Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

Kwa maelezo haya,mleta "ka~uzi" hakuwepo Ilula.Hamna ukweli ndani yake na kwa nini utetee uhuni?
 
Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.
Kama umetumwa na hivyo vipolisi vyenzako kutetea mauaji na ufe wewe, na hao polisi kwa maumivu makali
 
navyojua Mimi,polisi wangetekeleza majukumu yao kwa urafiki na taratibu,raia wamekua wanaona polisi kama mnyama wa kuogopwa,lililofanyika halikua sahihi either side!nimeshuhudia siku moja watu wanakurupuka mbioo kisaa wameona gwanda!Rai Yangu..polisi wajitahidi kienforce sheria pasipo nguvu raia wataelewa vizuri wakiwa na upendo bila hofu yoyote vilevile hebu raia tuheshimu sheria na taratibu!Amani ya nchi ni kwa manufaa YETU
 
Back
Top Bottom