Tuongee Kifamilia leo, kama unataka kuoa au kuolewa na mna imani za dini tofauti jitafakari upya

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,593
93,311
Nitaandika kwa kifupi tu, kuna case nimeshindwa kuipa suluhu nimeitwa kuleta amani kwenye nyumba ya hawa wanandoa.

Wewe ni mwanamke muislamu olewa na mwislamu mwenzako, na kama wewe mwanaume ni Mkristo oa Mkristo mwenzako.

Issue ni ngumu, Mkristo kaowa mwanamke muislamu kipindi mahaba ndindindi, Sasa ndoa imejibu Watoto Wawili, mwanamke wote anadai ni Watoto wake na wote wanakwenda madrasa za kiislamu.

Sasa sitaki mada hii iwe ni mihadhara au jukwaa la kukashifu dini nyingine, nimeweka hii mada ili kutowa ushauri wa bure.

Ikiwa mwanamke na mwanaume mmekubaliana kuweka dini zenu pembeni na mfunge ndoa bomani basi jitahidini na swala la Watoto mkubaliane wakizaliwa wafuate imani gani au mgawane vipi urithi wa imani kwa Watoto na kwa hali ya Sasa muandikishiane kisheria ili lisilete tabu baadaye.

Nawapenda sana Mama zangu na Dada zangu lakini ukweli uko wazi wao ndio tatizo, wanaume huwa hawana ligi za kijinga.

Nimewashauri acheni Watoto wakiwa adult wachague imani wanayotaka ila mke wa ndoa anasema Watoto ni wake, ila kwenye kipengele cha school fees mke ndio anatambua kama Watoto wana baba.

Nimehairisha hii case namuomba Mungu anipe busara sijui muafaka utapatikana vipi? Inasikitisha sana Watoto wadogo kuwaharibu kisaikolojia kwa sababu ya kurithi dini za wakoloni.

Kwakweli mnaotegemea kuoa au kuolewa na watu wa dini tofauti msilipuuze hili muandikishiane kwa Wakili kama mlivyofunga mkataba wa ndoa Serikalini.

Wacha nipate kwanza lager zinipe hekima kulimaliza hili.
 
Huo mtihani unawakuta familia nyingi sana tangu enzi na enzi ila hawajifunzi sababu ya mapenzi pale mwanzoni yakinoga,

Suluhu yake, Watoto wasomeshwe dini zote mbili, madrasa waende na sunday school waende, wakikua watachagua upande wenyewe hakuna haja ya kugombana wazazi.
 
Umeonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye huu uzi. Ipo hivi, mume ndio kichwa cha familia na kama hivyo basi mke anapaswa afuatane ama aambatane na mume wake.

Yaani ndani ya nyumba mke na mume wanaweza wakajadiliana jambo, lakini mwisho wa siku mume ndio anabaki kuwa mtoa maamuzi ya mwisho.

Ingekuwa mimi ndio wewe ningewaambia mke afuate kile anachokisema mume, kama anaona ngumu basi ningewashauri waachane kwa amani tena kisheria/kwa maandishi
 
Barnaba amebadili dini na kuwa muislam.

Mara nyingi watoto hufauata dini ya mama ,maana muda mwingi mama ndiyo mlezi wa watoto hivyo atawajenga zaidi kwenye dini yake.
Kama ulifata dini ya mama yako ni uzembe wa baba yako,

Fatilia wanaume waliobadili dini kufata wanawake wanavyoonekana katika jamii
Anaeingia kwenye familia ya mwenzie ni ke, zamani hata ubini wa majina ya wanawake yalibadilika na kuwa ya waume zao,
Mfano mwingine

Me;Samweli
Ke;Grace

Ke ataitwa Mrs samweli kwanini isiwe Mrs Grace?
 
Back
Top Bottom