Tuseme ukweli: Wanawake wengi huwa wanatamani Sherehe na sio Maisha ya Ndoa

Nimejaribu kufatilia sana mijadala ya wanawake kuhusiana na mtazamo wao juu ya kuolewa kwanza nimegundua kila mwanamke anatamani sio tu kuolewa bali pia afanye sherehe ambayo atauonyesha ulimwengu kwamba Na yeye amepata wa kumheshimisha na kumchukua kama mke.
Ha ha ha ha 🤣

Umepiga kwenye uvimbe wa JINO....
 
Hii thread itageuka na kuwa kama ile ya "kutafuna vibint vidogo" kuna watu walicomment mule mpaka wengne wakaripot kwa admin. Wadada waliitwa wapigania uhuru mara wahenga mara wana matumbo makubwa yaaaaniii
 
Ndoa ni muunganiko kati ya mwanamume na mwanamke, walio amua kwa ridhaa yao wenyewe kuishi pamoja kama mke na Mume.

Harusi ni sherehe kwa ajili ya kufunga ndoa.
Aisee tuna bahati mbaya sana na wanawake wa leo mkuu
 
Mkuu yani leo asubuhi nilikua napiga story na dada fulani, kwa bahati mbaya leo hajahudhuria harusi kanisani kwao basi anajilaumu kwelikweli. Anasema anapenda kuona jinsi watu wanafanya sherehe na yeye anatamani mno.

Nikamuuliza vipi huwazi kuhusu maisha ya ndoa, aisee huwezi amini aliapia kabisa kua ye hayo ya ndani hayawazi ye anataka kvishwa pete mbele ya umati na sherehe kubwa, mengine mbele kwa mbele uko.
Aiseee
 
😲🤣
 
Ameeeen, nashukuru Jah akanikutanishaa na mtu sahihi kwangu, nikachukuliwa mazima.
Napambana na maisha ya ndoa now.

Hongera sana..watu wengi wakipata chance ya kuoa tena ama kuolewa tena..mke ama mume wangebadilisha
 
Back
Top Bottom