Tusiwaonee sana Polisi(Nijikite Ilula-Iringa)

TuntemekeSanga

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
1,346
861
Wakuu; heshima mbele!

Napenda kuwasihi sana Watanzania wenzangu kudumisha umoja,mshikamano na uzalendo. Hii nikutokana na mambo kadhaa yanayotokea nchini kwetu(hususan current Police v/s Citizens' Laments).

Nikijikita ktk suala la juzi pale Ilula-Iringa,nimeshuhudia baadhi ya Watanzania kadhaa ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na hata mitaani kote wakiendelea kulilalamikia Jeshi la Polisi kuwa, ni watesaji wasiozingatia misingi ya Utu.

Mimi naomba nitofautiane na malalamishi hayo(nikirejea tukio hilo hapo juu).

Ni ukweli uliowazi kwamba, Polisi walikuwa wanakwenda kutekeleza Ilani,Sheria na Utaratibu wa Nchi na Utawala-Mahalia (By-Laws),ambao ni mpango wakusimamia mienendo na taratibu za Wananchi kuhakikisha wanalisukuma vyema gurudumu la maendeleo.

Haipingiki kwamba,kuna mambo mengi sana yasiyokuwa ya msingi yanawafanya watu/wananchi kulegea na kushindwa kujihusisha kwa bidii na umakini kufanya shughuli za maendeleo. UNYWAJI HOLELA WA POMBE au ULEVI WA AINA YOYOTE, ni miongoni mwa mambo hayo.

Ni jukumu la Mamlaka kutunga sheria na utaratibu kufanya "perpendicular & mutual monitoring" kwa Raia wake ili kutimiza malengo ya maendeleo. Hicho ndicho kitendo kilichokuwa kinafanyika pale Ilula.

Si busara wala hekma kumwacha mtu/watu kuenenda katika njia mbovu badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo kwa wakati muafaka uliopangwa.

Yule mama aliyeanguka na kufariki (R.I.P), ni wazi kwamba,ilitokea bahati mbaya (kama inavyoweza kumtokea yeyote yule), na si kwamba alipigwa au kuteswa na Polisi.

Now; malalamiko yanayoendelea kutolewa na baadhi ya Watanzania juu ya tukio hilo(yakielekezwa kwa Polisi na Serikali), si sahihi hata kidogo. Mnyonge mnyongeni,lakini Hakhi yake mpeni.

Nchi kama CHINA,S.KOREA na RUSSIA,wako Serious mno kufuatilia nidhamu za Wananchi ktk uzalishaji mali na kujituma kwa Wananchi. Naamini that's why wako juu kiuchumi. **Sasa shida inakuja wapi kwa Serikali na Polisi wa Tanzania kusimamia Nidhamu ya kazi ya Raia wake?**

MY TAKE;
Watanzania tusihemke na kukengeuka bila sababu. Tuwe wawazi na Makini mbele za Mungu. Tusihamaki bila sababu za msingi. Tujitengenezee mazingira na Saikolojia yakutii sheria halali bila shuruti,kwa manufaa yetu binafsi,kizazi chetu na kwa Taifa letu Tanzania.

Nawasilisha.
 
Hata huyo mama alikuwa kazini akizalisha mali. Kwa lugha nyingine, polisi Tanzania walikuwa wakizuia uzalishaji mali!

Haukuwa wakati muafaka wa kifanya hivyo. By the way,dhana inafahamika kwamba kulikuwa na wauzaji & wanywaji wa pombe wakati ambao ulikuwa sio mujjarab.
 
Ileje


Hakuna By-Laws zinazotekelezwa bila kutolewa elimu/ushirikishwaji kwa wananchi.

Elimu na msisitizo hutolewa. UTEKELEZAJI & USIMAMIZI huamriwa na Mamlaka kwa muda na nafasi wanayoipanga. Si lazima kutangaza kwamba kesho msionekane Bar au msifanye hivi kwani Mamlaka itakuwa inakagua utekelezi.
 
Last edited by a moderator:
Tumeona matukio mengi police wakipiga raia kinyume na sheria sasa we sijui wamekutuma uwatetee.

Naafiki hoja yako kias fulani. Kuna mauaji kadhaa yamefanywa na Polisi kwa bahati mbaya (on routine) au kwa makusudi.

Nalaani yote yanayotokea kwa makusudi na uzembe wa Polisi. Lakini,mengine ni sababu ya utaratibu wetu mbovu na kiburi chetu wananchi.
 
Acha kushabikia mauaji. Sera nzuri ni kuwaelimisha wananchi kuhusu maendeleo na sio kuwalazimisha na kuwaua!

Mkuu; nitake radhi. Sishabikii mauaji wala namna yoyote ile kama hiyo.

Pia,
Hakuna By-Laws zinazotekelezwa bila kutolewa elimu/ushirikishwaji kwa wananchi.

Elimu na msisitizo hutolewa. UTEKELEZAJI & USIMAMIZI huamriwa na Mamlaka kwa muda na nafasi wanayoipanga. Si lazima kutangaza kwamba kesho msionekane Bar au msifanye hivi kwani Mamlaka itakuwa inakagua utekelezi.
 
Kwa hiyo hao Wachina na Wakorea unaowasifia wana wakati maalum wa kuzalisha mali?

Kwa taarifa yako, kuna baadhi ya sectors huko hufanya kazi zaid ya masaa 8. Sometimes hadi usiku kucha(over working). Na of course muda wa kazi unafahamika (hususan kipindi cha kazi au msimu wa Kilimo kwa Bongo).

Sasa M-Tz anagusa ofisini saa moja then anachepuka bar jirani kunitundika! Au Baba anatelekeza kazi za shambani kwa mke na watoto then anashinda kutwa nzima,wiki & mwezi mzima Bar anakunywa wanzuki,mnazi, #Ulanzi na kadhalika. Unatarajia jamii & Taifa litasonga mbele?
 
Kasumba ya kuwa "dawa ya moto ni moto" inapotosha. Wakati mwingine dawa ya moto ni baridi. Aliyetudanganya kuwa kila inapotokea wananchi wamechachama kwa sababu yeyote tutumie nguvu za ziada hususani mabamu ya machozi, risasi au kuwakamata.. huyu alitupotosha. Uzoefu labda kama lengo ni kujenga hofu ndani ya wananchi, lakini nafikiri tulipofikia, ni vema kutumia busara, psychology na hekima katika kutatua na kudhibiti hali kama hii kila inmapojitokeza. Na tukumbuke kuwa dawa ya moto si kila wakati iwe ni moto.

Mbona wananchi wamekiuka miiko na kuondokana na maadili ya mababu zetu? Polisi au vazi la polisi lilikuwa na heshima yake enzi zetu. Vazi la polisi lilibeba miiko kwa wananchi: palipo na ishara ya polisi ilimaanisha AMANI, UTULIVU, KIMBILIO, HAKUNA GHASIA... hata kama kungelikuwepo na vurugu, kitendo cha kuona mtu aliyevalia kama polisi,... wangelikimbilia huko... iweje siku hizi, wananchi wamechoka kuona "polisi"
 
Back
Top Bottom