Ukishaoa au kuolewa Ukweni panakuwa Kwenu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,325
51,817
UKISHAOA AU KUOLEWA UKWENI PANAKUWA KWENU,

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kwenu(ulipozaliwa) sio kwako. Weka Akilini. Kwako patageuka "kwenu" ya watoto wako.
Ukiwa kijana ambaye hujaoa na unaishi kwenye na unaakili unatambua kabisa hapo unapoishi kwa wazazi wako sio Kwako bali ni kwenu na ndugu zako(kama wapo).

Unapoenda kuanzisha mji wako kisha ukaoa au kuolewa automatically eneo lako au mali zako zinakuwa zenu wewe na mwenzako. Utasema Kwako ukirejelea umoja wa wewe na mumeo au mkeo. Na utasema kwenu ukirejelea mahali ulipotoka au alipotoka mkeo/mumeo.

Ni kwenu kwa sababu ninyi ni Familia, mwili mmoja.
Hakuna cha mambo ya Ukweni endapo mnapendana kweli. Ukweni ni neno la kibanafsi linalochochea kumbukumbu ya tahadhari ya kuwa mwangalifu na kuitenganisha familia.

Taikon sipendi uongo kwa sababu uongo sio sehemu ya Watibeli. Mtu fulani atafikiri na kuniambia, Taikon mtazamo wako huu kuhusu hili umejaribu kuukimbia ukweli.
Sijakimbia Ukweli. Kwa mtu ambaye hajaoa au hajaolewa Rasmi na hajajitokeza kwa wazazi wa mwenza wake, yaani hana ndoa. Huyo ndio tunaweza kusema anaenda UKWENI ili kupitia ndoa familia mbili ziungane ziwe kitu kimoja.

Unapooa au kuolewa tayari familia na ukoo wa upande wa pili wanageuka kuwa sehemu yako. Ni nchi mbili zilizoungana kuunda nchi moja.
"uhalisia" Kiasili(Nature) haitambui Ukweni. Uhalisia pale unapoona au kuolewa na mtu basi kizazi chenu kinakuwa kimoja. Sio ajabu Watoto wako wakachukua sura na mienendo ya Mama au Baba wa mkeo/mumeo, au wajomba au shangazi au Babu.

Ubinafsi na kiburi cha zama za zamani kupitia mfumo dume ndio kilipelekea mgawanyiko huu usio na manufaa.

Kuchukua Mwanamke na kumtenga na watu wa nyumbani kwao(al kwa kile kiitwacho kumtolea Mahari, kumnunua.
Kupitia ndoa za kibinafsi na kinyanyasaji ambazo Watibeli hatuzifuati.

Mateso ya ndoa za kikatili kwa kile kiitwacho mama mkwe au mawifi kimekuwa mwiba mkali kwa pande zote pindi ambazo kwa Unafiki zinakiri watoto wao waliunganisha familia hizo lakini kwa uhalisia hakukuwa na muungano huo)ndoa.
Sio ajabu Mama wa mwanaume hushutumiwa kuwapelekesha Wakamwana wao(wake za vijana wao) kwa vile sio watoto wao wa kuwazaa.

Taikon huwaga nasema, maisha hayanaga maana kwa Watu Wabinafsi, wenye roho mbaya, wakatili na wenye kiburi.

Haya unakuta kijana kwa vile hana pesa basi upande wa mkewe wanamnyanyasa na kujaribu kumtenganisha binti yao na hiyo kijana. Hii yote ni kutokana na ubinafsi, roho mbaya, kiburi na ukatili. Ile roho ya upendo mtu akiwa nayo lazima maisha yawe kwake na maana. Lazima amchukulie kijana aliyemuoa binti yake kama kijana aliyemzaa. Upendo ungemfanya ajiulize vipi kijana huyu ningemzaa Mimi. Au vipi vijana niliowazaa wenye hali kama kijana huyu anayetaka kuoa binti yangu.

Watibeli tunapooa au kuolewa, upendo unafuta yale matabaka, mipaka ambayo ilikuwepo. Tunakuwa ndugu, tunakuwa familia moja. Hakuna cha Baba mkwe wala Mama mkwe. Wote ni wazazi wetu kwa sababu sisi(mimi na mke wangu au wewe na mkeo/mumeo) ni mwili mmoja.

Masuala ya Maslahi ya kiuchumi kama kusaidia Wazazi na ndugu ni jambo ambalo linapaswa liendeshwe kwa upendo na kwa sheria bila upendeleo ili kuleta umoja wa kifamilia.

Mfano, Mama anashida na kwa upande wa Watu wa nje atarejelewa kama Mamamkwe wa Mwanamke au mwanaume. Ila kwenu atakuwa ni mama yenu. Msaada utafanyika kulingana na jinsi sheria zenu za familia kuhusu Kusaidia wazazi na ndugu. Kisha sheria za kusaidia jamii na watu wa nje ndio na undugu.

Huwezi leta upendo na kujenga familia kwenye ubinafsi. Hiyo sio familia bali ni ulaghai flani wa kinyonyaji.

Wazazi kuwalea huo ulikuwa wajibu wao. Ndugu kuwasaidia ilikuwa ni kulingana na utashi na upendo wao. Huwezi sema Mama yangu au baba yangu alinisomesha na kunihangaikia sana hivyo Wewe mke/mume wangu nafasi yako ni ya pili. Huko ni kujiangamiza wewe mwenyewe. Na huo ni ubinafsi wa hali ya juu. Ni kweli Baba au mama yako alihangaika lakini hiyo sio sababu ya kukugeuza Mbinafsi na kuiangusha nyumba yako mwenyewe.

Wewe ni mke/mume wangu. Sisi ni kitu kimoja. Wazazi wako ni wazazi wangu. Ndugu zako ni ndugu zangu. Taifa lako ni taifa langu.
Kila kitu kiwe na mipaka ya upendo na sio mipaka ya ubinafsi. Mipaka ya Wema na sio mipaka ya Ubaya.

Kuhusu Kifo, je kifo kinaweza kuvunja Undugu? Au familia?
Kifo hakina uwezo wa kuvunja Upendo wala familia? Kifo ni tukio la kuondoa mhusika fulani ndani ya familia jamii.
Kifo hakina nguvu mbele ya upendo kwa sababu upendo haufi, upendo unaishi Rohoni na kwenye Nafsi.
Kinachokufa ni mwili na sio nafsi au Roho.

Watibeli kwetu Mume au mke anapokufa familia itaendelea kudumu. Hasa kama kuna watoto. Hivyo mke au mume ataachiwa mali zote mpaka pale atakapoamua kuzirithisha kwa Watoto wake.
Kwa Watibeli Mwanamke na mwanaume wana Haki Sawa ingawaje hazilingani. Hivyo mke au mume anayo ruhusa ya kuolewa au kuoa(kuunganisha undugu kwa familia nyingine hata nje ya mumewe au mkewe wa awali) kwa utashi wake mwenyewe. Na anayoruhusa ya kutumia Mali zake(ingawaje zilikuwa zake na mumewe au mkewe alipokuwa hai) pasipokuingiliwa na yeyote hata Watoto wake mwenyewe(ikiwemo aliozaa na Mumewe au mkewe wa awali).

Baada ya kumpenda Mungu na kupenda wengine, sheria kuu inayofuata kwetu Watibeli ni kufanya Kazi kwa Bidii. Ili kila mtu ajichumie mali yake mwenyewe pasipo kutegemea Urithi kutoka kwa Wazazi wake au mtu yeyote.

Urithi kwa Watibeli ni sehemu ya Hiyari/Mapenzi ya mtu hasa Mzazi kwa Watoto au ndugu. Sio lazima. Hii ni kuhakikisha kuwa kila mwanadamu atahangaika kujitegemea ili kuepukana na athari mbaya za kutegemea Mali ambazo wametafuta wengine.

Taikon nimemaliza, acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mkuu tutafutie Kwa ufupi na somo la expectation( before marriage) Vs reality (ndani ya ndoa) tujue mambo angalau yaliyopo ndani ya ndoa kidogo expectation tunazo.
 
Mkuu tutafutie Kwa ufupi na somo la expectation( before marriage) Vs reality (ndani ya ndoa) tujue mambo angalau yaliyopo ndani ya ndoa kidogo expectation tunazo .
Sawasawa Mkuu.

Mwanaume wa kukuoa humtafuti na kamwe hutoweza kumpata kwa kumtafuta. Bali atakuja mwenyewe. Nazungumzia mwanaume sahihi.
Halikadhalika na mwanamke sahihi hatafutwi. Utashangaa tuu huyu hapa.

Ni muhimu kuomba upewe macho na masikio ya kumuona na kumsikia mwenza wako sahihi. Pale siku utakapoletewa.

Ndoa haihitaji Matarajio, mawazo yaliyokichwani, ndoa au maisha yanahitaji kuishi. Tumia yale uliyonayo na uyafurahie.
 
UKISHAOA AU KUOLEWA UKWENI PANAKUWA KWENU,

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kwenu(ulipozaliwa) sio kwako. Weka Akilini. Kwako patageuka "kwenu" ya watoto wako.
Ukiwa kijana ambaye hujaoa na unaishi kwenye na unaakili unatambua kabisa hapo unapoishi kwa wazazi wako sio Kwako bali ni kwenu na ndugu zako(kama wapo).

Unapoenda kuanzisha mji wako kisha ukaoa au kuolewa automatically eneo lako au mali zako zinakuwa zenu wewe na mwenzako. Utasema Kwako ukirejelea umoja wa wewe na mumeo au mkeo. Na utasema kwenu ukirejelea mahali ulipotoka au alipotoka mkeo/mumeo.

Ni kwenu kwa sababu ninyi ni Familia, mwili mmoja.
Hakuna cha mambo ya Ukweni endapo mnapendana kweli. Ukweni ni neno la kibanafsi linalochochea kumbukumbu ya tahadhari ya kuwa mwangalifu na kuitenganisha familia.

Taikon sipendi uongo kwa sababu uongo sio sehemu ya Watibeli. Mtu fulani atafikiri na kuniambia, Taikon mtazamo wako huu kuhusu hili umejaribu kuukimbia ukweli.
Sijakimbia Ukweli. Kwa mtu ambaye hajaoa au hajaolewa Rasmi na hajajitokeza kwa wazazi wa mwenza wake, yaani hana ndoa. Huyo ndio tunaweza kusema anaenda UKWENI ili kupitia ndoa familia mbili ziungane ziwe kitu kimoja.

Unapooa au kuolewa tayari familia na ukoo wa upande wa pili wanageuka kuwa sehemu yako. Ni nchi mbili zilizoungana kuunda nchi moja.
"uhalisia" Kiasili(Nature) haitambui Ukweni. Uhalisia pale unapoona au kuolewa na mtu basi kizazi chenu kinakuwa kimoja. Sio ajabu Watoto wako wakachukua sura na mienendo ya Mama au Baba wa mkeo/mumeo, au wajomba au shangazi au Babu.

Ubinafsi na kiburi cha zama za zamani kupitia mfumo dume ndio kilipelekea mgawanyiko huu usio na manufaa.

Kuchukua Mwanamke na kumtenga na watu wa nyumbani kwao(al kwa kile kiitwacho kumtolea Mahari, kumnunua.
Kupitia ndoa za kibinafsi na kinyanyasaji ambazo Watibeli hatuzifuati.

Mateso ya ndoa za kikatili kwa kile kiitwacho mama mkwe au mawifi kimekuwa mwiba mkali kwa pande zote pindi ambazo kwa Unafiki zinakiri watoto wao waliunganisha familia hizo lakini kwa uhalisia hakukuwa na muungano huo)ndoa.
Sio ajabu Mama wa mwanaume hushutumiwa kuwapelekesha Wakamwana wao(wake za vijana wao) kwa vile sio watoto wao wa kuwazaa.

Taikon huwaga nasema, maisha hayanaga maana kwa Watu Wabinafsi, wenye roho mbaya, wakatili na wenye kiburi.

Haya unakuta kijana kwa vile hana pesa basi upande wa mkewe wanamnyanyasa na kujaribu kumtenganisha binti yao na hiyo kijana. Hii yote ni kutokana na ubinafsi, roho mbaya, kiburi na ukatili. Ile roho ya upendo mtu akiwa nayo lazima maisha yawe kwake na maana. Lazima amchukulie kijana aliyemuoa binti yake kama kijana aliyemzaa. Upendo ungemfanya ajiulize vipi kijana huyu ningemzaa Mimi. Au vipi vijana niliowazaa wenye hali kama kijana huyu anayetaka kuoa binti yangu.

Watibeli tunapooa au kuolewa, upendo unafuta yale matabaka, mipaka ambayo ilikuwepo. Tunakuwa ndugu, tunakuwa familia moja. Hakuna cha Baba mkwe wala Mama mkwe. Wote ni wazazi wetu kwa sababu sisi(mimi na mke wangu au wewe na mkeo/mumeo) ni mwili mmoja.

Masuala ya Maslahi ya kiuchumi kama kusaidia Wazazi na ndugu ni jambo ambalo linapaswa liendeshwe kwa upendo na kwa sheria bila upendeleo ili kuleta umoja wa kifamilia.

Mfano, Mama anashida na kwa upande wa Watu wa nje atarejelewa kama Mamamkwe wa Mwanamke au mwanaume. Ila kwenu atakuwa ni mama yenu. Msaada utafanyika kulingana na jinsi sheria zenu za familia kuhusu Kusaidia wazazi na ndugu. Kisha sheria za kusaidia jamii na watu wa nje ndio na undugu.

Huwezi leta upendo na kujenga familia kwenye ubinafsi. Hiyo sio familia bali ni ulaghai flani wa kinyonyaji.

Wazazi kuwalea huo ulikuwa wajibu wao. Ndugu kuwasaidia ilikuwa ni kulingana na utashi na upendo wao. Huwezi sema Mama yangu au baba yangu alinisomesha na kunihangaikia sana hivyo Wewe mke/mume wangu nafasi yako ni ya pili. Huko ni kujiangamiza wewe mwenyewe. Na huo ni ubinafsi wa hali ya juu. Ni kweli Baba au mama yako alihangaika lakini hiyo sio sababu ya kukugeuza Mbinafsi na kuiangusha nyumba yako mwenyewe.

Wewe ni mke/mume wangu. Sisi ni kitu kimoja. Wazazi wako ni wazazi wangu. Ndugu zako ni ndugu zangu. Taifa lako ni taifa langu.
Kila kitu kiwe na mipaka ya upendo na sio mipaka ya ubinafsi. Mipaka ya Wema na sio mipaka ya Ubaya.

Kuhusu Kifo, je kifo kinaweza kuvunja Undugu? Au familia?
Kifo hakina uwezo wa kuvunja Upendo wala familia? Kifo ni tukio la kuondoa mhusika fulani ndani ya familia jamii.
Kifo hakina nguvu mbele ya upendo kwa sababu upendo haufi, upendo unaishi Rohoni na kwenye Nafsi.
Kinachokufa ni mwili na sio nafsi au Roho.

Watibeli kwetu Mume au mke anapokufa familia itaendelea kudumu. Hasa kama kuna watoto. Hivyo mke au mume ataachiwa mali zote mpaka pale atakapoamua kuzirithisha kwa Watoto wake.
Kwa Watibeli Mwanamke na mwanaume wana Haki Sawa ingawaje hazilingani. Hivyo mke au mume anayo ruhusa ya kuolewa au kuoa(kuunganisha undugu kwa familia nyingine hata nje ya mumewe au mkewe wa awali) kwa utashi wake mwenyewe. Na anayoruhusa ya kutumia Mali zake(ingawaje zilikuwa zake na mumewe au mkewe alipokuwa hai) pasipokuingiliwa na yeyote hata Watoto wake mwenyewe(ikiwemo aliozaa na Mumewe au mkewe wa awali).

Baada ya kumpenda Mungu na kupenda wengine, sheria kuu inayofuata kwetu Watibeli ni kufanya Kazi kwa Bidii. Ili kila mtu ajichumie mali yake mwenyewe pasipo kutegemea Urithi kutoka kwa Wazazi wake au mtu yeyote.

Urithi kwa Watibeli ni sehemu ya Hiyari/Mapenzi ya mtu hasa Mzazi kwa Watoto au ndugu. Sio lazima. Hii ni kuhakikisha kuwa kila mwanadamu atahangaika kujitegemea ili kuepukana na athari mbaya za kutegemea Mali ambazo wametafuta wengine.

Taikon nimemaliza, acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ushauri Mzuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom