NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
Madhara ya sigara:
Ocean road pale hospitali ya cancer wapo wagonjwa wengi wenye kansa ya mapafu, fizi, koo, n.k. kwasababu ya matumizi ya muda mrefu ya sigara. Cancer inaharibu koo kiasi kwamba wengine wamechomolewa makoo wanaongea kwa kuwekewa mashine, sauti inatoka kwenye spika
Watu zaidi ya elfu moja wanakufa kwasababu ya sigara kila siku
Madhara ya Pombe.
Hii ndio ina madhara makubwa zaidi, takribani watu milioni 3 hufa kwa jili ya pombe kila mwaka aidha kwa magonjwa inayosababisha, ajali, n.k.
- Huchochea uzinzi (huwa inashuka chini)
- Ugomvi - hupunguza uwezo wa kucontroll hasira.
- Kutukana matusi - Mdomo utasema unachotaka
- addiction / uraibu
- imefanya wengi kufukuzwa kazini hadi mawaziri
- Kuzima
- Kutembea kwa kupepesuka bila balance
- kujisaidia hadharani
- Maumivu ya kichwa
Bangi:
-Haisababishi kansa yoyote, Inatibu kansa.
-Haitoi umakini wa kazi kama ilivyo kwa Pombe mtu akiitumia anavuruga kazi hata iwe ya kuhutubia tu.
-Ina addiction ndogo na ni rahisi kuacha ukitaka kuacha, sio kama pombe na sigara,
- Hakuna vifo vinavyosababishwa na bangi kwa magonjwa
Ni kwanini baadhi ya watumiaji wa Bangi wa Tanzania wanapatwa na madhara kiakili tofauti na nchi zingine, kwanini iwe Tanzania na sio kwengine ?
Elimu ndio ufunguo wa kuweza kuyaishi haya maisha, ukitumia kitu bila kuwa na elimu nacho utapatwa na madhara, nikiri wazi kwamba watumiaji wengi wa kilevi hiki wanakurupuka kukitumia bila kujua chochote zaidi ya kuiga na matokeo yake Bangi huonekana mbaya.
- Watu hutumia bangi ambayo maua yake bado hayajakomaa vizuri na wao hawajui kutambua.
-Kinachovutwa ni maua tu, watu huvuta mpaka majani, vijiti na mbegu na kupata madhara zaidi.
-matumiz ya bangi iliyovunwa ikiwa bado mbichi
-Matumizi ya bangi ambayo baada ya kuvunwa haijaoshwa wala kukaushwa vizuri
-Bangi za mtaani kwa kiasi kikubwa zimechanganywa na sumu za panya na madawa ya kulevya.