ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,116
- 49,840
Hayo yameelezwa na Dr.Japhet Swali wa Hospital ya Taifa ya Magonjwa ya Akili-Mirembe.
Kwamba pombe Haina tofauti na Madawa ya kulevya kama bangi,coceine,heroine,mirungi nk hivyo kuhatarisha Afya ya Akili kwani inatenda Yale Yale ambayo Madawa ya kulevya hufanya.
---
Kama wewe ni mnywaji wa pombe, sasa kaa mkao wa tahadhari!
Kama hukuwa unajua hili, leo ndio siku yako ya kubaini kuwa kinywaji unachokunywa ni sawa na dawa yoyote ile ya kulevya.
Kwa mujibu wa mtaalamu bingwa wa saikolojia na afya ya akili kutoka Hospitali ya Afya ya Akili Mirembe, Dk Japheth Swai, kinachoifanya pombe iwe sehemu ya kundi hilo ni tabia zake inapotumika katika mwili wa binadamu.
"Pombe inalevya, pombe inafubaza, pombe inakujengea uraibu na pombe inakufanya ufanye kitu kinyume na uhalisia wako, inakupa ujasiri wa uongo, hivi ni vitu vinavyofanywa na dawa za kulevya,’’ anasema na kuongeza:
“Dawa ya kulevya ni dawa yoyote utakayoitumia ikakufanya uwe katika hali ya ulevi au kufanya ubongo wako usifanye kazi kama ilivyo kawaida,” anasema.
Hata hivyo, mtaalamu huyo anasema hatari ya pombe ni kubwa zaidi ukilinganisha na dawa nyingine za kulevya.
Hilo linatokana na kile anachofafanua kuwa pombe ndiyo mlango wa matumizi ya dawa nyingine zote za kulevya.
Chanzo: Mwananchi
My Take
Serikali pigeni marufuku pombe 😂😂