Tusilaumu mabinti wanaokwepa wanaume maskini, ndoa za kiafrika ni muunganiko wa familia mbili, upo tayar binti yenu aolewe na maskini?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Walengwa ni mabinti wenye soko kubwa chini ya miaka 28

Kwa ulaya na Marekani mambo ya kuhusisha familia hayana uzito, hata binti aolewe na kapuku hayo ni maamuzi yake na atapewa kila baraka.

Shida inakuja kwetu Afrika

1.familia ya binti ipo vizuri kiuchumi, binti, kaka, dada na wadogo zake wamesomeshwa shule private, hawajawai kulala njaa, parking ina gari kadhaa, n.k.

ndugu wengine nao hasa wa upande wa baba kina baba mdogo / mkubwa nao wapo vizuri

binti anaweza kukuelewa na kuzimika kwako lakini kuhusu suala la ndoa sahau kabisa, familia yake na ndugu zake wana status ya juu, wewe ulie na hali ya chini ni kama unaenda kuweka doa.

mwanaume huna hata pikipiki, binti wa watu kalelewa mambo safi, hao kaka zake watakuelewa kweli umtoe dada yao ushuani umpeleke uswazi ? Hawataamini kuwa dada yao kakupenda bali umemroga na watakuona mchawi.
 
Na hiyo ndio tofauti ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea!

Hiyo ni kama Imani tu watu wakipendana na wakiamua lao wameamua, unataka ukute penye fedha ili we ukapate urahisi tu. Umasikini ni vile utautafsiri maskini sio kukosa tu mali bali kutokuwa na uwezo wa kuzalisha mali!

Binti anaweza kuolewa penye mali na akaitapanya mali bure ikaisha na ndoa ikafa!

Nafikiri Kuna namna malezi fulani ama elimu fulani inakosekana kwenye jamii yetu na ndio maana tunakutana na haya mambo pamoja na mikwamo mingi yakiuchumi!,yote kwa yote ukiwa kama mzazi ukiona watoto wako hawapo vizuri kiuchumi ni jukumu lako kuwainua ili wafurahie kidogo maisha yao mafupi waliyonayo.
 
labda awe kafika 30 hajaolewa ama familia ilishamkatia tamaa.

binti yupo chini ya 25 ni ngumu sana
Mdogo mtoto wa baba mdogo, kwao wako vizuri kiuchumi aliolewa na kijana kitanda chake ni mabox ila dogo ni mpambanaji na home hakupewa chochote ila leo hii pamoja na shem ni mwalimu tena primary anaendesha land-rover dsc 4 na mjengo wa maana na duka ujenzi.
 
Mdogo mtoto wa baba mdogo, kwao wako vizuri kiuchumi aliolewa na kijana kitanda chake ni mabox ila dogo ni mpambanaji na home hakupewa chochote ila leo hii pamoja na shem ni mwalimu tena primary anaendesha land-rover dsc 4 na mjengo wa maana na duka ujenzi
kwamba baba wa binti aliridhia kirahisi binti yake anaelala kitandani aende kuanza kulalia kwenye mabox ?

ngumu kumesa
 
Mie mwenyewe akipenda na kuridhia mimi sina shida, namuozesha tu, labda alete jitu huni halieleweki hapo ndipo sintajali kipato nitatia ngumu, ila kijana anaeleweka, uchawi kipato tu, namuozesha bila tabu.
Mkuu naomba tufahamiane mapema... unao mabinti wangapi?
 
Ni uvivu wa kufikiri, mke na mume wanapaswa kuanzisha familia yao na kutafuta vya kwao, urithi ni matokeo tu.

Ingekuwa hiyo ni point ndoa kama za kina Le Mutuz mtoto wa Waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais, na Neema Ngwilulupi zingedumu, tena talaka wanapeana New York City, hawa walikuwa na njaa?

Think big.
 
Mdogo mtoto wa baba mdogo, kwao wako vizuri kiuchumi aliolewa na kijana kitanda chake ni mabox ila dogo ni mpambanaji na home hakupewa chochote ila leo hii pamoja na shem ni mwalimu tena primary anaendesha land-rover dsc 4 na mjengo wa maana na duka ujenzi
Story yako ina vitu vimerukwa, eg dogo akapewa 30M za biashara na wakwe,
Ni kawaida tu sio kwa ubaya
 
Story yako ina vitu vimerukwa, eg dogo akapewa 30M za biashara na wakwe,
Ni kawaida tu sio kwa ubaya
Mimi ndio najua vizuri hajapewa chochote zaidi ya zawadi ya kitanda na godoro sema dogo alikuwa kichwa ajira yake aliitumia vizuri
 
Walengwa ni mabinti wenye soko kubwa chini ya miaka 28

Kwa ulaya na Marekani mambo ya kuhusisha familia hayana uzito kama huku kwetu, hata binti aolewe na kapuku hayo ni maamuzi yake na atapewa kila baraka.

Shida inakuja kwetu Afrika

1.familia ya binti ipo vizuri kiuchumi, binti, kaka, dada na wadogo zake wamesomeshwa shule private, hawajawai kulala njaa, parking ina gari kadhaa, n.k.

ndugu wengine nao hasa wa upande wa baba kina baba mdogo / mkubwa nao wapo vizuri

binti anaona kabisa familia yake na ndugu zake wana status ya juu, wewe ulie na hali ya chini ni kama unaenda kuweka doa.

mwanaume huna hata pikipiki, binti wa watu kalelewa mambo safi, hao kaka zake watakuelewa kweli umtoe dada yao ushuani umpeleke uswazi ?
Tatizo sio hela tatizo ni mindset inayotengenezwa na hali ya kiuchumi. Nina mademu wawili mmoja familia inajiweza na mwingine familia ya kipato cha chini sana. Huyo wanaojiweza kwao mapenzi hajui ila yuko real, nikitaka kuoa kuhusu yeye sijiulizi mara mbili. Ana akili ya maisha kuliko maelezo, ana uzoefu na shughuli za nyumbani kwao na akishauri kitu unajua hapa kuna uhai wa akili. Nimeanza kumuona tupo sekondari, form four kapiga Div. 1 ya 10 serikalini, dip kamaliza na 4+ GPA.

Huyu mwingine mrembo zaidi, bright future behind her, ngozi nyororo na mapenzi anayajua sana. Huyu nimemkamata anacheat mara mbili, mara moja na mbaba mtu mzima kama sponsor. Tatizo ni umaskini hadi kodi ananitegemea wakati yuko chuo. Wadogo zake wote hawajafika form four wanakataa shule, yeye tu ndio kapiga diploma kwa mbinde na penyewe kasoma mwaka mmoja wa ziada kisa akili chache kichwani na kuendekeza starehe akafeli mtihani (sababu kwao huwezi pata starehe, na elimu sio kipaumbele ukoo mzima). Mdogo wake aliumwa familia ikashindwa kumpeleka hospitali baadae mara mapepo mara malaria imepanda kichwani.

Kuna muda wote nilitaka kuwaacha, huyu matako makubwa akasikitika kwanini namuacha wakati natakiwa kumlipia kodi mwezi unaofuata.
Huyu mwingine alidai anajifunza kunizoea maana namkaripia na mimi ni mkorofi (ni kweli), kwanza niko mpenzi wake wa kwanza.

Huyo mmoja kasoro zake zote nikitafuta chanzo ni hali duni ya nyumbani kwao ambayo imemuingia akilini na kwenye lifestyle. Anapenda sherehe kama MC, kuchangisha birthday parties, kwenda harusini kiholela na beach parties. Familia yao ina matatizo ambayo ukizaa naye tu lazima watoto wayaridhi na siko tiyari. We unaunganisha familia ambayo wajomba walikataa shule, binamu alijiua kisa umaskini, kule walikosa hela ya kwenda hospitali wakampeleka kwa mchungaji kuombewa. Tafrani tu.

Kinachokataliwa sio umaskini ni madhara yatokanayo na umaskini. Sasa nije kuoa miaka 5 au 6 baadae niambiwe nimebagua si kunisingizia, kwanza huyo matako makubwa najitahidi kumuacha. My worst nightmare ni itakuwaje nikimpa mimba? Maana habari za hubby na kunitajia majina ya watoto zimeanza.
 
Back
Top Bottom