Masimango na kejeli kwa wanaoonekana wamechelewa kuoa/ kuolewa na kupata watoto uzeeni au umri ukiwa umekwenda

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,143
32,857
Habari za muda huu marafiki,

Siku za hivi karibuni kumekuwa na hali ya kushangaza kustaajabisha kwenye jamii yetu na hasa huku mitandaoni.

Kumekuwa na wimbi la watu kuwasimanga, kuwakejeli na hata kuwacheka ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu wanaoonekana kwa vigezo, mitazamo na viwango vilivyowekwa kwenye jamii kuwa wamechelewa kuoa au kuolewa hivyo kuonekana wamepata watoto wa uzeeni.

Ni jambo linaloonekana kama la kawaida lakini kwa upande mwingine linasononesha na kuvunja mioyo ya watu walioamua kujenga familia.

Ni kauli za kitoto zinazoonyesha kuwa bado hawajakomaa kiakili kwenye ulimwengu huu uliojaa harakati na purukushani za kila aina.

Ningependa kuchukua nafasi hii kuwakumbusha hao wenye kuwakejeli wengine kwenye hili ya kuwa.

1) Maisha ni fumbo zito Sana ambalo mara nyingi ni wachache Sana wenye kufumbua. Mara nyingi mipango yako inaweza ikapishana na mipango ya Mungu.

2) Uhai na kifo ni vyake Mungu mwenyewe kwani hakuna ajuaye kuwa amebakisha muda gani wa kuishi hapa duniani. Wapo vijana wengi wametangulia mbele za haki wakiacha watoto wao na familia zao zikiteseka na kuwaacha wazee wakiendelea kulea watoto wao wa uzeeni mpaka wakijitegemea na kufurahia matunda yao. Hivyo kusema kuwa mwanaao akifika miaka kadhaa wewe utakuwa umeshachoka au umeshakufa ni maneno ya kufuru au ya mtu asiye na Imani kwa mola wake mlezi.

3) Kwenye maisha kila mtu Mungu amemuwekea wakati wake wa kufanya jambo lake kwa rehema zake. Wapo watu waliowahi kuoa lakini Mungu akawanyima watoto mpaka wanazeeka na wengine wanawapata uzeeni kabisa. Wapo watu wamejikuta wapo jela wakitumikia vifungo virefu na mpaka wanatoka umri umekwenda na wanaamua kujenga familia. Wapo watu walikuwa wanaugua kwa muda mrefu na hatimaye wakapona na kuanzisha familia. Hivyo basi kama wewe umewahi ni sahihi kwako lakini haiwezi kuwa makosa kwa anayeonekana amechelewa.

4) Changamoto za kifamilia na vifo.
Kuna mwingine anawahi kuoa lakini Kati Kati ya safari anawapoteza mke na watoto wote kwa pamoja Kwa ajali au maladhi ya kawaida na anaamua kuoa na kuanzisha familia upyaaa.

Kwa kifupi mambo na changamoto za kidunia ni nyingi zinazopelekea watu kuonekana wamechelewa kupata watoto au kuoa na kuolewa. Tujifunze kuwa wastaarabu kwenye maisha ya watu kwani hatujui matamshi yetu yanawaathiri vipi wenzetu.

Niko tayari kusahihishwa.

Nawasilisha.
 
Unawazungumziaje wanaokosa familia kutokana na sababu hizi

1. Uzembe, dating for fun
2. Peer pressure, kufata mkumbo wa wasiooa bila kujiuliza kesho itakuwaje
3. Tamaa, kutaka mwenza asie wa levo yako na kuangalia vigezo feki kama shepu au maokoto
4. Kujiona mtoto kumbe umri umeenda
5. Kutokujitambua na kutowajibika
6. Utapeli wa mapenzi
7. Kununua ngono
 
Unawazungumziaje wanaokosa familia kutokana na sababu hizi
1. Uzembe, dating for fun
2. Peer pressure, kufata mkumbo wa wasiooa bila kujiuliza kesho itakuwaje
3. Tamaa, kutaka mwenza asie wa levo yako na kuangalia vigezo feki kama shepu au maokoto
4. Kujiona mtoto kumbe umri umeenda
5. Kutokujitambua na kutowajibika
6. Utapeli wa mapenzi
7. Kununua ngono
Yoyote yanawezekana kutafsirika kwa vyovyote kutokana na mazingira na upeo wa akili kwa nyakati hizi lakini zinapomrudia fikra sahihi za kuanzisha familia basi haipaswi kuwa ndio mlango wa kejeli na dharau kwa watu wa aina hiyo.

Kuna watu wanachelewa kupata mwanga kwenye maisha yao na wengine mpaka waangaziwe na wengine wanakuwa wanakosa muongozo wa kimaisha wa kujua njia ipi sahihi na ipi mbaya na kujiendesha kwa matakwa ya nafsi jambo ambalo linawapeleka kwenye upotevu.
 
Back
Top Bottom