Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

Mmesahau Zanzibar kwenye maandamano ya CUF ambavyo Polisi walikuwa wanawafuata wananchi ndani ya Nyumba kabisa vyumbani walipojificha wanawatoa nje na kuwaua? Msione watanzania tumenyamza mkadhani hatuoni wala hasikii maumivu, tumebeba mizigo mizito sana juu ya polisi na selikali yetu, pressure ikitujaa sana tutakuja kulipuka mpaka pasiwepo pa kujificha. Damu ya Mwandosi na wananchi wasio na hatia iko nyuma yenu,na lazima italipa kisasi
 
Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.

Hujielewi wewe, kuua raia ni kutekeleza sheria! mlaaniwe wote wewe na police wako.
 
Polisi huwa wana kawaida ya kuvuta migawo kwa hawa watu kwa hawa akina mama wauza na wao wanakuwa wakiwalinda. Na mara nyingi inakuwa utaratibu wao kila mwisho wa mwezi wanavuta. Inawezekana (kama ni kwenye vilabu vya pombe za kienyeji) walipishana kiswahili. Halafu nawaasa msiwachokoze Wahehe waacheni wale Ugimbi wao iwe mkangafu ama mdindifu. Msiwakwaze watu ati wanakunywa pombe za kienyeji wakati wa mchana nendeni na kwenye magesti mkakamate watu.
 
Angalieni muda alioweka hii post,kama yuko tanzania ni wazi kakosa usingizi au mamsap/bamsap kamnyima unyumba hivyo hasira zake kazimalizia Ilula.Mwenye information atujuze huo mtaa anaongoza wa chama gani?
 
Wewe tuntemeke sijui umelala umeota mini Leo mpaka umetuletea matapishi haya, au ni siku nyingi sana hujasikia kiungo cha uzazi cha mamaako kikitajwa hadharani?
 
Mkuu; nitake radhi. Sishabikii mauaji wala namna yoyote ile kama hiyo.

Pia,
Hakuna By-Laws zinazotekelezwa bila kutolewa elimu/ushirikishwaji kwa wananchi.

Elimu na msisitizo hutolewa. UTEKELEZAJI & USIMAMIZI huamriwa na Mamlaka kwa muda na nafasi wanayoipanga. Si lazima kutangaza kwamba kesho msionekane Bar au msifanye hivi kwani Mamlaka itakuwa inakagua utekelezi.

hiz by-laws zinafanya kazi kwa wanyonge tu?? Ni mabaa mangapi yanafunguliwa kuanzia asubuh had asubuh watu wanakaa wanakunywa bia ya elfu 2+ hawaguswi then mtu anakamtaji kake kaa elfu 80 kila siku polis wanachukua percent toka kwake, watu wanaingiza madawa ya kulevya wala hawaguswi, wanasafirisha twiga kikubwa wanajiuzulu, mtu kasababisha upotevu wa bn 320+ ila hatua anayochukuliwa anaombwa kujiuzulu, mwangos kauwawa hiv hiv then mhusika akapewa zawad na mkulu, huu ni upumbavu na uonevu na ni matokeo ya uongozi mbovu na dhaifu hlf jitu linakuja hapa linaanza kutetea uonevu peleka mav huko kwa waliokutuma
 
Watu ilula hawana ratiba kama ya kwako bwana mwingine asubuhi ndio starehe jioni kazini. Halafu Ilula inaongoza kwa kulima nyanya uzalishaji gani wanataka.
 
Wewe tuntemeke sijui umelala umeota mini Leo mpaka umetuletea matapishi haya, au ni siku nyingi sana hujasikia kiungo cha uzazi cha mamaako kikitajwa hadharani?

sio siri atakuwa anataman kukisikia maana anajaribu kucheza na hisia za watu
 
Hichi kitendo angefanyiwa mama yako hlf ukaja kuwatetea kwa pumba zako kama ulivyotumwa ningekupa pongezi ila naamin kwako inawezekana maana huna hata chembe ya utu
 
Kasumba ya kuwa "dawa ya moto ni moto" inapotosha. Wakati mwingine dawa ya moto ni baridi. Aliyetudanganya kuwa kila inapotokea wananchi wamechachama kwa sababu yeyote tutumie nguvu za ziada hususani mabamu ya machozi, risasi au kuwakamata.. huyu alitupotosha. Uzoefu labda kama lengo ni kujenga hofu ndani ya wananchi, lakini nafikiri tulipofikia, ni vema kutumia busara, psychology na hekima katika kutatua na kudhibiti hali kama hii kila inmapojitokeza. Na tukumbuke kuwa dawa ya moto si kila wakati iwe ni moto.

Mbona wananchi wamekiuka miiko na kuondokana na maadili ya mababu zetu? Polisi au vazi la polisi lilikuwa na heshima yake enzi zetu. Vazi la polisi lilibeba miiko kwa wananchi: palipo na ishara ya polisi ilimaanisha AMANI, UTULIVU, KIMBILIO, HAKUNA GHASIA... hata kama kungelikuwepo na vurugu, kitendo cha kuona mtu aliyevalia kama polisi,... wangelikimbilia huko... iweje siku hizi, wananchi wamechoka kuona "polisi"

Hilo ndo neno. Polisi wajiulize, ni wapi wameenda kutuliza ghasia wakaituliza?? Kuwasambaratisha makundi ya watu kwa mabomu Je ndo kutuliza ghasia?? Mbona hiyo Wizara inatumia rasilimali nyingi mno kununulia hayo mabomu na maji ya kuwasha kama kwamba nchi imekuwa ya kuwawasha watu wala si kuwatuliza watu? Basi tubadilishe msemo; Badala ya Kikosi cha kutuliza ghasia, tukiite kikosi cha Kuongeza ghasia. Mmeua, Mmejeruhi hadi kuwaletea wananchi wenu ulemavu wa kudumu, Mmejitafutia chuki za kudumu, hamyaoni hayo enyi mapolisi??? Nasema, wanao uhitaji msaada wa saikolojia ni hao viongozi wa Polisi. Polisi sio mbwa mnyama, ni mtu, mwenye reasoning capacity, kama ati ni kujitetea kuwa Polisi ni kufuata Commanding Order, sasa badilisheni. Naye Commander asipokee Order kutoka kwa asiye askari (Wanasiasa uchwara). Hawa wanawatumia Polisi ka To.ilet Paper kwa maslahi yao ya kutaka kukaa madarakani hata kama wamekataliwa. Nisameheni kwa niliye muudhi
 
Mkuu mtoa mada ningekuona wa maana zaidi kama ungetupa ushahidi wa kile kilichokuwa kikiendelea kwenye eneo la tukio,nadharia hapa haina mashiko zaidi utajikuta unapotoka kitu ambacho hata wewe jutarajii,najua hapa kuna watu ambao wanajifanya wapo kwenye nafasi ambazo hawawezi kukutana na matatizo mbalimbali ila kama kweli ingekuwa ni mama,dada au ndugu yako anayekugusa sidhani kama ungeandika ulichokiandika hapa.
Tubaki kwenye msingi wa tatizo ni kuwa jeshi letu linatakiwa kufanyiwa mabadiliko makubwa ya kifikra na kimfumo,namna ambavyo wanafanya kazi siku moja italeta maafa makubwa zaidi nchini mwetu maana hawa hawa Polisi tunaishi nao mtaani na wana familia na wala si miungu watu,ni suala la wananchi kuamua tu sema siku haijafika.
 
Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.

Nimekaa Iringa sana,WAHEHE ni watu wanaojituma sana na shughuli zao kubwa ni kilimo.Hivyo basi mtu anapoamua kwenda kunywa pombe wewe unaouita au polisi wanaouita ni muda wa kazi yawezekana wao siyo muda wao wa kazi.Kumbuka huko ni kijijini,wanamashamba yao na huu ni wakati wa kupalilia au kupanda inategema na eneo husika.Polisi hawakustahili kwenda kwenye hivyo vilabu?

Mbona mjini Bar zinafunguliwa mchana kweupe,na unawakuta hao wanaojifanya wameenda kuwaondoa watu ndiyo wako kwenye viti virefu huku UHALIFU ukitokea,ila sababu hao wanajiji ni wanyonge wengi wao hawajui sheria mbio kwenda kuwatoa uhai.

Tuntemeke Sanga,wahehe wana hata viongozi wao wakimila,Machifu,wapo watu ambao wanaheshimika sana sana na kama walitaka kuwaeleza kuhusu unywaji wa pombe basi wangepitia mila na desturi zao!!!!!!!

Tuache kutetea mauaji,hakuna mtu mwenye haki juu ya UHAI wa mwingine,viongozi wetu wanaliibia TAIFA mbona hawaendi kuwaua?

Na Iringa VITA ya ASKARI POLISI na RAIA ndiyo kwanza imeanza,waambie wale siyo waArusha mnawaua kwa mabomu wanayamaza hiyo nchi nyingine kaka,huko SWELA ni mawili ajitoe ROHO au AKUTOE ROHO.

Kumbuka hao wanaojiita polisi wanakaa kwenye hizo nyumba za waliowaita MBWA.Sasa cha moto watakiona ndiyo wamewachokoza watarajie kula ASALI ya wahehe.Hao siyo wakwere ambao ni WAVIVU kupindukia hao wanalima sana ili kujikimu na maisha yao ni wachapa kazi.............

Kwa sasa hata nikimkuta POLISI anapigwa na raia wala sishughuliki kutetea nitawaacha wapigwe tu hata wakimwangosi shauri yake.Ila kwa sasa tumewachoka wajifunze kufanya kazi kitaaluma............
 
Kufanya kazi hakulazimishwi. Ilula imepiga maendeleo saaana ya kiuchumi kupitia Kilimo (nyanya na mahindi) na biashara za huduma (hotel/migahawa na Guest Houses) huku vilabu vya pombe vikifunguliwa muda wowote kwa miaka yote hiyo. Ilula Mtua palipotokea kadhia ndio eneo kuu la biashara na almost 90% wamejiajiri so wanajua na kujipangia wenyewe muda wa kazi tofauti na mwajiriwa ambae anapangiwa muda wa kuingia na kutoka kazini. Issue ya vilabu vya pombe za kienyeji kufunguliwa mapema ni nchi nzima na afrika nzima (niliiona kenya, afrika kusini na zimbabwe). Mazingira mabovu ya kiuchumi yanayotengenezwa na serikali ya CCM (ukosefu wa masoko ya mazao, ufisadi katika pembejeo za ruzuku za mazao na mifugo, kukupowa mazao na serikali, nk) ndio kumefanya kasi ya maendeleo kwenye jamii wa wakulima kuzidi kushuka miaka baada ya miaka sasa wana-cover up eti wakafanye kazi kwa mijeledi......hii inatofauti gani na mkoloni?. Kipindi hiki pale Ilula ni kupalilia nyanya sasa mkulima hawezi kuacha palizi akashinde kilabu cha pombe. Anaenda kwa sababu hana farm activity. Ninachosikitika zaidi ni kwanini hakuna Police Officer aliyeuwawa??
 
Tatizo kubwa ni polisi kujiingiza kwenye siasa kwa kuegemea upande wa ccm.
Hivyo watu kuwachukia polisi kama wanavyoichukia ccm ni sawasawa kabisa.

Ccm inahusikaje hapo!!!! We ---- sana wewe!!!endelea ns mjadala uliyopo na si kuhusisha vyama vya siasa!!mbwa we!!!
 
Kwa taarifa yako, kuna baadhi ya sectors huko hufanya kazi zaid ya masaa 8. Sometimes hadi usiku kucha(over working). Na of course muda wa kazi unafahamika (hususan kipindi cha kazi au msimu wa Kilimo kwa Bongo).

Sasa M-Tz anagusa ofisini saa moja then anachepuka bar jirani kunitundika! Au Baba anatelekeza kazi za shambani kwa mke na watoto then anashinda kutwa nzima,wiki & mwezi mzima Bar anakunywa wanzuki,mnazi, #Ulanzi na kadhalika. Unatarajia jamii & Taifa litasonga mbele?
Kwa lugha nyingine, una maana huyo mama alikuwa sahihi kufanya kazi katika kipindi kirefu cha siku?
 
MTOA MADA UMEKURUPUKA!

Kwanza kabisa bora ungekaa tu kimya. Umekurupuka kuandika tukio ambalo hata hujui undani wake. Unasema eti ni tukio la JUZI pale hapa Ilula. Hivi tarehe 24/02/2015 ndio juzi?. Hii ni dhahiri kuwa huenda umesimuliwa tu na mtu ambaye naye hajui A-Z ya tukio hili.

SIKILIZA; Mimi ni mkazi wa Ilula, chanzo cha hili tukio nakijua kwa kina zaidi ya unavofikiria coz nilikua eneo la tukio.

Uvumi unaosambaa kuwa eti mara mama huyo alikuwa anakunywa pombe asubuhi; mara alikuwa anauza pombe kilabuni; zote hizo ni za UONGO!

Kibaya zaidi kuna jambo linaloniumiza zaidi ninapoambiwa eti mama huyo alikuwa anauza pombe haramu aina ya GONGO!

UKWELI ni kuwa, na napenda kuwajuza members wengine wa JF kwamba:
Ni kweli polisi walikuwa kwenye doria ya kukamata watu wanaokunywa pombe asubuhi. Katika doria hiyo ni kweli walifanikiwa kuwatia mbaroni baadhi ya watu kutoka sehemu mbalimbali hapa Ilula.

Walipofika mtaa flani unaoitwa Ilala hapa Ilula ndipo tatizo lilipoanzia. Huyo mama ambaye mauti yalimkuta (Jina nalilihifadhi) alikuwa ANAFANYA USAFI, kwa lugha nyepesi alikuwa ANAFAGIA.

Kwa bahati mbaya wakati akifanya huo usafi polisi nao wakawa wameshafika eneo la tukio ndipo wenzake waliokuwa karibu wakamshtua kuwa POLISI WANAKUJA!

Mama huyo alianza kukimbia, kwa bahat mbaya alikuwa ameshachelewa kwani huyo polisi (ALIYESABABISHA KIFO CHAKE) tayari alikuwa yupo karibu naye. Ile anakimbia maskini mama wa watu ALIPIGWA BUTI LA NGUVU na huyo polisi na kuanguka vibaya sana hadi kufikia KUFARIKI DUNIA. (R.I.P)

Hapo Haki iko wapi? Ni kweli mama wa watu alikutwa maeneo ya vilabu vya pombe na hawakumkuta anakunywa wala kuuza pombe. Mama alikuwa anafanya usafi. Ilikuwaje kwa askari huyo kumkimbiza na kumpiga mtama?

Na suala la kusema maeneo aliyokuwepo huyo mama ni maeneo ambayo inauzwa pombe haramu ya gongo ni UONGO ULIOKITHIRI! Na ni kauli inayotaka kutetea upande wa polisi kuwa walikuwa sahihi kwani serikali inapinga vikari uuzwaji na unywaji wa pombe haramu aina ya gongo

Kwa wakazi wa mkoa wa Iringa natumai wanajua kuwa Iringa kuna pombe maarufu aina ya ulanzi na pombe ya mahindi inayojulikana kwa jina la komoni. Maeneo ya Ilula pombe hizo ndizo maarufu sana.

Hiv kwanza twende mbele na kurudi nyuma; Ni maeneo gani Tanzania ambapo pombe haramu ya gongo inawezwa kuuzwa hadharani? Coz hivyo vilabu vya pombe vya Ilala vyote vipo pembezoni kabisa mwa barabara.


Kwa mazingira hayo ya hilo tukio ndo iliwatia hasira wananchi wa Ilula ndipo kuanza kuwashushia kipigo hao askari, kuvunja na kuchoma moto magari yao, kuvamia kituo cha polisi, kupora siraha, kuchoma baadhi ya dokumenti za polisi, kuchoma matairi na kupanga mawe barabarani.

Washukuru FFU na jeshi la zimamoto toka Iringa mjini vinginevyo hawa askari wangechezea sana kichapo, na baadhi ya raia walipanga hata kuchoma moto nyumba zao. WANANCHI TUKIAMUA TUNAWEZA!
 
Huyu ni polisi na amekuja kupima upepo.Nchi hii ina mambo ya ajabu sana.
 
Kwa taarifa ni kua polisi walikunywa kwanza bia ndo wakaenda kufanya vurugu, sasa kwao polisi haikua muda wa kazi? au wanaokunywa bia asubuhi wao wanayoruhuusa?
 
Back
Top Bottom