Bongolander,
Nashukuru kwa mchango wako, na hasa majibu yako ambayo kwa kweli yanapelekea tuzidi kuchimba bongo zetu katika kutafuta ukweli;
Mimi nadhani ushirikiano wa muda mrefu kijamii na kiuchumi baina ya Tanganyika na Zanzibar ulikuwepo, lakini suala la kuzingatia zaidi hapa ni kwamba – inawezekana hii ilikuwa ni sababu ya kuhalalisha sababu nyingine kubwa, either Panafricanist au imperialist, in nature;
Tukianza na imperialistic…
Kuna argument kwamba Muungano wetu ulitokana na Cold War Politics; Sultani aliangushwa na itikadi ya kikomunisti, chini ya kina ABURAHAMAN BABU; Na tukichimba bongo zetu kidogo, hapa tutaona kwamba hizi hazikuwa Good News kwa viongozi wengine wa ukanda wa afrika mashariki ambao ndio kwanza walikuwa wamejipatia uhuru, hasa kutokana na ukweli kwamba, uhuru wao ulikuwa ni wa kisiasa tu, kwani mfumo mzima wa uchumi uliendelea kuwa ni ule ule wa kikoloni; Kwahiyo, Mapinduzi ya KIKOMUNISTI kuonekana ni mafanikio hapo jirani, became a MAJOR THREAT to Nyerere, Kenyatta na Obote; Kitu kingine muhimu hapa pia ni kwamba - kwa vile former colonial powers zilikuwa kwenye vita dhidi ya Ukomunisti, hawa colonial powers hawakuwa tayari kuona mapinduzi ya kikomunisti yaki propagate Afrika Mashariki ambako walikuwa na strategic interests kubwa; Kwa maana nyingine rahisi, they viewed Zanzibar as a potential Cuba in East and Central Africa;
Tukija kwenye Panafranist…
Tunaelewa kwamba Kwame Nkrumah alikuwa ni visionary wa PANAFRICANISM, huku Nyerere akiwa close to that; Lakini kulikuwa na tofauti kubwa zilizojitokeza baina ya Nkrumah na Nyerere in relation to Panafricanism: Kwa upande mmoja, Nkrumah aliamini katika rapid integration – kwa maana ya kwamba tuanze na Umoja wa Afrika ‘fasta fasta', na hakuna haja ya kusubiri masuala mengine; Kwa upande mwingine, Nyerere akihimiza umuhimu kwanza wa kukomboa nchi zilizosalia, na baada ya hapo, kuanza integration by regional blocks, halafu dio lije suala la kuunganisha afrika nzima kwa ndoto za Nkrumah, lakini baada kwanza ya Afrka kuungana kwa njia ya blocks; Hii ikawa ndio sababu kubwa ya Nkrumah na Nyerere kutokuwa na mtazamo mmoja kuhusu the future of Africa i.e. while the end was justified kwa wote, the Means wasn't; Kwa wakati ule, wengi walimwona Nyerere kwamba hakuwa "A TRUE PANAFRICANIST" kama Nkrumah, historia baadae ikaja kumpa Nyerere ushindi wa nguvu ya hoja, kwani regional integration ndio njia effective kwa sasa kuelekea United States of Africa;
Pamoja na haya, binafsi naona kwamba, katika mazingira ya blocks, kosa la Nyerere lilikuwa kutumia Nkrumah's approach – yani kuweka mbele POLITICAL UNION/Ushirikiano wa KISIASA badala ya kufuata a conventional method - ‘baby steps; Kwa maana nyingine rahisi, Nyerere aliona Muungano uanze na SIASA, kwa matarajio kwamba it would trickle down into the ECONOMICS and SOCIAL; In my humble opinion, this was and still is, a wrong approach; Hakuna sehemu duniani yenye Muungano ulioanza namna hii ambao tunaweza kusema ni mfano wa kuigwa; Kwahiyo, approach ya Nyerere ya kuanza na SIASA, kwa mtazamo wangu ndio ilichangia sana contradictions between yaliyokuwemo ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964, na yaliyokuwepo akili mwa Nyerere; Na hapa ndio nyumbani kwa mjadala kwamba lengo la Muungano wetu ilikuwa ni serikali mbili, moja…;
Vinginevyo, mimi nitaendelea kuamini kwamba, Mkataba wa Muungano, 1964 ulilenga shirikisho la serikali tatu Serikali ya JMT, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar; Lakini kwa maelezo ya hapo juu, in practice, mambo yakaanza kuchakachuliwa, ingawa kwa nia njema, lakini madhara yake ndio haya; Kwahiyo Suala la kujadili ni kwamba:
- Kwanini Theory and Practice ya mfumo wa Muungano vinapishana?
Ningependa kuzidi kutoa ushahidi kwanini nasema Nyerere in theory alilenga mfumo wa shirikisho:
Kwa mfano, tazama hotuba ya Mwalimu Nyerere (1960) kwenye kikao cha Kwanza cha OAU, Addis Ababa, Kikao cha Pan African Freedom Movement for East Africa (PAFMECA, 1960):
"Wengi wetu tunakubali bila hoja kuwa shirikisho la nchi za afrika mashariki ni jambo linalokubalika; tumesema hayo kwa imani kuwa mipaka ya nchi iliyopo sasa imetengenezwa na mabeberu, na sio sisi wenyewe, na katika hali hiyo basi ipo kama kizingiti kwa Muungano baina yetu; lazima tuikabili ofisi ya mkoloni na kudai uhuru sio wa Tanganyika, na baadae Kenya, Uganda na Zanzibar kila nchi peke yake, bali uhuru huo tuudai tukionyesha sote ni wajoma kisiasa."
Source: Tanganyika Standard, 16/11/1964.
Kuna masuala mawili muhimu ya kuyatazama ndani ya hotuba hii:
Kwanza, Mwalimu anaweka wazi kabisa kwamba kipaumbele ilikuwa ni
UMOJA WA KISIASA. Lakini kama nilivyojadili hapo juu, Muungano wa mataifa huru hupitia njia mbalimbali, lakini UMOJA WA KISIASA HUWA NI HATUA YA MWISHO KABISA; Sasa kwa suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, I am of conviction kwamba, Mwalimu alikuwa na nia ya kuufanya Muungano wetu uanze na ngazi ya mwisho katika process ya mahusiano ya mataifa, yani SIASA/Political Union, kwa matarajio kwamba it would trickle down into the ECONOMICS and SOCIAL; Lakini pengine aliona akiweka hili wazi ndani ya Mkataba wa Muungano, Wazanzibari wataweza kuona hii itakuwa ni kuwameza, hasa ukizingatia udogo wa taifa lile; Kutokana na hili, kiini macho ndio kikazaliwa;
Kilichotokea baada ya Mkataba kusainiwa ni kama nilivyojadili, na Muungano ulikamilishwa chini ya katiba ya kudumu ya 1977, ambapo baada ya chama cha ASP kupewa muda wa kufikiria ndoa yake na TANU, kwa miaka kumi na mbili, ASP finally ikakubali ndoa ile; Na katika kipindi kile cha miaka kumi na mbili cha katiba ya Muda (1965) bila ASP, chama cha TANU ikajiingiza kwenye Katiba ya Muda (1965), na kuanza kuendesha shughuli za kisiasa za Muungano, nje ya makubaliano ya Mkataba, 1964, kuuendesha Muungano huu kwa matakwa yake; Kwa mfano, TANU ambayo ndio ilikomboa Tanganyika, TANU hiyo hiyo ikafuta taifa hilo kupitia sheria ya bunge namba 24, 1964;
Pia TANU ikaweka kipengele ndani ya katiba ya muda (1965) kwamba, ‘Tanzania itakuwa ni nchi yenye mfumo wa chama kimoja', huku ikijulikana wazi kwamba kulikuwa na chama cha ASP upande mwingine wa muungano; Muungano wa KISIASA (Per Vision ya Nyerere kwenye Mkutano wa PAFMECA), ukakamilika mwaka 1977, ambapo TANU + ASP ikazaa CCM, huku CCM ikipewa nguvu na mamlaka kubwa kuliko Katiba Mpya na ya Kudumu (1977); And in principles, miaka ile 12 ya katiba ya muda ilikuwa tosha kwa TANU na baadae CCM kuwa ndio wasemaji wakuu wa Muungano, hasa kwa vile ASP haikuwa na sauti juu ya Muungano kwa miaka kumi na mbili (1965 – 1977)!!!!
Ebu tuzidi kutazama matukio mengine kabla ya Muungano, 1964.
Kwanza ni azimio la kikao kingine cha PAFMECA (1963), hasa azimio kuu, kikao ambacho kilihudhuriwa na viongozi wa Kenya, Tanganyika na Uganda:
"Sisi viongozi wa nchi na serikali za afrika mashariki, tunajifunga kisiasa kuwa na shirikisho la afrika mashariki…
Mkutano wetu wa leo unaongozwa nahamu ya kuunganisha bara la afrika na sio ubinafsi wa maslahi ya maeneo yetu…
Leo ni siku ya vitendo katika kuelekea katika maadili tunayoyaamini na umoja na uhuru ambao sote tumeupatia mateso na kujitolea muhanga kwa ajili hiyo."
(Source: A declaration of Federation by the governments of east Africa on June, 5, 1963, lilichapishwa katika meetings and discussions on the proposed East Africa Federation (Dar-es-salaam: Tanganyika Government, Ministry of Information, 1964).
Kuna Masuala Mawili Muhimu Hapa Pia ya Kutazama:
Kwanza, neno KISIASA limejirudia tena – kuashiria kwamba Muungano alioutaka Mwalimu ni wa kisiasa;
Pili, neno shirikisho ndio lilitawala mijadala hii ambayo Nyerere alikuwa na influence kubwa; Ndio maana kuna kila sababu ya kuamini kwamba ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964, lengo ilikuwa ni mfumo wa serikali wa shirikisho kuendana na idadi ya nchi husika, mfano kama ni nchi mbili, basi serikali tatu – serikali kuu kushughulikia mambo yaliyokubaliwa yawe chini ya shirikisho, na serikali mbili za Tanganyika na Zanzibar – kila moja ikiendelea na shughuli zake ambazo hazipo katika orodha ya masuala ya shirikisho;
SUALA LA ZANZIBAR KATIKA MAZINGIRA YA PAFMECA, KABLA YA MUUNGANO WA 1964
Tulitazame hili kwa undani kidogo; Kama unavyoona, vikao vya PAFMECA nilivyojadili, vilifanyika wakati Zanzibar ikiwa bado sio nchi huru, na ndio maana haikushiriki; Lakini pamoja na hayo, Nyerere aliizungumzia kwenye vikao hivi, tena kwa kwa lugha ya Shirikisho; Kwa mfano, Mwalimu alisema hivi:
"Ingawaje Zanzibar haikuwakilishwa katika mkutano huu, inatulazimu tuseme wazi kuwa nayo inakaribishwa kujiunga na mkutano huu wenye kulenga kuwa na shirikisho; Mara tu baada ya Zanzibar kumaliza taratibu zake za uchaguzi serikali yake itashirikishwa katika kamati ya kufuatilia jambo hilo au kamati nyengine yoyote ili itakayoanzishwa katika kufikia lengo la shirikisho;"
Source: Julius Nyerere, The Nature and Requirements of African Unity, in African Forum Vol.1 (1965), uk 46, pp.38-52);
Kwa maneno haya, Nyerere anazidi kuthibitisha kwamba hata kwenye suala la Zanzibar, lengo ilikuwa ni kuja kuihusisha kwa mfumo wa shirikisho. Ndio maana hata baada ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika, Nyerere alitamka haya Aprili 20, 1968 kwenye gazeti moja la Uingereza (The Observer):
"Iwapo UMMA wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha…
Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kuukana."
Ikumbukwe tu kwamba, the ‘exit' option huwa ipo sana katika mashirikisho/federal systems, na Mkataba wa Muungano, 1964, uliwapa viongozi fursa hii; Vinginevyo chini ya unitary systems of government, the right to ‘exit' haipo straight forward na ndio hupelekea mabomu anayojadili Mwalimu hapo juu;
cc: jmushi1, jokakuu & nguruvi3