Ijapokuwa Ole Sabaya anatuhumiwa kufanya uovu mkubwa wakati akiwa DC Hai, alipaswa kufunguliwa mashtaka ya jinai kortini. Kwa TAKUKURU kumweka mahabusu kwa wiki nzima ni kukiuka sheria za nchi yetu & kuendeleza tabia ya ukiukaji wa haki za binadamu ya vyombo vyetu vya usalama!
"Ijapokuwa Ole Sabaya anatuhumiwa kufanya uovu mkubwa akiwa DC Hai, alipaswa kufunguliwa mashtaka ya jinai kortini. Kwa TAKUKURU kumweka mahabusu kwa wiki nzima ni kukiuka sheria za nchi yetu & kuendeleza tabia ya ukiukaji wa haki za binadamu ya vyombo vyetu vya usalama!"
Upeo na hekima wa hayo maneno ya Lissu hapo kwenye mambo ya kisheria na utetezi wa haki za binadamu ni darasa tosha kwa kila mwanasiasa na raia wa kawaida katika jamii yetu. Siasa sio uadui na sheria sio hisia binafsi.
Namuelewa sana Tundu Lisu. Hawa maccm tukiyaacha yakiuke sheria kwasabb tu anayeteswa ni yule tusiyempenda (Sabaya), kuna siku yatageuza kibao kwa watu tunaowapenda.
Lissu yuko sahihi kabisa. Haki ya kisheria kwa Olesabaya ni muhimu mno maana haya yanaweza mpata mtu yeyote haijalishi umefanya au haujafanya makosa. Hii trend ya kushikilia watu kwa muda mrefu kwa sababu wanazojua wao si poa. Unaweza kuwa unashangilia leo lakini hauwezi jua kesho ni nini kitakupata.