Ni wakati muafaka wa kuja na muswada wa sheria ya kulinda watoto na ndoa

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,889
7,114
Siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi kubwa sana la watu kuuana kutokana na wivu wa kimapenzi. Jambo hili lilianza kusikika kidogo kidogo lakini kwa sasa limekua likitokea kila siku. Hali imekua ni mbaya sana kila kukicha stori kubwa mitaani na kwenye mitandao ni masuala ya vifo au migogoro ya kimapenzi.

Jamii katika suala hili imegawanyika mara mbili; kuna wanaounga mkono wale wanaojichukulia sheria mkononi na wengine wanawalaumu wale wanaochukua sheria mikononi. Yote kwa yote kila upande ukiusikiliza kwa makini utaona kuwa una sababu zenye mashiko.

Akiuawa mwanaume, wanawake na baadhi ya wanaume hasa wale ambao wamewahi kuguswa na kadhia inayotokana na usaliti, basi kwa nguvu kubwa wanashangilia na kusema wanaume wamezidi, wanaume hawajatulia, wanaume wameizidi umalaya na tamaa acha achomwe moto au amwagiwe maji ya moto.

Wakati huo huo wanaume wengi Wanabaki kulaani tukio la mwanaume mwenzao kuuawa kwa wivu wa kimapenzi. Lakini pia hali inakua hivyo hivyo pale anapouawa mwanamke kwa wivu wa mapenzi.

Hapo kwa kweli wanaolaani wanakuwa ni wengi zaidi, kwani wanawake wanaalaani kwa nguvu kubwa na wanaume pia na watoto pia wanapata madhara makubwa kwa kupoteza mama . Hapa pia kuna kundi dogo ambalo nalo linaunga mkono kuuawa kwa mwanamke anayefanya usaliti kwenye ndoa yake.

Sasa jamii imebaki njia panda, serikali nayo imekaa kimya na kulichukulia kama suala la kibinafsi tu na sasa wanasiasa na wasomi wetu wanalihusisha na wivu unaotokana mapenzi na magonjwa ya akili tu na msongo wa mawazo. Viongozi wa dini wanalihusisha na shetani. Jamii na mila zetu za Kiafrika inalihusisha na kupotea kwa maadili ya Mwafrika.

Sasa hebu tuangalie:
Je, hili suala la mauaji ya kila siku la wivu wa kimapenzi hasa kwa wanandoa linatokana na Ugonjwa wa akili, stress na wivu uliyopitiliza hivyo dawa yake ni kutafuta ushauri nasaha na matibabu ya kitaalamu? Je ,ni sawa Kwa serikali kuja na majibu mepesi kama hayo huku jamii ikiendelea kuona Kasina kubwa ya usaliti kwenye ndoa na watu kuuna na watoto kubaki yatima siku Hadi siku huku?

Hebu nitoe mfano kule Kenya Leo hii Kuna Rais mpya anaakili timamu na Hana msongo wa Mawazo Wala Hana wivu uliopitiliza; Je, anaweza au system inaweza kuruhusu Mtu yeyote kuanza kuchepuka na mke wake kisa eti wamekubaliana wenyewe na pia ni suala la madai TU na akiona Vipi Bora waachane TU Kwa wema?
Hali kadhali Tanzania kuna wakubwa wa Serikali wenye ndoa na wake zao au waume zao;

Je, Yule Bwana Mkubwa atakua mvumilivu au atakubali kuona mkewe anatembea na mfanyakazi wa ofisi yake au jirani yake na akapewa Taarifa na akafanikiwa kumjua mwizi wake na kuchukulia poa tu eti yeye sio mgonjwa wa akili na Hana stress hivyo atatoa TU Talaka na kumpa Sasa ruhusa kamili huyo mgoni wake au mchepuko wa mkewe wakajinafasi na kumwacha yeye kama Waziri mkubwa kubaki Hana mke na watoto wakose nyumba kamili ya kukaa na kuwaona wazazi wao? Hii haikubaliki Mbinguni na Duniani. Adhabu ya mzinifu ni lazima iwe Kali sana kuepusha haya yanayotokea.

Au mfano Jaji mkuu au kwanasharia mkuu wa Serikali ghafla apate Taarifa kuwa Kuna mtu anatembea na mke wake. Sidhani kuwa atapuuza na kujifanya kuwa yeye anaakili timamu na Hana stress Kwa vyovyote atafuatilia akijua ukweli na akamuonya mgoni waki kirafiki lakini akaendelea huku mkewe akiwa anaonyesha dharau kuwa kama Vipi tuachane nikale Bata na mchepuko wangu; Je,atakubali kutoa Talaka na kumwacha mkewe na furaha Kwa mwizi wake huku yeye akibaki peke yake na watoto wakiwa hawana uelekeo Maalumu wa kifamilia na malezi ya baba na mama kisa mama ameendekeza tamaa zake za kimwili na baba Mwingine ambaye naye ana mke wake na watoto ?

Au mkuu wa majeshi asikie mke awe anachepuka na mlinzi wa getini na afanye uchunguzi agundue ni kweli au awafumanie kabisa ? Je, atachukua karatasi na kuandika barua ya Talaka badala ya kuchukua bastola na kumchakaza mlinzi risasi ya kichwa.?

Au mfano Daktari wa magonjwa ya akili mwenye akili timamu kabisa asikie kuwa mkewe ambaye ni nesi kweye Hospitali hiyo kuwa anatembea/anachepuka na mtu ambaye hua anakuja kutibiwa kwake au kupata ushauri kwake? Je, huyo Daktari ataweza kumhudumia vizuri huyo mteja wake kisa TU Hana Ugonjwa wa akili au stress au wivu Kwa mkewe? Bila shaka hataweza kumhudumia?

Hapo nimetoa TU mifano Kwa watu walioko juu kwenye serikali na vyombo vyake lakini najua wazi kuwa walioko juu familia zao zinalindwa sana na haziwezi kufikiwa kirahisi na kila mwenye tamaa ya ngono . Na pia walioko juu wao Wana Mapesa Mengi wanasafari nyingi wakiwa hata na michepuko mitatu minne Kwa pamoja .

Hawawazi sana wake zao mana mara nyingine wameshawakinai. Lakini Kwa mtu wa kawaida mwenye kipato Cha chini na ambaye anapambana kumhudumia familia yake akiwemo mke wake na nimwaminifu Kwa mkewe au Mumewe halafu anamfumania mkewe au Mumewe ambaye ana ndoa na waliapa kuishi Kwa uaminifu inakua ni mtihani sana kumwacha mwizi wake salama.

Hukuna shujaa anayekimbia vita. Na siku zote mashujaa ni wale waliokufa wakipigania mataifa yao . Kuna wakati unakuta mchepuko unamfokea na kumtishia mwenye mke au mume halali wa ndoa na mwenza wake akiulizwa anasema wewe una wivu wa kijinga ? Kisa labda mchepuko unajiona una sura zaidi au pesa zaidi au cheo kikubwa. Hapo na majibu kama hayo jamii inategemea Nini zaidi ya mauaji kuongezeka!?

Siku hizi wengi wanajificha kwenye simu eti ooh simu ya mume wake anaiangalia ya Nini? Ukiona ameiangalia basi ujue Kuna mahali anaona mabadiliko ,hakuna mtu anayeweza kuficha hisia zake Moja Kwa Moja labda kama Mumewe au mkewe amelogwa ili awe taahira hafuatiilii chochote Cha mke wake.

Kwenye mauaji haya ya wanandoa wahanga zaidi ni wale watu wanyonge na sio wakubwa. Hawa wanyonge ambao Kwa Sasa kulingana na ugumu wa maisha ndoa zao zinaingilika kirahisi sana ; Je, ndao zao na watoto wao wanalindwaje dhidi ya wanaume na Wanawake Wazinzi wasiojali ndoa na hatima ya watoto wa wenzao? Ni kweli kuwa Kwa Sasa suala la kuchepuka Kwa Wanawake limekua kama mashindano Kati ya walioko kwenye ndoa na walioko nje ya Ndoa. Wanawake wanahujumiana wenyewe Kwa wenyewe.

Yani tamaa imeongezeka sana kutokana na mitandao mtu yupo Mwanza anamtongoza Mwanamke aliyeko Dar es salaam kirahisi sana . Hali hii ni janga kubwa sana siku zinavyoendelea Kwa sababu hakuna Tena heshima ya Ndoa . Ndoa inaonekana kama ndoano na Wazinzi wanafanya makusudi kuzini na waume na wake za watu ili kuzidi kuvuruga ndoa na kuwafanya wanaume na Wanawake wawe wa kila mtu bila utaratibu.
Ikitokea Ugonjwa wa kuambikiza kama ilivyokuwa AIDS miaka ya 1980 kuelekea 1990 mpaka 2020 Watanzania wataisha.

Sasa hivi hata biashara ya Kondom Haina soko Tena mana virusi vimshafubaa na hakuna wagonjwa Tena. Woga haupo Tena hasa Kwa wanandoa ndio Hali ni mbaya zaidi. Hata hivyo vifo vimegeukia vya kuuana badala ya magonjwa Sasa ni kuuna Kwa kukataa mapanga na kumwagiana maji ya moto na risasi.

Watawala walioko juu na wanasiasa waliangalie jambo hili la Wana ndoa kuuana Kwa jicho la tatu. Hali ni mbaya kwenye ndoa nyingi. Wanaume wengi Kwa Sasa wanaugulia ndani hasa wa kipato Cha chini na Vijana .
Siku hizi hakuna kijana asiye na pesa anayeweza kuwa na mchumba mrembo na wakafikia ndoa. Hata wakiona wanaishia kuuana. Yote ni Kwa sababu hakuna SHERIA Kali ya kulinda kizazi Cha kesho na maadili.
Hivi Hawa wa maisha ya chini hasa wa kiume Watakuja kuwa na familia yenye mama,baba na watoto kama serikali itaendelea kukaa kimya kwenye hili tatizo la wanandoa kuuana?

SHERIA ya Sasa ya Ndoa imebaki kuwalinda Wazinzi wenye pesa huku maskini wakiishia makaburini au gerezani au kuishi na stress na kufa kabla ya wakati. Mzinzi Mwenye pesa anaweza akamchukua mke wa mtu bila woga mana anajua hata akifumaniwa hakuna SHERIA Kali ya kumbana zaidi ya kesi ya madai ambayo maskini hawezi kuifungua. Lakini pia akipewa vitisho anatoa pesa nyingi na kitakatisha fumanizi lake.

Maskini mzinzi akifumaniwa anauawa au kulawitiwa mana Hana Cha kulipa. Hapa maskini ndiye anayeumizwa na SHERIA hii ya Ndoa ambayo inatoa fursa Kwa Wazinzi wenye fedha kujitwalia Wanawake mpaka kwenye ndoa za watu. Maskini anapoona anaporwa mpaka mke wake au mume wake ambaye kwenye kiapo Chao Cha ndoa aliapo kuwa faraja kwake basi anaamua kuua. Hapo hakuna namna mana Hana wa kumkimbilia ili apate msaada wa kulipiwa kisasi chake . Kazi ya serikali ni kulipa kisasi badala ya mdhulumiwa Vinginevyo mdhulumiwa analipa Mwenyewe.

Serikali inawatupia mzigo viongozi wa kidini kuwa watoe Elimu ya kiroho zaidi lakini ukweli ni kwamba nao pia ni ama ni wahanga au vikwazo kutokana na ukweli kuwa wapo pia viongozi wa dini Wazinzi wanaovuruga ndoa za watu.
Wanafanya makusudi mana hakuna SHERIA Kali ya kulinda ndoa za watu.

NINI CHA KUFANYA:-
Ni wakati Sasa wa kubadili SHERIA ya Ndoa ili Suala la Kuzini na Mke au mume wa mtu liwe ni jinai Moja Kwa Moja hasa inapotokea Kuna ushahidi wa kutosha. Yaani pawe na ufuatilliaji mpaka wa kimtandaoa mana mitandao inetumika sana kwenye kuvuruga ndoa za watu. Iwe suala la kushea simu Kwa wanandoa wenye ndoa ya mke mmoja liwe ni wazi au kukubaliana lakini iwe ni haki ya Mwana ndoa ya mke mmoja kuomba kufuatilia mienendo ya mwenza wake na kufungua kesi ya Jinai ili kumbaini anayevuruga ndoa yake na kufikshwa mahakamani na kupewa kifungo.

Lengo ni kulinda ndoa maana mtu anapoamua kuoa mke mmoja na mume mmoja basi amefanya hivyo Kwa taratibu za kisheria ili awe na familia yenye ustawi. Sasa tukiwaachia watu wakae bila kubanwa na SHERIA Hakika miaka ishirini ijayo ndoa za mashoga zitakua nyingi sana mana watoto wengi watakosa Bora. Lakini pia kuwaacha watu wenye stress na vinyongo kwenye jamii ni hatari Kwa amani ya nchi.

Mtu ambaye alikua anampenda mke wake au mume wake halafu ghafla akajikuta ameachana na mke wake au mume wake Kwa sababu TU Kuna Mzinzi mmoja mwenye pesa au anayejifanya yeye ni kidume au kipisi kali Cha kutembea na wake au waume za watu, rahisi Sana mtu kama huyo kufanya tukio baya au uhalifu mbaya .
Hata ugaidi hua mara nyingi unatokana na masuala ya Ndoa. Ukiangalia mfano suala la mahakama ya Kadhi nchini Tanzania lilikua hasa linalenga masuala ya Ndoa.

Waliponyimwa paliibuka chuki za chini Kwa chini na hata kuibuka Kwa vitendo vya kigaidi. Kijana mfano alikua na mchumba wake mzuri halafu anatokea Mzee wa miaka 60 mwenye pesa na mke wake na watoto na wajukuu anakuja anamrubuni mchumba wa huyo kijana na kusababisha kijana anashidwa kumuoa Tena. Bila shaka kijana huyo anakua na hasira na kinyongo na Hana pa kwenda ili kisasi chake kilipwe badala yake anaambiwa aende akafungue kesi madia mahakamani ili alipwe fidia. Fidia ya Nini wakati shida yake sio pesa ni mke? Kijana kama huyu ni rahisi kulipa kisasi au kuwa na roho mbaya na hata kujiunga na ugaidi.

Hata utendaji kwenye maofisi ya umma unashuka Kwa sababu ya migogoro ya Ndoa. Watu wanaingia kazini na stress wanashindwa kutoa huduma nzuri.

Watu wanafanya ufisadi ili wawe na fedha nyingi mana wanajua ndoa za watu maskini Kwa Sasa hazina Tena uaminifu na uvumilivu. Wamama wanakopa vikoba pesa wanahonga Vijana matokeo yake Wanabaki na madeni.

Kwa Wanasiasa wenye migogoro ya Ndoa wanaweza kuhamasisha maandamano yaliyojaa chuki na hata kuvuruga amani ya nchi.

Serikali ije na MUSWADA WA kurekebisha SHERIA ya Ndoa ili hata waislam wenye wake wanne wote watambulike kwenye haki zao Kwa watumishi wa umma.

Mtu yeyote mwenye ndoa ya mke mmoja akifumaniwa na au akivuriga ndoa ya mtu afungwe gerezani.
Mwenye ndoa ya wake wengi pia akifumaniwa afungwe gerezani na faini juu mana alikua na fursa ya kuoa mke Mwingine ili kukidhi tamaa zake. Ifikie mahali tujenge jamii iliyostarabika sio kuuana Kwa sababu ya kuishi kama nguruwe na mbwa na Kuku. Hii itarudisha heshima ya Ndoa na kulinda watoto na pia kupunguza mauaji. Na pia itahamasisha Vijana kuoa na kuolewa mana watakosa urahisi wanaoupata ngono kama ilivyo Sasa. Kijana au Binti atajua akitembea na mume au mke wa mtu kifungo kinamsubiri.

Lakini pia suala la kupima DNA Kwa wanandoa wapya liwe ni lazima mana watoto wengi wanaozaliwa sio wa baba wa kwenye ndoa na wamezaliwa sio Kwa sababu ya kukosa uzazi Bali kwa sababu ya kuchepuka na wengine kuapa kuwapa michepuko yao zawadi ya kumzalia mtoto. Hii ni hatari hasa mwanaume anapojua anawaza jinsi Nmanavyohangaika na maisha kumbe baadhi ya watoto sio wake.
Hapa kuzaa nje ya Ndoa libaki kama makubaliano au asiyeweza kukaa na mwenza asiyezaa basi aombe Talaka au wakapandikize mtoto Kwa kuridhiana sio kusalitiana.

Kwa upande wa Viongozi wa dini waache mahubiri ya kugemea upande mmoja na kusema kuwa wanaume ndio wanaochepuka , Hali inayowafanya Wanawake kuona kuwa wao hawaonekani na hivyo wanaendelea kuchepuka kwa kujificha na wakiona wanabainika wanajificha kwenye mgongo wa viongozi wa dini wakati ukweli ni kwamba Wana ndoa wa kike na kiume ndio wanaoongoza kuchepuka.

Lakini pia serikali iangalie zaidi SHERIA zinazoruhusu ndoa ya wake wengi ipewe kipao mbele mana inaonekana kuwa Wanawake wapenda kuchangia wanaume ndio maana wengi wanapenda waume za watu.
Na wanaume wengi HAWAWEZI kuwa na mke mmoja hivyo waoe wake wengi sio kuvuruga ndoa za watu.

Haiwezekani mwizi aibe Kuku wa Kienyeji anayeishi Kwa kula mchwa maporini na majalani na Hana gharama yoyote lakini akiibiwa basi mwizi anafungwa miaka sana lakini mtu anaingia na kuiba mke au mume wa mtu anayemgharamikia kuanzia mahari na matunzo na kulea watoto halafu eti iwe ni kesi ya madai TU au mtu avumilie TU. Lakini akimkuta maskini anaiba mbuzi wake anaweza kumpigia mshale au kumpeleka Polisi na akafungwa miaka sana. Kuku mmoja Tena kutokana na umaskini TU haiwezi kuwa ni kosa kubwa kuliko kutenganisha mtu na familia yake na kuacha watoto WAKITESEKA. Wote Hawa ni Wahalifu mana wanavunja ustawi wa jamii na kuleta chuki kwenye jamii.

Serikali na Bunge wasipochukua hatua Kwa sababu tu wao hawaguswi sana kadhia hii ya kuachiwa watoto yatima kutokana na mauaji ya wivu wa mapenzi wajue ipo siku Watajua kuwa walitunga SHERIA ya Ndoa ya mazingira ya Ulaya bila kuangalia mazingira ya kiafrika.
 
Mjuni Lwambo

JF-Expert Member
Apr 25, 2012
8,451
7,038
Sheria ya haki ya kuishi mbona ipo?
Mleta mada ametoa maelezo meeengi, ilihali pointi yake ni ndogo tu, anataka itungwe sheria ambayo ipo upande wa Zanzibar.. KUWA NA MAHUSIANO NA MKE WA MTU IWE JINAI.

Ukitunga sheria hiyo, ni kama unataka kuweka sheria kwamba, KUWA NA MAHUSIANO NJE YA NDOA AU BILA NDOA, ni jinai. Je ni sawa? Kutunga sheria kuzuia watu kufanya ngono hadi wawe kwenye ndoa?

Inaonekana wewe una wivu sana, namaanisha roho mbaya sana kiasi kwamba unaona haifai kumwacha mkeo kwa amani aendelee na mchepuko wake.

Jiangalie kwa umakini, unaweza ukawa na magonjwa ya akili!
 
Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
1,539
3,694
Kama ndoa inakutesa, utawa would be your best option... 😀😀
By the way, hongera kwa uwasilishaji mzuri. Umeandika kwa kirefu sana na kwa hisia.

Sehemu ya suluhisho nilishaitoa huko nyuma kwa kusema, ili ndoa iwe na afya, ni vyema master bed room iwe na vitanda viwili; kila mtu awe na cha kwake. Watu walale pamoja siku wanapohitajiana.
Kulala pamoja kila siku lets say kwa miaka mitano mfululizo, hufanya wanandoa kuchokana haraka na kufikia hatua ya kuchepuka ili kubadilisha ladha.
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,889
7,114
Mleta mada ametoa maelezo meeengi, ilihali pointi yake ni ndogo tu, anataka itungwe sheria ambayo ipo upande wa Zanzibar.. KUWA NA MAHUSIANO NA MKE WA MTU IWE JINAI.

Ukitunga sheria hiyo, ni kama unataka kuweka sheria kwamba, KUWA NA MAHUSIANO NJE YA NDOA AU BILA NDOA, ni jinai. Je ni sawa? Kutunga sheria kuzuia watu kufanya ngono hadi wawe kwenye ndoa?

Inaonekana wewe una wivu sana, namaanisha roho mbaya sana kiasi kwamba unaona haifai kumwacha mkeo kwa amani aendelee na mchepuko wake.

Jiangalie kwa umakini, unaweza ukawa na magonjwa ya akili!
Kipi Kizuri kuacha watu wauane na kuacha watoto wateseke kisa TU Kuna watu hawataki SHERIA Kali. Miaka ya Nyuma Wanawake maofisini walikua ni kama halali Kwa mabosi na walikua hawana pa kukimbilia. Ilikua ni apende asipende bosi akimtaka ni lazima au akose kazi . Hali ikaendelea hivyo huku ubakaji ukiwa ni halali Kwa wanaume. Ukatili wa kijinsia umepunguzwa Kwa kutunga SHERIA Kali .
Watoto wa shule walikua wanapewa mimba mpaka na walimu wao . Hakuna aliyekua anajali na kuwaza kuacha mpaka SHERIA Kali ilipotungwa . Kwa Nini watu wasihamasishwe kuoa wake wake wengi badala kuwa na michepuko mingi na kuanza kuuana ? Hao wenye wivu kupita kiasi lakini Wana wake au waume zao halali wa ndoa wanalindwaje na sheria.

Huu ni mwanzo tuu watauawa sana mana hili ni agizo la Mungu. Ndio maana wasipouawa basi yanakuja magonjwa na kuua. Mungu alishaelekeza namna Bora ya kuishi Kwa kila mtu kuwa na mke au Mume wake na Kwa Waislam na Mila zetu hatukatazwi kuoa mke zaidi ya mmoja.

Hao watoto wanaoachwa yatima Kwa Nini hatuoni kuwa Jamii imezembea kuweka SHERIA inayozuia migogoro inayosabanishwa na watu kuendekeza tamaa zao?
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,889
7,114
Yaani badala ya kuishi na mke kwa upendo, tuishi na wake zetu kwa mujibu wa sheria?
Hata Adamu Mungu alimpenda sana lakini alimwekea SHERIA asile tunda la mti wa kati.
Na alipoivunja Ile SHERIA Mungu alimfukuzilia mbali bila kupepesa mana alijua mtu asiyetii SHERIA hawezi kuendelea kumpa nafasi ya kuingia kwenye Bustani za Peponi.

Yesu anawapenda Sana binadam hata akaamua kufa Kwa ajili yao lakini amesema wazi asiye muamini atapotea na kutupwa Jehanam kwenye moto wa milele.

Wanandoa ni akina nani waishi bila SHERIA .
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,889
7,114
Sheria ya haki ya kuishi mbona ipo?
Haki ya kusihi inafikia mwisho wakati wa hasira Kali.
Ndio maana mtu aliyewahi kuvamiwa na kuibiwa vitu vyake na Panya Road akifanikiwa kumkamata mmoja anamuua Kwa kumchoma na moto.
Hii ni kutokana na hasira.Ni halali kabisa mana jamii imezembea mpaka wakaibuka Wahalifu waliotokana na kushindwa kutunga SHERIA zinazozuia Vijana kutoka vijijini kwenda mijini bila kazi Maalumu inayotambulika.
Haki ya kuishi ipo lakini haijawekewa mazingira mazuri.
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,889
7,114
Maisha hayarudi nyuma, acha iendelee kunyesha.
Jamii imezembea Sana na wote tukikaa kimya tutakuwa tumeshiriki dhambi kubwa sana.
Kwa Sasa jamii nzima imejaa uhalifu unaoumiza wengine bila kujali.
Panya Road, zinaa zinazoleta wivu wa mapenzi. Matumizi mabaya ya mitandao . Mtu ana mke wake lakini kucha kutwa anachati na wake au waume za watu huku akishindwa kuchati na mume au mke wake. Matokeo yake simu inakua ni Kama Bomu kuigusa.
Jamii haikemei Tena madhambi matokeo yake kila mtu anafanya kulingana na urefu wa kamba yake.
Yaani ukiweza kumtongoza na kumla mke wa mtu yeyote ni sawa TU hakuna SHERIA inayokukataza unaamua TU Mwenyewe . Wakati Mungu amekataza hata kumtamani mke wa jirani yako.

Dunia imewapa wasimamizi na watunga sheria wenye mioyo ya tamaa na wasiomuogopa Mungu matokeo yake jamii nzima inakua ni uwanja wa shetani kufanyia sherehe.
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,889
7,114
Mleta mada ametoa maelezo meeengi, ilihali pointi yake ni ndogo tu, anataka itungwe sheria ambayo ipo upande wa Zanzibar.. KUWA NA MAHUSIANO NA MKE WA MTU IWE JINAI.

Ukitunga sheria hiyo, ni kama unataka kuweka sheria kwamba, KUWA NA MAHUSIANO NJE YA NDOA AU BILA NDOA, ni jinai. Je ni sawa? Kutunga sheria kuzuia watu kufanya ngono hadi wawe kwenye ndoa?

Inaonekana wewe una wivu sana, namaanisha roho mbaya sana kiasi kwamba unaona haifai kumwacha mkeo kwa amani aendelee na mchepuko wake.

Jiangalie kwa umakini, unaweza ukawa na magonjwa ya akili!
Mwenye Ugonjwa wa akili ni yule anayoona jamii inafanya maovu halafu anafumba macho na kusema Bora liende. Ana mtoto wa kike anarudi nyumbani saa Saba usiku anakaa kimya mana akimuadhibu au kumkemea ataambiwa ana Ugonjwa wa akili, ana dada yake anafanya zinaa na Vijana wahuni bila mpango wa kuoana na kutoa TU mimba halafu anaangalia TU Kwa sababu akisema ataambiwa ana Ugonjwa wa akili.

Mgonjwa hatari wa akili na kichaa ni yule anayeshindwa kujua mema na mabaya.

Kama jamii nzima haioni kuwa Kuna Tatizo kubwa sana kwenye SHERIA ya Ndoa inayowapa Wazini nafasi ya kuvuruga ndoa za watu na kuleta mauaji na kuwaacha watoto wadogo wakihangaika na kuwa Panya road basi jamiii yetu Ina Vichaa na wapumbavu wengi sana.
Kama Jamii nzima haioni tatizo la kuwa na sharia ya Ndoa isiyo na meno na inayoweza ikasababisha magonjwa Kwa wasio na vifo Kwa wasio na hatia basi ni jamii mfu au inayosubiri kufa.

Miaka ya 1990 + ukimwi uliua sana wanandoa wengi kuliko wasio na doa watoto wakazaliwa na ukimwi na kufa . Hata baada ya Janga Hilo kutokea lakini jamii mpaka Leo haijajifunza TU kuwa Kuna Tatizo kwenye ndoa watu wengi hawaheshimu ndoa za watu Wala za kwao wenyewe .
Sasa ukimwi hauna makali lakini watu wanauana na kuambukizana saratani ya kizazi Kwa Kasi sana ndani ya Ndoa.
Bado TU jamii haioni . Cha ajabu wengi wenye tabia za hovyo ni wasomi wanajifariji Kwa ulevi lakini jamii inaangamia.Wanaona kuwa wao sio wagonjwa wa akili kumbe ni Vichaa na hawaoni Tena jema na baya.

Usipoziba ufa utajenga ukuta.
Panya rodi wataongezeka sana mana kila mtu anatafuta pesa za anasa ,ulevi na Kununua Wanawake mana hakuna Tena mahusiano yenye kanuni zaidi ya tamaa. Vijana hawawazi kuoa Tena na kuwa na familia. Hivi Mtu hawazi kuwa na familia au kuwa na mke wake atakua Vipi mtu Bora kwenye jamiii.

Mara nyingi watu wanaepuka kuvunja SHERIA Kwa sababu wanawaza wake zao na watoto wao basi wanaogopa kifungo gerezani na kuachana na uhalifu.

Sasa ukiwa na jamii isiyowaza Tena familia ujue ni janga kubwa na watakaolia sana ni wale walioona kabla wakakaa kimya. Hasa wasomi na watunga SHERIA mana wao wataguswa na matokeo ya kuvurugika Kwa familia za wenzao kupitia Panya road waliokosa malezi ya baba na mama. Watoto wa zinaa ni wengi mpaka kwenye ndoa.Hao wanakua watu wema pale TU wanapobahatika kupata fursa ila wakikosa fursa wanakua wanaya kuliko unaya wenyewe.
 
Mjuni Lwambo

JF-Expert Member
Apr 25, 2012
8,451
7,038
Kipi Kizuri kuacha watu wauane na kuacha watoto wateseke kisa TU Kuna watu hawataki SHERIA Kali. Miaka ya Nyuma Wanawake maofisini walikua ni kama halali Kwa mabosi na walikua hawana pa kukimbilia. Ilikua ni apende asipende bosi akimtaka ni lazima au akose kazi . Hali ikaendelea hivyo huku ubakaji ukiwa ni halali Kwa wanaume. Ukatili wa kijinsia umepunguzwa Kwa kutunga SHERIA Kali .
Watoto wa shule walikua wanapewa mimba mpaka na walimu wao . Hakuna aliyekua anajali na kuwaza kuacha mpaka SHERIA Kali ilipotungwa . Kwa Nini watu wasihamasishwe kuoa wake wake wengi badala kuwa na michepuko mingi na kuanza kuuana ? Hao wenye wivu kupita kiasi lakini Wana wake au waume zao halali wa ndoa wanalindwaje na sheria.

Huu ni mwanzo tuu watauawa sana mana hili ni agizo la Mungu. Ndio maana wasipouawa basi yanakuja magonjwa na kuua. Mungu alishaelekeza namna Bora ya kuishi Kwa kila mtu kuwa na mke au Mume wake na Kwa Waislam na Mila zetu hatukatazwi kuoa mke zaidi ya mmoja.

Hao watoto wanaoachwa yatima Kwa Nini hatuoni kuwa Jamii imezembea kuweka SHERIA inayozuia migogoro inayosabanishwa na watu kuendekeza tamaa zao?
Mkuu, nilikuwa nataka tujadili kwa upana hii mada, lakini ulipoingiza mambo ya dini umeharibu. Dini ni hiari ya mtu. Hatuwezi kutunga sheria kwa kufuata maagizo ya dini.

Hao wanaoua ua watu kwa kusingizia wivu wana matatizo ya akili, wapelekwe milembe!
 
Mjuni Lwambo

JF-Expert Member
Apr 25, 2012
8,451
7,038
Mwenye Ugonjwa wa akili ni yule anayoona jamii inafanya maovu halafu anafumba macho na kusema Bora liende. Ana mtoto wa kike anarudi nyumbani saa Saba usiku anakaa kimya mana akimuadhibu au kumkemea ataambiwa ana Ugonjwa wa akili, ana dada yake anafanya zinaa na Vijana wahuni bila mpango wa kuoana na kutoa TU mimba halafu anaangalia TU Kwa sababu akisema ataambiwa ana Ugonjwa wa akili.

Mgonjwa hatari wa akili na kichaa ni yule anayeshindwa kujua mema na mabaya.

Kama jamii nzima haioni kuwa Kuna Tatizo kubwa sana kwenye SHERIA ya Ndoa inayowapa Wazini nafasi ya kuvuruga ndoa za watu na kuleta mauaji na kuwaacha watoto wadogo wakihangaika na kuwa Panya road basi jamiii yetu Ina Vichaa na wapumbavu wengi sana.
Kama Jamii nzima haioni tatizo la kuwa na sharia ya Ndoa isiyo na meno na inayoweza ikasababisha magonjwa Kwa wasio na vifo Kwa wasio na hatia basi ni jamii mfu au inayosubiri kufa.

Miaka ya 1990 + ukimwi uliua sana wanandoa wengi kuliko wasio na doa watoto wakazaliwa na ukimwi na kufa . Hata baada ya Janga Hilo kutokea lakini jamii mpaka Leo haijajifunza TU kuwa Kuna Tatizo kwenye ndoa watu wengi hawaheshimu ndoa za watu Wala za kwao wenyewe .
Sasa ukimwi hauna makali lakini watu wanauana na kuambukizana saratani ya kizazi Kwa Kasi sana ndani ya Ndoa.
Bado TU jamii haioni . Cha ajabu wengi wenye tabia za hovyo ni wasomi wanajifariji Kwa ulevi lakini jamii inaangamia.Wanaona kuwa wao sio wagonjwa wa akili kumbe ni Vichaa na hawaoni Tena jema na baya.

Usipoziba ufa utajenga ukuta.
Panya rodi wataongezeka sana mana kila mtu anatafuta pesa za anasa ,ulevi na Kununua Wanawake mana hakuna Tena mahusiano yenye kanuni zaidi ya tamaa. Vijana hawawazi kuoa Tena na kuwa na familia. Hivi Mtu hawazi kuwa na familia au kuwa na mke wake atakua Vipi mtu Bora kwenye jamiii.

Mara nyingi watu wanaepuka kuvunja SHERIA Kwa sababu wanawaza wake zao na watoto wao basi wanaogopa kifungo gerezani na kuachana na uhalifu.

Sasa ukiwa na jamii isiyowaza Tena familia ujue ni janga kubwa na watakaolia sana ni wale walioona kabla wakakaa kimya. Hasa wasomi na watunga SHERIA mana wao wataguswa na matokeo ya kuvurugika Kwa familia za wenzao kupitia Panya road waliokosa malezi ya baba na mama. Watoto wa zinaa ni wengi mpaka kwenye ndoa.Hao wanakua watu wema pale TU wanapobahatika kupata fursa ila wakikosa fursa wanakua wanaya kuliko unaya wenyewe.
Wewe unazungumzia mambo ya maovu, wazini na ndoa huku umeegemea kwenye dini. Huwezi kuwa objective!
 
Killing machine

JF-Expert Member
Jul 24, 2022
581
498
Siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi kubwa sana la watu kuuana kutokana na wivu wa kimapenzi. Jambo hili lilianza kusikika kidogo kidogo lakini kwa sasa limekua likitokea kila siku. Hali imekua ni mbaya sana kila kukicha stori kubwa mitaani na kwenye mitandao ni masuala ya vifo au migogoro ya kimapenzi.

Jamii katika suala hili imegawanyika mara mbili; kuna wanaounga mkono wale wanaojichukulia sheria mkononi na wengine wanawalaumu wale wanaochukua sheria mikononi. Yote kwa yote kila upande ukiusikiliza kwa makini utaona kuwa una sababu zenye mashiko.

Akiuawa mwanaume, wanawake na baadhi ya wanaume hasa wale ambao wamewahi kuguswa na kadhia inayotokana na usaliti, basi kwa nguvu kubwa wanashangilia na kusema wanaume wamezidi, wanaume hawajatulia, wanaume wameizidi umalaya na tamaa acha achomwe moto au amwagiwe maji ya moto.

Wakati huo huo wanaume wengi Wanabaki kulaani tukio la mwanaume mwenzao kuuawa kwa wivu wa kimapenzi. Lakini pia hali inakua hivyo hivyo pale anapouawa mwanamke kwa wivu wa mapenzi.

Hapo kwa kweli wanaolaani wanakuwa ni wengi zaidi, kwani wanawake wanaalaani kwa nguvu kubwa na wanaume pia na watoto pia wanapata madhara makubwa kwa kupoteza mama . Hapa pia kuna kundi dogo ambalo nalo linaunga mkono kuuawa kwa mwanamke anayefanya usaliti kwenye ndoa yake.

Sasa jamii imebaki njia panda, serikali nayo imekaa kimya na kulichukulia kama suala la kibinafsi tu na sasa wanasiasa na wasomi wetu wanalihusisha na wivu unaotokana mapenzi na magonjwa ya akili tu na msongo wa mawazo. Viongozi wa dini wanalihusisha na shetani. Jamii na mila zetu za Kiafrika inalihusisha na kupotea kwa maadili ya Mwafrika.

Sasa hebu tuangalie:
Je, hili suala la mauaji ya kila siku la wivu wa kimapenzi hasa kwa wanandoa linatokana na Ugonjwa wa akili, stress na wivu uliyopitiliza hivyo dawa yake ni kutafuta ushauri nasaha na matibabu ya kitaalamu? Je ,ni sawa Kwa serikali kuja na majibu mepesi kama hayo huku jamii ikiendelea kuona Kasina kubwa ya usaliti kwenye ndoa na watu kuuna na watoto kubaki yatima siku Hadi siku huku?

Hebu nitoe mfano kule Kenya Leo hii Kuna Rais mpya anaakili timamu na Hana msongo wa Mawazo Wala Hana wivu uliopitiliza; Je, anaweza au system inaweza kuruhusu Mtu yeyote kuanza kuchepuka na mke wake kisa eti wamekubaliana wenyewe na pia ni suala la madai TU na akiona Vipi Bora waachane TU Kwa wema?
Hali kadhali Tanzania kuna wakubwa wa Serikali wenye ndoa na wake zao au waume zao;

Je, Yule Bwana Mkubwa atakua mvumilivu au atakubali kuona mkewe anatembea na mfanyakazi wa ofisi yake au jirani yake na akapewa Taarifa na akafanikiwa kumjua mwizi wake na kuchukulia poa tu eti yeye sio mgonjwa wa akili na Hana stress hivyo atatoa TU Talaka na kumpa Sasa ruhusa kamili huyo mgoni wake au mchepuko wa mkewe wakajinafasi na kumwacha yeye kama Waziri mkubwa kubaki Hana mke na watoto wakose nyumba kamili ya kukaa na kuwaona wazazi wao? Hii haikubaliki Mbinguni na Duniani. Adhabu ya mzinifu ni lazima iwe Kali sana kuepusha haya yanayotokea.

Au mfano Jaji mkuu au kwanasharia mkuu wa Serikali ghafla apate Taarifa kuwa Kuna mtu anatembea na mke wake. Sidhani kuwa atapuuza na kujifanya kuwa yeye anaakili timamu na Hana stress Kwa vyovyote atafuatilia akijua ukweli na akamuonya mgoni waki kirafiki lakini akaendelea huku mkewe akiwa anaonyesha dharau kuwa kama Vipi tuachane nikale Bata na mchepuko wangu; Je,atakubali kutoa Talaka na kumwacha mkewe na furaha Kwa mwizi wake huku yeye akibaki peke yake na watoto wakiwa hawana uelekeo Maalumu wa kifamilia na malezi ya baba na mama kisa mama ameendekeza tamaa zake za kimwili na baba Mwingine ambaye naye ana mke wake na watoto ?

Au mkuu wa majeshi asikie mke awe anachepuka na mlinzi wa getini na afanye uchunguzi agundue ni kweli au awafumanie kabisa ? Je, atachukua karatasi na kuandika barua ya Talaka badala ya kuchukua bastola na kumchakaza mlinzi risasi ya kichwa.?

Au mfano Daktari wa magonjwa ya akili mwenye akili timamu kabisa asikie kuwa mkewe ambaye ni nesi kweye Hospitali hiyo kuwa anatembea/anachepuka na mtu ambaye hua anakuja kutibiwa kwake au kupata ushauri kwake? Je, huyo Daktari ataweza kumhudumia vizuri huyo mteja wake kisa TU Hana Ugonjwa wa akili au stress au wivu Kwa mkewe? Bila shaka hataweza kumhudumia?

Hapo nimetoa TU mifano Kwa watu walioko juu kwenye serikali na vyombo vyake lakini najua wazi kuwa walioko juu familia zao zinalindwa sana na haziwezi kufikiwa kirahisi na kila mwenye tamaa ya ngono . Na pia walioko juu wao Wana Mapesa Mengi wanasafari nyingi wakiwa hata na michepuko mitatu minne Kwa pamoja .

Hawawazi sana wake zao mana mara nyingine wameshawakinai. Lakini Kwa mtu wa kawaida mwenye kipato Cha chini na ambaye anapambana kumhudumia familia yake akiwemo mke wake na nimwaminifu Kwa mkewe au Mumewe halafu anamfumania mkewe au Mumewe ambaye ana ndoa na waliapa kuishi Kwa uaminifu inakua ni mtihani sana kumwacha mwizi wake salama.

Hukuna shujaa anayekimbia vita. Na siku zote mashujaa ni wale waliokufa wakipigania mataifa yao . Kuna wakati unakuta mchepuko unamfokea na kumtishia mwenye mke au mume halali wa ndoa na mwenza wake akiulizwa anasema wewe una wivu wa kijinga ? Kisa labda mchepuko unajiona una sura zaidi au pesa zaidi au cheo kikubwa. Hapo na majibu kama hayo jamii inategemea Nini zaidi ya mauaji kuongezeka!?

Siku hizi wengi wanajificha kwenye simu eti ooh simu ya mume wake anaiangalia ya Nini? Ukiona ameiangalia basi ujue Kuna mahali anaona mabadiliko ,hakuna mtu anayeweza kuficha hisia zake Moja Kwa Moja labda kama Mumewe au mkewe amelogwa ili awe taahira hafuatiilii chochote Cha mke wake.

Kwenye mauaji haya ya wanandoa wahanga zaidi ni wale watu wanyonge na sio wakubwa. Hawa wanyonge ambao Kwa Sasa kulingana na ugumu wa maisha ndoa zao zinaingilika kirahisi sana ; Je, ndao zao na watoto wao wanalindwaje dhidi ya wanaume na Wanawake Wazinzi wasiojali ndoa na hatima ya watoto wa wenzao? Ni kweli kuwa Kwa Sasa suala la kuchepuka Kwa Wanawake limekua kama mashindano Kati ya walioko kwenye ndoa na walioko nje ya Ndoa. Wanawake wanahujumiana wenyewe Kwa wenyewe.

Yani tamaa imeongezeka sana kutokana na mitandao mtu yupo Mwanza anamtongoza Mwanamke aliyeko Dar es salaam kirahisi sana . Hali hii ni janga kubwa sana siku zinavyoendelea Kwa sababu hakuna Tena heshima ya Ndoa . Ndoa inaonekana kama ndoano na Wazinzi wanafanya makusudi kuzini na waume na wake za watu ili kuzidi kuvuruga ndoa na kuwafanya wanaume na Wanawake wawe wa kila mtu bila utaratibu.
Ikitokea Ugonjwa wa kuambikiza kama ilivyokuwa AIDS miaka ya 1980 kuelekea 1990 mpaka 2020 Watanzania wataisha.

Sasa hivi hata biashara ya Kondom Haina soko Tena mana virusi vimshafubaa na hakuna wagonjwa Tena. Woga haupo Tena hasa Kwa wanandoa ndio Hali ni mbaya zaidi. Hata hivyo vifo vimegeukia vya kuuana badala ya magonjwa Sasa ni kuuna Kwa kukataa mapanga na kumwagiana maji ya moto na risasi.

Watawala walioko juu na wanasiasa waliangalie jambo hili la Wana ndoa kuuana Kwa jicho la tatu. Hali ni mbaya kwenye ndoa nyingi. Wanaume wengi Kwa Sasa wanaugulia ndani hasa wa kipato Cha chini na Vijana .
Siku hizi hakuna kijana asiye na pesa anayeweza kuwa na mchumba mrembo na wakafikia ndoa. Hata wakiona wanaishia kuuana. Yote ni Kwa sababu hakuna SHERIA Kali ya kulinda kizazi Cha kesho na maadili.
Hivi Hawa wa maisha ya chini hasa wa kiume Watakuja kuwa na familia yenye mama,baba na watoto kama serikali itaendelea kukaa kimya kwenye hili tatizo la wanandoa kuuana?

SHERIA ya Sasa ya Ndoa imebaki kuwalinda Wazinzi wenye pesa huku maskini wakiishia makaburini au gerezani au kuishi na stress na kufa kabla ya wakati. Mzinzi Mwenye pesa anaweza akamchukua mke wa mtu bila woga mana anajua hata akifumaniwa hakuna SHERIA Kali ya kumbana zaidi ya kesi ya madai ambayo maskini hawezi kuifungua. Lakini pia akipewa vitisho anatoa pesa nyingi na kitakatisha fumanizi lake.

Maskini mzinzi akifumaniwa anauawa au kulawitiwa mana Hana Cha kulipa. Hapa maskini ndiye anayeumizwa na SHERIA hii ya Ndoa ambayo inatoa fursa Kwa Wazinzi wenye fedha kujitwalia Wanawake mpaka kwenye ndoa za watu. Maskini anapoona anaporwa mpaka mke wake au mume wake ambaye kwenye kiapo Chao Cha ndoa aliapo kuwa faraja kwake basi anaamua kuua. Hapo hakuna namna mana Hana wa kumkimbilia ili apate msaada wa kulipiwa kisasi chake . Kazi ya serikali ni kulipa kisasi badala ya mdhulumiwa Vinginevyo mdhulumiwa analipa Mwenyewe.

Serikali inawatupia mzigo viongozi wa kidini kuwa watoe Elimu ya kiroho zaidi lakini ukweli ni kwamba nao pia ni ama ni wahanga au vikwazo kutokana na ukweli kuwa wapo pia viongozi wa dini Wazinzi wanaovuruga ndoa za watu.
Wanafanya makusudi mana hakuna SHERIA Kali ya kulinda ndoa za watu.

NINI CHA KUFANYA:-
Ni wakati Sasa wa kubadili SHERIA ya Ndoa ili Suala la Kuzini na Mke au mume wa mtu liwe ni jinai Moja Kwa Moja hasa inapotokea Kuna ushahidi wa kutosha. Yaani pawe na ufuatilliaji mpaka wa kimtandaoa mana mitandao inetumika sana kwenye kuvuruga ndoa za watu. Iwe suala la kushea simu Kwa wanandoa wenye ndoa ya mke mmoja liwe ni wazi au kukubaliana lakini iwe ni haki ya Mwana ndoa ya mke mmoja kuomba kufuatilia mienendo ya mwenza wake na kufungua kesi ya Jinai ili kumbaini anayevuruga ndoa yake na kufikshwa mahakamani na kupewa kifungo.

Lengo ni kulinda ndoa maana mtu anapoamua kuoa mke mmoja na mume mmoja basi amefanya hivyo Kwa taratibu za kisheria ili awe na familia yenye ustawi. Sasa tukiwaachia watu wakae bila kubanwa na SHERIA Hakika miaka ishirini ijayo ndoa za mashoga zitakua nyingi sana mana watoto wengi watakosa Bora. Lakini pia kuwaacha watu wenye stress na vinyongo kwenye jamii ni hatari Kwa amani ya nchi.

Mtu ambaye alikua anampenda mke wake au mume wake halafu ghafla akajikuta ameachana na mke wake au mume wake Kwa sababu TU Kuna Mzinzi mmoja mwenye pesa au anayejifanya yeye ni kidume au kipisi kali Cha kutembea na wake au waume za watu, rahisi Sana mtu kama huyo kufanya tukio baya au uhalifu mbaya .
Hata ugaidi hua mara nyingi unatokana na masuala ya Ndoa. Ukiangalia mfano suala la mahakama ya Kadhi nchini Tanzania lilikua hasa linalenga masuala ya Ndoa.

Waliponyimwa paliibuka chuki za chini Kwa chini na hata kuibuka Kwa vitendo vya kigaidi. Kijana mfano alikua na mchumba wake mzuri halafu anatokea Mzee wa miaka 60 mwenye pesa na mke wake na watoto na wajukuu anakuja anamrubuni mchumba wa huyo kijana na kusababisha kijana anashidwa kumuoa Tena. Bila shaka kijana huyo anakua na hasira na kinyongo na Hana pa kwenda ili kisasi chake kilipwe badala yake anaambiwa aende akafungue kesi madia mahakamani ili alipwe fidia. Fidia ya Nini wakati shida yake sio pesa ni mke? Kijana kama huyu ni rahisi kulipa kisasi au kuwa na roho mbaya na hata kujiunga na ugaidi.

Hata utendaji kwenye maofisi ya umma unashuka Kwa sababu ya migogoro ya Ndoa. Watu wanaingia kazini na stress wanashindwa kutoa huduma nzuri.

Watu wanafanya ufisadi ili wawe na fedha nyingi mana wanajua ndoa za watu maskini Kwa Sasa hazina Tena uaminifu na uvumilivu. Wamama wanakopa vikoba pesa wanahonga Vijana matokeo yake Wanabaki na madeni.

Kwa Wanasiasa wenye migogoro ya Ndoa wanaweza kuhamasisha maandamano yaliyojaa chuki na hata kuvuruga amani ya nchi.

Serikali ije na MUSWADA WA kurekebisha SHERIA ya Ndoa ili hata waislam wenye wake wanne wote watambulike kwenye haki zao Kwa watumishi wa umma.

Mtu yeyote mwenye ndoa ya mke mmoja akifumaniwa na au akivuriga ndoa ya mtu afungwe gerezani.
Mwenye ndoa ya wake wengi pia akifumaniwa afungwe gerezani na faini juu mana alikua na fursa ya kuoa mke Mwingine ili kukidhi tamaa zake. Ifikie mahali tujenge jamii iliyostarabika sio kuuana Kwa sababu ya kuishi kama nguruwe na mbwa na Kuku. Hii itarudisha heshima ya Ndoa na kulinda watoto na pia kupunguza mauaji. Na pia itahamasisha Vijana kuoa na kuolewa mana watakosa urahisi wanaoupata ngono kama ilivyo Sasa. Kijana au Binti atajua akitembea na mume au mke wa mtu kifungo kinamsubiri.

Lakini pia suala la kupima DNA Kwa wanandoa wapya liwe ni lazima mana watoto wengi wanaozaliwa sio wa baba wa kwenye ndoa na wamezaliwa sio Kwa sababu ya kukosa uzazi Bali kwa sababu ya kuchepuka na wengine kuapa kuwapa michepuko yao zawadi ya kumzalia mtoto. Hii ni hatari hasa mwanaume anapojua anawaza jinsi Nmanavyohangaika na maisha kumbe baadhi ya watoto sio wake.
Hapa kuzaa nje ya Ndoa libaki kama makubaliano au asiyeweza kukaa na mwenza asiyezaa basi aombe Talaka au wakapandikize mtoto Kwa kuridhiana sio kusalitiana.

Kwa upande wa Viongozi wa dini waache mahubiri ya kugemea upande mmoja na kusema kuwa wanaume ndio wanaochepuka , Hali inayowafanya Wanawake kuona kuwa wao hawaonekani na hivyo wanaendelea kuchepuka kwa kujificha na wakiona wanabainika wanajificha kwenye mgongo wa viongozi wa dini wakati ukweli ni kwamba Wana ndoa wa kike na kiume ndio wanaoongoza kuchepuka.

Lakini pia serikali iangalie zaidi SHERIA zinazoruhusu ndoa ya wake wengi ipewe kipao mbele mana inaonekana kuwa Wanawake wapenda kuchangia wanaume ndio maana wengi wanapenda waume za watu.
Na wanaume wengi HAWAWEZI kuwa na mke mmoja hivyo waoe wake wengi sio kuvuruga ndoa za watu.

Haiwezekani mwizi aibe Kuku wa Kienyeji anayeishi Kwa kula mchwa maporini na majalani na Hana gharama yoyote lakini akiibiwa basi mwizi anafungwa miaka sana lakini mtu anaingia na kuiba mke au mume wa mtu anayemgharamikia kuanzia mahari na matunzo na kulea watoto halafu eti iwe ni kesi ya madai TU au mtu avumilie TU. Lakini akimkuta maskini anaiba mbuzi wake anaweza kumpigia mshale au kumpeleka Polisi na akafungwa miaka sana. Kuku mmoja Tena kutokana na umaskini TU haiwezi kuwa ni kosa kubwa kuliko kutenganisha mtu na familia yake na kuacha watoto WAKITESEKA. Wote Hawa ni Wahalifu mana wanavunja ustawi wa jamii na kuleta chuki kwenye jamii.

Serikali na Bunge wasipochukua hatua Kwa sababu tu wao hawaguswi sana kadhia hii ya kuachiwa watoto yatima kutokana na mauaji ya wivu wa mapenzi wajue ipo siku Watajua kuwa walitunga SHERIA ya Ndoa ya mazingira ya Ulaya bila kuangalia mazingira ya kiafrika.
Vikivunjwa hivi yote hayo yata Kwisha 1,HAKISAWA 2,DAWATI LA JINSIA NA WTOTO 3,maswala ya kesi za ndoa yarudi kwa viongozi wa dini na family so polisi Tena wala mahakaman
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,889
7,114
Wewe unazungumzia mambo ya maovu, wazini na ndoa huku umeegemea kwenye dini. Huwezi kuwa objective!
Asili ya SHERIA zote ni dini na Mila za watu . Lakini Bunge hua linatunga SHERIA pale wanapoona uhalifu Fulani unakithiri. Mfano Ugaidi kidini ugaidi sio kosa lakini Mabunge yametunga SHERIA za dharura kudhibiti ugaidi.
Kwa Sasa Kuna mauaji Mengi sana na watu wanaugulia sana mioyoni mwao Kwa sababu ya masuala ya Ndoa . Je, jamii iendelee kuwapa unafuu wale wanaohamasisha na kufanya uzinzi na kuvuruga ndoa za watu hasa wanyonge ambao hawana power ya kuingia kwenye ndoa za watu wengine . Je, jamii inalinda Vipi watoto waliozaliwa kwenye ndoa pasipo wa kurudhia halafu anatokea TU mtu anajifanya ni mjanja na kuharibu ndoa ya mtu halafu anaambiwa hakuna SHERIA ? Je, anayeona ameumizwa nani wa kulipa kisasi chake? Hivi ni sawa Kwa mtu aliyeiba Kuku wa Kienyeji ambaye Hana gharama yoyote kufungwa miaka Saba halafu kumwacha mtu anayeingia na kuvuruga ndoa ya mtu anayehangaika kulea familia yake Kwa mamilioni ya pesa huku akiwa na ndoa na amelipa mahari ya ng'ombe mpaka 50. Yani mke wake avurugwe TU Kwa vishawishi na utapeli kama ulivyoutapeli mwingene . Nani analipa kisasi Cha huyu mtendewa ? Bila shaka serikali isipobeba Jukumu la kuweka mazingira ya mtu kwenda kushtaki na mtu kukamatwa na kuwekwa ndani na kesi kusikilizwa upelelezi kufanyika kujua chanzo Cha hayo na mwanye kuvuruga akafahami na kufungwa basi ni wazi kuwa kisasi kitakua ni juu ya mtendewa Mwenyewe. Huwezi kujenga maadili kwenye jamii bila kudili na suala la familia. Pakiwa na jinai kwenye masuala ya Ndoa ni wazi kuwa hata wale wanaume wanaotelekeza familia zao watapungua. Na Vijana wengi wataoa na wasichana wengi wataolewa na ndoa nyingi zitadumu . Na jamii itakua na amani sana na uwajibikaji utaongezeka makazini. Wafanyakazi wengi wakiwa maofisini ni stori za ngono TU na simu za mapenzi na ulevi hakuna kazi Wala ubunifu. Watu wanaosubiri muda wa lunch waanze Kupiga mizinga na offer Kwa malipo ya ngono.
Vyuo hakuna wahitimu Wanawake wenye uwezo ni digrii za ngono.Ni wachache sana wanaobahatika kumaliza bila kuwekewa vikwazo na Wahadhiri ili TU wakubali kutoa miili yao wafaulishwe kwanye mitihani.

Na Wahadhiri wanofanya hivyo wengi wako kwenye ndoa . Wanawahujumu watoto wa wenzao Kwa tamaa zao na kuzalisha wasomi wapumbavu ambao nao wakifika maofisini wanawenga mbele rushwa za ngono. Where are we going as a Nation?
Kwenye siasa ni hivyo hivyo !!
Kila mahali ni tabia chafu za kuzalisha jamii isiyo na maadili Wala mipaka katika masuala ya Ndoa.
 
Inawezekana una pointi, nakuja tujadili.
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom