Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
UPDATES

Ni miaka karibia miwili sasa (2012), tangia tuanzishe mjadala huu humu JamiiForums juu ya umuhimu wa kuizindua Tanganyika kama njia ya kuboresha na kudumisha muungano. Miaka miwili iliyopita (2012), wengi walibeza na kukebehi hoja yetu juu ya umuhimu wa kuizindua Tanganyika humu JamiiForums. Lakini kebehi hizi hazikuwa katika mitandao ya kijamii peke yake bali hata kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mfano, Mbunge wa Singida Mashariki (Tundu Lissu) alipoibua hoja hii bungeni mwaka 2012, mbunge huyu alibezwa na wabunge walio wengi, na hoja ya Tanganyika ikaendelea kufichwa chini ya zulia. Lakini ndani ya miaka miwili tu, uelewa na mwamko wa wananchi juu ya "maana na umuhimu" wa kuizindua Tanganyika ndani ya muungano (serikali tatu) unazidi kukua siku hadi siku, huku mwamko na uelewa huo pia ukizidi kukua miongoni mwa wajumbe wa bunge la katiba, ikiwa ni pamoja na miongoni mwa baadhi ya wabunge wa chama tawala (CCM).

Tujikumbushe mwaka 2012 tulijadili nini katika bandiko #1 la uzi huu:

Sehemu ya Kwanza: Utangulizi

Mjadala wowote juu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa kawaida unahitaji maandalizi makubwa na pia umakini wa hali ya juu, hasa iwapo unalenga hoja zenye kuuboresha kwa njia ya kuondokana na kero mbalimbali zilizopo, badala ya kuuvunja. Iwapo kuna masuala ambayo baadhi yenu mtadhania nimeyasahau au kuyaacha, ni kwa sababu ni vigumu sana kuja na mada kuhusu muungano ambayo inajitosheleza. Pamoja na hayo yote, kuna mengi nimeyaacha kwa makusudi lakini kwa lengo la kuyajadili zaidi baadae; Vinginevyo naomba mniwie radhi kwa mapungufu yoyote ambayo yatajitokeza.

Kupitia nafasi yake kama Msemaji Mkuu wa Upinzani Bungeni (Ofisi Ya Makamu Wa Rais – MUUNGANO), katika kikao cha Bajeti cha Mwaka wa Fedha, 2012-2013, Tundu Lissu (MB), aliwasilisha maoni kuhusu mtazamo na msimamo wa kambi hiyo juu ya Muungano Wetu. Kwa wale waliopata fursa ya kuisikiliza hotuba ya Lissu kwa makini, wengi watakubaliana na mimi kwamba hotuba yake ilijaa YALIO MEMA kuliko YASIYO MEMA, sio tu kwa Muungano wetu, bali pia kwa taifa letu. Vile vile, hotuba ya Lissu ina dhamira njema na yenye manufaa, sio tu kwa kizazi cha sasa, bali pia kizazi cha baadae. Lakini kama kawaida yetu, nchini Tanzania, "POLITICS HAVE BECOME SURPEME TO EVERYTHING, INCLUDING EVEN RATIONALITY AND COMMON SENSE", kwani hoja ya Lissu imepotoshwa;

Tanzania tuna desturi mbaya sana ya ku ‘politicize' kila kwa maslahi binafsi; mfano ni suala zima la mjadala wa Tanganyika ambapo wale wanaopinga hoja hii ni hodari wa kutumia SIASA kupotosha mengi, na pia kuwatia HOFU watanzania, kwa mfano hoja kwamba – kujadili mfumo wa muungano wetu ni tishio kwa Amani na Utulivu wa Nchi yetu; Wanaojenga hoja hizi wakitakiwa watoe ufafanuzi juu ya hoja zao, ni kawaida sana kwa wao kuuacha Maswali mengi kuliko Majibu
;

Kuna jambo moja linanishangaza. Pamoja na umuhimu wa hotuba ya Lissu aliyoitoa Bungeni, hotuba hii haipo kwenye Hansard ya Bunge. Kwa kweli this is both - Very Unusual and Very Wrong; Lakini kukosekana kwa hotuba hii kwenye Hansard haiwezi kutuwekea kikwazo sisi wananchi kuendeleza mjadala ule huku uraiani kwa nia ya kujenga, na sio kubomoa, na kwa maslahi ya taifa letu, hasa vizazi vya baadae; Sidhani kama kuna yoyote miongoni mwetu ambaye ana nia ya kuachia watoto na wajukuu zake taifa lililojaa migogoro; Kuzuia mjadala huu au kuhofia kujadili hoja hii, ni mwanzo wa maandalizi ya kuachia vizazi vyetu vya baadae MGOGORO mkubwa sana;

Nilibahatika kunukuu baadhi ya maeneo muhimu kutoka katika hotuba ya Tundu Lissu kupitia TBC1. Kwa kifupi, Lissu alikuwa ana ‘challenge' hoja ya Serikali iliyotolewa na Waziri husika wa muungano kuhusu ya hali ya muungano wetu, miaka 48 baadae [1964-2012]. Waziri huyo alizungumza mengi ikiwa ni pamoja na haya yafuatayo:

["…Katika Kipindi hicho muungano wetu umekuwa na mafanikio katika maeneo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa…muungano wetu ndio nguzo kuu ya umoja na amani…"]

Katika sehemu ya majibu yake juu ya hoja hii ya Serikali, pamoja na mambo mengine, TUNDU LISSU alitamka yafuatayo:

["…hata hivyo mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri aliliambia bunge lako tukufu kwamba, licha ya mafanikio hayo, zipo changamoto katika kumaliza vikwazo vinavyokwamisha shughuli za muungano. Mheshimiwa Spika, Waziri hakuzitaja Changamoto hizo."]


"…Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka Serikali itoe kauli mbele ya Bunge hili tukufu ni namna gani maoni ya wale wanaotaka kiini macho hiki cha Muungano kiishe yatashughulikiwa na Tume ambayo imepewa jukumu kisheria la kukihifadhi na kukidumisha kiini macho hicho? Ni kipi kitakachoizuia Tume ya Warioba kupuuza maoni ya watu hao kwa hoja kwamba Sheria inaielekeza Tume kuratibu na kukusanya maoni na kutoa mapendekezo ya kuhifadhi na kudumisha Muungano?"]

Kiini macho anachozungumzia Tundu Lissu ni Serikali Ya Tanganyika kupotea KIMAZINGAOMBWE, kinyume na makubaliano yaliyomo ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964, pamoja na athari zake kwa taifa kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa, Mazingaombwe haya ndio chanzo cha mgogoro wa muungano wetu huku hisia tofauti zikizidi kujengeka miongoni mwa wananchi wa pande zote mbili za muungano, kila upande ukiamini kwamba mfumo wa sasa wa Muungano hauwatendei haki. Tutaliona hili kwa undani baadae katika mjadala.

Nia ya mada yangu ni kuendeleza mjadala wa Lissu, hasa kwa kuzingatia kwamba hoja yake haikupewa nafasi ya kutosha kujadiliwa bungeni; Naomba nirudie tena kusema kwamba - tofauti na UMMA unavyoaminishwa, nina amini kwamba Hotuba ya Lissu inabeba Mema kuliko Mabaya. Mjadala juu ya Muungano wetu umetawaliwa na WOGA mkubwa sana, lakini sisi kama raia wa Tanzania, nina amini kwamba ni haki yetu sote ‘kikatiba kutoa maoni yetu juu ya suala hili;

Nimekuwa napokea maneno kadhaa ya vitisho na ya kunikatisha tamaa kutokana na misimamo na maoni yangu mbalimbali humu Jamiiforums, hasa kutokana na ukweli kwamba najulikana kutokana na kuweka picha yangu ya kweli humu; Pamoja na hayo, ni muhimu wajue kwamba vitisho vyao ni motisha zaidi kwangu ya kuendelea kutumia uhuru wangu wa mawazo, hivyo sitaacha kusema ukweli mpaka pale mauti itakaponikuta; Isitoshe, TO GOD, ONE IS MAJORITY.

Sehemu ya Pili: Ujenzi Wa Muktadha wa Mjadala pamoja na yaliyomo.

Katika sehemu hii ya pili, nitajadili masuala makuu matano kama ifuatavyo:

Suala la kwanza. Ni jadi kwa viongozi wengi wa CCM (sio wote), kuwa na misimamo inayo unga mkono mfumo wa sasa wa muungano wetu – yani mfumo wa Serikali Mbili, huku wengine wakiwa na mtazamo wa serikali moja; Wengi ya viongozi hawa huwa na mtazamo kwamba, madai ya Serikali ya Tanganyika hayana nia Njema kwa muungano wetu na taifa letu kwa ujumla; Kuna sehemu kubwa sana ya UMMA ambayo inanunua kauli hizi. Ni muhimu UMMA ukaelewa kwanini viongozi wengi huwa na mtazamo huo. Sababu kuu ni Viapo wanavyokuwa baada ya kuteuliwa KUSHIKA DHAMANA ZA UMMA. Viongozi wetu huapa hivi:

"Mimi ...................bin........ ..........naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba nitaahifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ewe mwenyenzi mungu nisaidie."

Ni muhimu kwa kiongozi yoyote anayeteuliwa kushika cheo kama DHAMANA, kwani kinyume chake ni kujiweka hatarini kupoteza madaraka; Lakini viongozi wengi hujisahau kwamba vyeo hivi sio lolote zaidi ya Dhamana, na wenye mamlaka ya juu kabisa na nchi yetu ni UMMA wa Tanzania, Sio VIONGOZI. Tukirejea kwenye hoja ya msingi katika hili, viongozi hawa hawana jinsi bali kuunga mkono muungano wetu kama ulivyo, vinginevyo kufanya kinyume ‘is to contravene with the cocountry's Constitution, 1977', hivyo kujiweka pabaya na madaraka/vyeo walivyonavyo.

Sehemu ya Kwanza ya Katiba yetu (1977) inazungumzia: Jamhuri ya Muungano na Watu, na inatamka hivi:

1. Tanzania ni nchi Moja na Ni Jamhuri ya Muungano.

2. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Kwa maana hii, tusitegemee kiongozi yoyote aliyekula kiapo cha "kuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano, na kuhifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", aje na msimamo tofauti au aunge mkono hoja ya kudai Tanganyika.

Ukitizama kwa makini maneno haya yaliyomo ndani ya Katiba Ya JMT (1977), licha ya Tanzania kuwa mtoto wa Tanganyika na Zanzibar, nchi ya ‘Tanganyika' haipo, na badala yake, mzazi huyu wa Tanzania amepewa jina la ‘Tanzania Bara'; Hiki ni kiini macho cha hali ya juu; Tangia lini mzazi anapewa jina tofauti baada ya kuzaa mtoto? Suala lingine muhimu zaidi hapa ni kwamba, HUU NI UCHAKACHUAJI na ni KINYUME NA MKATABA WA MUUNGANO, 1964.

Tukirejea kwenye suala la viapo vya viongozi wetu, cha kustaajabisha ni kwamba, imekuwa ni jadi kwa viongozi wetu wengi, katika nyakati tofauti kufanya maamuzi au matendo ambayo yanakiuka Katiba ya JMT, 1977, tena kwa makusudi, and still get away with it; mifano hai ipo mingi, na tunazidi kushuhudia jinsi gani wapo tayari kuvunja Katiba ya Nchi ilikufanikisha masuala mbalimbali ya KISIASA, hata kama hayana maslahi kwa UMMA; Lakini linapokuja suala la kujadili Muungano, hasa TANGANYIKA, suala ambalo lina maslahi kwa umma, viongozi hawa hawapo tayari kufanya hivyo. Cha ajabu zaidi ni kwamba, Mkataba wa Muungano, 1964, unatoa fursa ya wazi kabisa kwa viongozi wa pande zote mbili kuujadili na kuurekebisha muungano, kila inapobidi, na hata ikibidi, KUUFUTA KABISA;

Suala la Pili. Tofauti na viongozi hawa, raia wengine wanapozaliwa, hawali kiapo cha kulinda katiba, muungano….; Vile vile kabla ya kupewa pasi zeti za kusafiria kama watanzania, hakuna kiapo tunachokula; tunapoajiriwa katika sekta sekta binafsi n.k, vile vile hakuna kiapo tunachokula; tunapoamua kuwa wajasiriamali na kupokea usajili wa makampuni yetu kule BRELA au kupokea mbalimbali zinazo turuhusu leseni kuendesha biashara zetu n.k, hatuli kiapo kama cha hawa wakubwa. Sasa iwaje tuogope kujadili muungano kama nia yetu ni kuuboresha? So Let the People Speak. Isitoshe, hatima ya nchi yetu ya Tanzania pamoja na Muungano wetu, ipo mikononi mwa UMMA, sio Viongozi hawa wanaokula viapo, kwani UMMA ndio wenye mamlaka ya mwisho katika taifa letu. Na haki ya raia kutoa mawazo yao ni kwa mujibu wa Katiba (1977);

Suala la Tatu. Kwa Mtazamo wangu, Mtanzania yeyote mwenye nia njema na muungano wetu ni lazima kwanza awe Mwaminifu Kwa Mkataba wa Muungano, 1964, badala ya kuwa Mwaminifu kwa Katiba ya JMT, 1977; Hii ni kwa sababu, Katiba ya JMT, 1997, haina mema na muungano wetu, kwani Katiba hii mbovu ndio chanzo kikubwa cha mgogoro ulipo sasa; Tutalijadili hili kwa kina baadae, hasa jinsi gani Katiba ya JMT, 1977, ilivyouchakachua Mkataba wa Muungano, 1964.

Kama tutakavyoona, Mkataba wa Muungano, 1964, ulikuwa na nia ni njema kabisa – ya kuunganisha watu wa Tanganyika na Zanzibar, huku kila taifa likiwa huru na kujiamulia mambo yake yasiyo ya muungano; Badala yake, kilichokuja kutokea baadae ni mazingaombwe na uchakachuaji ambayo ulifanya tupoteze nchi ya Tanganyika, ambae ni Mmoja ya Wazazi wa Tanzania, na mzazi huyu kupewa jina jipya la "Tanzania Bara", mara tu alipojifungua mtoto wake "Tanzania", huku mzazi mwenza "Zanzibar", nae akipewa jina jipya "Tanzania Visiwani", lakini kwa kuogopa kumchakachua zaidi, akaachiwa awe na majina mawili – yani Zanzibar na Tanzania Visiwani (kabla ya wazanzibari kulikataa jina hili)
, huku uchakachuaji juu yake ukiendelea kwa njia ya kuongeza orodha ya masuala ya muungano, Kinyume na Mkataba wa Muungano, 1964;

Suala la nne, ni kuhusu arrangement ya Katiba ya Tanzania, 1977. Shivji (2006) analiweka hili kwa lugha rahisi zaidi kueleweka pale anaposema kwamba: "The underbelly of Tanzania's constitutional arrangement is and has been the union or Zanzibar."

Kwa bahati mbaya sana, msimamo wa ndugu zetu wazanzibari juu ya muungano umekuwa unapotoshwa, na kuwekwa completely out of context. Je ni kwa madhumuni gani? Ni vigumu kuelewa; Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba throughout, ndugu zetu wazanzibari wamekuwa na tatizo moja tu kuhusu muungano, na hili sio jingine bali "Loss of Their Autonomy". Kwa sababu tusizozijua, hoja yao hii ambayo ni LEGIT kabisa, hasa kwa kufuatana na Makubaliano chini ya Mkataba wa Muungano, 1964, msimamo wao umekuwa ‘politicized', na kupelekea ujenzi wa chuki kubwa baina ya ndugu hawa wawili – wazanzibari na watanganyika; Imekuwa jadi kwa baadhi ya watu kuwashutumu ndugu zetu wazanzibari kwamba misimamo yao juu ya Muungano wetu una msukumo wa kidini; huu ni upotoshwaji wa hali ya juu; Ukweli ni kwamba - throughout, Wazanzibari wamekuwa na nia njema kabisa na Muungano, lakini kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, ambapo Serikali Tatu was envisaged;


Ningependa kusema kitu kimoja at this juncture:

Kwa sababu kadhaa, ndugu zetu wazanzibari wamekuwa ni waelewa zaidi juu ya kiini macho cha muungano kuliko wengi wetu wa upande wa bara; Mbaya zaidi ni kwamba, badala ya sisi kujikita katika kuelewa tatizo la msingi lipo wapi, hasa jinsi gani Katiba ya JMT 1977 ilivyofanya mazingaombwe na kuchakachua Mkataba wa Muungano, 1964, na badala ya na sisi kuwaiga na kudai Tanganyika yetu, kitu ambacho wao throughout wamependelea kiwepo, badala yake tunaelezeka juhudi zetu kubwa sana to fight the wrong enemy i.e. kuwakosoa ndugu zetu wa Zanzibar juu ya madai yao, badala ya kuwaelewa na kuwaiga;


Wengi wetu tunajenga hoja potofu kwamba wazanzibari wanafaidika zaidi na muungano, au wanatunyonya; hii hoja sio sahihi kwa sababu – kama ni kweli Bara tunanyonywa na muungano huu, basi ni kwa sababu ya makosa yetu wenyewe ya Kukiuka Mkataba wa muungano, 1964, kupitia katiba ya JMT, 1977; Isitoshe – iwapo mtoto wako haumpi ‘autonomy' au haumfundishi maisha ya kujitegemea, kwanini sasa uanze kumgeuka na kumuona kwamba ni mzigo kwako? Ni dhahiri kwamba, iwapo wangepewa Autonomy kwa Mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, Zanzibar ingeweza kabisa kujitegemea; Kinyume chake, baada ya Muungano, serikali ya Muungano ikaanza taratibu kunyakua mambo mbalimbali na kuyatumbukiza kama nyongeza ya masuala ya muungano, kinyume kabisa na Mkataba wa Muungano, 1964; Leo hii tunaposema ndugu zetu wazanzibari ni mzigo, hii ni dhambi kubwa sana kwetu watu wabara;


Pia wengi tunasahau kwamba, Zanzibar ilijiunga na Tanganyika miezi minne na nusu tu baada ya kufanikisha Mapinduzi yake mwaka 1964 yaliyotokomeza Utawala wa Kisultani; Ikumbukwe pia kwamba, katika kipindi hiki cha miezi minne na nusu Ya UHURU Wao [DECEMBER 10[SUP]th[/SUP] 1963 – APRIL 26[SUP]th [/SUP]1964], Zanzibar waliamua kukaa kimya kabisa na kutokimbilia kujiingiza katika Mikataba yoyote au makubaliano yoyote ngazi ya Kimataifa; kwa maana nyingine, hawakutaka kuwa signatories wa suala lolote ngazi ya kimataifa mpaka pale watakapojipanga; Mkataba wao wa kwanza ukawa ni ule wa Muungano na Tanganyika na hatimaye kujikuta kwamba, mengi ambayo Tanganyika walikuwa wamesha establish position yake kimataifa, yakageuka kuwa binding kwa Zanzibar pia; Lakini kwa ajabu, wengi wetu suala hili tunalipuuza;


Ni muhimu tukaelewa pia kwamba - tofauti na nchi zilizokuwa jirani yake (Zanzibar), yani Tanganyika, Kenya na Uganda ambazo uhuru wao ulipatikana kwenye Board Rooms za Lancaster Hall huko London, huku wahusika wakiwa wamevaa suti na kunywa wine na kahawa katika mijadala, ndugu zetu wa Zanzibar hali ilikuwa ni tofauti; Wao uhuru wao ulipatikana "in the streets", kupitia mtutu wa bunduki; The bottom line hapa ni kwamba, mtazamo wa baadhi ya watu wa "Tanzania bara" kwamba eti Wazanzibari wanatulalia, umejaa upotoshwaji mkubwa sana.

Suala la Tano na la mwisho kujadili katika sehemu hii, ni kwamba – Kama wapo watanzania wenye ujasiri wa kumkosoa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, basi ni wachache sana; Wale wenye uoga juu ya hilo wanasahau kwamba Nyerere alikuwa ni binadamu kama wao; Mimi ni muumini mkubwa sana wa Falsafa ya Mwalimu, including suala la Muungano wetu, lakini nina amini kwamba kuna baadhi ya maeneo ambayo Mwalimu kama binadamu, aliyakosea, licha ya yeye kuwa na nia njema kwa taifa letu, hasa ikizingatiwa kwamba "Nyerere Did Not PROFIT From Politics"; Makosa ya Mwalimu juu ya muungano yalikuwa na yanaendelea kuwepo kwenye "MFUMO", sio kwenye NIA; Nyerere alikuwa was a ‘True Panafrianist', na kuna wakati alikuwa yupo tayari hata kuifanya Afrika ya Mashariki iwe ni nchi moja baada ya uhuru na kabla ya muungano na Zanzibar, kwa nia nzuri kabisa; Kwahiyo when it comes to suala la Muungano na Mwalimu, "The END" Was Justified, But Not The "MEANS"; Wasiwasi wa Mwalimu juu ya hatima ya Muungano iwapo Tanganyika itarudi, upo LEGIT; lakini tutaendelea kukaa na hofu hii mpaka lini, hasa ikizingatiwa kwamba Mgogoro wa muungano wetu unatokana na Ukiukwaji wa Mkataba wa Muungano, 1964?


Machafuko yote yaliyojitokeza Zanzibar miaka ya nyuma, na ambayo yanaendelea leo chini kwa chini, chanzo chake ni mgogoro wa Kikatiba unaotokana na Katiba ya JMT, 1977, kuchakachua Mkataba wa Muungano, 1964. Kwa mtazamo wangu, mgogoro huu wa kikatiba Poses More Threat to our Peace and Tranquility kuliko ujio wa Tanganyika; Isitoshe, hata Tanganyika ikizaliwa, nchi yetu ya Tanzania itabakia kuwa ile ile, hasa mipaka na mahusiano ya watu wake; Kitachobadilika kitakuwa ni Mfumo tu wa Serikali; Hivyo mimi sioni busara kwa Watanzania kufanya maamuzi KIHOFU HOFU na kuacha mgogoro huu ubakie kama ulivyo; Tutakuwa ni wabinafsi sana iwapo tutarithisha vizazi vyetu vyaa baadae hali hii hii ya HOFU hii lakini pia MGOGORO huu huu, ambao kiini chake ni Ukiukwaji wa Mkataba wa Muungano, 1964. Hivi kweli, Vizazi Vya Baadae Vitafikiria Sisi Tulikuwa ni Watu wa Namna Gani?

Baada ya kujadili haya, sasa nifungue mjadala kwa msisitizo kwamba, naunga mkono hoja ya Tundu Lissu kuhusu kiini macho cha muungano wetu kwa sababu nilizojadili; Nina imani kwamba mjadala utakaouzaliwa kutokana na maswali yafuatayo utatuaidia kupata mwanga zaidi juu ya kiini macho cha muungano wetu, lakini muhimu zaidi, mawazo ya kutusaidia kuboresha muungano wetu kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae:

Kwanza: JE, Madhumuni ya Muungano Baina ya Tanganyika na Zanzibar, kwa Mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, Yalikuwa Ni Yepi na ni Mfumo wa Serikali ngapi ndio uliokusudiwa chini ya Mkataba huu wa Mwaka 1964?

Pili: JE, Viongozi Wetu na Wananchi Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo hii, Wana Nia ile ile Adhimu na Malengo Yale Yale Yaliyowekwa katika Utangulizi wa Mkataba wa Muungano, 1964?

Tatu: Ifikapo Mwaka 2014, Muungano Wetu Utakuwa Umetimiza Miaka 50; By Coincidence, Kipindi hicho hicho pia Tunategemea Kupata Katiba Yetu Mpya; Swali linalofuata ni, JE: Katika Kipindi Hiki Cha Miaka 50 Ya Muungano, tutakuwa tumefikia wapi katika Kufanikisha Madhumuni Kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964?

Nne: Je, makosa ambayo yanapelekea muungano wetu kuyumba yalijitokeza wapi, na tuchukue hatua gani kurekebisha makosa haya, na kurudisha matakwa na dhamira iliyowekwa wazi kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964?


BILA TANGANYIKA, TANZANIA HAIWEZEKANI. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
===========

Soma kuhusu Mkataba wa Muungano wa 1964 katika POST #6

Soma alichosema Lissu Bungeni hapa na VIDEO hapa

===========


Tangia tuje na mjadala huu (rejea nukuu hapo juu), mengi ya tuliyojadili wakati ule yameanza kujitokeza taratibu, huku pia wananchi wengi wakizidi kupata ufahamu juu ya umuhimu wa kuizindua Tanganyika, kama njia ya kuboresha na kudumisha muungano. Wakati bunge maalum la katiba likiwa linaendelea, yapo mambo mawili muhimu ya kuyafuatilia kwa karibu:

1. Jambo la Kwanza, CCM imeamua kuendeleza kosa lake la kufanya suala la muungano kuwa ni suala la "Chama Cha Siasa" badala ya kulifanya liwe ni suala la "kitaifa" ili kuendana na mazingira ya sasa ya kisiasa na kidemokrasia nchini. CCM imeshafanya uamuzi rasmi kuhakikisha kwamba Katiba ijayo haikidhi maoni ya wananchi walio wengi bila ya kujalisha imani na itikadi zao za vyama (Tanzania bara na Zanzibar) pamoja na taasisi zote muhimu za umma, ambazo kwa pamoja, walipendekeza mfumo wa serikali tatu kama njia ya kuboresha na kudumisha muungano.

2. Jambo la Pili - wakati kamati za bunge maalum la Katiba zikiwa zimeshaanza rasmi kujadili rarimu ya katiba, hati za muungano zimeibua utata. Yapo madai kutoka kwa baadhi ya wajumbe bado hawajapatiwa nakala za hati hizi kama walivyoomba. Kanuni zinaruhusu wajumbe hawa kupatiwa nyaraka zozote ambazo zimejadiliwa ndani ya rasimu ya katiba. Pia yapo baadhi ya wajumbe wanaodai kwamba saini ya Nyerere (Rais wa kwanza wa Tanganyika huru na Tanzania) na saini ya Katibu wa Bunge wa wakati ule (Pius Msekwa) zinazofautiana na saini halisi zilizopo kwenye nyaraka. Kwa maana nyingine, nakala za hati walizopewa wajumbe wa bunge hili maalum, zimechakachuliwa.

Maswali yanayofuatia ni je:


  • Kuibuka kwa suala la hati za muungano kunabadili vipi upepo wa Serikali tatu (Tanganyika) katika bunge hili maalum la katiba?
  • Nini itakuwa hatima ya CCM?


Tuendelee kusemezana...


Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.
 
Mchambuzi,mjadala utakuwa mzuri,ingewezekana tuwekee na hiyo nakala ya hotuba ya Lissu pamoja na mkataba wa muungano wa 1964.(muhimu sana hiyo nakala ya mkataba wa muungano),ili tuone vyema ulivyochakachuliwa na katiba ya muungano ya 1977.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi said:
Pia wengi tunasahau kwamba, Zanzibar ilijiunga na Tanganyika miezi minne na nusu tu baada ya kufanikisha Mapinduzi yake mwaka 1964 yaliyotokomeza Utawala wa Kisultani; Ikumbukwe pia kwamba, katika kipindi hiki cha miezi minne na nusu Ya UHURU Wao [DECEMBER 10[SUP]th[/SUP] 1963 – APRIL 26[SUP]th [/SUP]1964],
Halafu mkuu mapinduzi ya Zanzibar si yalikuwa january 12 1964?I stand to be corrected.
 


Kwanza: JE, Madhumuni ya Muungano Baina ya Tanganyika na Zanzibar, kwa Mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, Yalikuwa Ni Yepi?

"WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar being mindful of the long association of the peoples of these lands and of their ties of kinship and amity, and being desirous of furthering that associatio! n and strengthening of these ties and of furthering the unity of African peoples have met and considered the union of the Republic of Tanganyika with the Peoples Republic of Zanzibar"- Articles of the Union, 25 Jun, 1964.

Serikali zetu ndiyo zilizokubaliana. Hii haionyeshi kama ni democratic process on the basis ya kwamba serikali ya mapinduzi Zanzibar haikuchaguliwa na wananchi wa zanzibar ingawa ili -represent matakwa ya weusi wengi/wananchi wengi wa Zanzibar.Na utaona kwamba lengo la serikali hizo mbili lilikuwa ni Kuungana kwa kuwa sisi ni ndugu, kwa muda mrefu.



Pili: JE, Viongozi Wetu na Wananchi Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo hii, Wana Nia ile ile Adhimu na Malengo Yale Yale Yaliyowekwa katika Utangulizi wa Mkataba wa Muungano, 1964?
Nadhani watanganyika wengi hawana tabu na muungano kama utaleta nchi kuwa moja, na zanzibar ife, iwe mkoa/mikoa. Wazanzibari wengi nadhani wanataka kuwa na nchi yao tofauti na Tanzania (kitu ambacho wanacho tayari) na bila kuwa na ushirikiano wowote na Tanganyika other than diplomatic and Trade.


Tatu: Ifikapo Mwaka 2014, Muungano Wetu Utakuwa Umetimiza Miaka 50; By Coincidence, Kipindi hicho hicho pia Tunategemea Kupata Katiba Yetu Mpya; Swali linalofuata ni, JE: Katika Kipindi Hiki Cha Miaka 50 Ya Muungano, tutakuwa tumefikia wapi katika Kufanikisha Madhumuni Kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964?
Tutakuwa tumepiga hatua, especially wakati wa Mwinyi maana hatuendi Zanzibar na passport nao hawaji na passport. Mengine yapo vilevile, umedumu ila unakoelekea ni kuvunjika kama siyo kuwa nchi moja.


Nne: Je, makosa ambayo yanapelekea muungano wetu kuyumba yalijitokeza wapi, na tuchukue hatua gani kurekebisha makosa haya, na kurudisha matakwa na dhamira iliyowekwa wazi kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964?
Yalijitokeza mwanzo ambapo wananchi wa nchi hizi mbili hawakuhusishwa (political will).Hili kosa haliwezi kurekebishwa bali kwa njia ya sanduku la kura.



BILA TANGANYIKA, TANZANIA HAIWEZEKANI. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
Nadhani inawezekana, labda ungefafanua hili. Maana Tanganyika ikiungana na Zanzibar tunaweza kuwa na Tanzania, tatizo ni muundo wa huo muungano.
Nota benne:
Siungi mkono serikali tatu, ni upotevu wa kodi.
 
Re: Mkataba wa Muungano wa 1964


MKATABA WA MUUNGANO
Baina ya
JAMHURI YA TANGANYIKA
Na
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR

Kwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zinafahamu uhusiano wa muda mrefu watu wake na mshikamano na kukuza uhusiano huo na kuimarisha mshikamano na kukuza umoja wa watu wa Afrika, zimekutana na kutafakari Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

Na kwa kuwa Serikali za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar, zinapendelea ya kwamba Jamhuri hizi mbili ziungane kuwa Jamhuri moja huru moja kwa amasharti ya makubaliano yafuatayo:

Kwa hiyo IMEKUBALIWA baina ya Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar kama ifuatavyo:-

(i) Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa Jamhuri huru moja.

ii) Katika kipindi cha kuanza kwa Muungano mpaka Baraza la Kutunga katiba lililotajwa katika ibara ya (vii) litakapokutana na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano (Kuanzia hapa kitaitwa kipindi cha mpito), Jamhuri ya Muungano itaongozwa kwa masharti ya ibara ya (iii) mpaka ya (vi).

(iii) Katika kipindi cha mpito katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ili kuweka:

a) Chombo tofauti cha kutunga sheria na Serikali kwa ajili ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zilizopo za Zanzibar na vitakuwa na mamlaka ya mwisho katika Zanzibar kwa mambo yote isipokuwa yale tu yaliyo chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano;

b) Nafasi ya makamo wawili wa Rais mmoja kati yao akiwa ni mkaazi wa Zanzibar atakuwa ndiye kiongozi wa Serikali iliyotajwa kwa ajili ya Zanzibar na atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano katika utekelezaji wa kazi za Serikali kwa upande wa Zanzibar;

c) Uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano;

d) Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu.

(iv) Mambo yafuatayo yatakuwa chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano:-
a) Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
b) Mambo ya nchi za nje
c) Ulinzi
d) Polisi
e) Mamlaka yanayohusika na hali ya hatari
f) Uraia
g) Uhamiaji
h) Mikopo na biashara ya nchi za nje
i) Utumishi katika Jamhuri ya Muungano.
j) Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha
k) Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, Posta na Simu

v) Bunge na Serikali vilivyotajwa vitakuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote yahusuyo Jamhuri ya Muungano na kuongezea mamlaka juu ya mambo yote yahusuyo Tanganyika.

Sheria zote zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutumika katika maeneo yao bila kuathiri:-

a) Masharti yoyote yatakayowekwa na chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria.
b) Masharti yatakayowekwa kwa amri ya Rais wa Zanzibar juu ya sheria yoyote inayohusu jambo lolote lililotajwa kwenye ibara ya (iv), na kufuta sheria yoyote inayolingana Zanzibar.
c) Mabadiliko yoyote kama yataonekana yanafaa au kuhitajika ili kufanikisha Muungano na mkataba huu.

(vi) (a) Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano atakuwa ni Mwalimu J. K. Nyerere na ataongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kufuata masharti ya mkataba hu na kwa kusaidiwa na maofisa wengine atakaowateuwa toka Tanganyika na Zanzibar na watumishi wa Serikali zao.

b) Makamo wa kwanza wa Rais kutoka Zanzibar aliyeteuliwa kwa kufuata marekebisho kama yalivyoelezwa na ibara ya 3, atakuwa Sheikh Abeid Karume.

(vii) Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamo wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar
a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.
b) Ataitisha Baraza la kutunga katiba ikiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itakayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakarimapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano.

(viii) Mkataba huu utahitaji kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.

KWA KUSHUHUDIA HAPA Julius K. Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na abeid Karume, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, wametia saini nakala mbili za mkataba huu, hapa Zanzibar siku ya tarehe Ishirini na mbili ya mwezi Aprili, 1964.
___________________________
Umepitishwa katika Bunge siku ya tarehe Ishirini na Tano ya Aprili, 1964.
P. MSEKWA
…………………..Karani wa Bunge

Nathibitisha kwamba Muswada wa Sheria hii ulipitishwa na Bunge kwa mujibu wa ibara ya 35 ya katiba.
A.S. MKWAWA
..........………………………..Spika

25, Aprili 1964.



______________________________________________________________________________________________________

Source: Jumbe, A (1995), The Partner - Ship: Muungano Wa Tanganyika na Zanzibar: Miaka 30 Ya Dhoruba.

Kuhusu hotuba Kamili ya Lissu nitaiwasilisha mara tu nitakapoipata kwani, again, kama nilivyoeleza kwenye my original Post i.e. Post Number 1, hotuba ya Lissu kwa bahati mbaya sana, haipo kwenye Hansard ya Bunge; Vinginevyo hata bila ya hotuba hiyo, hoja yangu inaunga tu mkono hoja ya Lissu juu ya kiini macho cha muungano wetu, vinginevyo nilichowasilisha kinajitegemea;
 


"WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar being mindful of the long association of the peoples of these lands and of their ties of kinship and amity, and being desirous of furthering that associatio! n and strengthening of these ties and of furthering the unity of African peoples have met and considered the union of the Republic of Tanganyika with the Peoples Republic of Zanzibar"- Articles of the Union, 25 Jun, 1964.

Serikali zetu ndiyo zilizokubaliana. Hii haionyeshi kama ni democratic process on the basis ya kwamba serikali ya mapinduzi Zanzibar haikuchaguliwa na wananchi wa zanzibar ingawa ili -represent matakwa ya weusi wengi/wananchi wengi wa Zanzibar.Na utaona kwamba lengo la serikali hizo mbili lilikuwa ni Kuungana kwa kuwa sisi ni ndugu, kwa muda mrefu.


Kimsingi, nakubaliana na wewe, hasa the fact kwamba haya yalikuwa ni makubaliano baina ya viongozi wawili - Karume na Nyerere; Vinginevyo hakuan rekodi inayoonyesha kwamba suala hili lilipata baraka za chombo chochote kinachowakilisha umma/wananchi Zanzibar; Vile vile, hakuna popote tunaweza kupata ushahidi kwamba suala hili lilitangazwa kwa umma, kwa mfano kupitia gazeti la serikali, zanzibar na Tanganyika ili kuwapa fursa wananchi wa pande zote mbili kuli digest na kutoa maoni yao kupitia a referendum au kitu kinachofanania na hili; Kilichotokea kwa umma ilikuwa tu ni breaking news, suala likamalizika;

Lakini katika swali langu hili la kwanza, nilikuwa nalenga zaidi kuuliza - je, what kind of system was envisaged in the original articles of the union, je, serikali moja, mbili, tatu? Ntarekebisha hili swali;

Nadhani watanganyika wengi hawana tabu na muungano kama utaleta nchi kuwa moja, na zanzibar ife, iwe mkoa/mikoa. Wazanzibari wengi nadhani wanataka kuwa na nchi yao tofauti na Tanzania (kitu ambacho wanacho tayari) na bila kuwa na ushirikiano wowote na Tanganyika other than diplomatic and Trade.

Kwahiyo mtazamo wako ni kwamba watanganyika ambao kwa mujibu wa katiba ya JMT 1977 wanaitwa watanzania bara, wana prefer serikali moja na sio serikali tatu? Nini kinakufanya uje na mtazamo huu? Na kwanini unadhani watanganyika walichelewa kuamka kujua kiini macho kilichopo, tofauti na ndugu zetu wa zanzibar ambao waligundua kiini macho from the let go?

Tutakuwa tumepiga hatua, especially wakati wa Mwinyi maana hatuendi Zanzibar na passport nao hawaji na passport. Mengine yapo vilevile, umedumu ila unakoelekea ni kuvunjika kama siyo kuwa nchi moja.

Nilicholenga hasa ni kuuliza, je: given malengo chini ya mkataba wa Muungano, 1964, ni masuala yepi ambayo tutakuwa tumefanikisha kufikia 2014 - kisiasa, kiuchumi na kijamii?

Yalijitokeza mwanzo ambapo wananchi wa nchi hizi mbili hawakuhusishwa (political will).Hili kosa haliwezi kurekebishwa bali kwa njia ya sanduku la kura.

Naunga mkono hoja yako hii iwapo maana yako hapa ni REFERENDUM.

Nadhani inawezekana, labda ungefafanua hili. Maana Tanganyika ikiungana na Zanzibar tunaweza kuwa na Tanzania, tatizo ni muundo wa huo muungano.
Nota benne:
Siungi mkono serikali tatu, ni upotevu wa kodi.

Maana yangu rahisi hapa ni kwamba - Tanzania ni mtoto wa Tanganyika na Zanzibar, so bila ya kuwapa heshima yao stahiki pamoja na pia ku recognize uwepo wao, Tanzania mtoto Tanzania hatakuwa na mashiko; Mtazamo wangu huu lakini unaegemea zaidi Serikali tatu kwani Serikali moja n kitu ambacho kwa sasa hakiwezekani; hili ni suala ambalo litakuja over time, na ni vyema tusiwe wabinafsi na kuharakisha mchakato tu, tunachotakiwa kufanya ni kuwekea wajukuu zetu misingi imara ambayo itaondoa migogoro iliyopo na kuwapa nafasi huko mbeleni kuja fanya maamuzi ya serikali moja bila mikwaruzo;

Vinginevyo katika mazingira ambayo Zanzibar ilipigania uhuru wake in the streets kwa mtutu wa bunduki, na kuwa taifa huru kwa miezi minne na nusu kabla ya kutekwa autonomy yake tena kwa miaka 48 sasa, serikali moja ni suala ambalo tutapoteza tu muda kulizungumzia; isitoshe, tumeshaona kwamba serikali mbili ni tatizo, serikali moja will create a massacre; Kwa wale ambao bado wanaupenda muungano huu, serikali tatu ndio solution ya pekee kwa kuanzia; anything nje ya serikali tatu ni safari fupi zaidi towards kuvunjika kwa muungano;
 
Mchambuzi,mjadala utakuwa mzuri,ingewezekana tuwekee na hiyo nakala ya hotuba ya Lissu

Alichosema Lissu Bungeni:


MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO),
MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU (MB.) KUHUSU MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO) KWA MWAKA 2012/2013

(Kanuni ya 99(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007)

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,

Mwaka huu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetimiza miaka arobaini na nane tangu kuzaliwa kwake baada ya Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Mwalimu Nyerere kutia saini Makubaliano ya Muungano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Sheikh Abedi Amani Karume tarehe 22 Aprili, 1964.

Wakati anawasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2011/2012, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) aliliambia Bunge lako tukufu kwamba “... katika kipindi hicho Muungano wetu umekuwa na mafanikio katika maeneo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.... Muungano wetu ndio nguzo kuu ya umoja na amani.”

Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri aliliambia Bunge lako tukufu kwamba, licha ya mafanikio hayo, “... zipo changamoto katika kumaliza vikwazo vinavyokwamisha shughuli za Muungano.” Mheshimiwa Waziri hakuzitaja changamoto hizo.

‘MAPITO’ YA MUUNGANO

Mheshimiwa Spika,

Katika Utangulizi wake kwa Chapisho la Pili la Mhadhara wa Kiprofesa (Professorial Inaugural Lecture) uliotolewa Januari 1990 na Profesa Issa G. Shivji na kupewa kichwa cha Tanzania: The Legal Foundations of the Union, Profesa Yash Ghai - aliyekuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wa kwanza kutoka Afrika Mashariki - anasema kwamba kwa kuzingatia mazingira ya kuanzishwa kwa Muungano na historia yake, “... kitu cha ajabu sio kwamba umekuwa na matatizo, bali ni kwamba umedumu (licha ya matatizo hayo) – na kwenda kinyume na mwelekeo katika Afrika.”

Muungano ulidumu misuguano ya miaka ya mwanzo kati ya Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume iliyohusu kuongezwa kwa masuala ya fedha na sarafu katika orodha ya Mambo ya Muungano. Aidha, Muungano ulidumu mauaji ya viongozi waandamizi na wajumbe wa Baraza la Mapinduzi la kwanza la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Abdallah Kassim Hanga, Waziri wa Fedha Abdul Aziz Twala, Othman Sharrif, Mdungi Ussi, Saleh Saadalla na wengine wengi.

Vile vile, Muungano ulidumu mauaji ya Sheikh Karume mwenyewe mwaka 1972; ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa’ Zanzibar iliyopelekea kung’olewa madarakani kwa Rais Aboud Jumbe mwaka 1984; alichokiita Mwalimu Nyerere ‘udhaifu’ wa Rais Mwinyi; na kifo cha Mwalimu Nyerere mwaka 1999.

Kwa bahati mbaya, Mheshimiwa Spika, ‘mapito’ haya ya Muungano yamekuwa yanafichwa fichwa, licha ya kauli za mara kwa mara za ‘kuelimisha umma juu ya Muungano.’ Kwa sababu hiyo, zaidi ya tendo la kuchanganya udongo na matukio mengine yaliyofanyika hadharani, historia halisi ya Muungano wetu haifahamiki kwa wananchi walio wengi. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba wakati umefika sasa kwa Serikali kuweka wazi nyaraka mbali mbali zinazohusu historia ya Muungano wetu na ‘mapito’ yake ili Watanzania waelewe masuala yote yaliyotokea yanayouhusu.

Hii ni muhimu zaidi kwa kuzingatia ukweli kwamba mataifa ya magharibi kama vile Marekani na Uingereza yalikwishatoa hadharani nyaraka za mashirika yao ya kijasusi pamoja na balozi zao za Tanzania zinazoonyesha jinsi ambavyo serikali za mataifa hayo zilihusika katika kuzaliwa kwa Muungano.

Mheshimiwa Spika,

Kuanikwa kwa nyaraka zilizoko katika mamlaka mbali mbali za Serikali kutasaidia kuthibitisha au kukanusha taarifa ambazo chanzo chake ni nyaraka za kidiplomasia na kijasusi za nchi hizo kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitokana na njama za kibeberu za kudhibiti ushawishi wa siasa za kimapinduzi za Chama cha Umma na viongozi wake ndani ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar la wakati huo.

Aidha, nyaraka hizo zitatoa mwanga juu ya kilichowasibu viongozi waandamizi wa chama hicho ambao bila uwepo wao kutambuliwa rasmi, historia ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Muungano inabaki pungufu. Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, miaka karibu hamsini ya Muungano ni umri wa kutosha kwa taifa la Tanzania kuambiwa ukweli wote juu ya kuzaliwa kwake na mapito ambayo limepitia katika kipindi hicho.

UKIUKWAJI MAKUBALIANO/SHERIA YA MUUNGANO

Mheshimiwa Spika,

Makubaliano ya Muungano ya tarehe 22 Aprili 1964 yalikuwa ni mkataba wa kimataifa kati ya nchi mbili huru zilizokubaliana kuunda ‘nchi moja huru’, kwa mujibu wa ibara ya (i) ya Hati ya Muungano. Ili kutekeleza Makubaliano ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Tanganyika lilitunga Sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, 1964, Sura ya 557 ya Sheria za Tanzania. Kifungu cha 4 cha Sheria hiyo kilitangaza kuunganishwa kwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuwa ‘Jamhuri moja huru itakayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.’

Kwa upande wa Zanzibar, Baraza la Mapinduzi – ambalo ndio lilikuwa ‘Bunge’ la Zanzibar wakati huo – halikutunga sheria ya kuridhia Makubaliano ya Muungano. Jambo hili limekuwa chanzo cha mjadala mkali katika duru za kitaaluma na kisheria juu ya uhalali wa Muungano wenyewe. Kwa vyovyote vile, matokeo ya kusainiwa Makubaliano ya Muungano ni kwamba Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zilikufa na nchi moja – iliyokuja baadae kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - kuzaliwa.

Mheshimiwa Spika,

Kwa mujibu wa aya ya (iv) ya Makubaliano ya Muungano na kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Muungano, Mambo ya Muungano yaliyokubaliwa kwenye Makubaliano ya Muungano yalikuwa kumi na moja. Haya ni mambo yaliyoko katika vipengele vya 1 hadi 11 vya Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya Muungano. Hata hivyo, kati ya mwaka 1964 and 1973 mambo mengine sita – yanayoonekana katika vipengele 12 hadi 16 vya Nyongeza ya Kwanza – yaliongezwa katika orodha ya Mambo ya Muungano.

Hivyo basi, mwaka 1965 masuala ya fedha, sarafu na benki yaliongezwa; mwaka 1967 leseni ya viwanda na takwimu, elimu ya juu na mambo yaliyokuwa katika Nyongeza ya X ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliongezwa; mwaka 1968 yaliongezwa mambo ya maliasili ya mafuta, petroli na gesi asilia; na mwaka 1973 mambo yanayohusu Baraza la Mitihani la Taifa yaliongezwa.

Aidha, Mheshimiwa Spika, Mabadiliko ya Tano ya Katiba ya mwaka 1984 yaligawa kipengele cha Nyongeza ya X ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutengeneza vipengele vinne vinavyojitegemea katika orodha ya Mambo ya Muungano, yaani usafiri na usafirishaji wa anga, utafiti, utabiri wa hali ya hewa na takwimu.

Vile vile, Mabadiliko hayo yaliongeza kitu kipya katika orodha ya Mambo ya Muungano: Mahakama ya Rufani ya Tanzania. Aidha, kipengele cha 3, yaani ulinzi, kilifanyiwa marekebisho na kuwa ‘ulinzi na usalama.’ Na mwaka 1992 ‘uandikishwaji wa vyama vya siasa’ nao uliongezwa katika orodha ya Mambo ya Muungano.

Mheshimiwa Spika,

Mambo yote yaliyoongezwa katika orodha ya Mambo ya Muungano baada ya mwaka 1964 yalikuwa nje ya Makubaliano ya Muungano na nje ya Sheria ya Muungano na kwa hiyo yalikuwa batili. Hii ni kwa sababu Sheria ya Muungano – na sio Katiba za Muda za 1964 au 1965 au ya sasa - ndio Sheria Mama iliyozaa Muungano na kuweka mgawanyo wa madaraka kati ya mamlaka za Jamhuri ya Muungano na mamlaka za Zanzibar. Sheria ya Muungano ilitungwa na Bunge la Katiba tofauti na sheria za kawaida.

Aidha, Katiba ya Muda, 1965 iliyotawala Tanzania hadi 1977 iliiweka Sheria hiyo kama Nyongeza ya Pili katika Katiba na kuweka masharti kwamba Sheria hiyo haiwezi kurekebishwa bila marekebisho hayo kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wabunge wote wa Tanganyika na wale wa Zanzibar. Vile vile, Katiba ya Muunganoinataja, katika Orodha ya Kwanza ya Nyongeza ya Pili, kwamba moja ya Sheria ambazo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wabunge wote ni “Sura ya 557 (Toleo la 1965), Sheria ya Kuthibitisha Mapatano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964.”

Mambo yote haya, Mheshimiwa Spika, yanaifanya Sheria ya Muungano kuwa na haiba ya Katiba. Kama alivyosema Profesa Issa Shivji katika The Legal Foundations of the Union: “Kila mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria amefundishwa kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapatikana katika waraka unaoitwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. Lakini, nachelea kusema, kila mwanafunzi amefundishwa visivyo.

Katiba ya Tanzania inapatikana sio katika waraka mmoja, bali katika nyaraka mbili. Sheria ya Muungano, Sura ya 557 ya Sheria za Tanzania na Sheria ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.... Vivyo hivyo, Katiba ya Zanzibar inapatikana katika (1) Sheria ya Muungano na (2) Katiba ya Zanzibar, 1984.” Katika masuala yanayohusu Muungano, kwa mujibu wa Profesa Shivji, waraka unaotawala ni Sheria ya Muungano.

Hii ndio kusema kwamba panapotokea mgongano kati ya Katiba au Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Muungano, ni Sheria ya Muungano ndio inayokuwa na Katiba au Katiba ya Zanzibar inakuwa batili kwa kiasi cha ukiukaji wake wa Sheria ya Muungano.

Mheshimiwa Spika,

Kifungu cha 5 cha Sheria ya Muungano, ambacho ndicho chenye misingi mikuu ya Muungano hakijawahi kurekebishwa tangu Sheria yenyewe ilipotungwa mwaka 1964. Badala yake, Bunge limekuwa na tabia ya kukwepa kuigusa kabisa Sheria ya Muungano na badala yake limekuwa likifanya marekebisho ya orodha ya Mambo ya Muungano iliyowekwa kwa mara ya kwanza katika Katiba za Muda za mwaka 1964 na 1965 kwa kuongeza vipengele katika orodha hiyo. Lengo la marekebisho haya, Mheshimiwa Spika, limekuwa mara zote ni kuinyang’anya Zanzibar mamlaka yake chini ya Sheria ya Muungano.

Ndio maana katika Mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya CCM Kuhusu Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Katiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliyotolewa tarehe 27 Januari, 1983, CCM ilitamka kwamba “... msingi wa kuwa na orodha ya mambo ya muungano katika Katiba ni kuonyesha mamlaka ya Serikali ya Zanzibar ambayo yalikabidhiwa kwa Serikali ya Muungano; na msingi wa kuongeza mambo zaidi katika orodha ya mambo ya muungano, kama ambavyo imefanyika mara kwa mara, ni kuhamisha mamlaka zaidi ya Serikali ya Zanzibar kwenda kwa Serikali ya Muungano.”

Mheshimiwa Spika,

Profesa Shivji anasema - katika The Legal Foundations of the Union - kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano halikupewa mamlaka ya kuongeza Mambo ya Muungano bali lilipewa mamlaka ya kutunga sheria zinazohusu Mambo ya Muungano kama yalivyofafanuliwa katika Sheria ya Muungano. Kwa maana hiyo, nyongeza zote zilizofanyika katika orodha ya Mambo ya Muungano tangu mwaka 1964 zilikiuka Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano na ni batili. Ndio maana, kwa muda mrefu, Wazanzibari wamelalamikia masuala haya, hasa hasa masuala ya fedha, sarafu na mafuta na gesi asilia.

Mheshimiwa Spika,

Vitendo vya kupuuza Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano iliyoridhia Makubaliano vilifikia kilele chake tarehe 21 Novemba, 2000 pale Mahakama ya Rufani ya Tanzania ilipotamka – katika kesi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar dhidi ya Machano Khamis Ali na Wenzake 17 – kwamba Zanzibar sio nchi na wala sio dola. Bali, kwa mujibu wa Mahakama ya Rufani, ‘hakuna ubishi wa aina yoyote kwamba Jamhuri ya Muungano ni nchi moja na dola moja.’

Kama tulivyokwisha kuonyesha, suala la Mahakama ya Rufani ya Tanzania yenyewe kuwa suala la Muungano liliingizwa kwenye orodha ya Mambo ya Muungano kinyemela na kinyume na Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano. Jibu la Wazanzibari juu ya ukiukwaji wa muda mrefu wa Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano iliyoridhia Makubaliano hayo lilikuwa ni kupitisha Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar mwaka 2010.

KATIBA YA MUAFAKA AU KATIBA YA UHURU?

Mheshimiwa Spika,

Misukosuko ambayo imeukumba Muungano wetu tangu mwaka 1964 hailingani na hatari kubwa inayoukabili hivi sasa. Kama tulivyomweleza Rais Kikwete katika waraka wetu wa tarehe 27 Novemba, 2011, “Muungano wetu upo katika hatari kubwa ya kuvunjika kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya kikatiba ambayo yamefanyika katika Katiba ya Zanzibar, 1984 na kutokana na Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Hii ni kwa sababu Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba, 2010, inaashiria tafsiri mpya ya Makubaliano ya Muungano na ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inahoji misingi ya Jamhuri ya Muungano kama nchi moja, mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, na mambo muhimu ya Muungano....” Ili kufahamu jambo hili vizuri, ni muhimu kuelewa kwa undani yaliyomo katika Sheria hiyo ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba Zanzibar.
Mheshimiwa Spika,

Tarehe 13 Agosti, 2010, wakati Bunge la Jamhuri ya Muungano likiwa limevunjwa kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar lilipitisha Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar, 1984. Mabadiliko haya yaliweka msingi wa kikatiba wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar inayoshirikisha CCM na Chama cha Wananchi (CUF). Kwa sababu hiyo, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imepigiwa upatu kama Katiba ya Muafaka na, kwa kiasi fulani, hii ni kweli.

Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imekwenda mbali zaidi. Sheria hii sio tu imehoji uhalali wa orodha ya Mambo ya Muungano ya tangu mwaka 1964 na nyongeza zake zilizofuata, bali pia imehoji pia misingi muhimu ya Sheria ya Muungano iliyoridhia Makubaliano ya Muungano. Kwa mtazamo huu, Katiba ya sasa ya Zanzibar inaelekea kuwa ni tangazo la uhuru wa Zanzibar zaidi kuliko waraka wa muafaka kati ya vyama viwili vilivyokuwa mahasimu.

Mheshimiwa Spika,

Aya ya (i) ya Makubaliano ya Muungano na kifungu cha 4 cha Sheria ya Muungano vilitangaza muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuundwa kwa ‘Jamhuri moja huru itakayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.’

Huu ndio msingi wa maneno ya ibara ya 1 ya Katiba ya Muungano kwamba ‘Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.’ Na huu ndio ulikuwa msingi wa maneno ya ibara ya 1 ya Katiba ya Zanzibar ya kabla ya Mabadiliko ya 2010 kwamba ‘Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano.’ Sasa msingi huu wa Muungano umehojiwa na maneno ya ibara ya 2 ya Katiba mpya ya Zanzibar yanayotamka kwamba ‘Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’

Mheshimiwa Spika,

Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Muungano inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano – kwa kushauriana kwanza na Rais wa Zanzibar - mamlaka ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika mikoa, wilaya au maeneo mengineyo. Vile vile, ibara ya 61(3) ya Katiba ya Muungano inampa Rais wa Zanzibar mamlaka ya kuteua Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Zanzibar ‘baada ya kushauriana na Rais.’ Masuala ya mgawanyo wa nchi katika mikoa na mamlaka za mikoa hiyo sio, na hayajawahi kuwa, Mambo ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Muungano.

Vile vile hayapo katika orodha ya Mambo ya Muungano. Ni wazi kwa hiyo, kwamba ibara za 2(2) na 61(3) za Katiba ya Muungano zilikuwa zinakiuka matakwa ya Sheria ya Muungano na kwa hiyo ni batili. Sasa wazanzibari ‘wamejitangazia uhuru’ kwa kutangaza – katika ibara ya 2A ya Katiba mpya ya Zanzibar – kwamba “... Rais (wa Zanzibar) aweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.” Aidha, kwa ibara ya 61(1), Rais wa Zanzibar hawajibiki tena kushauriana na Rais wa Muungano pale anapofanya uteuzi wa wakuu wa mikoa ya Zanzibar.

Mheshimiwa Spika,

Wakati ambapo Sheria ya Muungano ilikuwa imetambua na kuhifadhi mamlaka ya Rais wa Zanzibar kama mkuu wa dola ya Zanzibar, Mahakama ya Rufani ya Tanzania – katika Kesi ya Machano Khamis Ali na Wenzake – ilitishia moja kwa moja msingi huo kwa kutamka kwamba Zanzibar sio nchi na wala sio dola na kwa hiyo haiwezi kutishiwa na kosa la uhaini.

Sasa ibara ya 26(1) ya Katiba mpya Zanzibar ‘imerudisha’ dola ya Zanzibar kwa kutamka kwamba “kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa Mkuu wa Nchi ya Zanzibar, Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.” Aidha, kwa kutambua kwamba ‘Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano’ sio moja ya Mambo ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Muungano, Katiba ya sasa ya Zanzibar imetamka kwamba katika kesi zinazohusu ‘kinga za haki za lazima, wajibu na uhuru wa mtu binafsi’, uamuzi wa majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar “... utakuwa ni wa mwisho na hautokatiwa rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Tanzania.”

Mheshimiwa Spika,

Kifungu cha 5(1)(a)(iii) na (iv) cha Sheria ya Muungano kinataja ‘ulinzi’ na ‘polisi’ kama sehemu ya mambo kumi na moja ya Muungano. Na hivyo ndivyo inavyosema aya ya (iv)(c) na (d) ya Makubaliano ya Muungano. Ijapokuwa ‘ulinzi’ ulichakachuliwa baadae kwa kuongezwa maneno ‘na usalama’, bado ni sahihi kusema kwamba masuala ya ulinzi na polisi ni masuala halali ambayo Sheria ya Muungano iliyakasimu kwa Serikali ya Muungano.

Na kwa sababu hiyo, ni sahihi kwa Katiba ya Muungano kutamka – kama inavyofanya katika ibara ya 33(2) - kwamba ‘Rais (wa Jamhuri ya Muungano) atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.’

Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, katika kile kinachoonekana kama hojaji kubwa ya msingi huu wa Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano, ibara ya 121 ya Katiba ya sasa ya Zanzibar imeunda majeshi ya Zanzibar inayoyaita ‘Idara Maalum.’

Majeshi haya, kwa mujibu wa ibara ya 121(2) ni Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU); Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM); Chuo cha Mafunzo (cha wahalifu), na Idara Maalum nyingine yoyote ambayo Rais wa Zanzibar anaweza kuianzisha ‘ikiwa ataona inafaa....’ Kuthibitisha kwamba Idara Maalum ni majeshi, ibara ya 121(4) inakataza watumishi wa Idara Maalum ‘... kujishughulisha na mambo ya siasa....’ Makatazo haya hayatofautiani na makatazo ya wanajeshi kujiunga na vyama vya siasa yaliyoko katika ibara ya 147(3) ya Katiba ya Muungano.

Mheshimiwa Spika,

Sio tu kwamba Katiba mpya ya Zanzibar inaanzisha majeshi bali pia inamfanya Rais wa Zanzibar kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi hayo. Kwa mujibu wa ibara ya 123(1) ya Katiba hiyo, “Rais atakuwa Kamanda Mkuu wa Idara Maalum na atakuwa na uwezo wa kufanya chochote kile anachohisi, kwa maslahi ya Taifa (la Zanzibar), kinafaa.” Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 123(2), mamlaka ya Rais wa Zanzibar chini ya ibara ndogo ya (1) yanaingiza “... uwezo wa kutoa amri ya kufanya shughuli yoyote inayohusiana na Idara hiyo kwa manufaa ya Taifa.”

Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, haya ni mamlaka ya kutangaza au kuendesha vita ambayo, kwa mujibu wa ibara ya 44(1) ya Katiba ya Muungano, ni mamlaka pekee ya Rais wa Jamhuri ya Muungano. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe kauli rasmi mbele ya Bunge hili tukufu kama tafsiri hii ya ibara ya 123 ya Katiba mpya ya Zanzibar ni sahihi.

Na kama ni sahihi, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali itoe tamko Bungeni ni kwa nini imeiruhusu Zanzibar kujinyakulia mamlaka juu ya mambo ya ulinzi na usalama ambayo kwa historia yote ya Muungano yamekuwa ni mamlaka pekee ya Serikali ya Muungano.

Mheshimiwa Spika,

Kifungu cha 5(1)(b) cha Sheria ya Muungano kilitamka kwamba muundo wa Serikali ya Zanzibar utakuwa kama utakavyoamuliwa na sheria za Zanzibar pekee. Na hivyo ndivyo ilivyokubaliwa katika aya ya (iii)(a) ya Makubaliano ya Muungano. Hata hivyo, licha ya muundo wa Serikali ya Zanzibar kutokuwepo katika orodha ya Mambo ya Muungano, Katiba ya Muungano imetenga Sura ya Nne nzima kuzungumzia ‘Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.’

Kwa mujibu wa Profesa Shivji katika The Legal Foundations of the Union, Sura ya Nne ya Katiba ya Muungano “... haina ulazima wowote na ni kuingilia, bila kualikwa, kwenye mambo ambayo yako ndani ya mamlaka pekee ya Zanzibar.” Ndio maana Katiba mpya ya Zanzibar – kwa usahihi kabisa - imefanya mabadiliko katika muundo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bila ya kuzingatia matakwa ya Sura ya Nne ya Katiba ya Muungano.

Mheshimiwa Spika,

Katiba mpya ya Zanzibar sio tu kwamba ‘imetangaza uhuru’ wa Zanzibar kwa kuhoji misingi muhimu ya Makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano, bali pia imehakikisha kwamba uhuru huo utalindwa dhidi ya tishio lolote la Serikali ya Muungano. Hii imefanywa kwa kuweka utaratibu wa kuwepo kura ya maoni ya wananchi wa Zanzibar kuhusu mabadiliko ya vifungu kadhaa vya Katiba ya Zanzibar. Kwa mujibu wa ibara ya 80A(1) ya Katiba hiyo, “... Baraza la Wawakilishi halitaweza kufanya mabadiliko ya Katiba kuhusiana na sharti lolote lililomo katika kifungu chochote kilichoainishwa katika kijifungu cha (2) cha kifungu hiki, mpaka kwanza mabadiliko hayo yakubaliwe na wananchi kwa kura ya maoni.”

Vifungu vinavyohitaji kura ya maoni ni vifungu vyote vya Sehemu ya Kwanza ya Sura ya Kwanza inayohusu Zanzibar kama nchi na/au dola; kifungu cha 9 kinachohusu Serikali na watu wa Zanzibar; vifungu vyote vya Sura ya Tatu inayohusu kinga ya haki za lazima, wajibu na uhuru wa mtu binafsi; na kifungu cha 26 kinachohusu Rais wa Zanzibar na mamlaka yake.

Vifungu vingine ni pamoja na kifungu cha 28 kinachohusu muda wa urais; Sehemu ya Pili na ya Tatu ya Sura ya Nne zinazohusu Makamu wawili wa Rais, Baraza la Mawaziri na Baraza la Mapinduzi; kifungu cha 80A kinachohifadhi haki ya kura ya maoni; na vifungu vya 121 na 123 vinavyohusu Idara Maalum na mambo yanayohusiana nayo.

Mheshimiwa Spika,

Kuweka masharti ya kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya vifungu tajwa vya Katiba mpya ya Zanzibar kuna athari ya moja kwa moja kwa uhai wa Muungano wetu. Hii ni kwa sababu hata vifungu ambavyo tumeonyesha kwamba vinakiuka misingi mikuu ya Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano haviwezi kubadilishwa bila kura ya maoni ya Wazanzibari.

Kwa maneno mengine, kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Zanzibar, masuala ya kama Tanzania ni nchi moja au la, majeshi ya ulinzi, polisi, n.k. ambayo yamekuwa Mambo ya Muungano kwa mujibu wa Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano sio Mambo ya Muungano tena hadi hapo wananchi wa Zanzibar watakapoamua – kwa kura ya maoni – kuyarudisha kwa mamlaka ya Muungano. Huku, Mheshimiwa Spika, ni kutangaza uhuru wa Zanzibar bila kutaja neno uhuru! Huku ni kuua Muungano bila kukiri hadharani!

Mheshimiwa Spika,

Kwa mtazamo wa Katiba ya sasa ya Zanzibar, hatuna tena nchi moja inayozungumzwa katika Katiba ya Muungano bali tuna nchi mbili. Kwa mtazamo huo huo, masuala ya ulinzi na usalama, polisi, n.k. sio tena Mambo ya Muungano kwa sababu sasa kila nchi ina majeshi yake na kila moja ina Amiri Jeshi Mkuu wake. Aidha, tuna marais wawili, wakuu wa nchi wawili viongozi wa serikali wawili. Haya yote yanakiuka moja kwa moja Makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano.

Kwa upande mwingine, kwa mtazamo wa Katiba ya sasa ya Zanzibar, Rais wa Muungano hana tena mamlaka ya kugawa mikoa na wilaya kwa upande wa Zanzibar, na wala hawezi kumshauri tena Rais wa Zanzibar anapoteua Wakuu wa Mikoa wa Tanzania Zanzibar. Aidha, Mahakama ya Rufani ya Tanzania – licha ya kuwa moja ya Mambo ya Muungano kwa mujibu wa Katiba ya Muungano - haina tena mamlaka ya kusikiliza na kuamua rufaa zinazohusu haki za msingi na uhuru wa mtu binafsi zinazotoka Zanzibar. Yote haya hayapo katika Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano lakini yapo katika Katiba ya Muungano.

KURUDISHWA KWA SERIKALI YA TANGANYIKA

Mheshimiwa Spika,

Katika maoni yetu kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilionyesha jinsi ambavyo “tafsiri hii mpya ya Makubaliano ya Muungano na Katiba ya Jamhuri ya Muungano imetiliwa nguvu kubwa na Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo imeipa Zanzibar nafasi na ushawishi mkubwa katika utungaji wa Katiba Mpya.”

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilionyesha kwamba, kwa mujibu wa Sheria hiyo, “Rais wa Zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano bali pia ana kura ya turufu katika mchakato mzima wa Katiba Mpya.” Aidha, tulithibitisha jinsi ambavyo “... ushawishi mkubwa wa Zanzibar hauishii katika kura ya turufu aliyo nayo Rais wa Zanzibar pekee yake (bali) Zanzibar ina ushawishi mkubwa vile vile kutokana na nafasi kubwa iliyo nayo katika vyombo vingine vinavyoundwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba....”

Mheshimiwa Spika,

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inarudia tena tahadhari iliyoitoa wakati huo kwamba: “Masharti haya ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yana athari kubwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu yanakiuka Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964, Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano na hata Katiba ya sasa ya Zanzibar....” Na kama tulivyosema wakati huo, “... tafsiri hii mpya ya Makubaliano ya Muungano na ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inarudisha mezani mjadala juu ya muundo wa Muungano wetu na nafasi ya iliyokuwa Tanganyika katika Muungano huo.”

Mheshimiwa Spika,

Kama ilivyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano umejitangazia uhuru kama ambavyo tumeonyesha hapa, huu ni wakati muafaka kuanzishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika.

Katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano sio tu una Serikali kamili, Bunge kamili, Mahakama kamili, wimbo wa taifa, bendera ya taifa, na sasa una nchi kamili yenye mipaka na eneo la bahari linalojulikana, una majeshi yake na Amiri Jeshi Mkuu wake, huu ni muda mzuri kwa Serikali ya Tanganyika kuzaliwa upya. Katika mazingira kama haya, Mheshimiwa Spika, upande wa pili wa Muungano unatakiwa kuwa na vitu vyote hivyo pia ili uweze kujadiliana na upande wa kwanza katika hali ya usawa.

Huu ni wakati wa kurudishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika kama ilivyopendekezwa na Tume ya Rais ya Chama Kimoja au Vyama vingi mwaka 1991 na Tume ya Kissanga mwaka 1998, na kama ilivyopendekezwa na Kundi la Wabunge 55 wa Bunge hili tukufu na kuungwa mkono na Serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi kabla ya hoja hiyo kutunguliwa na Baba wa Taifa mwaka 1993!

KURA YA MAONI JUU YA MUUNGANO

Mheshimiwa Spika,

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambua kwamba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inaielekeza Tume ya Katiba kuongozwa na misingi mikuu ya kitaifa ya kuhifadhi na kudumisha ‘kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano.’ Hata hivyo, baada ya kujitokeza kwa wananchi wanaopinga kuendelea kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kwamba wale wanaopinga Muungano nao wajitokeze kutoa maoni yao kwa Tume.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka Serikali itoe kauli mbele ya Bunge hili tukufu ni namna gani maoni ya wale wanaotaka kiini macho hiki cha Muungano kiishe yatashughulikiwa na Tume ambayo imepewa jukumu kisheria la kukihifadhi na kukidumisha kiini macho hicho? Ni kipi kitakachoizuia Tume ya Warioba kupuuza maoni ya watu hao kwa hoja kwamba Sheria inaielekeza Tume kuratibu na kukusanya maoni na kutoa mapendekezo ya kuhifadhi na kudumisha Muungano?

Mheshimiwa Spika,

Katika miezi ya karibuni kumejitokeza makundi ya wananchi, hasa kwa upande wa Zanzibar, ambayo yamedai kwamba iitishwe kura ya maoni ya wananchi ili kuamua kama bado kuna haja ya kuendelea na Muungano. Makundi haya, yakiongozwa na kundi la Uamsho, yameshambuliwa sana hadharani kwa kudaiwa kwamba yanataka kuvunja Muungano. Na watu ambao wameongoza mashambulizi dhidi ya wana-Uamsho ni viongozi waandamizi wa CCM, wakiwemo viongozi wakuu wastaafu wa chama hicho.

Mheshimiwa Spika,

Katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tulisema kwamba “... hofu ... ya kuwaudhi ‘Wazanzibari’ ndio imepelekea kimya kikuu – ndani ya CCM na ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano - juu ya ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano uliofanywa na Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar, 2010.” Naomba nikiri kwamba tulikosea kusema hivyo.

Tulichotakiwa kusema wakati ule, na tunachokisema sasa, ni kwamba kimya kikuu ndani ya CCM na ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya ukiukwaji mkubwa wa Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano pamoja na Katiba kinatokana sio tu na ‘hofu’ ya kuwaudhi Wazanzibari bali pia kinatokana na ukweli kwamba viongozi waandamizi wa CCM pamoja na wa Serikali yake walishiriki katika ukiukwaji huo!

Wao ndio wanaoongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ndio waliondaa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar. Na wao ndio wanaoongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano waliokula kiapo cha kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Na kwa hiyo wao ndio walioiruhusu Zanzibar kutangaza uhuru kwa Mabadiliko haya ya Katiba yake.

Mheshimiwa Spika,

Kwa viongozi hawa na chama chao kuibuka sasa na kuwatuhumu wana-Uamsho na makundi mengine kwamba wanataka kuvunja Muungano kwa kudai kura ya maoni ya wananchi wakati wao wenyewe wamekaa na kupitisha marekebisho ya Katiba ambayo tayari yamevunja Makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano ni kilele cha juu cha unafiki wa kisiasa. Mashabiki hawa wa Muungano waeleze walikuwa wapi wakati Zanzibar inatangaza uhuru wake kwa kuchanachana Makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano.

Mheshimiwa Spika,

Kwa wale wanaodai kwamba wana-Uamsho wanataka kuvunja Muungano kwa sababu tu ya kudai kura ya maoni, tunaomba tuwakumbushe yafuatayo. Kwanza, kwa mujibu wa Baba wa Taifa katika kitabu chake Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania: “Huko nyuma baadhi ya viongozi wa Zanzibar wapinzani wa Muungano wamewahi kudai tufanye referendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano. Tukakataa kwa sababu safi kabisa.”

Hapa Mwalimu alikuwa anamzungumzia aliyekuwa Rais wa Zanzibar Alhaj Aboud Jumbe, Waziri Kiongozi Ramadhani Haji Faki na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Bashir Ebassuah Kwaw Swanzy waliong’olewa madarakani mwaka 1984 baada ya ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa.’

Aidha, Mheshimiwa Spika, katika kitabu hicho hicho Mwalimu Nyerere anasema yafuatayo juu ya kilichotokea kwenye Bunge hili hili wakati wa Bunge la bajeti la mwaka 1993: “Tarehe 30 Julai, 1993 wakati wa mkutano wa bunge la bajeti ukiendelea, zaidi ya wabunge 50 kwa pamoja walitoa taarifa ya kusudio la kuwasilisha hoja Bungeni ambayo inadai (kwamba) kuendelea na mfumo huu wa Muungano usiowaridhisha wananchi wengi wa upande mmoja ni kuhatarisha kuendelea kudumu kwa Muungano....

Hivyo basi wabunge hawa wanaliomba Bunge ... liazimie kwamba Serikali ... ilete Muswada Bungeni kabla ya Februari 1994, kurekebisha katiba ya Jamhuri ya Muungano ili kuwezesha uundaji wa ‘Serikali ya Tanganyika’ ndani ya Muungano.... Tarehe 20 Agosti, 1993 wabunge wahusika waliwasilisha taarifa nyingine ... iliyokuwa inalitaka Bunge ... liazimie kwamba Serikali ... iandae kura ya maoni ambayo itafanyika kabla ya 31 Desemba, 1994 ili kupata maoni ya wananchi wa Tanzania juu ya kuundwa kwa “Serikali ya Tanganyika” ndani ya Muundo wa Muungano....”

Pili, Mheshimiwa Spika, Katiba ya sasa ya Zanzibar ambayo mashabiki wa Muungano wameileta kwa kupitia Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba tayari imewapa wananchi wa Zanzibar haki ya kuamua, kwa kura ya maoni, mambo mbali mbali yanayoihusu nchi hiyo na namna itakavyoongozwa. Mashabiki hawa wa Muungano wakubali kuvuna walichopanda, wasibeze wale wote wanaotaka kutumia haki ya kura ya maoni kuamua hatma ya Muungano na nafasi ya Zanzibar ndani au nje yake.

Mheshimiwa Spika,

Ni wazi, kwa kuzingatia ushahidi huu, kwamba madai ya kuwa na kura ya maoni ya wananchi ili kuamua masuala makubwa yanayohusu Muungano wetu ni ya siku nyingi na yametolewa na watu na taasisi mbali mbali. Madai haya hayajaanzishwa na wana-Uamsho wala CHADEMA. Ni wazi vile vile kwamba kura ya maoni inaruhusiwa kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Zanzibar.

Kwa sababu hizi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaungana na wale wote ambao wamedai, na wanaendelea kudai kuitishwa kura ya maoni ya wananchi ili waweze kuamua mustakbala wa nchi yetu. Kuendelea na kiini macho cha Muungano wakati Serikali zote mbili na chama tawala cha CCM wanauvunja kivitendo kutaipelekea nchi yetu kwenye njia ya Ethiopia na Eritrea, au Sudan na Sudan Kusini au Yugoslavia ya zamani.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka Watanzania waamue, kwa kura ya maoni, kama bado wanataka kuendelea na Muungano na kama jibu lao ni ndio, ni muundo gani wa Muungano wanautaka. Kama, kwa busara zao, wataamua kwamba nusu karne ya Muungano inatosha basi itakuwa afadhali kwenda njia ya Czechoslovakia ya zamani kuliko kwenda njia ya Yugoslavia ya zamani, au Ethiopia na Eritrea au Sudan na Sudan Kusini.

Mwisho, Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali iwaeleze Watanzania juu ya hatua, kama zipo, ilizozichukua kuzuia ukiukwaji huu wa Makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba. Na mwisho, Serikali itoe kauli mbele ya Bunge hili tukufu kama - kwa ukiukwaji huu wa Makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano – Bunge hili tukufu litakuwa ndani ya mamlaka yake kuchukua hatua za kumshtaki Rais kwa mujibu wa ibara ya 46A ya Katiba kwa kushindwa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Muungano kama kiapo cha kazi yake kinavyomtaka.

HITIMISHO

Mheshimiwa Spika,

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wajumbe wote wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni chini ya uongozi wa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mheshimiwa Freeman A. Mbowe kwa ushauri na ushirikiano uliowezesha maandalizi ya maoni haya. Aidha, niwashukuru familia yangu – mke wangu mpenzi Alicia Bosensera na mapacha wetu Agostino Lissu na Edward Bulali – kwa kuendelea kuvumilia upweke unaotokana na ‘Daddy’ kuwa mbali muda mwingi kwa sababu ya majukumu mazito ya kibunge.

Aidha, niwashukuru wapiga kura wangu wa Jimbo la Singida Mashariki kwa imani na nguvu wanayonipa kila siku kwa kuendeleza msimamo wetu thabiti wa kukataa kunyanyaswa, kunyonywa na kupuuzwa na ‘Ndaa ya Njou’! Mwisho naomba nichukue fursa hii kuwashukuru viongozi, wanachama na wapenzi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wananchi wote wa Tanzania ambao wameendelea kutuunga mkono na kututia nguvu katika kipindi hiki muhimu katika historia ya nchi yetu. Ninawaomba waendelee kutuunga mkono na kututia nguvu katika siku ngumu na za majaribu makubwa zinazokuja!

Mheshimiwa Spika,

Baada ya maelezo haya marefu, naomba kukushukuru na wewe binafsi na naomba kuwasilisha.

---------------------------------------------------------------
Tundu Antiphas Mughwai Lissu

MSEMAJI & WAZIRI KIVULI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO)
KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
 
EMT,

nashukuru kwa Hotuba hii ya Tundu Lissa, sasa nadhani tuna nyenzo zote muhimu za kutusaidia kubaini zaidi kiini macho hiki, lengo likiwa ni kuboresha muungano wetu, sio kuuvunja;

cc: jmushi1
 
Mchambuzi,

..huwezi kuwa ktk muungano huku ukiendelea kuwa na autonomy.

..hata ktk mfumo wa shirikisho nchi wanachama hupoteza autonomy.

..kama tunataka autonomy basi tunapaswa kuunda jumuiya ya Tanganyika na Zanzibar, kama zilivyo jumuiya za EAC, na SADC.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi,

..huwezi kuwa ktk muungano huku ukiendelea kuwa na autonomy.

..hata ktk mfumo wa shirikisho nchi wanachama hupoteza autonomy.

..kama tunataka autonomy basi tunapaswa kuunda jumuiya ya Tanganyika na Zanzibar, kama zilivyo jumuiya za EAC, na SADC.
Mkubwa,
Muungano wa nchi na nchi sidhani kama una formula. Ila ninachodhani ni kuwa
Ridhaa ya wananchi ndiyo "nucleus" ya muungano baina ya nchi mbili huru.
 
Mchambuzi,

..huwezi kuwa ktk muungano huku ukiendelea kuwa na autonomy.

..hata ktk mfumo wa shirikisho nchi wanachama hupoteza autonomy.

..kama tunataka autonomy basi tunapaswa kuunda jumuiya ya Tanganyika na Zanzibar, kama zilivyo jumuiya za EAC, na SADC.

Asante kwa mchango wako Joka Kuu,

Msingi wa hoja yangu ni katika mazingira ya Serikali tatu i.e. a federation, and not a unitary state kama ilivyo hivi sasa chini ya kiini macho hiki; Katika autonomy, nacholenga zaidi ni suala la fiscal autonomy - fiscal decentralization ambapo different states have the autonomy to set their own levels of taxes etc; Kwa mfano,Marekani is a Federal Republic with autonomous states, and each state ina fiscal autonomy; kabla ya Marekani kuamia kuwa na a federation, ilikuwa na a confederation na moja ya masuala ambayo yalileta mgogoro mkubwa sana uliotishia kuvunjika kwa confederation ile ilikuwa ni suala la fiscal autonomy ambapo baadhi ya states zilikuwa zinahisi kutotendewa haki; suala hili linajitokeza katika muungano wetu, lakini ni kwa sababu ya kiini macho nilichokijadili kuliko suala lingine lolote;

Ebu jiulize - Muungano wa aina gani huu ambao mwasisi wake aliweka bayana kwamba unaiga mfumo wa UK, na pale ulipoanza kupata msuko suko baada ya kujisahau kwamba Tanzania haiwezi kuwa nchi ya chama kimoja daima, likawa tatizo, na Judge Bomani akapewa kazi ya kurekebisha hilo na baadae kuja na ushauri wa kufuata system ya mgombea mwenza ya marekani ili isitokee/kuokoa aibu ya chama kimoja kushinda bara, na kingine kushinda visiwani hivyo kuvuruga mfumo wa rais na makamo wa rais?

Muungano wetu wa sasa mfumo wake ni wa ovyo, hauna any originality zaidi ya uchakachuaji na copy and paste ya US na UK; thats the bottom line; na kuupeleka towards serikali moja au kuubakisha chini ya serikali mbili kama sasa is only a disaster waiting to happen; We need serikali tatu kama kweli tuna nia ya kuokoa muungano wetu, na pia kudumisha amani na umoja; tuwajengee wajukuu zetu misingi ya wao kuja weka serikali moja baadae, tusiwe wabinafsi kutaka kuacha legacy kwa kukimbiza mambo ovyo; Rome wasn't built in a day;
 
Mkubwa,
Muungano wa nchi na nchi sidhani kama una formula. Ila ninachodhani ni kuwa
Ridhaa ya wananchi ndiyo "nucleus" ya muungano baina ya nchi mbili huru.
Kobello,

..nakubaliana na hoja yako.

..lakini lazima tuwe wakweli kwamba mambo yale 11 ya muungano ndiyo kiini cha Tanganyika na Zanzibar kupoteza "autonomy."

..kwa maana nyingine ni kwamba Tanganyika na Zanzibar zilikoma kuwa dola au nchi mbili tofauti, na badala yake zikaunda dola au nchi kubwa inayoitwa TANZANIA.
 
Last edited by a moderator:
Kobello,

..nakubaliana na hoja yako.

..lakini lazima tuwe wakweli kwamba mambo yale 11 ya muungano ndiyo kiini cha Tanganyika na Zanzibar kupoteza "autonomy."

Ni muhimu ugundue kwamba Mkataba ule haukuwa final, ilitakiwa ndani ya mwaka mmoja izaliwe katiba itakayo simamia autonomy of each state; Articles zile zilikuwa ni kama katiba ya muda, lakini badala yake, mwaka 1965, katiba iliyokuja ikawa bado ni ya muda, na ikabakia hivyo kwa miaka 12; na ndani ya kipindi hiki, kilichokuwa kinaendelea ni udonoaji wa autonomy ya Zanzibar kwa kuzidi kuongeza orodha ya masuala ya muungano kinyume na mkataba wa muungano wa 1964, huku Tanganyika ikiwa inaendelea kuongozwa kwa muda na Rais ambae alitakiwa asimamie masuala ya muungano tu;

..kwa maana nyingine ni kwamba Tanganyika na Zanzibar zilikoma kuwa dola au nchi mbili tofauti, na badala yake zikaunda dola au nchi kubwa inayoitwa TANZANIA.

hazikukoma kuwa dola moja, bali zilibakia kuwa dola mbili, huku zanzibar ikipewa dola yake kwa mkono wa kulia, na kupokonywa kwa mkono wa kushoto, na huku Tanganyika ikiendelea kuongozwa na Rais ambae ilitakiwa asimamie masuala ya muungano tu; Nitarejea, umeme umekatika, nadhani nimeeleweka lakini; nitarudi kufafanua zaidi na kurudia nilichoandika kwani laptop inazima muda wowote;
 
Asante kwa mchango wako Joka Kuu,

Msingi wa hoja yangu ni katika mazingira ya Serikali tatu i.e. a federation, and not a unitary state kama ilivyo hivi sasa chini ya kiini macho hiki; Katika autonomy, nacholenga zaidi ni suala la fiscal autonomy - fiscal decentralization ambapo different states have the autonomy to set their own levels of taxes etc; Kwa mfano,Marekani is a Federal Republic with autonomous states, and each state ina fiscal autonomy; kabla ya Marekani kuamia kuwa na a federation, ilikuwa na a confederation na moja ya masuala ambayo yalileta mgogoro mkubwa sana uliotishia kuvunjika kwa confederation ile ilikuwa ni suala la fiscal autonomy ambapo baadhi ya states zilikuwa zinahisi kutotendewa haki; suala hili linajitokeza katika muungano wetu, lakini ni kwa sababu ya kiini macho nilichokijadili kuliko suala lingine lolote;

Ebu jiulize - Muungano wa aina gani huu ambao mwasisi wake aliweka bayana kwamba unaiga mfumo wa UK, na pale ulipoanza kupata msuko suko baada ya kujisahau kwamba Tanzania haiwezi kuwa nchi ya chama kimoja daima, likawa tatizo, na Judge Bomani akapewa kazi ya kurekebisha hilo na baadae kuja na ushauri wa kufuata system ya mgombea mwenza ya marekani ili isitokee/kuokoa aibu ya chama kimoja kushinda bara, na kingine kushinda visiwani hivyo kuvuruga mfumo wa rais na makamo wa rais?

Muungano wetu wa sasa mfumo wake ni wa ovyo, hauna any originality zaidi ya uchakachuaji na copy and paste ya US na UK; thats the bottom line; na kuupeleka towards serikali moja au kuubakisha chini ya serikali mbili kama sasa is only a disaster waiting to happen; We need serikali tatu kama kweli tuna nia ya kuokoa muungano wetu, na pia kudumisha amani na umoja; tuwajengee wajukuu zetu misingi ya wao kuja weka serikali moja baadae, tusiwe wabinafsi kutaka kuacha legacy kwa kukimbiza mambo ovyo; Rome wasn't built in a day;
Mchambuzi,

..Lakini ZNZ ina some autonomy at the fiscal level kwa maana ya kutoza kodi mbalimbali. kipo chombo kinaitwa Zanzibar Revenue board naomba uchunguze kina mamlaka gani huko ZNZ.

..kuhusu mfumo wa serikali 3 baadhi yetu tulishaona tangu zamani kwamba mfumo huo hauwezi kukidhi matamanio waliyonayo kizazi cha sasa cha Wazanzibari.

..Mimi nadhani tuwasikilize wa-ZNZ wanataka nini sasa hivi. Kwa mtizamo wangu hawataki muungano. Hizi lugha za "muungano wa mkataba" may be they r just trying to be diplomatic.

..zaidi, nadhani Tanganyika is too big kuwa na muungano na nchi ndogo kama Zanzibar bila kuwa na migogoro isiyokwisha.
 
Last edited by a moderator:
Ni muhimu ugundue kwamba Mkataba ule haukuwa final, ilitakiwa ndani ya mwaka mmoja izaliwe katiba itakayo simamia autonomy of each state; Articles zile zilikuwa ni kama katiba ya muda, lakini badala yake, mwaka 1965, katiba iliyokuja ikawa bado ni ya muda, na ikabakia hivyo kwa miaka 12; na ndani ya kipindi hiki, kilichokuwa kinaendelea ni udonoaji wa autonomy ya Zanzibar kwa kuzidi kuongeza orodha ya masuala ya muungano kinyume na mkataba wa muungano wa 1964, huku Tanganyika ikiwa inaendelea kuongozwa kwa muda na Rais ambae alitakiwa asimamie masuala ya muungano tu;
Tanganyika ilishaondolewa. Sasa Zanzibar nayo ilkuwa inaondolewa. Hilo ndilo lengo la muungano. Yaani kuwa na nchi moja na siyo federation of states.Ili tuimartishe muungano ni lazima Zanzibar ipoteze mamlaka yake na kuwa chini ya Tanzania. Kama haiwezedkani, basi tuache tu, kwa sababu si lazima na sioni umhimu wa kuwa na muungano kama upande mmoja hawataki kabisa kuwa na muungano.



hazikukoma kuwa dola moja, bali zilibakia kuwa dola mbili, huku zanzibar ikipewa dola yake kwa mkono wa kulia, na kupokonywa kwa mkono wa kushoto, na huku Tanganyika ikiendelea kuongozwa na Rais ambae ilitakiwa asimamie masuala ya muungano tu; Nitarejea, umeme umekatika, nadhani nimeeleweka lakini; nitarudi kufafanua zaidi na kurudia nilichoandika kwani laptop inazima muda wowote;
Nadhani hilo lilikuwa ni lengo zuri tu as long as wananchi wamekubali. Kulikuwa na Tanzania na Zanzibar, Tanganyika haikuwepo. Passport ya Tanzania ndiyo unaingia nayo Zanzibar na wazanzibari walitumia passport ya Tanzania kwenda nchi za nje.Hakukuweas na passport ya Zanzibar (was it?)
 
Asante kwa mchango wako Joka Kuu,

Msingi wa hoja yangu ni katika mazingira ya Serikali tatu i.e. a federation, and not a unitary state kama ilivyo hivi sasa chini ya kiini macho hiki; Katika autonomy, nacholenga zaidi ni suala la fiscal autonomy - fiscal decentralization ambapo different states have the autonomy to set their own levels of taxes etc; Kwa mfano,Marekani is a Federal Republic with autonomous states, and each state ina fiscal autonomy; kabla ya Marekani kuamia kuwa na a federation, ilikuwa na a confederation na moja ya masuala ambayo yalileta mgogoro mkubwa sana uliotishia kuvunjika kwa confederation ile ilikuwa ni suala la fiscal autonomy ambapo baadhi ya states zilikuwa zinahisi kutotendewa haki; suala hili linajitokeza katika muungano wetu, lakini ni kwa sababu ya kiini macho nilichokijadili kuliko suala lingine lolote;

Ebu jiulize - Muungano wa aina gani huu ambao mwasisi wake aliweka bayana kwamba unaiga mfumo wa UK, na pale ulipoanza kupata msuko suko baada ya kujisahau kwamba Tanzania haiwezi kuwa nchi ya chama kimoja daima, likawa tatizo, na Judge Bomani akapewa kazi ya kurekebisha hilo na baadae kuja na ushauri wa kufuata system ya mgombea mwenza ya marekani ili isitokee/kuokoa aibu ya chama kimoja kushinda bara, na kingine kushinda visiwani hivyo kuvuruga mfumo wa rais na makamo wa rais?

Muungano wetu wa sasa mfumo wake ni wa ovyo, hauna any originality zaidi ya uchakachuaji na copy and paste ya US na UK; thats the bottom line; na kuupeleka towards serikali moja au kuubakisha chini ya serikali mbili kama sasa is only a disaster waiting to happen; We need serikali tatu kama kweli tuna nia ya kuokoa muungano wetu, na pia kudumisha amani na umoja; tuwajengee wajukuu zetu misingi ya wao kuja weka serikali moja baadae, tusiwe wabinafsi kutaka kuacha legacy kwa kukimbiza mambo ovyo; Rome wasn't built in a day;
Unaweza kuwa na nchi mbili zilzoungana na zote zikawa na complete autonomy, mfano mzuri ni Inner Mongolia na China. Mfano ulioutumia wa US ni tofauti kidogo kwa sababu autonomy ya states za USA zipo highly debatable.Na Zanbzibar wana madaraka yote iliyonayo state yeyote ya Marekani. Zanzibar is a state within a State.
Kuhusu serikali tatu, labda ungetuelezea kivipi? Yaani bunge gani litaamua hilo? Kama ni bunge la JMT, huoni kuwa huo ni ukiukwaji wa katiba? kuruhusu kuongezwa au kupunguzwa vipengele kama mh. Lissu alivyodai.

Umesisitiza sana suala la serikali tatu, lakini hebu tupe maelezo zaidi ni kivipi zitausaidia muungano kiuchumi, kijamii na kisiasa.
 
Muungano wetu ni utata mtupu,nakubaliana na dhana ya kwamba wakomunisti kina Babu na Hanga walikuwa wakihofiwa na ndiyo maana mwingireza alimsaidia mwalimu kwenye hilo.

Lakini pia ni mwingereza huyo huyo alimsaidia Sultan kwa kumkabidhi uhuru wa watu wa Zanzibar.Na mapinduzi yalipofanyika,muungano ulikuwa ni for the better of British kwa kufear communism ya kina Babu,pamoja na Karume aliyekuwa akiogopa influence ya kina Babu,na yeye pia akajificha chini ya mwavuli huo wa ukomunisti kuutaka muungano na kuwa neutralise kina Babu.

Mwalimu yeye nia yake kiukweli inaonekana ilikuwa ni muungano kwasababu pan africanism "spirit" yake inaprove hilo.Tatizo ni means za muungano huo pamoja na hidden agendas za waingereza.Na ndiyo maana muungano ni kama ulilipuliwa lipuliwa tu.

Siyo muungano uliokubaliwa na wananchi wa pande zote kwasababu hilo haliwezekani given the fact that muungano ulifanyika miezi 3 tu baada ya mapinduzi.

Sheria ya mkataba wa muungano ya 1964 haikuwa na madhumuni mengine zaidi ya kuestablish ama kuthibitisha hati za muungano,pamoja na kubainisha mgawanyo wa madaraka chini ya muungano ie Rais na makamu wa rais,pamoja na muundo wa muungano na katiba ya muungano.Bunge la Tanganyika ndilo lilipitisha sheria hizo za muungano,na baraza la wawakilishi lilifanya kuthibitisha tu.

Pia ni ukweli kuwa Zanzibar hawakuwa na katiba,bali walikuwa na presidential decrees,na ndiyo maana wakai adopt katiba ya Tanganyika(adopted from colonial era) na kuitumia kama katiba ya muda kwenye kipindi cha mpito.

Katiba hiyo ni ya Tanganyika ya mwaka 1962,ambapo walifanya marekebisho kadhaa na kuweka cheo cha makamu wa kwanza wa rais ambaye ndiye rais wa Zanzibar na pia msaidizi wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika masuala yote ya kiutawala kwa upande wa Zanzibar,na makamu wa pili wa rais akiwa ni waziri mkuu na msaidizi wa rais(wa jamuhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar) kwenye masuala yote ya utawala upande wa Tanganyika na pia kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.Na ni katiba hiyo ya muda ya mwaka 1965 ambayo iliainisha maazimio 11 ambayo yalikubalika kuwa ni ya muungano na kwamba yatakuwa chini ya muungano kama alivyoelezea mh Lissu.

Utata mwingine ni kwamba,mkataba huo ulianisha uongozi chini ya utawala wa chama kimoja,lakini maajabu ni kwamba kulikuwepo vyama viwili,yaani TANU na ASP huko Zanzibar.

Utata mwingine ni pia hapo kwenye hizo nyongeza.Ni ukweli kwamba hayo makubaliano yaliyoongezwa kwenye katiba ya 1965 yalikiuka sheria ya muungano ya 1964?Kwasababu kiukweli,sheria za muungano zilitungwa na bunge la Tanganyika na baraza la wawakilishi hawakuwa na any say zaidi ya kuithibitisha tu pengine kwa shinikizo.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom