hivi why mnatumia jina tuntemeke sanga vibaya?? he was a man of honor... why using his name kikuku-kuku?
....kwa nini huyo mama asianguke siku nyingine yoyote isipokuwa siku ya ambush iliyofanywa na polisi?
Tuntemeke mimi ni mtu muelewa sana na najua nini maana ya jukwaa kama hili,tukio la hayo maafa limetokea jana tu hata bado maiti haijazikwa wewe unaanza kuleta utetezi kama huu?unataka kutuambia kuwa jambo likifanywa na polisi sisi raia hatuna nafasi ya kulaani hilo tukio?
Mama wa watu Muuza Pombe au Makongoro ya Miguu KIFO chake unalinganisha na Jambazi ...hongera wewe familia bora !!!!
Wakuu; heshima mbele!
Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).
Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.
Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).
Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.
Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.
Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.
Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.
Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.
Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.
Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**
MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.
Nawasilisha.
Mkuu; Dunia ya leo si ya kale! We people have changed. We have grown a sortie of aggression.
Ushauri wako ni bora na umetoa mchango ulioutukuka ktk mada hii. Bravo!
Hope Polisi na wakubwa wao wangezingatia dhana hiyo. Si kila purukushani hutulizwa na Purukushani. Wanapaswa kuongeza weledi na maarifa zaid.
Pia, ni vyema nasie wananchi kujitahidi kuwa na simile. Kuna matukio au visa tunavifanya sometimes kwa namna ambayo haipendezi. Tujitahidi kuheshimu Mamlaka na kuwa watulivu ktk nyakati fulanifulani za matukio na visa. Sio kuwa aggressive na ushabiki usio na msingi.
Hivi mtu anaweza kujichagulia siku ya kuanguka na kuvunjika mguu. Tumia akili kijana
Waliokwapua kwenye EPA, RICHMOND, DOWANS, MEREMETA, ESCROW walitii sheria ipi bila shuruti. Mchimba kaburi huingia mwenyewe.
Watz kama hatutabadilika maendeleo tutayaona kwenye TV inasikitisha kuona hasa vijana kushabikia unywaji pombe wakati wa kazi. Mama huyo kama alikuwa anakimbia uwezekano Wa kuanguka Na kufa siyo ajabu. Watz tujikite kwenye mambo ya kujenga uchumi wetu siyo kuwa kwenye vilabu vya pombe kuanzia asubuhi!! Ndo maana sheria ziliwekwa kwa ajili hiyo tujifunze kwa wenzetu hata hapa Rwanda ni marufuku kuuza pombe muda wa kazi unaona maendeleo yanaonekana msifikiri maendeleo maendeleo yatakuja kwa kuwa kwenye vilabu vya pombe muda wote. Shame to you TZ wanaoshinda vilabuni. Achani siasa ukwara!!
Sikatai kulaani (in case kuna fyongo Polisi wamefanya). Lakini pia,si vyema kutafsiri kila jambo kwa mlengo hasi.
Nivyema kuwa makini na wawazi ktk kujadili na kuchambua mambo. Better to be more deductive than shooting out phenomena.
Mimi kama Tuntemeke, nimeona vyema kuwashirikisha wanajukwaa mambo hayo hapo juu. Si vinginevyo. Huo ndio mtazamo wangu,si wa wote.
Kila mtu ana'Views zake.
Umemuona mpugususu huyo? Mambo mengine mtu inabidi ucheke sana tu! Eti alikuwa muuza chakula.
Na jamaa zetu hawa wamejikita ktk upuuzi na mihemko tu badala ya uhalisia. Sasa nadhani umeona wanavyotapika ovyo.
Tanzania bwana!!
Mkuu Ghosryder , nashukuru kwa mchango wako mahsusi. Kukosoa tukosoe. Lakini pia tukubali kukosolewa kama wananchi pale tunapokiuka utaratibu.
Watu wanachangia kwa ushabiki wa ovyo tu. They have been Fooling themselves wakidhani kuna Serikali itakayokuja ifumbie macho Ukiukwaji washeria na Taratibu za nchi.
Watu hawajiongezi. Wamekalia ujima,ushabiki,ukereketwa na Siasa majitaka tu.
Thanks a Millions!
Nimejaribu kukusoma kuanzia post yako na majibu unayotoa unajichanganya tu.Naafiki hoja yako kias fulani. Kuna mauaji kadhaa yamefanywa na Polisi kwa bahati mbaya (on routine) au kwa makusudi.
Nalaani yote yanayotokea kwa makusudi na uzembe wa Polisi. Lakini,mengine ni sababu ya utaratibu wetu mbovu na kiburi chetu wananchi.
Kama uumakini unaoutambua wewe ni kukimbilia mahakamani na kuweka zuio ili wananchi wasihoji mambo ya msingi, huo ni ujinga na ujuha ulikithiri. Usijione wewe ndiye unayejua kila kitu na wengine ni mbulula, vyombo vya habari vipo kwetu sote pamoja na mitandao.Ulizia vizuri mambo haya uelimishwe. Fuatilia ITV taarifa ya leo. CHENGE KAFANYWA NINI?
Serikali iko makini.