Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,900
MWANAMKE LAZIMA ABADILI DINI NA IMANI ILI IFANANE NA YAKO NDIPO UMUOE.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Moja ya ishara za awali Kwa Mwanamke anayekupenda na anayeweza kuwa Mkeo ni kukuamini, na kuamini Kwa kile ukifanyacho na kile unachokiamini. Kwa Mwanamke Hisia na Imani vinaenda sambamba. Mwanamke akishakuwa na hisia za upendo na wewe hapo moja Kwa moja atakuwa na Imani na wewe. Atakuamini. Kila unachomwambia Mwanamke anakiamini. Weka akilini hiyo.
Mwanamke akikupenda, atapenda unayoyapenda. Mtazamo wake utabadilika utakuwa Sawa na wako. Ndio maana ni rahisi kumbadilisha Mwanamke hata kama alikuwa ni kahaba lakini akishakupenda atauacha ukahaba wake. Ishu hapo ni hivi, Kwenye Moyo WA Mwanamke kuna Hisia na Imani. Wakati Sisi wanaume Imani Ipo kwenye Ubongo. Yaani hatuwezi kuamini Jambo bila kulitafakari Kutumia ubongo Akili.
Wakati Wanawake hawawezi kukuamini Jambo pasipo kuwa na hisia nalo, yaani kulipenda.
Sasa ili Mwanamke apende Jambo kuna michakato kadha wa kadha. Na yote lazima itimize imagination zake.
Ukiona umemtongoza Mwanamke mkaingia kwenye mahusiano alafu mpaka mnamaliza miezi sita hajataka Kubadili Imani na dini, jua huyo hujamkamata, yaani hujauteka moyo wake. Huyo hakufai. Hakuna mahali mtaenda.
Tena akikuambia wewe ndio umfuate ndio kabisa. Sisi Watibeli na wataalamu WA hayo mambo tunajua kuwa huyo Mwanamke Hakupendi, lakini pia atakupelekesha tuu.
Kingine ni lazima utashindwa kwenye ishu ya malezi. Yaani Watoto lazima wakushinde Kwa sababu tayari ulimshindwa Mama Yao.
Kubaniwa papuchi na kupewa chakula cha Usiku Kwa vipimo litakuwa ni Jambo la kawaida kwako na hautakuwa na chakufanya. Kiufupi utakuwa Dume-jike ambalo limeoa.
Asije akakudanganya MTU kuwa ndoa ya MKE na Mume WA Imani tofauti zinadumu au zinakuwa na Amani, hakuna kitu kama hicho.
Kingine cha muhimu zaidi ni kuwaz kamwe usimwambie Mwanamke abadili dini ili UMUOE. Hilo ni kosa la kiufundi. Mwanamke akishakupenda hatasubiri umwambie abadili Dini. Atabadili mwenyewe tuu Kwa mapenzi na uelewa wake kuhusu dini yako.
Kama hataki Kubadili dini yake Kwa hiyari jua huyo moyo wake haukupendi. Na kamwe hatakutii wala kukusikiliza Ila wewe ndiye utamtii na kumsikiliza. Atakupelekesha vile atakavyo.
Kesi nyingi za wanaowasiliana na Mimi nyingi zipo Kwa wanandoa ambao ni Aidha Mume alibadili dini na kufuata dini ya MKE. Au kila MTU alibaki na Dini yake wakafunga ndoa za bomani(serikalini).
Au mwanaume alitumia nguvu kumbadilisha Mwanamke Imani na Dini.
Elewa kuwa, kwenye mapenzi sio lazima uwe na MTU Fulani hasa kama hakupendi.
Elewa kuwa , mapenzi hayalazimishwi.
Elewa kuwa, kila mtu anauhuru wa Kutumia mwili wake. Hivyo usimpangie mkeo au mumeo matumizi ya mwili wake. Bali jipangie mwenyewe. Kama anakupenda basi ataji-commit kwako na sio wewe umlazimishe aji-commit kwako. Ila unaweza kujipangia kuwa huwezi ishi na Mwanamke au Mwanaume aliyeamua kuutumia mwili wake kufanya uasherati na uzinzi.
Hivyo katika mkataba wenu wa mahusiano ya ndoa, uwepo sheria iliyosainiwa au kukubaliana kuwa Kila MTU anauhuru wa Kutumia mwili wake atakavyo pasipo kuingiliwa na mwingine lakini Mimi(unaweza kuwa MKE au Mume) hutoweza kuishi na mtu mchafu (mzinzi na muasherati) hivyo Talaka itatoka ili kumpa MKE/mume Uhuru wa kuutumia mwili wake katika uchafu kadiri ya atakavyo.
Na hakutakuwa na Mijadala wala usuluhishi Kwa sababu ni Jambo lililojulikana mapema.
Hakutakuwa na hiyo nafasi ya kumshauri, kumfundisha mtu mzima aliyeko kwenye ndoa namna ya kuutumia mwili wake. Ila kila litakalofanyika litahesabika kama uamuzi wa Makusudi uliodhamiriwa na Mhusika.
Msamaha WA pekee utatolewa Baada ya Talaka kukabidhiwa. Kila MTU aishi Maisha yake lakini tukiwa tumesameheana. Hizo ni Kanuni za Watibeli.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam