haiwezekani na haikubaliki kuwapa kibano mpaka wanaishiwa risasi halafu mnawaacha wazima!! Hili lilipaswa liwe fundisho na ndo ungekuwa mwisho Wa uonevu!!
 
Kwa nini hawakushirikisha serikali ya mtaa/kijiji katika operation yao kwa sababu hata viongozi wa Ilula hawakuwa na taarifa!

huna akili timamu nyau we, kuna siku uliambiwa utekelezaji wa sheria lazima ushirikishe wanasiasa ili polisi wawajibike ktk majukumu yao? hao hao wenyeviti wa vijiji ndo wapika gongo wakuu, fikiri vizuri.
 
Kasumba ya kuwa "dawa ya moto ni moto" inapotosha. Wakati mwingine dawa ya moto ni baridi. Aliyetudanganya kuwa kila inapotokea wananchi wamechachama kwa sababu yeyote tutumie nguvu za ziada hususani mabamu ya machozi, risasi au kuwakamata.. huyu alitupotosha. Uzoefu labda kama lengo ni kujenga hofu ndani ya wananchi, lakini nafikiri tulipofikia, ni vema kutumia busara, psychology na hekima katika kutatua na kudhibiti hali kama hii kila inmapojitokeza. Na tukumbuke kuwa dawa ya moto si kila wakati iwe ni moto.

Mbona wananchi wamekiuka miiko na kuondokana na maadili ya mababu zetu? Polisi au vazi la polisi lilikuwa na heshima yake enzi zetu. Vazi la polisi lilibeba miiko kwa wananchi: palipo na ishara ya polisi ilimaanisha AMANI, UTULIVU, KIMBILIO, HAKUNA GHASIA... hata kama kungelikuwepo na vurugu, kitendo cha kuona mtu aliyevalia kama polisi,... wangelikimbilia huko... iweje siku hizi, wananchi wamechoka kuona "polisi"

Waliochoka kuona polisi wote ni criminals
 
Mimi naona kila amaeandila hajui uchungu wa kuondokewa na mpendwa wako ktk mazingira yale,hebu chukulia mkeo,mama yako,mtoto wako yupo kijijini baada ya kutafuta kazi kwa miaka mingi akakosa,katafuta mtaji wa biashara kakosa alafu akaambiwa biashara ya mtaji mdogo ni pombe ambayo inaweza kukuletea chakula,kusomesha watoto,kulipa pango alafu mpendwa hiyo anakufa kwa staili yoyote ile inayosababishwa na polisi ktk kudhibiti asifanye biashara ile,unazani utafanyaje?wanaotetea ujinga wa kuua nazani na wao siku moja wapenwa wao wauliwe tuone
 
Uchungu wa kuondokewa na muuza gongo! cut the ----...!
 
TUNTEMEKE SANGA NI KUWADI WA WATESAJI.Hv Unaweza Kueleza Kwanini Bar Za Hapo Ilula Zilikuwa Zinauza Bia Muda Huo Wa Asubuh Tena Ikiwemo Kanti Ya Polisi? Kwanini Hawakuanzia Kwenye Kantii Yao Na Kwenye Mabaa? Na Kwanini Walipofika Kwenye Kilabu Hicho Wakawatembezea Kipigo Kwa Kila Aliyekuwepo?
 
Kuwa na uchungu wa maisha ya binadamu wenzako kama ambavyo nawe ungependa kuishi
Swala la kuuza gongo haliondoi dhamani ya ubinaadamu wake kabisa
Kama tatizo ni kuuza gongo basi ungefuatwa utaratibu wa adhabu zilizoko kisheria
Na mimi nadhani tufike mahala tuheshimiane kama binadamu hata kama nafanya kazi isiyokupendeza, ila kumbuka hali ngumu ya maisha ndo imemfanya mama huyu kujitafutia riziki kwa njia hiyo ndugu.
Natumaini utanielewa vizuri tu.

Unapiga mayowe tuu, kwani nani kampiga na kumuua huyo muuza gongo? mtaje na uthibitishe.
 
Hivi Tuntemeke Sanga Unaakili Sawa Sawa? Haya Huyo Waliemuua Kwanza Yeye Si Muuza Pombe, Bali Ni Mama Lishe. Pili, Huyo Amekufa Baada Ya Kuchotwa Mtama Na Askari.Hvy Kisheria Mtuhumiwa Wa Mauaji Ni Askari Aliyemchota Mtama.Sasa Unatetea Nini? Hivi Angekuwa Ni Raia Kamchota Mtama Askari Akafa Ungesema Amekufa Kwa Mapenzi Ya Mungu? Ficha Upumbavu Wako Hapa. Kumbe Wewe Ni Kuwadi Uliyetumwa Kusafisha Waovu!
 
Tatizo kubwa ni polisi kujiingiza kwenye siasa kwa kuegemea upande wa ccm.
Hivyo watu kuwachukia polisi kama wanavyoichukia ccm ni sawasawa kabisa.
 
Jina hili linatendewa hakhi na mtumiaji huyu. By the way,you never know kama ndo jina langu halisi au la!

Tuntemeke Sanga alikua hero wetu, he challenged the status quo and he had right questions to the situation

Wewe na yule shogamboga Mtela, mnalitumia vibaya hili jina??

Kwa wahehe, wabena na wakinga, Mzee Tuntemeke was beyond normal person

Mnakosea sana, na mnatuumiza sana
 
Huyo Mama Hakuwa Muuza Pombe, Bali Alikuwa Muuza Chakula. WAUAJI NI WEWE MWENYEWE UKISHIRIKIANA NA HAO MABWANA ZAKO BAADA YA KUMCHOTA MTAMA HUYO MAMA NA AKAFARIKI PALEPALE.

achana na huyo... ni fal@ fulani alishakua hapa akapaparikia u-system, wakamfiz, akajaribu kupiga mikwara akina MMM, naona sasa kaishia kuwa shoga mboga tu, na frustrations kibao
 
Usijipendekeze,sio kazi ya polisi kusaka wanywa pombe wakati wa kazi.MBONA zipo bar zingine zinakuwa wazi polisi hawaendi huko.
 
Back
Top Bottom