Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Not necessarily kuungana kwa nchi mbili lazima kuwe na taifa moja tu baada ya hapo. Miuongano inamakubaliano yake na chi zinaweza zikawa na maamuzi yake mara nyingi taifa lenye nguvu ndio upoteza baadhi ya democratic rights, kikubwa ni sababu za muungano.

Nadhani Nyerere aliliona hili kama muungano wa UK kushinda wa Marekani na yote hiyo hina historia zake, za kwanini miuongano yao ikawa na misingi tofauti yaani unitary states na federal state. Kikubwa hapa kilikuwa ni watu kujitambua ni wa aina moja na miungano yao utayaweka mataifa katika better position defensly esdpecially Marekani baada ya kuchoka kuburuzwa na sera za uingereza na waingereza wenyewe baada ya vita vya muda na majirani zao particularly scotland.

Kwa kuwa ni mataifa yanaungana therefore devolution is required for those states to maintain some aspects of their democracy, way of thinking and even economical comparative advantage na mengine ndio yanaenda central.

sasa wewe sijui umeitimishaje kwamba muungano lazima ubakie na nchi moja. Hata huko ulipo zinaitwa united states unajua maana ya hilo neno 'state'?

Ukienda uingereza kuna scotland, wales and N.Ireland ambazo zinatambulika kama nchi independently na wapo kwenye muungano point ya kusema eti nchi zikiungana lazima kuzaliwe kwa taifa moja ni hoja mfu.

well nilikuwa napita tu.

Sawa kabisa; aidha kwa makusudi au bahati mbaya, watu wanachanganya a republic, a federation and a state/government;
 
Ndugu zangu,

kabla hatujafanya maamuzi magumu juu ya muungano wetu, tufanye hivyo tukiwa na uelewa wa hoja za ndugu zetu wazanzibari ni nini; Mbali ya ukiukwaji wa Mkataba kama nilivyojadili, ebu tuangalie kwa undani suala lifuatalo - Sheria ya Muungano, 1964, ambayo nia yake ilikuwa ni kuhalalisha tu Mkataba ule, lakini badala yake, ikachomeka vitu kinyume kabisa na Makubaliano;

Kwanza - Mkataba ulisema kwamba katika kipindi cha mpito, "sheria zilizopo ndani ya Tanganyika na ndani ya Zanzibar, ziendelee kutumika" mpaka tume ya katiba itakapoteuliwa na kuanza mchakato wa Katiba mpya, ndani ya mwaka mmoja; Tume hii haiukuteuliwa, hivyo ibara ya saba ya Mkataba wa muungano, kupuuzwa, na kuhairishwa indefinitely kwa nguvu;

Muhimu - Kilichotokea ni sheria ya muungano, 1964, badala ya kuhalalisha Mkataba kama ulivyo, ukaja na uchakachuaji, hasa pale kwenye sheria namba '2' ya Muungano iliposema kwamba:"Sheria iliyopo ina maana sheria iliyoandikwa na isiyoandikwa ambazo zinatumika kabla kidogo ya siku ya muungano...;

Ukifananisha sheria hii, na makubaliano ndani ya Mkataba, ina maana kwamba kulikuwa na sheria nyingine ambazo zilikuwa zije kuingizwa kwa hila! Na ukizingatia kwamba katiba ya Tanganyika ilianza kutumika kwa JMT bila ya kufanyiwa marekebisha kama Mkataba wa Muungano, 1964, ibara ya '3' ilivyoelekeza, ina maana kwamba sheria za Tanganyika ndio zikawa supreme...Pia ndani ya sheria hii ya Muungano, zikaja AMRI, JAMANI AMRI!!!, Nje kabisa ya Mkataba wa Muungano, 1964, kwa kama nilivyosema awali, Sheria hii kazi yake ilikuwa ni kuhalalisha Mkataba wa Muungano, 1964,line by line, sio kuongeza au kuondoa kitu; Badala yake, Sheria ikaja na mambo kama haya:

AMRI YA UTARATIBU WA KIPINDI CHA MPITO, 1964.

​
Amri hizi zilikuwa jumla kumi na moja, lakini tutazame zaidi Amri namba tisa ambayo ilitamka hivi:

"(9) Mali zote na haki juu ya mali zote za aina yoyote ambazo zinamilikiwa na Serikali ya Tanganyika na pia mali zote na haki yote juu ya mali za JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR zinazomilikiwa au kutumiwa kuhusiana na masuala ya Muungano, zitakuwa kuanzia siku ya Muungano katika miliki ya Jamhuri ya Muungano."

​
Kwa wale wanaolaumu ndugu zetu kwamba ni mzigo kwa muungano, wanatunyonya, n.k, nadhani sana mnaona tatizo lipo wapi; Mali za Zanzibar zilichukuliwa bila hata ya kufanyiwa tathmini, na bila hata ya fidia; Ndugu zetu hawa hawakupata hata muda wa kujipanga na mali zao, kwani muungano ulitokea ndani ya miezi minne na nusu baada ya mapinduzi;

Mwaka mmoja baadae (1965), serikali ya Tanganyika inavunjwa kwa mujibu wa sheria ya bunge namba 24, na kuwa serikali ya Tanzania – kwa maana hii, serikali ya JMT inakuwa synonym to Serikali ya Tanganyika; Serikali hii sasa ikawa inasimamia masuala ya Muungano, na yale yaliyokuwa yasio ya Muungano bali ya Tanganyika, masuala ya Zanzibar yasiyo ya Muungano, yakizidi kuondolewa na kuongezewa kwenye orodha ya masuala ya Muungano, nje ya orodha ya awali chini ya Mkataba, iliyokuwa na masuala kumi na moja tu;

Mwaka huo huo wa 1965, bunge la JMT ambalo linatumia katiba ya Tanganyika bila ya kurekebisha kama ilivyoagizwa na Mkataba wa Muungano, ili iwe fair kwa Zanzibar na kutumika kama katiba ya muda ya JMT, bunge hili ambalo kwa maana hii ni bunge batili, linapitisha sheria ya kuhairisha INDEFINATELY, mchakato wa katiba mpya ya JMT, kinyume na sharti namba ‘7' la Mkataba wa Muungano, 1964, ambayo ilitaka hii kazi ifanyike ndani ya mwaka mmoja; Badala yake, bunge hili linakuja na katiba nyingine ya Muda (1965), ambayo inasema Tanzania itakuwa ni nchi ya Chama Kimoja (TANU), mpaka pale ASP watakapoungana na TANU; Kwa maana nyingine, ASP haikuwa na sauti na haikutambuliwa na katiba ya Tanzania kwa miaka 12 hadi pale walipokubali kuungana na TANU kuzaa CCM;

Mwaka 1977, TANU ilikuwa inasubiri ndoa hii na ASP ili ihalalishe mpango wake wa kuzidi kuzika Tanganyika na kuanza pia kuimeza taratibu Zanzibar kinyume na Mkataba wa Muungano, 1964; Maamuzi ya Katiba ya kudumu 1977, yalikuwa ni maamuzi yaliyotokanana misingi ya TANU iliyoiweka katika kipindi chote cha miaka kumi na mbili ya ASP kufikiria kuhusu pendekezo la ndoa kutoka kwa TANU; ASP ilipokubali ndoa, katiba ya nchi ikawa inferior to Katiba ya CCM kwa matamshi yaliyo rasmi kabisa ndani ya katiba hiyo, huku Zanzibar sasa ikibadilisha jina na kuitwa Tanzania Zanzibar; Kwa maana nyingine, tofauti na mkataba wa Muungano, 1964 ambapo ilitamka kwamba Muungano ni baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, sasa Muungano chini ya katiba ya JMT 1977, ukageuzwa kuwa Muungano baina ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani;

Ibara ya katiba ya JMT (1977) ikaja na mpya na kali pale iliposema ibara ya 2(1):

"Eneo la Jamhuri ya Muungano ni lile eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, pamoja na ENEO LAO LA BAHARI."


Eneo la Tanzania bara ni lipi? Lile TANU ilikomboa 1961 kutoka kwa mkoloni na kuliua chini ya sheria ya bunge namba 24, 1965?

Eneo la Tanzania Zanzibar ni lipi, lile lililojikomboa kwa mapinduzi kutoka kwa Sultani, 1964?

Jamani, hata tubishe vipi, Jina Tanzania Zanzibar (na hata Tanzania Bara), yakiwa sio masuala yaliyokubaliwa yawe ya muungano, Bunge la JMT halikuwa na nguvu ya kisheria kubadilisha jina la Zanzibar (na hata la Tanganyika), na hii ni kinyume na katiba;

Vinginevyo, chini ya shirikisho la Afrika Mashariki, iwapo Kenya na Uganda wangejiunga, nazo zingekuwa ni Kenya - Tanzania Bara na Uganda Tanzania Bara?

Kwa nini baadhi yetu hatuoni hoja za wazi kabisa za ndugu zetu wazanzibari?

Tanzania visiwani maana yake ni nini sasa - Kwanini visiwa vya Kilwa na Mafia vinabakia na majina yake, hivi navyo sio Tanzania visiwani? Mnaelewa kinachoendelea hapa?
 
Mkuu Mchambuzi,
Niliuliza swali ya kwamba , je tunahitaji muungano kwa sasa? Jibu lako lilikuwa kuwa tuwe na referundum wananchi waamue.
Nimekusoma katika mabandiko yako ya mwanzo na ya karibuni, nadhani unaegemea sana turudi katika mkataba wa mwaka 1964, kwani hicho ndicho wanacholalamikia Wazanzibar.

Kwa muonekano wa kawaida ni hivyo lakini ukifahamu azma ya Wazanzibar hicho sicho wanachokitaka.Nitafafanua huko mbeleni kwanini nasema hivi.

Mkataba wa muungano wa 1964 (1)(d)Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu' Ningeomba ufafanuzi, je hili lieleweke vipi? Nini maana ya kifungu hicho.
Mchambuzi;4783006]
HOJA KWAMBA SERIKALI YA TANGANYIKA ITAKUWA MZIGO KWA WALIPA KODI NI HOJA POTOFU KUTOKA KWA?

A) Zifuatazo ni Hoja Zangu Za Msingi Kupinga Hoja Kwamba Tanganyika Itakuwa ni Mzigo kwa Walipa Kodi;

B)Kwanza, chini ya mfumo wa shirikisho, ambao kimsingi ndio uliokubaliwa katika Mkataba wa Muungano, 1964, ni rahisi for supervision of the state(s) by the people na pia inaboresha maamuzi yawe ya haraka na yenye tija; vinavyogharimu sana walipa kodi; Serikali shirikishi ya Tanganyika ikirudi sambamba na serikali ya Zanzibar, kutakuwa na gharama ndogo zaidi za kusimamia watumishi wa umma,

kwani watumishi watakuwa ni wachache zaidi, miradi itakuwa ni michache zaidi, na hii itapunguza mzigo kwa walipa kodi; ili kuelewa hili kwa undani, zingatia mfumo wa sasa ambapo masuala ya muungano na masuala ya Tanganyika, yote yanagharimiwa na serikali ya Jamhuri wa Tanzania; huu ni mzigo mkubwa sana, lakini pia ni kinyume na Mkataba wa Muungano, 1964;

C)Pili, kwa sababu serikali/nchi shirikishi hazitakuwa na mamlaka .
mfumo wa shirikisho utapunguza sana this abuse of resources;

Tatu, mfumo wa shirikisho unazipa nchi washiriki motisha na uwanja mpana zaidi wa ushindani – kiutendaji, kiufanisi, balancing the budget n.k, kwani serikali itakayokosea katika haya itaonekama wazi; hii itapunguza sana ‘WASTES’ na inasaidia uwepo wa mchanganyiko mzuri baina ya mapato kutokana na KODI na HUDUMA za kijamii zinazotolewa

D)Nne, kwa vile Federation means Decentralization, hii insaidia sana supervision ya umma.

Ni suala la mantiki tu hapa kwamba chini ya shirikisho ambapo Tanganyika na Zanzibar zinakuwa na serikali zake huru, kiasi cha kodi kitachotumika kitakuwa ni kidogo zaidi

E)Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA inasimamia mambo yote ya muungano na yale ya Tanzania Bara (TANGANYIKA), ambayo SIYO ya Muungano, kama Afya, Elimu n.k; Huu ni mzigo mkubwa, lakini pia ni gharama kubwa zaidi kwa walipa kodi; Serikali ya sasa ya JMT ipo more Centralized na ni kubwa sana kuliko ingekuwa chini ya mfumo wa shirikisho;

F)Tukubali kwamba uwepo wa nchi kubwa (physical size) bila ya mfumo wa shirikisho is UNGOVERNABLE; Kwa mfano, tazama hali za wananchi wa vijijini nchini “TANZANIA BARA”; Serikali imekuwa mbali sana na wananchi hawa lakini ni kutokana na mfumo mbovu wa sasa wa serikali; …..mara nyingine hazifiki kabisa; Kwahiyo YES, tuna decentralization, but not in RESOURCES, and that makes a huge Difference
;Naomba nichangie hoja kama nilivyoziwekea herufi za rangi.

A)Inaposemwa hoja kuwa serikali 3 zitaongeza gharama hapa haina maana ya serikali ya Tanganyika. Ina maan serikali ya shirikisho. Serikali ya Tanganyika itakuwa na bajeti yake kama ya Zanzibar lakini ile ndogo ya JMT ndiyo itakuwa mzigo.
Hapa nadhani hukuielewa maana nzima ya serikali kuwa mzigo.

Hata hivyo nakubaliana na hoja yako (E)kuwa uwepo wa central government is ungovernable. Ndiyo maana napenda serikali za majimbo. Hilo litokee tukisha vunja muungano na kubaki kama Tanganyika.
Hii inakwenda samba samba na hoja (E) kuwa tunaingia gharama kwa mambo yasiyotuhusu kama elimu kwa Zanzibar, Ulinzi na usalama pamaoja na Afya. Tukibaki kama Tanganyika resource zetu tutazielekeza kwa Watanganyika.

Nakubaliana nawe(D) kuwa decentralization ina improve supervision.
Tuanze na decetralization ya Tanganyika bila Zanzibar kwanza.
Decentralization inawezekana na si lazima kuwa na federation. Hata katika nchi bado tunaweza kurudisha madaraka kwa wananchi. Mathalani majimbo yawe na serikali zao na yasimamie shughuli zao bila kuwa na viongozi kutoka serikali kuu.

Sikubaliani(c) na kwamba abuse ni matokeo ya centralization. Tatizo ni sisi wananchi tulioshindwa kuwawajibisha wahusika. Sidhani kuwa kama tumeshindwa kama taifa tunaweza tukiwa katika vikundi vidogo.

(b) Tukiwa na shirikisho hakutapunguza gharama, kutabebesha gharama kwa upande mmoja. Niseme kuwa tukiwa na shirikisho Zanzibar itakuwa sawa na Tanganyika, with great power comes responsibilities. Kimahesabu sijui tunawezaje kugawana gharama za serikali ya JMT ili kila mshiriki wa shirikisho aone kuwa ana haki sawa.
Hypothetically, gharama zinawaiana na bajeti.Let us make an assumption kuwa gharama ya serikali ya JMT itakuwa ni 600 Bilioni. Kwa mtazamo wa uswa ZNZ inatakiwa itoe Bilioni 300 na Tanganyika bilioni 300! Je, ZNZ itakubali? Huoni hapo tutarudi kwenye hesabu za uwiano, wakati hakuna uwiano katika madaraka?

Hoja hapo juu ndio imewafanya WZNZ wakatae msimamo wa serikali 3. Tuliieleza vizuri kuwa Tanganyika ikirudi haitakubali kuwa na ushiriki mkubwa au kutoa zaidi. Itasiamama toe to toe na ZNZ katika mambo yote ya uchumi, kijamii n.k. Hapo atakayeumia ni ZNZ kwasababu yeye bni tegemezi na ndiyo maana wanataka Mkataba.

Mkataba wanaoutaka si ule unaousema wewe wa mwaka 1964, huo wameukana kwasababu unawabana. Hapa ndipo naona bado hujawawelewa wenzetu. Na kwa mchezo wao Tanganyika inaweza kuwa loser mkubwa sana na kurithisha vizazi vyetu matatizo yaliyopo.

Tuangalie mambo ya Mkataba wa mwaka 1964 halafu tuopime kama mkataba wanaoutaka ni 1964
(iv) Mambo yafuatayo yatakuwa chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano:-
a) Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
b) Mambo ya nchi za nje
c) Ulinzi
d) Polisi
e) Mamlaka yanayohusika na hali ya hatari
f) Uraia
g) Uhamiaji
h) Mikopo na biashara ya nchi za nje
i) Utumishi katika Jamhuri ya Muungano.
j) Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha
k) Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, Posta na Simu

Inaendelea...........
 
a. Katiba ya JMT:
Hili WZNZ hawatalitambua kwa kuamini kuwa wao wana uzalendo zaidi kuliko Watanganyika. Kulikubali hili kutawanyima 'autonomy' kwasababu hawawezi kuwa na katiba yao wakatoa mambo mengine kwa JMT, hicho ndicho wanachokilalamikia. Wanataka wafanye maamuzi yao kila watakapojisikia na si katiba itakavyosema.

Mfano
b.Mambo ya nchi za nje, wanataka kiti katika UN,EAC n.k. Hilo litawezekana likiwa katika katiba ya Serikali ya shirikisho.
ZNZ hawakubali.
Hadi hapo yale mambo 11 ya mwaka 1964 yamebaki 10. tuendelee

c.Ulinzi; Hili watalikubali kwasababu hadi sasa hawana bajeti ya ulinzi na usalama.
Na moja ya mambo wanayoyapigia kelele katika mkataba wanaousema hili ni mojawapo, linawasadia.

d.Polisi; Hili pia wanalitaka kwasababu hawana bajeti ya jeshi la Polisi.

e.Mamlaka yanayohusu hali ya hatari: Hawatakubali kwasababu tayari watakuwa na serikali yao, na wanataka mamlaka kamili. Yale 10 ya mwaka 1964 sasa yamebaki 9.

f. Uraia: ZNZ wanataka hili liwe la shirikisho kwasababu takribani nusu yao ni raia wa Tanganyika kwasasa hivi na ustawi wa kiuchumi utategemea sana uraia.

g. Uhamiaji: Hilo pia Watalikubali kwasababu Uraia ni sehemu ya ufanisi wa mambo yao.
Wamapopata taabu ni pale wanapotaka kuwa na kiti UN kwasababu hilo tu litaondoa huo uraia na kuwafanya wawe wageni.

h.Mikopo na biashara za nje wanataka wawe huru. Maana yake ni pamoja na kujiunga na OIC(Sio tatizo).
Hili hawatalikubali kwa hiyo kati ya yale 9 ya 1964 yaliyobaki sasa yanakuwa 8.

i. Utumishi katika serikali ya shirikisho: Hili watalikubali kwasababu hakuna sehemu nyingine duniani iliyowapa ajira kama si serikali ya muungano wa sasa na wangependa iwe hivyo.

j.Kodi ya mapato na uhuru wa forodha: Hili hawatakubali kwasababu wanachotaka ni kupata mapato kutokana na biashara zao. Kinachowatatiza hapa ni kuwa soko la bidhaa zao ni Tanganyika na wangependa kuwe na makubaliano kuwa, wao wachukue kodi lakini bidhaa ziingie bure bara.

k.Bandari na Mambo ya nga:
WZNZ hawatakubali kwa kujua kuwa hicho ndicho chanzo pekee cha mapato yao. Kwa yale 8 ya muungano sasa yatabaki 7.

Hayo 6 ya mwaka 1964 yaliyobaki ni haya:
Ulinzi na usalama
Polisi
Uraia
Uhamiaji
Utumishi
Forodha

Tanganyika kama mbia mwenza ikiwa na serikali yake nayo itajiuliza mambo yafuatayo.
1. Kwa kushirikiana na Zanzibar katika ulinzi na usalama, gharama hizo zitagawanywaje ili kila mbia wa serikali ya shirikisho apate mafao?

2.Polisi: Nalo pia litakuwa kama la ulinzi. Kwamba Tanganyika itafaidika na nini kwa kuchangia idara ya Polisi.

3. Uraia: Tanganyika itauliza, je kuna umuhimu wa kuwa na ushirika katika Uraia? Watanganyika watapewa nafasi hiyo na ZNZ kama ambavyo WZN watakavyopewa? Nini manufaa ya jambo hili na kwanini tusibaki kama EAC ilivyo

4.Uhamiaji: Hili nalo ni kama namba 3 hapo juu, tatizo ni kuwa ZNZ kuwa na kiti UN itabidi waje kama wageni au Watanganyika waende kama wageni.

5.Utumishi: Tanganyika itajiuliza, gharama za utumishi zitafikiwajwe na wafanyakazi wa serikali ya shirikisho?
Katika muungano uliopo gharama zinabebwa na upande mmoja, kuna nini cha ziada?

6.Forodha: Hapo napo Serikali ya Tanganyika itajiuliza ni kwanini iwe soko la ZNZ bila mafao? kwa vile itakuwa serikali inayojitegemea basi suala hilo litakuwa ni la masilahi na hapo haitakuwa rahisi kuwashawishi Watanganyika kubaki kama soko la ZNZ. Kama ZNZ wabavyotaka mamlaka kamili Tanganyika nayo itapenda iwe hivyo.

Hadi hapo tunaona kuwa katika mambo 11 ya mkataba wa 1964 hakuna hata moja ambalo tunakubaliana nalo.
Kwa kutambua hatima ya kudai hayo 11, Zanzibar kwa sababu wasizozitaja wameacha hoja ya serikali tatu ambazo mkuu Mchambuzi anazipendelea.

Ushahidi wa kuwa shirikisho halitafanya kazi ni pamoja na ukweli kuwa HAKUNA mzanzibar anayekiri kuwa tuna Mkataba wa mwaka 1964. Wanaelewa kukiri huko kutazua swali la, je wanataka mkataba gani mwingine wakati tunao wa mwaka 1964?

Na kwa kuogopa kuweka hadharani kile wanachikitaka HAKUNA kiongozi au mwananchi wa Zanzibar anayeweza kusimama na kusema kwa dhati mkataba uwe wa kitu gani! Maana yake wanaelewa kuwa kila watakachosema huenda kipo katika ule wa mwaka 1964 au kitahojiwa umantiki wake.

Lakini pia lazima tuelewe kuwa tukikata mkataba kama wa mwaka 1964 basi yapaswa tuvunje uliopo.
Mchambuzi, umesema Wazanzibar ni werevu sana, je kwa hili kuna werevu? Kudai kilichopo ni uerevu?
Kutaka mkataba na si shirikisho ni uerevu"

Hadi hapo nahitimisha kwa kusema, Muungano wa shirikisho kwa serikali 3 ndio njia rahisi sana ya kuua muungano.
Unless uwe umelenga kwa hilo, hakuna sababu za kuwa na shirikisho. Hapa tulipofika ni yield point, We're at the point of no return and beyond repair. Tusiwe katika denial state! solution ni kuvunja muungano.
 
Nguruvi3,

Asante kwa mchango wako mzuri; nafarijika sana kwamba tunazidi kutaufa ukweli juu ya hili, na ni matarajio yangu kwamba mwisho wa siku, tutakuwa na uelewa mkubwa sana juu na kipi ni bora kwa taifa letu aidha la Tanzania iwapo referendum itapendelea ibakie hivyo, au taifa letu jipya la Tanganyika, iwapo pia referendum itapendelea iwe hivyo; Naomba sasa niingia katika hoja zako, na sio kutafuta ushindi, bali kuzidi kutafuta ukweli;

Mkataba wa muungano wa 1964 (1)(d)Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu' Ningeomba ufafanuzi, je hili lieleweke vipi? Nini maana ya kifungu hicho.

Overall objective ya ibara nzima ya tatu ya Mkataba wa Muungano ilitokana na ukweli kwamba mpaka kufikia tarehe ya Mkataba, Zanzibar ilikuwa haina Katiba kwani lilikuwa ni taifa lenye uhuru wa miezi minne na nusu tu; Kutokana na hali hiyo, huku kimsingi nia ya Muungano ni kuleta jamhuri hizi mbili HURU kushughulika na masuala yaliyo ya Muungano tu – yani yale masuala kumi na moja, ilibidi Zanzibar na wao wapewe Chombo chao tofauti cha kutunga sheria na serikali yao kama – kama kile walichokuwa nacho Tanganyika (KATIBA), ili kama ilivyo kwa Tanganyika, Zanzibar nao waweze kuendesha mambo yao ambayo yapo nje ya orodha ile ya masuala kumi na moja, mara tu baada ya Muungano, 1964; Hii ilikuwa iwe kwa mwaka mmoja tu – KIPINDI CHA MPITO;

Njia rahisi ya kufanikisha kuwapatia Zanzibar chombo cha kutunga sheria na kuunda serikali ikabainika na kukubaliwa kwamba ni kuichukua katiba iliyopo - ya Tanganyika, lakini baada ya kuifanyika marekebisho; Ile version iliyofanyiwa marekebisho ndio iwe Katiba ya muda ya Zanzibar, na ile original version iendelee kuwa Katiba ya Tanganyika kama ilivyokuwa kabla ya 1964 (yani 1961 – 1964); Lakini muhimu zaidi hapa ni kwamba - Katika kipindi hiki cha mpito, ibara ya ‘7' ya Mkataba wa Muungano, 1964, ifanyiwe kazi – yani ufanyike uteuzi wa tume ya katiba na bunge la katiba ili kuhalalisha Muungano ule KISHERIA, kwa maridhiano ya pande zote mbili, Per Articles of the Union, 1964; Kwa kufanya hivyo, JMT sasa ingeweza kutunga sheria na kuunda serikali kwa ajili ya masuala ya Muungano, huku kila serikali shirikishi (Tanganyika & Zanzibar) zikiwa na vyombo vyake huru na tofauti vya kutunga sheria na kuunda serikali kwa masuala yaliyo nje ya orodha ile yenye masuala kumi na moja ya muungango;

Kwahiyo ibara ya 3(d) uliyo inukuu hapo juu, haina uzito wa kujitegemea kwani uzito wake unabebwa na sehemu [3(a,b,c)] na ibara ya ‘7' ya Mkataba ambayo ndio muhimu kuliko kitu chochote ndani ya Mkataba ule, kwani ibara ya ‘3' nia yake ilikuwa ni kuendesha mmungano katika kipindi cha mpito tu (SIO ZAIDI YA MIEZi KUMI NA MBILI); Sasa kwa vile ibara hiyo ya 3(d) ‘as a stand alone…' ilikuwa haina maana yoyote yakusaidia kuchakachua, ndio maana ili kufanikisha zoezi la uchakachuaji, ikabidi ibara yote ya ‘3' ipuuzwe, na vile vile ibara ya saba;

…Kwa muonekano wa kawaida ni hivyo lakini ukifahamu azma ya Wazanzibar hicho sicho wanachokitaka.Nitafafanua huko mbeleni kwanini nasema hivi.
Ingawa umesema utafafanua hili zaidi, naomba nisisitize hapa kwamba - inawezekana ikawa kweli kwamba nia ya wazanzibari sio kurudi tena kwenye Mkataba wa Muungano, 1964, lakini nadhani unaelewa umuhimu wa kusubiri referendum juu ya hilo kuliko kusoma tu upepo wa kisiasa, na hili ulishakubaliana name huko nyuma;

A)Inaposemwa hoja kuwa serikali 3 zitaongeza gharama hapa haina maana ya serikali ya Tanganyika. Ina maan serikali ya shirikisho. Serikali ya Tanganyika itakuwa na bajeti yake kama ya Zanzibar lakini ile ndogo ya JMT ndiyo itakuwa mzigo. Hapa nadhani hukuielewa maana nzima ya serikali kuwa mzigo.

Nadhani wewe ndio hujaelewa kwa undani suala hili mkuu; Katika shirikisho, serikali kuu inatakiwa iwe ndogo relative to the ‘whole', ndio maana kwa mfano, hata kwenye shirikisho Marekani, California kama ‘a State', GDP yake ni ya tano kwa ukubwa duniani;

Huu mtazamo kwamba serikali ya JMT itakuwa mzigo ni mtazamo umetokana na kiini macho cha sasa ambapo tunaambiwa kuna serikali mbili, wakati ukiangalia sio kweli: nikuulize:


  • Je, masuala ya zamani ya Tanganyika yasiyokuwa ya Muungano yanaendeshwa na serikali ipi?

Serikali ya JMT imejiongezea masuala ya Muungano karibia maradufu ya yale chini ya Mkataba wa Muungano, 1964; In the process, serikali ya Tanganyika na ile ya Zanzibar, zimenyimwa uwanja wa kutumia rasilimali zao, kuwa na ari ya ushindani to balance their budgets etc etc; Serikali hizi zingepewa autonomy yake, zingejiendesha kwa ufanisi sana huku zikichangia kwenye serikali ya JMT ambayo inatakiwa kuwa serikali ndogo; nitafafanua zaidi hili huko chini kwani umejadili suala la gharama; vinginevyo, ukiwa na mtazamo wa kupunguza masuala ya Muungano, utagundua kwamba serikali kuu (JMT), itaishia kuwa ni chombo kidogo sana kimamlaka na kiulaji tofauti na sasa, na ndio maana wanasiasa hawataki hili kwani Rais wa JMT hatokuwa na nguvu za kuwaendesha ovyo marais wa serikali shirikishi kwa manufaa ya kisiasa lakini pia ulaji;

Ingawa hoja yako ya msingi na Mzigo wa serikali ya JMT, naomba pia nitumie fursa hii kufafanua kwanini sikubaliani na hoja kwamba Tanganyika ni Mzigo kwani kuna kiini macho cha Tanganyika hapa kinachofanya serikali ya JMT ionekane ni mzigo:

Nilikuwa nataka niandae uzi tofauti juu ya hili kuliko mjadala huu kujificha humu; Nianze kwa kukuuliza swali lifuatalo:

  • Tanganyika itakuwaje mzigo wakati kufikia siku ya Muungano, Tanganyika ilikuwa tayari ina taasisi zake kamili, watumishi na fedha zake za kuwezesha kuendesha shughuli zote ndani ya mamlaka yake ya Tanganyika juu ya masuala yasioyo ya muungano?

Vitu hivi vyote hadi leo vipo, lakini kinyume na Katiba, vimepigwa rangi ya ‘Muungano' wakati this is FALSE; Hii ni sehemu kubwa sana ya kiini macho;

Jambo la Kufanya:

Rangi hii inayoleta kiini macho itolewe upesi ili kuokoa fedha za walipa kodi; Vitu hivyo (rejea hapo juu kwenye swali) virudishwe mikononi mwa Tanganyika huku tukiachia serikali ya JMT isimamie masuala ya Muungano tu, na masuala haya yapunguzwe; Pia tunapoteza sana fedha za walipa kodi kwenye kuendesha serikali ya JMT - Baraza la Mawaziri, duplication ya wabunge – wa JMT na BLWl Bunge la sasa linachangia gharama kupia kiasi; Tukae chini na kuamua juu ya ukubwa na muundo wa bunge la JMT; Tanganyika (kama itakavyokuwa Zanzibar), iachiwe iwe na bunge lake kushughulikia mambo yasioyo ya Muungano, ambayo kwa sasa yanashughulikiwa na serikali ya Muungano, na kufanya mzigo kwa walipa kodi kuwa mkubwa sana;

Nadhani pia ulisoma hoja yangu kuhusu Sheria ya Muungano, juu ya Amri ya Tisa iliyopelekea mali zote za Zanzibar kuhamia Hazina Dar-es-salaam; Ifanyike tathmini na Zanzibar warudishiwe chao walichokuwa nacho kabla ya sheria hii kupita na Amri zake za KIMUNGU MTU;

Hata hivyo nakubaliana na hoja yako (E)kuwa uwepo wa central government is ungovernable. Ndiyo maana napenda serikali za majimbo. Hilo litokee tukisha vunja muungano na kubaki kama Tanganyika.
Hii inakwenda samba samba na hoja (E) kuwa tunaingia gharama kwa mambo yasiyotuhusu kama elimu kwa Zanzibar, Ulinzi na usalama pamaoja na Afya. Tukibaki kama Tanganyika resource zetu tutazielekeza kwa Watanganyika.
Kimsingi nakubaliana na wewe katika hili, na nadhani ukisoma vizuri hoja yangu ya awali hapo juu, utaelewa nini kinaendelea, na pia utaelewa kwanini tunapotoshwa kuhusu Tanganyika kuwa Mzigo; Vinginevyo ‘option' ya kuwa na serikali ya majimbo nayo ni nzuri tu, lakini hili lifikiriwe baada ya referendum kuamua tuvunje Muungano; Kujitoa tu haraka haraka na kubakisha Tanganyika italeta madhara makubwa sana iwapo uamuzi huo hautakuwa uamuzi wa walio wengi;

Sikubaliani(c) na kwamba abuse ni matokeo ya centralization. Tatizo ni sisi wananchi tulioshindwa kuwawajibisha wahusika. Sidhani kuwa kama tumeshindwa kama taifa tunaweza tukiwa katika vikundi vidogo.
Mtazamo wako ni sahihi, lakini pia uelewe tu kwamba centralization inakaba democracy and participatory decision making kwenye suala la kuamua nini viwe kipaumbele katika kupunguza umaskini, na jinsi gani fedha za walipa kodi zitumike; nadhani unajua moja ya sababu kwanini huduma za kijamii zimezorota, hasa elimu na afya ni kwamba sera ya decentralization inafanikishwa maeneo karibia yote lakini sio kwenye suala la FEDHA; hili linaendelea kuwa centralized; Tazama kwa mfano mfumo wa afya ulivyo – 75% ya mahitaji ya afya yanaweza kutimizwa kwenye ngazi ya chini, lakini 75% ya resources zinaishia kwenye ngazi za juu za mfumo wa afya;

Mfumo wa afya una ngazi kuu tatu – Basic clinics and dispensaries; District Hospitals; na Referral and Specialty Hospitals; wakati 75% of resources zinakuwa allocated kwenye Referal and Specialty, the main cause of illness zipo preventable na zinaweza kabisa kuwa treated kwenye level ya basic clinics and dispensaries;

Kwa ufupi, hoja yangu ya msingi hapa ni kwamba - centralization leads to top-down governance, which leads to abuse of power and resources while decentralization leads to bottom – up governance, hence less abuse of power and resources;

(b) Tukiwa na shirikisho hakutapunguza gharama, kutabebesha gharama kwa upande mmoja. Niseme kuwa tukiwa na shirikisho Zanzibar itakuwa sawa na Tanganyika, with great power comes responsibilities. Kimahesabu sijui tunawezaje kugawana gharama za serikali ya JMT ili kila mshiriki wa shirikisho aone kuwa ana haki sawa.
Hypothetically, gharama zinawaiana na bajeti.Let us make an assumption kuwa gharama ya serikali ya JMT itakuwa ni 600 Bilioni. Kwa mtazamo wa uswa ZNZ inatakiwa itoe Bilioni 300 na Tanganyika bilioni 300! Je, ZNZ itakubali? Huoni hapo tutarudi kwenye hesabu za uwiano, wakati hakuna uwiano katika madaraka?
Hoja hapo juu ndio imewafanya WZNZ wakatae msimamo wa serikali 3. Tuliieleza vizuri kuwa Tanganyika ikirudi haitakubali kuwa na ushiriki mkubwa au kutoa zaidi. Itasiamama toe to toe na ZNZ katika mambo yote ya uchumi, kijamii n.k. Hapo atakayeumia ni ZNZ kwasababu yeye bni tegemezi na ndiyo maana wanataka Mkataba.
Mkataba wanaoutaka si ule unaousema wewe wa mwaka 1964, huo wameukana kwasababu unawabana. Hapa ndipo naona bado hujawawelewa wenzetu. Na kwa mchezo wao Tanganyika inaweza kuwa loser mkubwa sana na kurithisha vizazi vyetu matatizo yaliyopo.

Kwanza, kwa hoja hii, inadhihirisha kwamba chini ya mfumo wa sasa, Muungano unapendelea upande mmoja – yani Tangayika, ingawa hili ilifichwa chini ya jina la Tanzania Bara huku wenzetu wakiitwa Tanzania Zanzibar na wakiendelea kuwa na serikali yao, huku masual yao ya ndani yakizidi kunyakuliwa na kufanywa yawe ya Muungano; Pia (rejea maelezo ya Muungano katika Katiba ya JMT, 1977, relative to maelezo ya Muungano katika Mkataba wa Muungano, 1964),

Pili, katika maelezo yako, kuna elements za mchanganyiko baina ya confederation na federation; Kwa upande mmoja, a federation ni union of self governing states ambazo zipo united by a central government; Kwa upande mwingine, A confederation ni union of "political units", and NOT ONLY UNITED BY A CENTRAL GOVERNMENT, lakini pia SUPPORTED BY A CENTRAL GOVERNMENT; Sasa kwa vile Muungano wetu kwa miaka mingi sana umekuwa unaegemea confederation, huku pia ukiwa na elements kubwa za unitary system of government, ni rahisi sasa kwa hoja ya serikali tatu in terms of federation ikaonekana kama ni mwendelezo wa mfumo wa sasa bila ya kutambua kwamba mfumo wa sasa unakaribia zaidi a onfederation kuliko a federaton; Ni muhimu tukaelewa hili;

Pia tukumbuke kwamba – Muungano wetu ulianza na Muungano wa KISIASA (common in unitary and confederation systems of governments), na ndio maana akilini tukifikiria serikali tatu, bila ya kujitambua, kiini macho kilichopo kinatuzuia kutambua suala la ‘confederation', na kuepelea wengi wetu kulichanganya na a ‘federation'; Faida nyingi chini ya centralization ambazo mimi na wewe nadhani sasa kimsingi tunakubaliana, faida hizi zinapatikana chini ya ‘federation'; Masuala mengi uliyojadili hapo juu yana mashiko sana, lakini ni muhimu iwapo utachambua nini kinaweza kutokea chini ya confederation na nini kinaweza epukwa chini ya federation;

Kumbuka pia kwamba - Confederation ya zile ‘13 States' za Marekani zilipata msuko suko mkubwa na unaofanania na hoja zako hapo juu, na kupelekea new articles ambazo zilizaa federation, ambayo inadumu sasa i.e. "The U.S.A"; Vinginevyo Federalism is the way forward in today's world, kwani ina faida nyingi kuliko hasara, na imebainika kuwa ni mfumo bora wa kuendesha serikali katika muktadha wa mahusiano baina ya mataifa kuliko mifumo mingine yote iliyopo; Lakini hapa sina maana yaku "brush off" pendekezo lako juu ya mfumo wa Majimbo; Pendekezo lako ni zuri na litatufaa sana LAKINI iwapo tu, tutajitenga na kubakia kama Taifa la Tanganyika;
 
hivi mwanakijiji hua anakuja hapa kuchota elimu?

apite apunguze chuki na husda. maana Mkjj usiombe akakuchukia atakuandikia makala kila siku. tena atalazazimisha kua ww hufai kwenye jamii.

maana jamaa alimchukia lowassa kisa alikataa kuhojiwa akamwambia anakula basi hadi leo hamuandiki vizuri. hutafuta kila penyenye amuandike kwa kumchafua. sawa na masuali ya zanzibar yy daima anataka watu waamini wazanzibari walalamishi, wanabebwa hawana fadhila. na kila baya. basi itokee kanisa limechomwa mara keshawapachika ma alshabaab. husahau kua kule ndio source za dini zote za kikoloni iwe uislam au ukristo.

MKJJ POPOTE ULIPO NJOO UKUNJE MAGOTI UPATE ELMU DUNIA. ILI UPUNGUZE CHUKI NA HASADA NA KUJIONA WW NDIO MJUZI WA USILOLIJUA
 
Nguruvi3,

Tuangalie mambo ya Mkataba wa mwaka 1964 halafu tuupime kama mkataba wanaoutaka ni 1964.

Kabla sijaingia katika mjadala huu uliopo kwenye bandiko namba 225, ningependa kuelewa - Je, tunapima iwapo Wazanzibar wabataka kurejea kwenye Muungano per Article za 1964 kwa kuzingatia nini hasa:


  • Maoni Per Refereundum?
  • Maoni Per Potential referendum?
  • Maoni Per Kauli (sio vitendo) Vya Maalim Seif, et. al?
  • Vitendo/Maamuzi yanayoendelea kutekelezwa chini ya Katiba ya Sasa Ya Zanzibar?

Majibu yako yatanisaidia jinsi gani nijenge hoja zangu, kwani kila elemeny hapo juu itanifanya nije na mpangilio tofauti kabisa wa hoja;
 
hivi mwanakijiji hua anakuja hapa kuchota elimu?

apite apunguze chuki na husda. maana Mkjj usiombe akakuchukia atakuandikia makala kila siku. tena atalazazimisha kua ww hufai kwenye jamii.

maana jamaa alimchukia lowassa kisa alikataa kuhojiwa akamwambia anakula basi hadi leo hamuandiki vizuri. hutafuta kila penyenye amuandike kwa kumchafua. sawa na masuali ya zanzibar yy daima anataka watu waamini wazanzibari walalamishi, wanabebwa hawana fadhila. na kila baya. basi itokee kanisa limechomwa mara keshawapachika ma alshabaab. husahau kua kule ndio source za dini zote za kikoloni iwe uislam au ukristo.

MKJJ POPOTE ULIPO NJOO UKUNJE MAGOTI UPATE ELMU DUNIA. ILI UPUNGUZE CHUKI NA HASADA NA KUJIONA WW NDIO MJUZI WA USILOLIJUA

Mzee Mwanakijiji hajaja humu, lakini msimamo wake juu ya muungano unatambulika na ni kinyume cha mtazamo wangu wa serikali tatu chini ya makubaliano yaliyopo kwenye Mkataba wa Muungano 1964, lakini kwanza kwa kupitia Referendum/kura ya maoni iwapo watanzania wa pande zote mbili wanataka tuendelee, hasa kwa kuanzia pale tulipojikwaa; Wakisema kwamba hawataki muungano uendelee kwa mfumo uliokubaliwa mwaka 1964 kwenye Mkataba wa Muungano, sasa options nyingine ambazo jokakuu, nguruvi3, mzee mwanakijiji na wengineo wanapendekeza, ndio zipewe uzito; huu ni mtazamo wangu tu, na nadhani kufikia tamati ya mjadala wetu huu, ambao nipo zaidi kujifunza kupitia hoja, na sipo kushinda kwa hoja, natumaini nitakuwa mwelewa zaidi, na pengine kuhamia upande wa wenzangu wa hoja;
 
Mkuu Mchammbuzi, kwa maelezo yako kifungu 3(d) kilikuwa wakati wa mpito na kilipoteza nguvu baada ya kipindo hicho kupita. Siwezi kuwa mtabiri endapo mambo yangefanyika tofauti kama mwaka mmoja uliokusudiwa ungetekelezwa.
Kwahiyo tukiache kama kilivyo.

Niliposema tuangalie mkataba wa mwaka 1964 nilimaanisha katika mfumo wa shirikisho unaoupendekeza urejewe.
Nakubalina nawe kuwa referendum ingatangulia uandikaji wa katiba mpya kwasababu hiyo ingeondoa uwezekano wa muungano au uwepo wake. Kwa bahati mbaya nafasi hiyo imepita.

Kwa mwendo huu tunaendelea kukungumizwa kukubali matatizo yaliyopo, kinachofanyika ni kutaka maboresho.
Sikubaliani na hili na sijui kwanini wananchi hawalioni. Zanzibar wenye fursa nzuri sana na wenye malalmiko ambayo unasema ni ya msingi na ni werevu nao pia wameshindwa kutetea uwepo wa referendum.

Kuhusu hoja ya Tanganyika kuwa mzigo, nadhani hapa kuna mahali tunatofautina.
Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi na vyombo vyao kisheria, hilo tunakubaliana.
Hoja iliyopo ni kuwa uwepo wa serikali ya tatu ambayo ni ya shirikisho utakuwa mzigo!
Pamoja na udogo wake ambao naukubali kutokana na majukumu ya muungano tu, bado hatuwezi kukwepa ukweli kuwa itahitaji gharama.

Swali ni kuwa gharama hizo zitakubaliwa na pande zote sawa sawa kama wabia sawa?
Niliposema gharama hizo zitabebwa na Tanganyika nilimaanisha kiuchumi, huo ndio ukweli.

Hapo ukanijibu kuwa mambo ya muungano imepewa Tanganyika uvunguni na hivyo kupendelewa.
Hili ndilo hasa tatizo la Wazanzibar kuamini kuwa Tanganyika inafaidika na Muungano.
Ukweli ni kuwa mambo yote yaliyo nje ya mkataba wa mwaka 1964 ni kuipendelea Zanzibar na si kinyume chake.
Kusema Tanganyika imependelewa bila kusema imeonewa si kuweka mizania katika hali halisi.

Kuhusu confederation na Federation, hii ni mifumo inayokaribiana kama ulivyoonyesha. Kitu kimoja ni kuwa hakuna taifa lenye mfumo wa confederation kwa sasa. Mataifa yote yaliyoanza na confederation mwishowe yamejikuta yakiwa na Federation, Canada ikiwa mojawapo.

Katika mifumo hiyo kuna mambo mawili muhimu sana, siasa za nje na ulinzi na usalama. Hayo huwa chini ya serikali ya shirikisho kwa mifumo yote. Huko siko walipo Wazanzibar, wao wanataka kiti UN halafu muungano wa mktaba ambao haujulikana ni upi kwasababu ule wa mwaka 1964 hawataki kuusikia. Tutarudije mwaka 1964?

Niliposema tuangalie mkataba wa mwaka 1964, nilimaanisha mkataba unaosema wewe tukirudi iwe kwa referendum au iwavyo tutakuwa tumeondoa tatizo. Hapo ndipo nasema tujadili theorically kabla ya referendum (na sijui kama itatokea) kuwa hivi tukirudi mwaka 1964 tunaweza kuwa tumepata ufumbuzi?

Ninasema theoritically kama njia mojawapo ya 'stress test' katika wakati huu ili tuweze kujipambanua tofauti na wenzetu ZNZ wanaosema muungano wa mkataba ambao HAWAWEZI KUUTETEA hata kwa sentesi moja.
Wao wanataka mkataba tu bila kujua wa nini.(au wanajua na wana siri moyoni)

Lakini pia si vibaya ukayaangalia katika vitendo na mamuzi chini ya katiba ya sasa ya Zanzibar.
 
Mkataba wa Muungano unasema

(viii) Mkataba huu utahitaji kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.

Mkataba wa Muungano haukutaka Baraza la Wawakilishi kuridhia Muungano na wala haikutaka Sheria kuundwa ili kuuridhia kama Barubaru na wengine wanavyootaka. Mkataba uko wazi.
 
Mkataba wa Muungano unasema



Mkataba wa Muungano haukutaka Baraza la Wawakilishi kuridhia Muungano na wala haikutaka Sheria kuundwa ili kuuridhia kama Barubaru na wengine wanavyootaka. Mkataba uko wazi.

Sijakusoma vizuri katika hili; Unaposema "kuridhia/kuuridhia", maana yako ni kwamba unatumia neno hili kwa nia ya kufananisha au kutofautisha na neno lile la "kuthibitishwa" lililopo kwenye ibara ya saba ya muungano?
 
Mkataba wa Muungano unasema



Mkataba wa Muungano haukutaka Baraza la Wawakilishi kuridhia Muungano na wala haikutaka Sheria kuundwa ili kuuridhia kama Barubaru na wengine wanavyootaka. Mkataba uko wazi.

Mkataba unaoandikwa kitapeli tapeli
Kama ni mkataba wa kimataifa basi mkataba huo utakuwa "null and void" au vipi, MMJ?

- One significant part of treaty making is that signing a treaty implies recognition that the other side is a sovereign state and that the agreement being considered is enforceable under international law.- Treaty - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Hata baraza la mawaziri likae retreat hawawezi mjibu Tundu Lissu
 
Zanzibar kufuata sheria ya uhamiaji ni kwa sababu both ni serikali ndogo na ilikubaliana kuwa serikali ndogo kwa kuweka kipengele hiki kwenye mkataba.

Uhusiano uliopo ni, serikali ya zanzibar (zanzibar siyo nchi) ipo subordinate kwa mambo 22. Yaani haina maamuzi kwenye mambo hayo na kwa kuwa haina maamuzi kwenbye mambo hayo, tayari imeshakuwa "inferior" to URT...

Zanzibar ni semi autonomous state.

Tanzania ni Jamhuri ya Muungano. Ni Muungano wa nchi mbili (Tanganyika naZanzibar) ambazo kabla ya Muungano huo zilikuwa huru na zenye mamlaka kamili. Vile vile nchi hizi zilikuwa na zinaendelea kuwa na historia mfumo wa Katiba ulio tofauti lakini unaingiliana. Katika kuelekea kwenye kutayarisha Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano suala hili ni lazima liwekwe wazi na lijadiliwe kikamilifu.

Hii ni kwa sababu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunazo Katiba mbili na siyo moja. Hizi ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984. Katika hali isiyo ya kawaida, Katiba hizi mbili zina hadhi sawa kutegemea pale zinapohusika. Hakuna iliyo na nguvu au uwezo kuliko nyingine. Hali hii inaufanya mjadala wa Katiba uwe mpana na uwe wa kuangalia kwa makini sana. uk2-3 link mwongozo
 
Tanzania ni Jamhuri ya Muungano. Ni Muungano wa nchi mbili (Tanganyika naZanzibar) ambazo kabla ya Muungano huo zilikuwa huru na zenye mamlaka kamili. Vile vile nchi hizi zilikuwa na zinaendelea kuwa na historia mfumo wa Katiba ulio tofauti lakini unaingiliana. Katika kuelekea kwenye kutayarisha Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano suala hili ni lazima liwekwe wazi na lijadiliwe kikamilifu.

Hii ni kwa sababu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunazo Katiba mbili na siyo moja. Hizi ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984. Katika hali isiyo ya kawaida, Katiba hizi mbili zina hadhi sawa kutegemea pale zinapohusika. Hakuna iliyo na nguvu au uwezo kuliko nyingine. Hali hii inaufanya mjadala wa Katiba uwe mpana na uwe wa kuangalia kwa makini sana. uk2-3 link mwongozo
hazina hadhi sawa. hivyo sasa ndiyo tunaviita viini macho.
 
Katiba inasema:

1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

Kwa nini kifungu hiki hakikuandikwa kama hivi?

Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Ni kwa sababu ukisoma kipengele cha pili tayari utakutana na uchakachuaji/ukiini macho.


Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Hiki pengele pia kingesomeka

Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanganyika na eneo lote la Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanganyika na Zanzibar inapakana nayo.

Katika umakini huu, kiini macho cha kufuta Tanganyika na utaifa wake, kisingefanikiwa.

Soma katiba uk 11 link katibamuungano

Wadanganyika, tuendelee kupiga usingizi?

 
Katiba inasema:

1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

Kwa nini kifungu hiki hakikuandikwa kama hivi?

Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Ni kwa sababu ukisoma kipengele cha pili tayari utakutana na uchakachuaji/ukiini macho.


Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Hiki pengele pia kingesomeka

Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanganyika na eneo lote la Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanganyika na Zanzibar inapakana nayo.

Katika umakini huu, kiini macho cha kufuta Tanganyika na utaifa wake, kisingefanikiwa.

Soma katiba uk 11 link katibamuungano

Wadanganyika, tuendelee kupiga usingizi?

Sawa sawa; ni kama kiini macho kwenye katiba ya JMT (1965) ambayo iliingiza masuala la vyama, kinyume na makubaliano ya Mkataba wa Muungano, 1964, kwani katika masuala yale kumi na moja, suala la siasa au vyama halikuwepo; Lakini kwa uchakachuajia, TANU ikajipenyeza kwenye katiba ya nchi na kuiacha ASP solemba ilipotamka hivi:

3(1) Kutakuwa na Chama kimoja cha siasa katika Tanzania.
(2) Mpaka hapo Tanganyika African National Union (TANU) itakapoungana na Afro Shiraz party (ASP), chama hicho kwa Tanganyika kitakuwa Tanganyika African National Union (TANU) na kwa Zanzibar, kitakuwa ni Afro Shiraz Party (ASP).
(3) Shughuli zote za kisiasa katika Tanzania zitafanywa chini ya usimamizi wa Chama.
(4) katiba iliyoonyeshwa katika nyongeza ya kwanza ya katiba hii itakuwa Katiba ya Tanganyika African National Union (TANU) na katiba hiyo inaweza kurekebishwa wakati wowote (na masharti yaliyomo ndani yake na baada na Muungano wa Tanganyika African National Union na Afro Shiraz Party (ASP) kwa mujibu wa masharti yaliyomo ndani ya katiba hiyo;

Nadhani kiini macho na pia uchakachuaji hapa upo wazi, pamoja na madhara yake kwa Jamhuri ya WATU wa Zanzibar; Muhimu hapa pia ni kwamba, kwanza, Zanzibar ilikuwe held at ransom mpaka ikubali kuungana na TANU; Muhimu zaidi ni kwamba,wakati ASP wakijifikiria na utongozaji huu wa TANU kabla ya ndoa, miaka 12 ya kusubiriwa kusema NDIO NIMEKUBALI AU HAPANA, TANU ilikuwa ndio inaendesha Muungano, na kwa matakwa yake, huku ikizidi kuvunja masharti ya Mkataba kama tulivyokwisha jadili;

By the time ASP wanasema NDIO, ni mwaka 1977, na kilichotokea ni TANU kuigeuza katiba ya nchi sasa kuwa ni katika ya CCM; Katiba ya nchi haikuwa na nguvu kuliko katiba ya CCM, kwa mfano tuliona jinsi gani wabunge wawili – Seif Sherrif Hamad na Rashid Hamad walipofukuzwa uanachama wa CCM kupitia katiba ya CCM, katiba ya JMT (1977) haikuwalinda; Lakini leo Hamad yule yule, na pia Kafulila, wamefukuzwa na vyama vyao, lakini Katiba ya JMT inawapa kinga, na sio kwamba ilibadilishwa katika eneo hilo baada ya vyama vingi, ni kwamba sasa utawala ni wa kufuata katiba ya JMT, sio za vyama;

CCM mwaka 1977 ikashika hatamu na sasa kwa vile ndoa na ASP ilishakamilika, Katiba ya JMT ikabadili na kusema ni Muungano baina ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar; Kwa mara ya kwanza, Zanzibar ndio wakaonja joto la jiwe lile lile la Tanganyika kufutwa kwa sheria ya bunge namba 24, mwaka 1967; Baada ya wazanzibari wakiongozwa na JUMBE kuanza kuwa na wasiwasi juu ya nini kitafuata, pengine Tanzania Zanzibar kugeuka kuwa Zanzibr Tabora, ndio kikatokea tunachoambiwa Mchafuko wa hali ya hewa ya kisiasa, na jumbe akajiuzulu;

Kina Maalim Seif leo hii wana nguvu kwa kutumia hoja ya JUMBE iliyompelekea ajiuzulu;
 
Back
Top Bottom