Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Na Mwandishi wetu

Dodoma

IMG-20240220-WA0020.jpg

Serikali kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imesema imepata mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya ambapo kuanzia mwezi Januari hadi Disemba 2023 kilogramu zaidi ya milioni moja za aina mbalimbali za dawa za kulevya zilikamatwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati akizungumza na waandishi wa habari tarehe 20 Februari 2024 Jijini Dodoma kuhusu taarifa ya mafanikio ya Serikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya .

Mhe. Jenista alisema Watuhumiwa 10,522 walikamatwa ambao kati yao wanaume ni 9,701 na wanawake ni 821 huku akisema kuwa jumla ya hekari 2,924 za mashamba ya bangi na mirungi ziliteketezwa.

“Kiasi cha dawa zilizokamatwa kwa mwaka mmoja ni zaidi ya mara tatu ya dawa za kulevya zilizokamatwa kwa kipindi cha miaka 11 hapa nchini, kwani miaka 11 iliyopita tulifanikiwa kukamata kilogramu 660,465 pekee. Aidha, Serikali imefanikiwa kuzuia uingizaji wa kilogramu 157,738.55 za kemikali bashirifu ambazo zingeweza kutumika kutengenezea dawa za kulevya kinyume cha sheria,” Alisema Mhe. Jenista.

Waziri Jenista amesema mafanikio ya ukamataji huu yanatokana na nia, utashi na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan. “Mara baada ya kuingia madarakani ameonesha dhamira yake kwa vitendo katika kuiimarisha Mamlaka kwa kuipa vitendea kazi vinavyohusianisha teknolojia ya kisasa ya kimkakati katika mapambano, kutoa mafunzo kwa watumishi ndani na nje ya nchi pamoja na uzalendo wa watendaji kwenye Mamlaka”.

Pia aliongeza kwamba Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa lengo la kutoa elimu ya dawa za kulevya na rushwa kupitia klabu za kupinga rushwa nchini ambapo sasa zitaitwa klabu za kupinga rushwa na dawa za kulevya.

“Tafiti zinaonesha kwamba, matumizi ya dawa yanaanza katika umri mdogo kati ya miaka 10 na 12 hivyo Serikali imeona iweke mkazo huko kwani watoto wengi wanapitia katika shule hizo na elimu imeendelea kutolewa katika makundi ya kijamii yakiwemo ya viongozi wa dini, viongozi wa kimila, waandishi wa habari, vyombo vya ulinzi na usalama, maafisa forodha na wakulima hasa katika maeneo yaliyokithiri kwa kilimo cha bangi na mirungi,”Alieleza.

Aidha alifafanua kwamba Serikali imeendelea kuimarisha huduma kwa kuongeza vituo vya kutolea tiba kwa waraibu kwa kutumia dawa na huduma za unasihi (MAT) ambapo kwa mwaka 2023 kituo kimoja kilifunguliwa mkoani Morogoro katika gereza la kihonda ambapo hadi kufikia mwezi Disemba 2023, jumla ya vituo 16 vilikuwa vinatoa huduma kwa walengwa.

“Vituo vingine viwili katika wilaya ya Muheza – Tanga na Chalinze - Pwani vinatarajia kukamilika ifikapo mwezi Aprili, 2024. Vituo vingine vitatu vitaanza kujengwa katika mikoa ya Shinyanga, Kilimanjaro na Pwani (Mkuranga). Aidha, serikali iko kwenye hatua za mwisho za ujenzi wa kituo kikubwa cha huduma za Tiba na utengamao (Rehabilitation centre) katika jiji la Dodoma,”Alibainisha Mhe. Jenista.

Kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Nchi zingine alisema kuwa Tanzania imekuwa ikishirikiana na nchi mbalimbali kikanda na kimataifa katika kupambana na dawa za kulevya ambao unahusisha kubadilishana taarifa za kiusalama kuhusu dawa kulevya, na kujengeana uwezo katika mapambano hayo.
“Hivi karibuni tumesaini hati ya makubaliano kati ya Tanzania na Zambia kushirikiana kudhibiti biashara ya dawa za kulevya.

Baadhi ya faida zilizotokana na ushirikiano huu ni kufanikisha ukamataji wa baadhi ya watuhumiwa wanaohusishwa na kilo 3,522. 52 za dawa za kulevya aina ya heroin na methamphetamine zilizokamatwa mwezi Disemba, 2023 pamoja na ukamataji wa kilo 423.54 za skanka ulitokana na ushirikiano mzuri kati yetu na Zambia,”Alifafanua.

Aidha alihitimisha kwa kueleza kuwa Serikali itaendelea kuiwezesha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya hususani katika uboreshaji wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ili kuongeza kasi ya mapambano na hatimaye kumaliza tatizo la dawa za kulevya nchini.

==============For English Audience Only===========
Achievements in the Fight Against Drug Abuse in Tanzania

The Tanzanian government, through the Drug Control and Enforcement Authority, has announced substantial success in the battle against drug abuse. From January to December 2023, over one million kilograms of various narcotics were seized across the country.

Jenista Mhagama, the Minister of State in the Prime Minister's Office for Policy, Parliament, and Coordination, shared these accomplishments during a press briefing in Dodoma. She reported that 10,522 suspects were apprehended, consisting of 9,701 males and 821 females. Additionally, a total of 2,924 hectares of cannabis and khat farms were destroyed.

"Over the past year, the amount of confiscated drugs has been more than three times the quantity seized in the past 11 years in our country. Eleven years ago, we successfully seized only 660,465 kilograms. The government has also prevented the importation of 157,738.55 kilograms of precursor chemicals that could have been used to produce illegal drugs," stated Minister Jenista.

She attributed these achievements to the determination and commitment of President Samia Suluhu Hassan, emphasizing that since taking office, President Hassan has demonstrated a strong resolve to strengthen the authority. This includes providing modern technological tools for strategic enforcement, offering training to both local and international personnel, and fostering patriotism among the authority's staff.

The government's decisive actions in the fight against drug abuse reflect a commitment to safeguarding public health and ensuring the well-being of Tanzanian citizens.
 
Serikali kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imesema imepata mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya ambapo kuanzia mwezi January hadi December 2023 kilogramu zaidi ya milioni moja za aina mbalimbali za dawa za kulevya zimekamatwa katika maeneo mbalimbali Nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama amesema hayo Jijini Dodoma leo wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Serikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya .

Jenista amesema Watuhumiwa 10,522 wamekamatwa ambao kati yao Wanaume ni 9,701 na Wanawake ni 821 huku akisema jumla ya hekari 2,924 za mashamba ya bangi na mirungi ziliteketezwa.

“Kiasi cha dawa zilizokamatwa kwa mwaka mmoja ni zaidi ya mara tatu ya dawa za kulevya zilizokamatwa kwa kipindi cha miaka 11 hapa nchini, kwani miaka 11 iliyopita tulifanikiwa kukamata kilogramu 660,465 pekee, Serikali imefanikiwa kuzuia uingizaji wa kilogramu 157,738.55 za kemikali bashirifu ambazo zingeweza kutumika kutengenezea dawa za kulevya kinyume cha sheria”

Waziri Jenista amesema mafanikio ya ukamataji huu yanatokana na nia, utashi na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan “Mara baada ya kuingia madarakani ameonesha dhamira yake kwa vitendo katika kuiimarisha Mamlaka kwa kuipa vitendea kazi vinavyohusianisha teknolojia ya kisasa ya kimkakati katika mapambano, kutoa mafunzo kwa watumishi ndani na nje ya nchi pamoja na uzalendo wa Watendaji kwenye Mamlaka”

Source: Millard Ayo
 
Ile kesi iliishia wapi?. Maana walianza kwa mbwembwe mwisho kukawa na ukimya.
 

WAZIRI MHAGAMA: MWAKA 2023 WATUHUMIWA 10,522 WA DAWA ZA KULEVYA WAMEKAMATWA

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Jenista Mhagama amesema kwa mwaka 2023, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanikiwa kuwakamatat watuhumiwa 10,522 ambao kati yao wanaume ni 9,701 na wanawake ni 821 walikamatwa kuhusika na dawa hizo, na jumla ya hekari 2,924 za mashamba ya bangi na mirungi ziliteketezwa.

"Serikali kupitia Mamlaka ya Kudhibiti Kupambana na Dawa za Kulevya imepata mafanikio makubwa ambapo kuanzia mwezi Januari hadi Disemba 2023 kilogramu 1,965,340.52 za aina mbalimbali za dawa za kulevya zilikamatwa katika maeneo mbalimbali nchini" alisema.

Mhagama ameyasema hayo leo February 20,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma juu ya Mafanikio ya Serikali katika Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya kwa mwaka 2023.

Amesema Kiasi cha dawa za kulevya kilichokamatwa katika kipindi cha mwaka mmoja pekee ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa hapa nchini kwani kinazidi kiasi cha kilogramu 660,465 zilichokamatwa katika kipindi cha miaka 11.

"Serikali imefanikiwa kuzuia uingizaji wa kilogramu 157,738.55 za kemikali bashirifu ambazo zingeweza kutumika kutengenezea dawa za kulevya kinyume cha sheria" alisema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama amesema tafiti zinaonesha kwamba, matumizi ya dawa yanaanza katika umri mdogo kati ya miaka 10 na 12. hivyo, Serikali imeona iweke mkazo huko kwani watoto wengi wanapitia katika shule hizo. Pia, elimu imeendelea kutolewa kwenye makundi mbalimbali ya kijamii yakiwemo ya viongozi wa dini, viongozi wa kimila, waandishi wa habari, vyombo vya ulinzi na usalama nk.

Kwa upande mwingine, Mhagama amesema Serikali imeendelea kuimarisha huduma kwa kuongeza vituo vya kutolea tiba kwa waraibu kwa kutumia dawa na huduma za unasihi (MAT) ambapo kwa mwaka 2023 kituo kimoja kimefunguliwa mkoani Morogoro katika gereza la kihonda ambapo hadi kufikia mwezi Disemba 2023, jumla ya vituo 16 vilikuwa vinatoa huduma kwa walengwa.
 

Attachments

  • GGx5L89W0AAxAP9.jpg
    GGx5L89W0AAxAP9.jpg
    147.5 KB · Views: 1
  • GGx4GzDXEAAosBm.jpg
    GGx4GzDXEAAosBm.jpg
    89 KB · Views: 1
  • GGx6LFDWoAAPpZP.jpg
    GGx6LFDWoAAPpZP.jpg
    145 KB · Views: 1
  • GGx6UNRWkAAvq3x.jpg
    GGx6UNRWkAAvq3x.jpg
    111.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom