Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.
Itanichukua miaka yote ya uhai wangu kuamini kuwa yule mama hakupigwa na polisi bali alianguka mwenyewe maana hata Mwangosi walisema amepigwa na kitu kisichojulikana???? Hakika inafika wakati natamani nchi yangu usalama wa Raia uwe chini ya sungusungu na si jeshi la polisi maana wanatekeleza Ilani ya Pinda na CCM
 
Naafiki hoja yako kias fulani. Kuna mauaji kadhaa yamefanywa na Polisi kwa bahati mbaya (on routine) au kwa makusudi.

Nalaani yote yanayotokea kwa makusudi na uzembe wa Polisi. Lakini,mengine ni sababu ya utaratibu wetu mbovu na kiburi chetu wananchi.

siyo kiburi bali hawaelewi sheria za nchi na mara nyingi huwa hazifuatwi na hata viongozi wa juu. Nchi ina sheria lakini hazifuatwi kwa ajili ya rushwa. Na hata hao police ukichunguza utavundua walikwenda kutafuta mapesa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Itanichukua miaka yote ya uhai wangu kuamini kuwa yule mama hakupigwa na polisi bali alianguka mwenyewe maana hata Mwangosi walisema amepigwa na kitu kisichojulikana???? Hakika inafika wakati natamani nchi yangu usalama wa Raia uwe chini ya sungusungu na si jeshi la polisi maana wanatekeleza Ilani ya Pinda na CCM

Unaish nchi gan wewe? Hivi unawafahamu Sungusungu?

Think Big!
 
Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.
ficha ujinga wako
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Haukuwa wakati muafaka wa kifanya hivyo. By the way,dhana inafahamika kwamba kulikuwa na wauzaji & wanywaji wa pombe wakati ambao ulikuwa sio mujjarab.

Samahani mkuu,mlishawapa semina hao watu kuhusu hizo sheria au sera na wakaenda kinyume? Je hiyo sheria inaapply kwa wao tu au ni kwa nchi nzima?

Na vipi mliwashirikisha viongozi wao wa mtaa,kijiji au hata kata?
 
Acha kuandika pumba bana kutaka kuhalalisha mauaji ya huyu mama asiye na hatia. Unadhani huyu mama angekuwa anakuhusu ungeandika hizi pumba zako!? Jitambue acha kushabikia unyanyasaji, uonevu na mauaji ya Watanzania wasio na hatia.

Haukuwa wakati muafaka wa kifanya hivyo. By the way,dhana inafahamika kwamba kulikuwa na wauzaji & wanywaji wa pombe wakati ambao ulikuwa sio mujjarab.
 
Nimejaribu kukusoma kuanzia post yako na majibu unayotoa unajichanganya tu.
Polisi wanaendelea kuua,iwe bahati mbaya iwe makusudi ila mwisho wa siku wapendwa wetu wanakufa,polisi ndio vinara wa rushwa na wananchi wamesema walichoka manyanyaso ya kuombwa rushwa ndo maana jana wakaamua MBWAI-MBWAI na ndo yaliyotokea.
Yote kwa yote mama wa watu amefariki,probably alikuwa akitegemewa,kuna maendeleo gani hapo tena kwa wategemezi walioachwa?
Unapata ujasiri wa kuandika unachoandika kwakua alopoteza maisha hakuhusu,humjui na hukuwa ukimtegemea ndo maana unabwabwaja tu,ila kumbuka Ilula watu leo wanaomboleza kuondokewa na mpendwa wao,imefika hatua Polisi nao wabadilishe mbinu zao,hii uaua yao sasa hivi imekithiri,hakuna cha kusema bahati mbaya au makusudi kuua ni kuua tu. Vaa viatu vya wafiwa ndo utoe vihoja vyako,ila kama una bundle za kutosha basi kadownload video au vitabu ujisomee.
mtu wa kulaani ungelaani tangu post yako ya mwanzo,ila mwanzo umesema "ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi". Sasa unalaani nini tena?

Ni imani yangu kwamba,post yangu imejitimilisha vyakutosha. Habari za kulaani,nimezitoa nikimjibu mwanaJukwaa fulani humu ndani.Tena kwa issue nyingine(sio hiyo ya Ilula).

Kifo chq huyo Mama nimekisikitikia coz ni uhai wa mtu umetoka na tayar kuna gape kaliacha ktk familia yake. But imetokea Bahati Mbaya. Si kwa kuteswa au namna yoyote ile.

Maelezo mengine uloyatoa,nadhani ni kiburi chako au kujitoa ufahamu kwani nimekwisha yatolea ufafanuzi hapo nyuma. Sasa sielewi unayashuku kwa lipi (ilhali umenambia kuwa umepitia michango yangu yote kuanzia Post).
 
Sasa unachokibishia kitu gan hapo? Kama upo close na media,umeshindwaje kuelewa nilichoeleza?

Chenge kashtakiwa na mamlaka ya Serikali. Kwa Upumbafu wake na kutapatapa, kaweka Pingamizi. Lakini InshaAllah nikwamba Tume ya Maadili imekwisha jiridhisha juu ya Tuhuma na Mashitaka ya Chenge ktk Escrow Saga.

Sioni unachokibishia au kukishabikia hapo. Asiposhughulikiwa vilivyo, ndipo uje unisute. Shakidinkili
 
Last edited by a moderator:
Acha kuandika pumba bana kutaka kuhalalisha mauaji ya huyu mama asiye na hatia. Unadhani huyu mama angekuwa anakuhusu ungeandika hizi pumba zako!? Jitambue acha kushabikia unyanyasaji, uonevu na mauaji ya Watanzania wasio na hatia.
BAK ;

Nimekwisha kujibu hoja hiyo ktk michango yangu zaid ya minne mitano hapo nyuma.
Nikuombe uirejee kwa ufafanuzi zaid.
 
Last edited by a moderator:
Kama uumakini unaoutambua wewe ni kukimbilia mahakamani na kuweka zuio ili wananchi wasihoji mambo ya msingi, huo ni ujinga na ujuha ulikithiri. Usijione wewe ndiye unayejua kila kitu na wengine ni mbulula, vyombo vya habari vipo kwetu sote pamoja na mitandao.
Khaa!! Sasa unataka apigwe mawe? Au siyo sisi tunaolilia utawala wa sheria kila siku?
 
Nakubaliana na mtoa hoja kwa maana ya umuhimu wa kutii sheria ikiwa ni pamoja na kutumia muda mwingi kufanya kazi badala ya kunywa pombe. Hata hivyo, kilichotokea Iringa ni mwendelezo wa mengi ya namna hiyo yanayotokea Tanzania. Uvunjifu wa sheria unaanzia juu kwa watunga sheria wenyewe, huu mfumo upo siku nyingi na kwa kuwa weledi wa watu siku za nyuma ulikuwa mdogo pamoja na kukosekana kwa media coverage ulikuwa hauwezi kuona sana au kupata taarifa au taarifa kuwafikia wananchi. Hivi sasa mambo mengi yamebadilika wa IT and mass media in the country watu wanaona namna hicho kinachoitwa sheria kinavyopinduliwa na watungaji na wasimamizi wa sheria zenyewe. Tatizo kubwa ni kuwa tumeshindwa kubadilika kulingana na mahitaji ya sasa. Hauwezi kutumia mabavu kila mahali na kunyatia katika kutekeleza sheria. Madhara ya kunyatia nini, upo uwezekano mkubwa mindset yako siyo kuhakikisha sheria iantekelezwa bali kukamata ili uweze kudai rushwa na matokeo yake ndiyo hayo kwa kuwa mlengwa naye anajua dhamira yako (mostly umefanya hivyo siyo mara moja) lazima pawepo na resistance. Tukubali kuwa makosa yapo pia katika mifumo yetu na mindset zetu halafu tuanza kujisahihisha.
 
Ni imani yangu kwamba,post yangu imejitimilisha vyakutosha. Habari za kulaani,nimezitoa nikimjibu mwanaJukwaa fulani humu ndani.Tena kwa issue nyingine(sio hiyo ya Ilula).

Kifo chq huyo Mama nimekisikitikia coz ni uhai wa mtu umetoka na tayar kuna gape kaliacha ktk familia yake. But imetokea Bahati Mbaya. Si kwa kuteswa au namna yoyote ile.

Maelezo mengine uloyatoa,nadhani ni kiburi chako au kujitoa ufahamu kwani nimekwisha yatolea ufafanuzi hapo nyuma. Sasa sielewi unayashuku kwa lipi (ilhali umenambia kuwa umepitia michango yangu yote kuanzia Post).

Endelea kudhania,ila nilichokieleza hapo hujakizingatia,polisi wanaua ndugu zetu na wanachekewa,usidhani post zako hapa zitabadil mtazamo hasi wa raia kwa polisi.Soma mwananchi la leo
 
Endelea kudhania,ila nilichokieleza hapo hujakizingatia,polisi wanaua ndugu zetu na wanachekewa,usidhani post zako hapa zitabadil mtazamo hasi wa raia kwa polisi.Soma mwananchi la leo[/COLOR][/FONT][/B][/SIZE]

Nia yangu sikulazimisha mtu kubadili mtizamo. Hayo ni maoni yangu. Kama mtu ataafikiana na mtazamo wangu, basi itakuwa vyema.

Lakini, wakati utafika. Ukweli huo utajidhihirisha.
 
Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.
Pita sehemu mbali mbali za miji ikwa ni pamoja na Iringa mjini utakuta baa ziko wazi na watu wanakunywa na kula muda wote. Lini ulisikia au kuona polisi wakienda kufanya msako au kufunga baa asubuhi au mchana? Hivi wanaokesha usiku wakiwa malindoni wao wanywe saa ngapi?! Hilo la vilabu nalo lilihitaji nguvu ya polisi? Pita kwenye baa mbali mbali hapa Dar asubuhi haalafu utwambie baa ipi haina watu. watu wanakunywa, wanakula michemsho, supi, kiti moto nk. Kwanini hao wa kilabuni ndio wapelekewe polisi?
 
we tuntemekesanga umamatatizo nahisi utakua unatetea baba zako ambao wako polis labuda nakuambie kitu polis wa leo sio wale unao wajuwa wewe hawa ni wacheza dili kunakituo kimoja cha polis sitakitaja jina ukikamatwa uzembe na udhululuji kesho yake watakuomba laki tatu kama hauna utapandishwa mahakamani mbaya zaidi huko mahakamani kesi unayosomewa sio uzembe na udhululuji utakutana na unyang'anyi wa kutumia silaha kuja ifahamike kesi si yako miaka sita au inaweza kukufunnga leo hii wewe unashawishi kuwa polis ni wema yawezekana ukawa unaongelea polis wa nchi nyingine ila si TANZANIA
 
Unaish nchi gan wewe? Hivi unawafahamu Sungusungu?

Think Big!
Yes nawafahamu! Nimewauliza wana Ilula kilichopo yule mama alipigwa mtama na polisi akaungukia kisogo ndio akafa hivo police aliua maana unaweza kuua kwa silaha au kwa njia nyingine kama kupga ngwara au kichwa n.k
 
Back
Top Bottom