Tundu Lissu: Spika Ndugai kati ya Wabunge wetu na Rais Magufuli nani Mtoro?

Eti Dunia nzima ifahamu? WTF, Dunia inafahamu kuhusu Raisi wa JMTZ Magufuli tu na siyo Esta Bulaya au sijui Zito Kabwe, ...
Kama ni kweli ilikuaje basi watu wa Kimara kuvunjiwa nyumba zao lkn zoezi lilipofikia huko kanda pendwa akasitisha zoezi eti MSIWAVUNJIE HAWA MAANA NDIYO WALIONIPA KURA?? Hilo pekee halitasahaulika kwa wale wote waliopatwa na madhara yale ya kibaguzi.

Hivi sasa yuko nyumbani kwake kajichimbia huko sababu hizo hizo mnazopigia kelelw kwa Wabunge wa Chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku umewahi kutumia akili huru kujadili jambo lolote humu? Kila wakati unapojadili jambo humu umekuwa makini sana kuhakikisha jambo hilo linaponda watu fulani na kusifia watu fulani tu.
Hakuna akili huru ya namna yako,sasa hapo nani ameoshwa akili?
Huyu Damu ya Mh Lissu bado inasumbua ubongo wake. Na hawatatulia hadi hapo watakapotembea uchi. Mkuu wala usiumeze kichwa kwa watu wenye laana kama hawa. Waache laana zao ziwe juu ya vichwa vyao wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi ya Wanasheria ni kutetea Mteja hata awe Mwizi,Jambazi mradi ni mteja
 
Hivi hii nchi sharia na katiba zinatumika kweli? tusipotezeane muda. Hii ni nchi mtu akiamua lake mradi ana nguvu litapita tu
 
Tundu acha kutetea utapeli, wanalipwa posho za kujikimu ili kuwawezesha kuhudhuria vikao vya bunge na si vinginevyo. Kujiweka karantini kuna taratibu zake na si mihemko ya Mbowe, Msigwa, Zitto wamekiri kuwa wapo Dar. Huu utapeli hata wewe uliutumia kukaa ubelgiji huku ukidai kulipwa stahiki za ubunge.

Yaani hata baada ya TL kukutofautishia kati ya Per diem na sitting allowance bado umeandika huu utumbo?

So sad.
 
Kasema katika hotuba yake alipokuwa anamuapisha Mwigulu kwamba; "yupo kwao na akifa atazikwa huko". Sasa unashindwaje kujibu hivyo??!!.
Nilijibu hivyo mkuu na nilikuwa tunabishana kazini kwangu nikaulizwa hapa ni kwenu? Nikasema hapana, nikaulizwa tena utazikwa hapa nikasema hapana. Nikaulizwa kwann upo hapa? Nikasema nipo kazini. Nikaambiwa ss kwann hufanyii utakapozikiwa? Huko nyumbani kwenu? Nikaishia kusema mimi si amiri jeshi mkuu na tupo hapa kufanya kazi si kubishana bishana.
 
Lissu upo vizuri mno; hujawahi niangusha kwa namna inavyowakilisha hoja zako ama namna unavyozijibu hoja za wengine.

Kila mara nikisoma mabandiko yako huwa natamani uendelee tu kuandika ili nisome zaidi.

Hapa JF wapo wengi wanaandika mabandiko ila ki ukweli mabandiko yako ndiyo yanayovutia wasomaji wengi...yameshiba hoja nzito na hazichoshi kuzisoma.

Kuhusu hoja hii ni wazi kabisa kwamba Spika anatumia kiti chake vibaya kujaribu kiwatoa kwenye reli wabunge wa CDM kitu ambacho hatakuja akiweze kamwe!!
POSHO haiwezi kuwa na umuhimu kuliko UHAI wa mtu...nani asiyejua kwamba Dunia nzima sasa tupo vitani against COVID-19.

TL your gifted brother; na ndiyo maana walitaka kukuua ila Mungu akawagomea.

Mungu aendelee kukulinda, wewe ni hazina ya Taifa letu.
 
Asante kwa kuelimisha umma kwa andiko safi uko vizur TL.

Huwa CCM wana laana hivyo kupelekea vichwa vyao kua vigumu kama jiwe.

Ubarikiwe TL na walaaniwe wale wote wanashabikia CCM.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom