FDA imependekeza bangi kuorodheshwa upya kama dawa yenye kiwango cha chini cha madhara

mofayah

New Member
Dec 6, 2013
2
3
MAMLAKA ya Kusimamia Vyakula na Dawa (FDA) imependekeza bangi kuorodheshwa upya kama dawa yenye kiwango cha chini cha madhara.

Hii ni baada ya wanasayansi kubaini kwamba bangi ina uwezo wa chini kutumiwa vibaya ikilinganishwa na dawa zingine za kulevya kama vile heroni.

Utafiti huo wa FDA, kamili kwa Kiingereza kama Food and Drug Administration, pia ulionyesha kuwa bangi ina kiwango cha chini kusababisha uzoefu kwa watumiaji wake.

FDA ni shirika lililoko chini ya Wizara ya Afya na Huduma kwa Binadamu, nchini Amerika.

Kwa sasa bangi imeorodheshwa kama dawa ya Kitengo cha Kwanza kinachosheheni dawa zenye kiwango cha juu zaidi cha kutumiwa vibaya na uwezo wa kusababisha watumiaji wake kushindwa kujitegemea kisaikolojia, au kimwili.

Watafiti hao wanataka bangi iwekwe katika Kitengo cha Tatu kinachosheheni uzoefu wa wastani hadi wa chini kimwili na kisaikolojia.

Mifano ya dawa za Kiwango cha Tatu ni: bidhaa zenye miligramu chini ya 90 kama vile Codeine kwa kila kipimo (Tylenol na Codeine), Ketamine, Steroids za Anabolic, na Testosterone.

Utafiti wa FDA pia umeainisha kiwango cha usaidizi wa Kisayansi bangi kutumika kwa minajili ya matibabu katika hospitali na kliniki kadha Amerika.

Aidha, bangi inaaminika kupunguza maumivu, kukabiliana na kero ya kutapika na kichefuchefu kinachotokana na matibabu ya Saratani – Chemotherapy, kulingana na watafiti.

Umauzi wa ikiwa bangi itaorodheshwa katika Kiwango cha Tatu, unasalia mikononi mwa Halmashauri ya Kimikakati Inayoshughulikia Masuala ya Dawa, ndiy Drug Enforcement Administration (DEA).
Nchini Kenya, bangi ni miongoni mwa dawa za kulevya zilizopigwa marufuku; kupandwa, kuuzwa na kutumika.

https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/wataalamu-wasema-bangi-haina-madhara
 
BANGI HIi hii tunayofahamu inayotia vijana wetu wehu?au lingine
Bangi ikitumika inavyotakiwa (Usipoivuta/isitumike kama sigara) ni moja kati ya mimea yenye manufaa makubwa kimwili - ni Tiba kwa maradhi mengi.
 
Haya sasa, mliokuwa mnauponda mmea kiko wapi ?

FxuhxAkWAAYWMvL.jpg
 
Vichaa waliopo mijini 90% wanatokana na matumizi ya bangi. Wafungwa Walio magereza 95% ama wamefunga kwa bangi au makosa waliyoyatenda walipata dutch courage baada ya kuvuta bangi.

Usikubali ndugu yako avute hilo dude atakuwa ANAFANYA mambo ya hovyo mpaka anazeeka atajiona bado msela kijana tuu kwa matendo na lugha
 
Vichaa waliopo mijini 90% wanatokana na matumizi ya bangi. Wafungwa Walio magereza 95% ama wamefunga kwa bangi au makosa waliyoyatenda walipata dutch courage baada ya kuvuta bangi. Usikubali ndugu yako avute hilo dude atakuwa ANAFANYA mambo ya hovyo mpaka anazeeka atajiona bado msela kijana tuu kwa matendo na lugha
 
Mateso yakizidi ukombozi unakaribia,tumenyanyasika mno..ifike pahala bangi iwe legalize
 
BANGI HIi hii tunayofahamu inayotia vijana wetu wehu? Au lingine

Shida inakuja pale inapotumika vibaya. Lakini ikitumika kiustaarabu na kwa utaratibu, ina faida lukuki kuliko madhara.
Chukulia mfano wa petrol au gundi, vijana wengi wameweuka kwa sababu ya matumizi yasiyo kubalika ya vitu hivyo. Lakini je pale inapotumika kwa utaratibu mzuri, si ndiyo faida tunaona kuwa ni kubwa kuliko kuliko hasara? Tafakari chukua hatua.
 
Back
Top Bottom