Tuongee Kifamilia leo, kama unataka kuoa au kuolewa na mna imani za dini tofauti jitafakari upya

Mm Nilkua naona tu Mkristo aoe/aoelewe na Mkristo na vice versa, wanaume n wengi kila dini pia wanawake n wengi kila dini tusifanye maisha kuwa magumu.
 
Kwa watu wasio wasomi, wenye Elimu ya chini, wasio na exposure, au upeo mkubwa wa uelewa, mambo ya ndoa na tofauti za dini, huwapa shida sana.

Mke wa Khasim Majaliwa, PM wa sasa ni mkristo na hakuna shida, mkuu wa mkoa wa zamani wa Kagera, Abdulaman Babu, alikuwa Mkristo, jamaa alikua anamleta kanisani kila Jumapili, wewe unaoa mtu sio dini, kwanza Kuna unafki mwingi sana, unakuta wote ni dini moja, lakini mnamaliza hata mwaka bila kwenda kanisani au masjid, sasa dini ya nini.

Kila mtu aabudu kivyake, ubovu wa Waafrika, dini inapewa nafasi kubwa kwenye mausiano na familia!!
Uchumi ndio iwe kiapumbele, katika kutafuta pesa, hakuna dini, tafuta pesa saidia wasiojiweza huo ndio Uislam, Ukristo mzuri!! Sio unaaacha msichana mzuri kisa dini yake??!!!!

Natamani wazazi wa watu wote wangelijua hili
Ila upeo wa mambo kuhusu hili wengi wanakua hawana
Watu wanapoteza wanaume au wanawake wazuri ambao wangeweza kuvumiliana kisa dini
So hurtful.
 
Huo mtihani unawakuta familia nyingi sana tangu enzi na enzi ila hawajifunzi sababu ya mapenzi pale mwanzoni yakinoga,

Suluhu yake, Watoto wasomeshwe dini zote mbili, madrasa waende na sunday school waende, wakikua watachagua upande wenyewe hakuna haja ya kugombana wazazi.

Nimekuelewa sana
Ndio maana haya nambo weww huyataki
 
Back
Top Bottom