Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Kobello

Unaelewa kuwa kuna kitu kinaitwa mgawanyo wa mamlaka/madaraka?
Umeshawahi kusikia au unafahamu kuwa Tanzania ina Muungano wenye serikali mbili (as per kiini macho)na mamlaka tatu kisheria?

Zanzibar ( au Ilala)kufuata Sheria za uhamiaji ni kwa sababu ya udogo wa serikali hii au ni kwa sababu uhamiaji imo katika mamlaka ya serikali ya Muungano?(jambo la muungano)

Usuperior (ukuu) wa serikali ya muungano upo kihisia au kisheria? Kama ni kisheria, sheria ipi inaipa serikali ya muungano hadhi/cheo cha serikali kuu dhidi ya Serikali ya Zanzibar?

Au sheria ipi inatamka kuwa serikali ya Zanzibar ni sub-ordinate kwa serikali ya Muungano?

Ni uhusiano upi uliopo baina ya serikali kuu na serikali za mitaa,wilaya,mikoa?

Serikali ya Zanzibar ipo kwenye kundi lipi?

Je Zanzibar ni mtaa, wilaya, mkoa au state?
Je Tz bara(Tanganyika) ni mtaa, wilaya, mkoa au state?
Sijawahi kusikia hilo la mamlaka tatu, ila nishawahi kusikia serikali mbili. Tushawahi kuwa na serikali mbili ila sasa tuna serikali kadhaa (mpaka za mitaa).Ila nadhani unamaanisha serikali kuu, ndiyo moja ya zanzibar na nyingine ya muungano.

Zanzibar kufuata sheria ya uhamiaji ni kwa sababu both ni serikali ndogo na ilikubaliana kuwa serikali ndogo kwa kuweka kipengele hiki kwenye mkataba.

Uhusiano uliopo ni, serikali ya zanzibar (zanzibar siyo nchi) ipo subordinate kwa mambo 22. Yaani haina maamuzi kwenye mambo hayo na kwa kuwa haina maamuzi kwenbye mambo hayo, tayari imeshakuwa "inferior" to URT. Serikali ya halmashauri ya wilaya ya Ilala ipo subordinate kwa mambo mengi zaidi (sijapata) hesabu yake lakini haipo inferior to the govt. of URT kwenye sheria kama ya (kwa mfano) kukusanya takataka siku ya jumatano, au kutokuuza nyanya pembezoni mwa barabara au kutoza ushuru wa aina fulani.

Zanzibar ni semi autonomous state.
 
Kobello,

Usijaribu ku – spin dhana ya Serikali;

Hoja zako juu ya hili inafanania na hoja nyingine nilizowahi sikia huko nyuma kwamba serikali za mitaa hazina katiba zake zenyewe; Serikali mbili tulizonazo leo haziwezi kufananishwa na Serikali Kuu na Serikali Za mitaa, vinginevyo ni sawa na kufafanisha embe na nazi; Tofauti kuu iliyopo na iliyo wazi kabisa ni kwamba – tofauti na serikali za mitaa, ambayo ipo subordinate kwa serikali kuu, serikali mbili au zaidi ndani ya mfumo shirikisho au Muungano wowote – THESE ARE NOT SURBODINATE TO EACH OTHER: Badala yake, serikali shirikishi are co-ordinate and of equal power and jurisdiction in their own sphere; THEY ARE MASTERS IN THEIR OWN HOUSE;

cc: nonda
Nitajibu hili kifupi, lol
Serikali ya zanzibar ni subordinate au "Inferior" to the government of URT legally and logically. You know some other legal issues are illogical, but the inferiority of Zanzibar govt to the goivt of URT is logical.

IN Tanzania, there are no two governments which have equal power and jurisdiction in their own spheres; no two governments in Tanzania are masters in their own houses.

But lets not go there, this is spinning right here.

Na Tatu, maneno haya ya Mwalimu (ambayo yapo mengine mengi tu), yanazidi kuweka bayana kwamba Mkataba ulilenga Shirikisho, vinginevyo mabadiliko baada ya kusainiwa mkataba, yalitokana na nia njema tu, hasa njozi ya kuifanya JMT iwe na Serikali moja siku za usoni, ikiwezekana akiwa bado hai, lakini kwa kuanzia, serikali mbili, kwani alijua fika kwamba ili wazanzibari wakubali, Mkataba ule ilibidi uweke mfumo wa serikali tatu;
Hapo kwenye nyekundu ndipo tulipokuwa tunabishana muda wote huu.Articles of the union zimeonyesha nia hiyo, jinsi zilivyokuwa drafted from the begginning.Nilikuwa nasisitiza nia hiyo, hata kama ningekuwa hakimu, ningekubaliana wazi kuwa hapo kwenye mkataba kulikuwa na nia ya kuwa na serikali moja.

Whatever the reason, nia ilikuwa serikali moja na hicho ndiyo msingi wa argument hii. Bado kabisa sijaona serikali tatu ikiwa kama ndiyo nia/lengo logically au legally na nitajitahidi kusoma maoni ya wengine ili nipate concept hii.

Tanganyika ilifutwa tarehe 25,april 1964, kwa nia nzuri ya kutaka kuwa na serikali moja. Kama wazanzibari hawataki hili (itabidi waulizwe) basi hakuna haja ya kuwa na muungano milele, tuwe kwenye mashirikisho.
 
Bongolander,

Kimsingi nakubaliana na hoja yako kuu, kwamba Muungano unatakiwa kuwa wazi na uboreshwe. Lakini kuna baadhi ya mambo ambayo sikubaliani na wewe.
Nakubaliana na kukuunga mkono kutokana na kujadili suala hili kwa hoja. Na siku zote wasio na elimu na wajinga, yaani ambao hawana uwezo wa kujibu hoja kwa hoja, ndio wanaotoa vitisho. Nasikitika sana kuona kuwa unatishiwa, unachosema ni haki ni kweli, na ni vema tukijadili wazi ili tukielewe,

Nashukuru sana kwa mchango wako, lakini pia kwa kunipa moyo nisirudi nyuma; Kuhusu suala la hoja kujibiwa kwa hoja, hata chama chenyewe yani CCM kinasema hivi kupitia ibara ya 53 ya Mwongozo wa CCM:

["Chama cha kijamaa kama vile CCM ni chombo cha uongozi. Hakifanyi kazi kwa amri zisizo msingi wala kufanya kazi zao kwa nguvu au vitisho vya nguvu; Kinaongoza kwa kuelimisha, kwa kuwashirikisha watu na kwa kuonesha njia na kwahivyo basi msingi wa nguvu zake na kuaminika kwake unatokana na kukubalika kwake kihalali miongoni mwa UMMA, mchanganyiko wa wanachama wake na msingi mzuri wa kisiasa ambayo inakwenda sawa na matakwa ya UMMA; ili kuweza kutimiza lengo hilo chama kinahitaji kuwa na NGUVU YA HOJA NA SIO HOJA YA NGUVU;"]

Hoja yako kuhusu mawaziri lakini pia viongozi mbalimbali wa CCM wa pande zote mbili za Muungano kuwa na misimamo tofauti juu ya Muungano wetu wakiwa kwenye vikao vyao vya kijamii, lakini kuwa na mtazamo wa kinafiki wanapokuwa majukwaani ni hoja sahihi kabisa; Lakini tufahamu kwamba wanafanya hivi kutokana na maslahi ya Chama chao na pia matumbo yao, na sio kwa ajili ya maslahi ya taifa; Ujue kwamba viongozi hawa wamekula viapo vya kuilinda na kuitetea katiba mbovu ya tuliyonayo sasa, lakini kama ulivyosema, chini kwa chini wana msimamo tofauti, hivyo basi kutokuwa wanaitetea kwa dhati;

Vile vile ufahamu kwamba sera ya Chama chao yani CCM ni Mfumo wa Serikali Mbili, na hilo lipo katika katiba ya Tanzania (1977), katiba ambayo CCM ilishika hatamu na kuwa superior kwa katiba ya nchi; with a few exceptions, this supremacy bado ipo hadi leo;

Bongolander, kinachokiua chama hivi sasa ni kukosekana kwa element ya ‘Tea Party'; Vyama vya siasa duniani kote huwa vinapitia changamoto mbalimbali kidira, kisera, n.k, lakini katika nchi zilizoendelea kidemokrasia, changamoto hizi huwa haziui vyama hivi, kwani kutokana na wanachama kupewa nafasi ya kukosoa chama, na pia kukosoana, vyama hivi huwa vinaendelea kupata imani mbele ya umma; Tazama suala la Republican party marekani kwa mfano, kwani bila ya uwepo wa TEA PARTY, chama hiki kingekuwa katika hatari kubwa ya kukaa benchi kwa kipindi kirefu sana ngazi ya Urais wa USA;

Tunahitaji tea party CCM, tena itakayoongozwa na vijana, huku wazee wao wakiwa ni washauri wakuu; Lakini kwa hali ya sasa, kanuni iliyopo ni ile ya "MSIMAMO WA CHAMA", na Either "You are With Us or Without US." Inapotokea wanachama au viongozi fulani fulani wanakikosoa chama kwa maslahi ya wazi kabisa ya taifa, wanaambiwa "WAKITAKA, WAONDOKE ZAO." Hii ndio hali halisi iliyopo ndaani ya chama chetu cha CCM, chama kilichoshiriki kuunda Muungano, lakini kilichochukua hatamu taratibu kikiwa TANU, kupitia Katiba ya Muda, 1965, na hatimaye kuchukua hatamu kwa ujumla, kupitia katiba ya JMT (1977), na kwa bahati mbaya sana, kwa mwendo wa kuvuruga Mkataba wa Muungano, 1964, badala ya kuujenga;

Lakini hebu tuangalie hoja za sasa. Anayesema anataka Zanzibar iwe huru maana yake nini? Na Zanzibar itakuwa tofauti kwa namna gani na sasa baada ya kuwa huru? Kuna hoja nyingi mbazo kwangu huwa naona ni za kipuuzi.
Iwapo unautazama Muungano wetu kwa kutumia Mkataba wa Muungano, 1964 kama kioo, nadhani utaelewa maana ya Zanzibar kutaka kuwa huru ni nini; Uhuru unaopiganiwa na Zanzibar ni autonomy ndani ya Muungano; Lakini hili linazidi kupotoshwa, hasa na viongozi kwa maslahi ya kisiasa; Ndio maana nakubaliana na mzee mwanakijiji kwamba wazanzibari wanapiga tu porojo kuhusu suala la kujitoa, lakini hawana uthubutu wa kufanya hivyo kwa vitendo; Bottom line hapa ni kwamba – ndugu zetu wazanzibari wamekuwa wanapigania autonomy na vile vile democracy, na hivi vingepatikana, wasingekuwa na vilio vyao vya sasa; vinginevyo, mpaka haya yafanyike, the union friction will remain to be the ZANZIBAR QUESTION, na pole pole kuchukua sura ya pili ya the TANGANYIKA QUESTION;

Angalia ni vipi ZNZ italipa gharama za idara zile za muungano zikiwa nje ya muungano, ni vipi itapoteza soko kwa wafanyabiashara wake waoneemeka huku bara, ni vipi wanaweza kumudu chakula kutoka bara kwa Forex, na kuingia bara kwa visa. Au wazenji wote wa bara kuwa foreigners na kuanza kuishi kwa vibali. Angalia econimics ya Zanzbiar kwanza. Ukiangalia hata Seif Sharif Hamadi Mwenyewe unaweza kuona kaka yake ana hoteli pale kisutu kama hawapendi muungano sijui kwanini walijenga ile hoteli pale kistu na zile biashara zao za jumba la sinema kule Mbeya.

Kwa hiyo ukisikia siasa unaona haziendani na realities za uchumi. So let us think of this without Seif Sharif's infulence na siasa zake.

Kuna suala linakuwa overlooked hapa na ni suala muhimu sana; ningewaomba nguruvi3, joka kuu na Mzee Mwanakijiji walitazame hili pia kwa muda wao; Suala hili litajibu hoja yako kuhusu economics za Zanzibar na madhara yake kwa Muungano wetu;
Mwaka 1964, mara tu baada ya mkataba wa Muungano kusainiwa, sheria mpya ya Muungano ilipitishwa to ratify makubaliano ya Muungano; lakini cha ajabu, badala ya kufanya ratification, bila ya kuongeza au kupunguza kitu ndani ya Mkataba wa Muungano, Sheria hii ikaanza uchakachuaji wa wazi wa Mkataba wa Muungano; Nilishajadili hili kwa kina elsewhere;

Nikirudi kwenye hoja ya msingi juu ya Economics Zanzibar, makosa yalitokana na ukiukwaji wa aidha makusidi, au bahati mbaya, wa Mkataba wa Muungano, 1964. Nitafafanua:

Mwaka 1964, Serikali ilikuja na Tangazo namba 245 lenye mahusiano na Sheria Mpya ya Muungano, 1964; Tangazo hili lilikuwa na ‘title' iliyosema:

"AMRI YA UTARATIBU WA KIPINDI CHA MPITO, 1964".

Wakuu zangu Bongolander, nguruvi3, Jokakuu, Mzee Mwanakijiji na wengine, nasisitiza tena "AMRI ya utaratibu."

Huu ndio ukawa umungu wa Tanganyika iliyojificha nyuma ya pazia la Tanzania kupitia sheria namba 24, ya bunge, 1967.

Tofauti na amri kumi za Mungu, Amri hizi zilikuwa jumla kumi na moja, lakini focus yangu hapa ni kwenye Amri namba tisa ambayo ilitamka hivi:

"(9) Mali zote na haki juu ya mali zote za aina yoyote ambazo zinamilikiwa na Serikali ya Tanganyika na pia mali zote na haki yote juu ya mali za JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR zinazomilikiwa au kutumiwa kuhusiana na masuala ya Muungano, zitakuwa kuanzia siku ya Muungano katika miliki ya Jamhuri ya Muungano"

Ukitazama hapa kwa makini, nadhani utapata jibu juu ya Economics za Zanzibar; Vile vile, ina maana chini ya Amri hii, Kwanza, Tanganyika ikaanza kupewa hadhi sawa na Tanzania, bila ya kushirikisha upande wa Zanzibar, lakini mbaya zaidi, kinyume na Mkataba wa Muungano, 1964; Pili, na muhimu zaidi – Amri hii ilikuwa ni sawa na kuinyang'anya Zanzibar Mali zake na kuzipeleka Tanganyika, huku tukikumbuka kwamba miaka mitatu baadae, Tanganyika ikafutwa kwa mujibu wa sheria ya bunge namba 24, 1967, na kubadilishwa jina kuwa Tanzania;

Kumbuka kwamba, hii nyang'anya nyang'anya ya mali ilitokea ndani ya miezi mitatu tu ya mapinduzi ya Zanzibar wakati jamhuri hii uhuru ya Zanzibar ilipokuwa inajiweka sawa katika dhamana zake mpya kama jamhuri na dola huru; Pia MALI ZAKE HIZI, zilikuwa hata hazijafanyiwa tathmini yoyote; tathmini ilikuwa ni muhimu iwapo ingebidi mali hizi zije kufidiwa na serikali ya JMT baada ya kuzichukua;

Pia kuhusu swali lako muhimu kwamba:

tuliungana kwa sababu gani?

Una maana per articles of the Union, au njozi zilizokuwepo kabla ya hapo?

Sikubaliani na wewe kuwa bila Tangayika Muungano hauwezekani

Naheshimu hoja hii, kwani mgongano wa mawazo ni jambo la kawaida; kama huwa unatembelea uzi wa Nguruvi3 wenye jina ‘mgongano wa mawazo', nadhani utabaini nina maanisha kitu gani;

Ningependa kuja na counter argument ifuatayo:

Mimi nauangalia Muungano kwa kuanzia tarehe ya Mkataba wa Muungano, 1964; siangalii Muungano wetu kwa tarehe kabla ya hiyo; hivyo, kwa mantiki rahisi tu, neno Muungano maana yake rahisi ni kuleta pamoja vitu viwili ambavyo ni independent vishirikiane huku kila upande ukiwa na independence au autonomy katika mambo ambayo wamekubaliana yasiye chini ya serikali kuu ya shirikisho;

Hoja yako kwamba bila Tanganyika Muungano unawezekana, ni lazima itakuwa hoja isiyo angalia historia ya Muungano wetu kwa kuanzia tarehe ile Mkataba wa Muungano ulipotiwa saini; Iwapo Zanzibar hakuungana na Tanganyika kuleta Muungano wa Tanzania, then Zanzibar aliungana na nani?

What if Zanzibar dies like Tanganyika did? Muungano hautawezekana?

Swali zuri na muhimu sana; Muungano utawezekana lakini hautakuwa na nguvu na uhalali wa kisheria ndani ya nchi shirikishi, na pia JMT;

Na mimi nikuulize:

Kwa mujibu wa Katiba ya JMT (1977), ambayo CCM ilikamata HATAMU na kuwa na mamlaka hata juu ya Katiba hii, Muungano wetu ni baina ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, sio tena baina ya Tanganyika na Zanzibar kwa Mujibu wa makubaliano ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964.

Swali langu kwako ni:

Je:
Muungano huu kwa mujibu wa Katiba ya JMT (1977), unawezekana?
 
Hapo kwenye nyekundu ndipo tulipokuwa tunabishana muda wote huu.Articles of the union zimeonyesha nia hiyo, jinsi zilivyokuwa drafted from the begginning.Nilikuwa nasisitiza nia hiyo, hata kama ningekuwa hakimu, ningekubaliana wazi kuwa hapo kwenye mkataba kulikuwa na nia ya kuwa na serikali moja.

Sikubaliani na wewe katika hili; Lakini pamoja na hayo, naomba nikuulize swali:

Inakuwaje sasa Sera RASMI ya Chama Cha Mapinduzi ni Muungano wenye Serikali Mbili?

Twende taratibu, tutafikia ukweli kwani lengo langu sio to win arguments bali to find the truth;

 
Sikubaliani na wewe katika hili; Lakini pamoja na hayo, naomba nikuulize swali:

Inakuwaje sasa Sera RASMI ya Chama Cha Mapinduzi ni Muungano wenye Serikali Mbili?

Twende taratibu, tutafikia ukweli kwani lengo langu sio to win arguments bali to find the truth;

Hata mimi sielewi.
Serikali mbili ni sera iliyoshindwa na haileti maana yeyote. Serikali moja ndiyo lengo na nia ya muungano.
Haya ya serikali mbili au tatu ni kutapatapa kwa JMT ambako kumetokana na serikali ya Zanzibar kutaka autonomy tangu 1984. Hapo ndiyo ilipodhihirika wazi kuwa hawataki muungano kama tunavyotaka sisi watanganyika.
 
Haya ya serikali mbili au tatu ni kutapatapa kwa JMT ambako kumetokana na serikali ya Zanzibar kutaka autonomy tangu 1984. Hapo ndiyo ilipodhihirika wazi kuwa hawataki muungano kama tunavyotaka sisi watanganyika.

UKIMWI FULL BLOWN ndio ulitokea mwaka 1984, lakini udhaifu wa kinga mwilini ulikuwa ukiendelea kupitia homa za mara kwa mara,kujisikia uchovu, kukosa hamu ya kula, n.k, tangia sheria ya Muungano ilipopitishwa 1964, na kuchakachua Mkataba wa Muungano;

Hata mimi sielewi.
Ni sawa na jibu 'Sielewi kwanini Tanzania Maskini', hivyo mbali ya kusisitiza usome bandiko langu tena namba 94 na unijibu yale maswali niliyoelekeza kwako, niliyo omba unijibu tena na tena na tena na wewe kupuuzia, basi i rest my case on this point;

Serikali mbili ni sera iliyoshindwa na haileti maana yeyote. Serikali moja ndiyo lengo na nia ya muungano.

Maana yake ikiwa kwamba, mpango wa kuchakachua Mkataba wa Muungano, 1964, ili usiendane na malengo yake ya kuja na shirikisho, UMESHINDWA; Mkataba ule haukulenga serikali moja, wala mbili, bali tatu, huku ikitarajia kupindisha mambo, pengine kwa nia nzuri, baada ya Mkataba kusainiwa, kwa kuanzia na uchakachauaji wa:

-Sheria ya muungano sheria namba mbili;
-uchakachuaji wa masharti ya Mkataba wa Muungano Per section three of the articles of the union, na
-chakachuaji wa ibara ya saba ya mkataba we muungano;


Na safari ya kuelekea serikali mbili, na baadae moja ilianza na kuuliwa kwa Tanganyika chini ya sheria namba 24 ya bunge la JMT, 1965; Ilipofika mwaka 1977, bunge hili hili likaichakachua Zanzibar na kuibadili jina kuitwa Tanzania Zanzibar, huku Tanganyika ambayo 1967 ilibadilishwa jina kuwa Tanzania (huku muungano pia ukiitwa TANZANIA), mwaka 1977 Tanganyika ya zamani nayo ikaitwa Tanzania Bara; Wazanzibari sasa wakaona kwamba very soon, changes za Zanzibar, to Tanzania Zanzibar, zitapelekea hata jina Zanzibar kuuliwa kwa mujibu wa sheria, na kuitwa sijui kitu gani?, na kuweka mazingira ya kuhalalisha serikali moja unayoisemea, KINYUME NA MKATABA WA MUUNGANO, 1964;

Suala la serikali moja ni suala la kulazimisha, especially in contrary to articles of the Union; Kama unataka iwepo, itakuwepo, kama serikali mbili za sasa zinavyolazimisha; Swali langu kwako:

Iwapo serikali mbili za sasa hazina uhalali wa kisheria, serikali moja itakuwa na uhalali upi?

Nadhani tukubali kutokukubaliana, na tusonge mbele kwenye hoja nyingine, wenye kukuunga mkono watakuunga mkono, wenye kuniunga mkono mimi, wataniunga mkono; vinginevyo kwangu mimi, haya ni maandalizi tu ya kujipanga ili referendum ikija, wenye kufanya uamuzi wa busara wafanye hivyo;
 
Siyo ukimwi full blown, ni more like Polonium poisoning ya muungano (result of a coward act). Matokeo ya maamuzi ya kidikteta kwa upande wa Zanzibar hasa Karume na baadae Seif, uamsho, kamahuru, CUF n.k

Kunirudisha kwenye hoja # 94 ni sawa na kupoteza muda wako. Msimamo wangu kuhusu nia ya muungano ni serikali moja na hoja zako kuwa articles of the union ilitaka serikali tatu inaweza kumake sense kwa watu wengine but so far sijui kwanini unaona mashiko ya hoja hii. Ili tusipoteze sana muda, ningeomba niangalie wengine wanavyoshusha hoja zao na so far sijaona mtu aliyeunganisha hizo articlkes na niua ya kuwa na serikali tatu.

Nikirudi kwenye maamuzi ya kidikteata, ni kuwa umaarufu wa mapinduzi ya mwaka 1964 ulikuwa exaggerrated, ilikuwa ni timing mbaya kujiunga na Zanzibar tukitegemea Karume aliwakilisha mawazo ya wazanzibari wengi bila kuwa na refferrendum au serikali iliyochaguliwa kama ya TANU. ASP na UMMA havikuwa kama TANU na ANC ya kina Mtemvu. The politics within Zanzibar were too complicated to form a union, any union.

Mradi tumekubaliana kuwa nia ya muungano ni kufikia hatima ya kuwa na serikali moja (ingawa wewe umeiita njozi aliyokuwa nayo mwalimu baada ya 1965) basi mimi najiona kama nimeshinda argument, even though ninge appreciate truth seekness element of arguing pia, but let me read from others ili nione mantiki ya serikali tatu.

Kwa kumalizia naomba nirudie ..... Tanganyika ilikufa tarehe 25, April 1964 kukiwa na nia ya kuleta serikali moja, nchi moja. Zanzibar siyo nchi, itakuwa nchi kama Tanganyika itarudi na tutashirikiana kwenye mashirikisho ya jumuiya za kimataifa. The rest is just politics
.
 
Tanzania tuna issues kubwa sana za kujadili,

Mojawapo ni muungano unatumia resources zetu hasa akili zetu.

Muungano thing can wait.

Muungano must go ili kupisha burning issues za uchumi na maendeleo.

Mpaka hapo nakubalianana wewe, ingawa kama muungano utaondoka kupitia referendum, sio maamuzi ya viongozi;

Sasa hivi tatizo kubwa kwa Tanzania ni kwamba hatuna leadership, kuna utapeli mwingi (aka ufisadi), umaskini, haki, miundo mbinu nk nk, these are burning issues, Muungano is in no way a cause of that.

Naelewa hoja yako ya msingi hapa ni nini; Nilijadili jinsi gani mfumo wa sasa wa muungano ni mzigo kuliko tungekuwa na serikali tatu, kinyume na upotoshwaji wa kisiasa unaoendelea; nilijadili mengi, na ilikuwa kujibu hoja ya Kobello na ndamo emmanuel, kwamba Serikali tatu itakuwa ni mzigo; ukipata muda, naomba upitie bandikonamba '85' la uzi huu; Kwa sasa naomba kusikia maoni yako kuhusu hoja yangu hii ambayo nimeichukua kama ilivyokuwa katika majibu yangu kwa kobello na ndamo emmanuel, nikilenga hasa kusikia mawazo yako in relation to nilicho ku-quote hapo juu. Nilisema hivi:

...Sababu nyingine kwanini shirikisho ni bora zaidi kwa wananchi ni kwamba – Serikali kubwa kama hii yetu ya JMT– ambayo tuna aminishwa ni Serikali mbili, ukweli ni kwamba – serikali ya Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA inasimamia mambo yote ya muungano na yale ya Tanzania Bara (TANGANYIKA), ambayo SIYO ya Muungano, kama Afya, Elimu n.k; Huu ni mzigo mkubwa, lakini pia ni gharama kubwa zaidi kwa walipa kodi; Serikali ya sasa ya JMT ipo more Centralized na ni kubwa sana kuliko ingekuwa chini ya mfumo wa shirikisho; Tatizo jingine linalojitokeza hapa ni kwamba, mfumo wa sasa una ‘encourage’ wasteful lobbying of different interest groups, suala ambalo Wachumi wanalijadili kama dhana ya ‘RENT SEEKING’ – kwa maana rahisi, rent seeking ni utafutaji wa benefits & priveledges za different interest groups, e.g. wawekezaji pamoja na wale wote wanaotaka kufanya biashara na Serikali; Tumekuwa tunashuhudia hili kwa miaka mingi sana tabia hii ya rent seeking; mabilioni yaliyopo Uswisi ni moja ya mifano hai;

Ni rahisi sana kwa tabia ya rent-seeking kulelewa chini ya mfumo wa serikali kubwa na centralized kama hii ya JMT kuliko chini ya serikali ndogo ambayo ipo more decentralized - shirikisho; kwa maana nyingine, ni rahisi sana kwa wananchi/UMMA kuona nini kinaendelea chini ya mfumo wa shirikisho kuliko chini ya mfumo wa sasa ambao, bila ya wabunge kuamua kumwaga siri hadharani, au watendaji serikalini kuamua kuvujisha siri za serikali, nchi yetu chini ya mfumo wa serikali mbili wa JMT, itaendelea kitafunwa mchana kweupe; Hii ni gharama kubwa kwa walipa kodi kwa maana rahisi sana – miradi mingi nchini, chini ya serikali ya mfumo wa sasa, maamuzi yake hayapo transparent, haieleweki upande gani wa muungano unachangia na unachangia kwa lipi, miradi mingi wananchi hawaijui, hawashirikishwi kimaamuzi, na tumeona kwamba wananchi wakija fahamu juu ya miradi hii, huwa hawaridhii baadhi ya miradi hiyo; ingawa inafanikishwa kupitia fedha zao; mifano hai ya miradi ya namna hii mnaijua...

Kwa sababu nisizo fahamu, hakuna aliyekuja ku challenge hoka hii; ipo kwa kirefu kwenye bando namba '85.'
 
Mchambuzi na Kobello,mkitaka kujuwa huu muungano ni fyongo,ama kwamba ulishindwa kabla hata haujaanza,ni kwamba "muungano" wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa mwaka 1964,lakini tena mwaka 1965,kukaja kitu kinaitwa "makubaliano 11 ya muungano",sasa hapo utajiuliza kile walichokubaliana 1964 ni kipi hadi waje kuainisha hayo mambo 11?muungano ulikuwa wa kukurupuka na ndiyo maana hayaishi haya mambo,mtabishana wee!lakini ukweli ndo huo,muungano huu ni wa kuvunjilia mbali halafu kama kuna haja ya kuungana tukae chini upya.

Kitangulie kipi, kuvunja muungano au kurudisha Tanganyika?
 
Kobello,

THESE ARE NOT SURBODINATE TO EACH OTHER: Badala yake, serikali shirikishi are co-ordinate and of equal power and jurisdiction in their own sphere; THEY ARE MASTERS IN THEIR OWN HOUSE;

cc: nonda
Kweli huu muungano ni kizungumkuti,hivi bado rais wa Zanzibar anachukuliwa kama "Mwakilishi/msaidizi wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwenye masuala yote ya kiutawala ya Zanzibar"?
 
Kitangulie kipi, kuvunja muungano au kurudisha Tanganyika?
Tukivunja muungano Tanganyika inarudi automatically.Kwa jinsi tulivyokwisha ona haya mambo ya muungano ambapo kweli ni kiini macho,kuirudisha Tanganyika hakuta solve lolote,the issue is bigger than that.Mambo yalifanywa haraka haraka bila kufikiri,na ndilo tatizo la kutokuwa na referendum,penye wengi hapaharibiki neno.
 
Kumbe mwalimu alikuwa ameweka wazi hayo maneno.. sasa kwanini CCM sasa hivi hawataki kusikia hoja za muungano

Wanaficha mambo gani nyuma ya muungano..?

Na hawa CUF plus wazanzibar kwanini bado wanaikataa chadema while chadema wanaweza na wana nia ya kuwapa hilo wanalo taka.. Zanzibar yenye mamlaka kamili?

Siwaelewi hawa watu,

Sera rasmi ya CCM ni Serikali mbili; its more of a liability than an asset katika siasa za sasa kwenda kugeuza kile ilichokifuta mwaka 1967 yani Tanganyika, kupitia sheria namba 24 ya bunge; It is an asset for Chadema, iwapo hilo litatokea, but a liability kwa CCM;

Kuhusu CUF kuikataa Chadema - Chadema ni chama cha tanganyika, kama ilivyokuwa TANU kabla ya Muungano; Uwepo wa Chadema ni kwa kupitia tu masharti ya Msajili wa vyama vya siasa;

Chini ya mfumo wa sasa wa serikali mbili, proper and effective presence ya Chadema Zanzibar itatokea iwapo tu Chadema watafunga ndoa na chama kingine cha upinzani Zanzibar (nje ya CUF), kwa mtindo ule ule wa TANU na ASP; Nje ya hapo, ni Chadema kuja na ujasiri wa kuanzisha hoja ya kuzaliwa Tanganyika, na ikiwezekana, hoja ya kuua muungano, kwa kuelimisha umma juu ya kinachoendelea, kwani hata Nyerere alishasema kama UMMA wa wazanzibari hautaki, hatowapiga mabomu, ata waacha waende na Zanzibar yao;

Je Chadema wana ujasiri huo? Wakiupata na waufanyia kazi vizuri, CCM itakufa, na wala haitabakia kuwa chama cha upinzani, kwani legitimacy and credibility ya CCM zilikuwa on two fronts: Moja azimio la arusha, lakini wameliua na kuleta azimio la zanzibar ambalo ndio limezaa ufisadi, kete ambayo Chadema wanacheza nayo vizuri sana; and the second front ya legitimacy and credibility ya CCM, actually the only remaining one ni Muungano, na ni hapa ndio siasa za chama kinachodumisha amani na utulivu zinapotokea; Muungano ukiondoka, CCM imeondoka kwani muungano ulianza na muungano wa siasa - TANU + ASP, kwa mategemeo kwamba, it would trickle down to the ECONOMICS and SOCIAL; Hili halikutokea, na halitatokea;

The Bottom Line is, nje ya nguvu ya dola, CCM is done, mjadala ni EXIT STRATEGY;
 
Kweli huu muungano ni kizungumkuti,hivi bado rais wa Zanzibar anachukuliwa kama "Mwakilishi/msaidizi wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwenye masuala yote ya kiutawala ya Zanzibar"?

Mwakilishi wake sasa ni Bilal, kwani kwa vile CCM haikujiandaa kuwa na vyama vingine vya upinzani, katiba ya 1977 ilijipanga kama vile CCM itashika hatamu daima; Lakini haikuwa kama walivyotegemea kwani vyama vingi vikaingia 1990s baada ya mageuzi; Ndio maana ikabidi CCM ijipange haraka, na Jaji Bomani akapewa jukumu la kushauri juu ya hilo; Akakamilisha ripoti yake ambayo ndiyo iliyopendekeza mfumo wa mgombea mwenza, huku akisema ameuchumua toka mfumo wa USA na kwamba utatufaa;

Hivi ndivyo CCM ikapona na aibu ya uwezekano wa CCM kushinda bara, na upinzani Zanzibar, hivyo kukosa mamlaka ya kuunda serikali; it was Dr. Omar Juma, Dr. Shein, na sasa Dr. Billal kwa sasa ndio wanachukuliwa kama "Mwakilishi/msaidizi wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwenye masuala yote ya kiutawala ya Zanzibar", ingawa theory and practice vinachanganyana - Shein, Balozi Seif Iddi, Bilal kutokana na GNU Zanzibar; Inategemea swali linalenga nini - mwakilishi wa CCM au Serikali? Both? Mind you, muungano huu ni wa CCM - TANU + ASP kwani ulianza kwanza kisiasa hoping mengine yafuate baadae - the economics, social etc....

Kwa kifupi, CCM is paying for ukiukwaji wa mkataba wa Muungano, 1964;
 
Sera rasmi ya CCM ni Serikali mbili; its more of a liability than an asset katika siasa za sasa kwenda kugeuza kile ilichokifuta mwaka 1967 yani Tanganyika, kupitia sheria namba 24 ya bunge; It is an asset for Chadema, iwapo hilo litatokea, but a liability kwa CCM;

Kuhusu CUF kuikataa Chadema - Chadema ni chama cha tanganyika, kama ilivyokuwa TANU kabla ya Muungano; Uwepo wa Chadema ni kwa kupitia tu masharti ya Msajili wa vyama vya siasa;

Chini ya mfumo wa sasa wa serikali mbili, proper and effective presence ya Chadema Zanzibar itatokea iwapo tu Chadema watafunga ndoa na chama kingine cha upinzani Zanzibar (nje ya CUF), kwa mtindo ule ule wa TANU na ASP; Nje ya hapo, ni Chadema kuja na ujasiri wa kuanzisha hoja ya kuzaliwa Tanganyika, na ikiwezekana, hoja ya kuua muungano, kwa kuelimisha umma juu ya kinachoendelea, kwani hata Nyerere alishasema kama UMMA wa wazanzibari hautaki, hatowapiga mabomu, ata waacha waende na Zanzibar yao;

Je Chadema wana ujasiri huo? Wakiupata na waufanyia kazi vizuri, CCM itakufa, na wala haitabakia kuwa chama cha upinzani, kwani legitimacy and credibility ya CCM zilikuwa on two fronts: Moja azimio la arusha, lakini wameliua na kuleta azimio la zanzibar ambalo ndio limezaa ufisadi, kete ambayo Chadema wanacheza nayo vizuri sana; and the second front ya legitimacy and credibility ya CCM, actually the only remaining one ni Muungano, na ni hapa ndio siasa za chama kinachodumisha amani na utulivu zinapotokea; Muungano ukiondoka, CCM imeondoka kwani muungano ulianza na muungano wa siasa - TANU + ASP, kwa mategemeo kwamba, it would trickle down to the ECONOMICS and SOCIAL; Hili halikutokea, na halitatokea;

The Bottom Line is, nje ya nguvu ya dola, CCM is done, mjadala ni EXIT STRATEGY;
CUF ndiyo tatizo kwenye issue hii,kwasababu wameingilia ndoa ya TANU na ASP,pengine kwa kukubali kuwa kimada,maana hawajaungana na CCM kuwa kitu kimoja kama ambavyo tunaamini ndoa huunganisha watu wawili kuwa kitu kimoja.(kama ilivyokuwa kwa TANU na ASP)

Kama sikosei,CUF kina nguvu zaidi kule Pemba,na CCM kina nguvu zaidi Unguja,hapo utaona kuwa kama si kubaguana,basi CUF isngepata nguvu Zanzibar na muungano kati ya TANU na ASP ungetosha kuwaunganisha wazanzibari,jambo ambalo halikutokea.

Kwasababu ni shida kuwaunganisha wazanzibari wenyewe(kumbuka nilishasaema hakuna Zanzibar nje ya muungano na haitatawalika),basi ina maana chadema hawataweza kupata chama cha kushirikiana nacho kule Zanzibar,unless kianzishwe chama ambacho kitakuwa na influence kwenye sect mojawapo ya wazanzibari,ama labda kuwepo na chama chenye influence in both Unguja na Pemba.

CCM na CUF vina influence huko Zanzibar,lakini ninakuhakikishia kinaweza kuanzishwa chama chenye mwelekeo wa tofauti na ule wa CUF na CCM na kikapata wanachama,lakini mwelekeo huo lazima uwe wa kibaguzi.
 
ZNZ = Zanzibar Nzuri Zamani
 

Attachments

  • znz.jpg
    znz.jpg
    57.3 KB · Views: 45
CUF ndiyo tatizo kwenye issue hii,kwasababu wameingilia ndoa ya TANU na ASP,pengine kwa kukubali kuwa kimada,maana hawajaungana na CCM kuwa kitu kimoja kama ambavyo tunaamini ndoa huunganisha watu wawili kuwa kitu kimoja.(kama ilivyokuwa kwa TANU na ASP)

Kama sikosei,CUF kina nguvu zaidi kule Pemba,na CCM kina nguvu zaidi Unguja,hapo utaona kuwa kama si kubaguana,basi CUF isngepata nguvu Zanzibar na muungano kati ya TANU na ASP ungetosha kuwaunganisha wazanzibari,jambo ambalo halikutokea.

Kwasababu ni shida kuwaunganisha wazanzibari wenyewe(kumbuka nilishasaema hakuna Zanzibar nje ya muungano na haitatawalika),basi ina maana chadema hawataweza kupata chama cha kushirikiana nacho kule Zanzibar,unless kianzishwe chama ambacho kitakuwa na influence kwenye sect mojawapo ya wazanzibari,ama labda kuwepo na chama chenye influence in both Unguja na Pemba.

CCM na CUF vina influence huko Zanzibar,lakini ninakuhakikishia kinaweza kuanzishwa chama chenye mwelekeo wa tofauti na ule wa CUF na CCM na kikapata wanachama,lakini mwelekeo huo lazima uwe wa kibaguzi.
Inasemekana, lakini iwapo sipo sahihi, wa kuelewa zaidi wanielimishe, kwamba - TANU ilipata support kubwa sana Zanzibar kutoka kwa kundi ambalo lilikuwa linapingana na mtandao wa ASP chini ya Karume ambao waliona ni wa kidikteta n.k; Madai yanazidi kusema kwamba - wazanzibari wengi wakati ule walikuwa wapo tayari chama kingine chochote kije kuikaba ASP, whether ni TANU etc, na yaliyotokea ndio yakatokea....;

Vile vile kuna suala linanitatiza kidogo - Jumbe alikuwa anataka kurudi kwenye Mkataba wa Muungano, 1964, hasa kurudishwa kwa autonomy ya ZNZ, ndio maana yakamkuta yaliyomkuta; Seif hakuwa na jumbe katika hilo; Je kwa waelewa wa haya mambo kwa kina, swali linalofuatia hapa ni JE: Tofauti kubwa ya mtazamo baina ya Jumbe wakati ule na Seif miaka hii ni nini?
 
Mwakilishi wake sasa ni Bilal, kwani kwa vile CCM haikujiandaa kuwa na vyama vingine vya upinzani, katiba ya 1977 ilijipanga kama vile CCM itashika hatamu daima; Lakini haikuwa kama walivyotegemea kwani vyama vingi vikaingia 1990s baada ya mageuzi; Ndio maana ikabidi CCM ijipange haraka, na Jaji Bomani akapewa jukumu la kushauri juu ya hilo; Akakamilisha ripoti yake ambayo ndiyo iliyopendekeza mfumo wa mgombea mwenza, huku akisema ameuchumua toka mfumo wa USA na kwamba utatufaa;

Hivi ndivyo CCM ikapona na aibu ya uwezekano wa CCM kushinda bara, na upinzani Zanzibar, hivyo kukosa mamlaka ya kuunda serikali; it was Dr. Omar Juma, Dr. Shein, na sasa Dr. Billal kwa sasa ndio wanachukuliwa kama "Mwakilishi/msaidizi wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwenye masuala yote ya kiutawala ya Zanzibar", ingawa theory and practice vinachanganyana - Shein, Balozi Seif Iddi, Bilal kutokana na GNU Zanzibar; Inategemea swali linalenga nini - mwakilishi wa CCM au Serikali? Both? Mind you, muungano huu ni wa CCM - TANU + ASP kwani ulianza kwanza kisiasa hoping mengine yafuate baadae - the economics, social etc....

Kwa kifupi, CCM is paying for ukiukwaji wa mkataba wa Muungano, 1964;
Ok mkuu,so mimi swali la msingi kwasasa ni hili;Ni kipengele ama vipengele gani haswa vya mkataba wa muungano 1964 ambavyo CCM walivikiuka na kwamba vingeufanya muungano huu kuwa stronger na bila viini macho?

Kwasababu one side of the coin,ni kama serikali ya Zanzibar ni subordinate,and on the side,tunaamisnishwa kwamba sivyo.Na hilo ndilo nadhani lilisababisha waangalie kwamba ni mambo gani ni ya muungano na yapi ni siyo ya muungano.Na hayo ndiyo yanaleta utata hadi siku ya leo.Hadi viongozi wetu wanashindwa kuja na majibu ya kueleweka,wengine wakisema Zanzibar ni nchi,wengine wakisema siyo.Nadhani unakumbuka kauli za kuchanganya,hata hivi majuzi tu Pinda naye alionekana kutoa kauli ya kuchanganya.
 
Ok mkuu,so mimi swali la msingi kwasasa ni hili;Ni kipengele ama vipengele gani haswa vya mkataba wa muungano 1964 ambavyo CCM walivikiuka na kwamba vingeufanya muungano huu kuwa stronger na bila viini macho?

Kwasababu one side of the coin,ni kama serikali ya Zanzibar ni subordinate,and on the side,tunaamisnishwa kwamba sivyo.Na hilo ndilo nadhani lilisababisha waangalie kwamba ni mambo gani ni ya muungano na yapi ni siyo ya muungano.Na hayo ndiyo yanaleta utata hadi siku ya leo.Hadi viongozi wetu wanashindwa kuja na majibu ya kueleweka,wengine wakisema Zanzibar ni nchi,wengine wakisema siyo.Nadhani unakumbuka kauli za kuchanganya,hata hivi majuzi tu Pinda naye alionekana kutoa kauli ya kuchanganya.

Kwanza tuweke suala hili kwenye muktadha uliopo sahihi; Yapo mengi lakini nitajadili yale ya msingi kwanza:

Kwanza – Mkataba wa Muungano, 1964, haukuweka masuala ya siasa za ndani ya nchi shiriki kama sehemu ya yale masuala kumi na moja ya Muungano;

Pili – Mkataba wa Muungano, 1964, uliweka masharti mengi lakini muhimi ni pamoja na haya

  • Katiba ya Tanganyika itumike kama katiba ya muda kwa JMT, hasa kwa vile ZNZ haikuwa na katiba yake, lakini kipindi hiki cha mpito kisizidi mwaka mmoja; (Tazama ibara ya pili na ya tatu ya Mkataba wa Muungano, 1964).

MUHIMU – Mkataba ukasema, katiba hii ya Tanganyika itumike kwa Muda chini ya SHARTI kwamba KWANZA - ifanyiwe marekebisho kadhaa ambayo yataitambua Zanzibar in terms of autonomy etc, katika kile kipindi cha mpito, mpaka pale Zanzibar itakapojiweka sawa; Sharti hili lipo ibara ya tatu ya mkataba wa muungano 1964, lakini halikutimizwa na badala yake katiba ya Tanganyika ndio ikawa ya JMT (including kwa masuala ya ZnZ, bila ya marekebisho).


  • Sharti la pili chini ya mkataba wa Muungano ni kwamba (ibara ya saba), katika kipindi hiki cha mpito, Rais wa JMT akishirikiana na Makamo wake ambae ni Rais wa ZnZ pia, watateuwa tume ya katiba itakayofuatiwa na bunge la katiba, ili JMT ipate sheria mama na iliyo na uhalali (katiba), vile vile ZNZ na Tanganyika; Sharti hili halikutekelezwa badala yake, bunge la JMT, kupitia katiba ile ile ya TG ambayo haikufanyiwa marekebisho, ikahairisha ibara hii ya saba ya mchakato wa katiba INDEFINATELY; Mbaya zaidi, bunge hili hili pia likapitisha katiba ya Muda ya JMT, kinyume na masharti ya Mkataba wa Muungano, ibara ya saba;

Tatu – Kinyume na Mkataba ambapo masuala ya siasa yaliachwa yawe ya nchi shirikishi, sio Muungano (rejea masuala 11 ya Muungano), TANU ikajipenyeza kwenye katiba ya muda (1965), huku ikitoa masharti kadhaa kwa ASP, kinyume cha Mkataba wa Muungano na kusema kwamba shughuli zote za kisiasa zitaendeshwa chini ya mamlaka ya Chama; Lakini muhimu hapa ni kwamba – Katiba ile ikatamka kwamba, "Kutakuwa na Chama Kimoja Cha Siasa", mpaka hapo TANU na ASP vitakapoungana." Nadhani ukichanganya masuala haya mawili utaelewa nini kiliendelea, kwani hali ilibakia hivi hivi kuanzia 1965 chini ya katiba ya muda, mpaka pale TANU na ASP vilipoungana na kuzaa CCM;

Nne – Bunge la JMT mwaka 1967 (bunge lisilokuwa halali kwani lilikuwa linatumia Katiba ya Tanganyika bila ya marekebisho per articles of the Union), likapitisha sheria namba 24 ya kuua Tanganyika, na kuibadili iwe Tanzania; Mind you, kuanzia sasa, Tanzania ikawa ni JMT na Tanzania pia ikawa Tanganyika, huku Zanzibar ikiendelea kuwa Zanzibar, lakini huku orodha ya Muungano ikiongezeka;

Tano – Ilipofika mwaka 1977 ambapo TANU na ASP vilizaliwa, CCM ikashika hatamu, na ikawa supreme even to Katika ya nchi ya 1977; Kwahiyo it was not a coincidence kwa TANU = ASP kkungana 1977, na Katiba ya Kudumu kuzaliwa 1977, baada ya nchi kuwa chini ya katiba ya muda kwa miaka kumi na mbili, kusubiria ASP wakubali kujiunga na TANU; Hapa ujue pia kwamba katika kipindi hiki cha miaka kumi na mbili chini ya katiba ya muda, shughuli zote za Siasa zilikuwa zinaendeshwa na TANU;

Sasa ilipofika mwaka 1977 ambapo katiba mpya ilizaliwa, ndani ya katiba ile, Muungano ukapewa jina tofauti na Mkataba wa Muungano; While Mkataba ulisema Muungano ni baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Katika ya 1977 ikasema ni Muungano baina ya TANZANIA BARA na TANZANIA ZANZIBAR; Kama upo makini hapa, ni kwamba Jina la Tanganyika liligeuka kuwa Tanzania 1967, halafu Tanzania bara 1977; kwa upande mwingine, jina la Zanzibar lilibakia kuwa hivyo hivyo kusubiria ASP wakubali ndoa na CCM; Walipokubali tu, Katiba ya 1977 ikabadili jina la Zanzibar kuwa TANZANIA ZANZIBAR; Its no coincidence kwa nchi kupewa mtazamo wa MCHAFUKO WA HALI YA KISIASA, miaka ya mwanzo ya themanini, kwani kina Jumbe walianza kunusa hili - kwamba mwenzako Tanganyika ananyolewa - wewe zanzibar tia maji kwani sasa unaitwa Tanzania Zanzibar, na utaishia kupotea taratibu;

Kuna maeneo mengine mengi sana ambayo CCM baada ya katiba ya 1977 ilizidi kwenda kinyume na Mkataba wa Muungano, 1964, na tutazidi kuyajadili kila nafasi itakapotokea;
 
Inasemekana, lakini iwapo sipo sahihi, wa kuelewa zaidi wanielimishe, kwamba - TANU ilipata support kubwa sana Zanzibar kutoka kwa kundi ambalo lilikuwa linapingana na mtandao wa ASP chini ya Karume ambao waliona ni wa kidikteta n.k; Madai yanazidi kusema kwamba - wazanzibari wengi wakati ule walikuwa wapo tayari chama kingine chochote kije kuikaba ASP, whether ni TANU etc, na yaliyotokea ndio yakatokea....;

Vile vile kuna suala linanitatiza kidogo - Jumbe alikuwa anataka kurudi kwenye Mkataba wa Muungano, 1964, hasa kurudishwa kwa autonomy ya ZNZ, ndio maana yakamkuta yaliyomkuta; Seif hakuwa na jumbe katika hilo; Je kwa waelewa wa haya mambo kwa kina, swali linalofuatia hapa ni JE: Tofauti kubwa ya mtazamo baina ya Jumbe wakati ule na Seif miaka hii ni nini?
Wale waliokuwa wakipingana na ASP,walishindwa kwasababu ya mapinduzi,kama unakumbuka,Abdulrahman Babu alishaanzisha chama cha UMMA(kabla ya mapinduzi), baada ya kutokushirikishwa kwenye serikali ya mseto(ile iliyosimamiwa na mkoloni chini ya muungano wa ZPP na ZNP cha Babu),na muda si mrefu,ndiyo mapinduzi yakafanyika,na chama cha UMMA kikavunjwa na kina Babu kujiunga na ASP chini ya uongozi wa Karume.

Hilo la kupingana na Karume kwa udikteta lilikuwepo,lakini udikteta wake ulifumbiwa macho simply kwasababu ya hofu ya ukomunisti wa kina Babu, mapenzi ya mwalimu kwenye muungano(Pan Africanism), na pengine the fact kwamba vyama hivyo vingine vilikuwa vya kibaguzi,so udikteta wa Karume ulikuwa ni sababu ya kuiweka Zanzibar pamoja,na pia ikiwa ni njia ya Karume kuhakikisha anabaki madarakani.

Na pia kuungana kwa ASP na TANU ilikuwa ni sababu hiyohiyo,yani kuipa nguvu zaidi serikali ya Zanzibar chini ya Jumbe.Nje ya hapo kungeendelea kuwepo kwa machafuko,na kama sivyo,bado kungekuwa na serikali dhalimu ya kibaguzi.(However bado serikali ya Karume ilikuwa na udhalimu wake)

Hata baada ya muungano,kuliendelea na kashfa za kutaka kupinduliwa kwa Karume kutoka kwa akina Hanga na Babu kwasababu hiyohiyo ya hofu ya ukomunisti wao na tamaa za kubakia madarakani za Karume.

Suala la muungano lilikuwa na matatizo huko Zanzibar toka hata wakati wa Karume,na hata Karume kuuwawa kwake inawezekana kulitokana na hilo,kumbuka Karume alishawahi kusema "Muungano ni kama koti,likikubana unaweza kulivua na ukaendelea na safari",hapo alijuwa kabisa kuwa kuna wengi tu walikuwa hawaupendi muungano,na yeye pia hakuupenda mungano kwa moyo wake wote zaidi ya hofu ya kutokuweza kuitawala Zanzibar.

Kwa hiyo Jumbe kuja baada ya Karume,alikutana na hali ile ile,lakini yeye hakuwa na tamaa binafsi za madaraka kama Karume na ndiyo maana akakubaliana na dhana ya kuuangalia muungano upya,jambo ambalo lilikuwa very popular na hadi sasa bado ni popular kwa wazanzibari,ni kwamba hawautaki muungano.(wananchi wake)

Kuna mambo mengi tu ambayo Karume alipingana na Mwalimu kuhusu mambo ambayo yatakuwa chini ya serikali ya muungano,alikataa kuhamishia mambo mengi ambayo yalitakiwa kuwa chini ya muungano,kwa mfano jeshi la ulinzi na idara ya uhamiaji,Karume aliendelea kuwa amiri jeshi mkuu wake.

Fedha lilikuwa jambo la muungano,lakini Karume alikataa serikali ya muungano kugusa akiba ya pesa za kigeni za Zanzibar.

Hata Azimio la Arusha Karume alilikataa,pamoja na mambo mengi ya kisera kutoka bara.So unaweza kuona kuwa suala la issue za muungano lilikuwa na matatizo toka enzi hizo na alichofanya Jumbe ni kutokufuata udikteta wa Karume aliyeuwawa na wanajeshi wake yeye mwenyewe.

Ndiyo maana makubaliano ya kufanya mchakato wa kupata katiba mpya ndani ya mwaka mmoja yalishindikana na hilo kupelekea Zanzibar iongozwe kwa katiba ya muda hadi 1977(miaka 13),tena baada ya Karume kuuwawa mwaka wa 1971.

Baada ya Jumbe kupitishwa na baraza la mapinduzi la Zanzibar hapo mwaka 1972 kuwa rais wa Zanzibar(mwaka mmoja baada ya Karume kuuwawa),walipitisha azimio kwamba watadumisha ,kulinda na kutetea fikra na malengo ya mapinduzi pamoja na sera alizoziacha Karume.

Na ukumbuke kuwa Karume na mwalimu walikuwa wanatofautiana sana kuhusu issue ya muungano,tena kuna nyakati Karume aliwahi kumwambia mwalimu pale walipopishana kuhusu issue mbali mbali za muungano "Sikubali,kama ni hivyo tuuvunje muungano",kauli ambazo inasemekana alimwambia hadharani pale walipokuwa wakipishana kuhusu issue za muungano.Na ndiyo maana mwalimu akaja na ile kauli kwamba wanaweza kuuvunja muungano kama wananchi wa Zanzibar wakitaka kufanya hivyo bila shinikizo kutoka nje.

Pia kuna nyakati ambazo mwalimu aliahirisha ziara zake kule Zanzibar "kwasababu za kiusalama"

ASP kilifanya mkutano wake mkuu mwaka 1972,ikiwa ni miaka kumi toka wafanye mkutano kama huo mwaka 1962.Mkutano huo ulihudhuriwa na Mwalimu Nyerere pamoja na wajumbe wengine wa TANU,pamoja na wajumbe kutoka mataifa 12 ya kiafrika.

Katika hotuba yake,Jumbe mbali na kulaani utawala wa kibabe na matumizi ya dola dhidi ya raia,alisema "Viongozi lazima wawatumikie watu na si watu wawatumikie viongozi".

Hilo linaweza kutufanya wengine tutafsiri kwamba msimamo wa Jumbe ulikuwa ni msimamo wa wananchi walio wengi wa Zanzibar(kuhusiana na muungano).

Kuhusu msimamo wa Seif Shariff,hapa nitasubiri wenye kuufahamu na utofauti wake na Jumbe watuelimishe kwenye hilo.
 
Hata mimi sielewi.
Serikali mbili ni sera iliyoshindwa na haileti maana yeyote. Serikali moja ndiyo lengo na nia ya muungano.
Haya ya serikali mbili au tatu ni kutapatapa kwa JMT ambako kumetokana na serikali ya Zanzibar kutaka autonomy tangu 1984. Hapo ndiyo ilipodhihirika wazi kuwa hawataki muungano kama tunavyotaka sisi watanganyika.
Mkuu Kobello

Kila nikisoma michango yako, inafurahisha.
sisi watanganyika
Tanganyika/Utanganyika unaupata wapi wakati unasema utanganyika umekufa, haupo?

Nani aliweka serikali mbili? Zilijiweka zenyewe?
Serikali moja ndio lengo na nia ya muungano.
Hii ni kauli yako? Maoni yako? Au maoni ya kundi/ kikundi kipi?
Haya ya serikali mbili au tatu ni kutapatapa kwa JMT ambako kumetokana na serikali ya Zanzibar kutaka autonomy tangu 1984.
Mkuu Kabello

Ingawaje unaamini kuwa serikali ya Muungano(JMT/SMJT) ni superior, lakini hii serikali haikujiunda/ haikujiumba. Ujio wake/ uwepo wake umetokana na makubaliano ya dola mbili huru, Tanganyika na Zanzibar ambazo ziliazimia kuunda serikali ya pamoja(muungano) ambayo waliipa mamlaka ya kusimamia mambo 11 tu. Usuperior unatoka wapi hapo? Kinyume chake siku mmoja ya wabia akisema basi yamenishinda, hii JMT(SMJT) inajifia. Unaikumbuka Soviet Union, Yugoslavia?

Kuna sehemu umekiri kuwa unaijua orodha ya mambo ya muungano.
Pia umesema kuwa kuna mambo yasiyo ya muungano kwa Zanzibar tu.(huu ni nusu ukweli). Yapo pia mambo ambayo si ya muungano kwa Tanganyika.

Jf ipo mijadala mingi inayohoji kwa nini wazanzibari wanapewa uwaziri wa wizara ambazo si wizara za muungano. Au wewe una maoni kuwa wizara zote ni wizara za mambo ya muungano?
JokaKuu kuja saidia hapa!

Nafikiri serikali ya muungano (SJMT) inatapatapa kwa sababu wewe unaipa usuperior na yenyewe inajipa mamlaka ambayo haina, haijapewa. Kumbuka SJMT haiwezi kujiundia/kujipa mamlaka ni lazima ipewe na wabia walioiunda serikali hiyo.(au kwa kutumia katiba iliyochakachuliwa)

Kuna kadhia ya EAC...kuna mambo 18(17) ambayo jumuiya hii inashughulika nao. Kati ya hayo ni manne tu ndio mambo ya muungano. Sasa hapa ndio changamoto inapotokea. Wakati mambo ya nje na ((ushikiano wa kimataifa),liliongezwa kinyemela baadae) ni jambo la muungano. Mambo 13(14) kati ya 18/17 ya EAC si mambo ya muungano. Wapi SJMT inatoa mamlaka ya kuiwakilisha/kuisemea Zanzibar kwa mambo hayo?
Ukitupia macho hili na kulifikiria sana utaelewa kwa nini Zanzibar inatetea autonomy yake.

Pia mamlaka ya serikali ya Tanganyika kama hayakukasimiwa kwa SJMT basi Tanganyika pia ingetetea autonomy yake katika yale mambo ya Tanganyika ambayo si mambo ya muungano. Ilivyo sasa SJMT inafanya kazi in duality, kama mwakilishi wa serikali ya Tanganyika na kama mamlaka ya mambo ya muungano.(ukiini macho, mzizi wake uko hapa na dhana ya usuperior unaitoa hapa)

Hapa ndio ile dhana uliyoisikia ya serikali mbili, moja ya Muungano(yenye mamlaka mbili ndani yake, mambo ya muungano na mambo yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanganyika) na serikali ya Zanzibar (mamlaka ya mambo yasiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar)....serikali mbili, mamlaka tatu kisheria...Muungano wa serikali mbili na mamlaka tatu kisheria. -Mchambuzi aliweka vifungu vya sheria kuthibitisha hili katika michango yake hapo mwanzoni.
Hapo ndiyo ilipodhihirika wazi kuwa hawataki muungano kama tunavyotaka sisi watanganyika.
Mkuu Kobello

Hapa unaanza kutapatapa kama JMT(SJMT).
Huwezi kushangilia uvunjifu wa mkataba wa muungano kwa upande mmoja na kusema unataka muungano.
Pia haiwezekani ukanyage haki ya mwenzako na anaposema unaniumiza au unanidhulumu ,useme:"wewe hutaki kushirikiana na mimi"

Unawasemea watanganyika wepi?
Wapo wasioataka muungano, kwao muungano umekuwa kero.Wanasema uvunjwe/uvunjike.
Wapo wanaotaka muungano. Hawa wapo wanaotaka serikali moja,(wewe unaingia hapa na MMJ), wapo wanaotaka status quo,serikali mbili. Hawa ni viongozi wa CCM pia walioaminishwa kuwa serikali zaidi ya mbili ni mzigo.
Wapo wanaotaka serikali tatu(Mchambuzi, CUF; CHADEMA, wenye kupenda utanganyika wao)

Makundi haya yaliyopo Tzbara(Tanganyika) pia yako Zanzibar. Naamini kama anavyoamini mleta mada, referendum ndio kipimo sahihi kitakachotoa jibu la nani anataka muungano na nani hataki. Kama wanataka muungano, ni muungano wa mfumo/muundo upi.

Mimi nitakubaliana na wewe, kama ni kutapa tapa, sio kutapa tapa tu bali pia woga kutawala SMJT ni katika kujaribu kubinya mjadala wa Muungano. Unapochelewasha tatizo, huwa unalikuza. Tumefanya hivyo kwa miaka 48.

Ok, wanaJF, watanzania,watanganyika, wazanzibari kwa umoja wetu tunatapatapa.
Lakini kutapatapa hakutasaidia kitu, inabidi tufanye maamuzi, hata kama ni magumu.

Pakuanzia ni kukiri kama alivyotuchambulia Mchambuzi kuwa tulikiuka Mkataba wa muungano (mhimili mkuu) katika kuunda JMT. Baada ya hapo tusahihishe makosa.

Kuna sehemu nilisoma hii:
the ‘Articles of Union’ are the Grundnorm, the fundamental law of the United Republic, on which the Constitutions of Tanzania and Zanzibar, and other laws, have to be based and from which they derive their legitimacy. Like any supreme law in any other legal system, no other law or constitutional act can be in conflict with it.

Mkuu Kobello kuna maswali mengi niliyokuuliza hukuyajibu katika michango ya nyuma(JokaKuu pia alikuiga katika hili). Na pale ulipojibu machache,ulijifanya jangala au pimbi....cheers!
 
Back
Top Bottom