Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Sawa sawa; ni kama kiini macho kwenye katiba ya JMT (1965) ambayo iliingiza masuala la vyama, kinyume na makubaliano ya Mkataba wa Muungano, 1964, kwani katika masuala yale kumi na moja, suala la siasa au vyama halikuwepo; Lakini kwa uchakachuajia, TANU ikajipenyeza kwenye katiba ya nchi na kuiacha ASP solemba ilipotamka hivi:

3(1) Kutakuwa na Chama kimoja cha siasa katika Tanzania.
(2) Mpaka hapo Tanganyika African National Union (TANU) itakapoungana na Afro Shiraz party (ASP), chama hicho kwa Tanganyika kitakuwa Tanganyika African National Union (TANU) na kwa Zanzibar, kitakuwa ni Afro Shiraz Party (ASP).
(3) Shughuli zote za kisiasa katika Tanzania zitafanywa chini ya usimamizi wa Chama.
(4) katiba iliyoonyeshwa katika nyongeza ya kwanza ya katiba hii itakuwa Katiba ya Tanganyika African National Union (TANU) na katiba hiyo inaweza kurekebishwa wakati wowote (na masharti yaliyomo ndani yake na baada na Muungano wa Tanganyika African National Union na Afro Shiraz Party (ASP) kwa mujibu wa masharti yaliyomo ndani ya katiba hiyo;

Nadhani kiini macho na pia uchakachuaji hapa upo wazi, pamoja na madhara yake kwa Jamhuri ya WATU wa Zanzibar; Muhimu hapa pia ni kwamba, kwanza, Zanzibar ilikuwe held at ransom mpaka ikubali kuungana na TANU; Muhimu zaidi ni kwamba,wakati ASP wakijifikiria na utongozaji huu wa TANU kabla ya ndoa, miaka 12 ya kusubiriwa kusema NDIO NIMEKUBALI AU HAPANA, TANU ilikuwa ndio inaendesha Muungano,
Mgombea urais wa JMT alichaguliwa na nani?
Kumbuka kulikuwa na majina 801 mwaka 1965, na jina la JKNB ndo lililopitishwa. Ni kikao gani, cha chama gani kilipitisha jina hilo?
 
Hiyo ni intro ya articles of the union ya 1707 na inafanana neno kwa neno kwa asilimia 90 na ile ya 1964.

Mwaka 1707, uingereza na scotland viliungana kufanya falme moja(kingdom). Madaraka ya kuwa na serikali ya scotland yamekuja miaka 300 baadfa yta kuwa serikali moja.
Tofauti ya muungano wa England na Scotland kuunda UK na muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni :
Wakati UK ina/imebaki na nchi wanachama waliounda umoja huo. link bilakiinimacho
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, muda mfupi baadae yalifanywa mazingaombwe na sasa Tanzania inasemwa haina nchi wanachama wake.Zinaitwa sehemu tu au pande mbili za muungano. Ili kufanikisha kiini macho, jina Tanzania lilibuniwa na hapo ikawa mwisho wa kuisikia Tanganyika ikitajwa na mikakati ya kuifuta Zanzibar inaendelea.

Habari ya karibuni inayohusu muungano wa England na Scotland ni hii: gonga link kipimajotochamuungano

Je tutaiga hili wanalolifanya UK kama tulivyoiga mfano wa muungano wao na kuingiza uchakachuaji ?
 
Tunaweza ila tumia nywele kidogo (samahani) na ulinganishe miaka hamsini baada ya Scotland kuungana na England.
1. Kulikuwa na mabunge mangapi.
2.Falme (executive) ngapi?
3.Mahakama ngapi?
Baina ya England na Scotland.
Vinginevyo ni sawa na kuita mkoa wa Katavi kuwa ni nchi mwanachama.... mkuu sasa unaanza kuleta mazingaombwe.
 
Sasa hapa wa kutumia nywele ni nani? mkuu Kobello.

Ni wazi unaanza kukiona kiini macho.
Wakati Mchambuzi amefafanua vya kutosha kuonesha mfumo wa muungano kulingana na mkataba ulitakiwa wa shirikisho, umelipinga hilo.
Umeandika sehemu kuwa muungano ni wa serikali moja.

Kiini macho unakiona hapo. Scotland ni nchi ndani ya muungano wa Uk kama ilivyo England, pia Wales.

Wewe unasema Tanganyika imekufa.Utaifa wa Tanganyika umekufa. Unasema Zanzibar ni taifa lakini si nchi.

Kwa nini Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa na serikali mbili tokea uchakachuaji wa mkataba wa muungano ulipofanywa? kwa nini kuna Katiba mbili?

Kwa nini kuna mambo yaTanganyika, mambo ya Zanzibar na mambo ya pamoja(muungano) baina ya Tanganyika na Zanzibar?

Cameroon amesema hivi:"This is an important day for our United Kingdom, but you can't hold a country in the United Kingdom against the will of its people," Cameron said.
Hapo hutafanya spin. a country ni Scotland. Pia umeshakubali hapo nyuma kuwa kuna utaifa unaoitwa scottish.link tumianywelekidogosamahani

Muungano wa Tanzania ni wa nchi ngapi? Muungano wa Tanzania ni wa mataifa mangapi? Je haya mataifa yapo leo, na hizo nchi zipo ndani ya muungano huu wa kiini macho?

Sasa tutumie hizo nywele.
 
Tunaweza ila tumia nywele kidogo (samahani) na ulinganishe miaka hamsini baada ya Scotland kuungana na England.
England na Scotland.
Vinginevyo ni sawa na kuita mkoa wa Katavi kuwa ni nchi mwanachama.... mkuu sasa unaanza kuleta mazingaombwe.
Mazingaombwe mengine haya.

Kuna mechi za kutafuta nafasi kucheza kombe la dunia huko Brazil unafuatilia?

Katavi - Ilala

Croatia - Wales , Belgium - Scotland , Poland-England

Michezo ilopita ya Olympic London, UK ilishiriki kama Muungano na wanamichezo waliounda timu hiyo ya UK walitoka katika nchi wanachama wa UK.

Kwa nini Tanganyika haiwezi kushiriki kama nchi?
Kwa nini Zanzibar haiwezi kushiriki kama nchi?

UK ni nchi moja? au ni muungano wa nchi nne?

Link http://www.bbc.co.uk/sport/football/fixtures

Au utaendelea kusema kuwa England,Scotland na Wales sio nchi?
Zenyewe ni sawa na Katavi au Ilala?
 
Bara is too big kuungana na Visiwani bila migogoro!

Jawabu tujitenge kila nchi ijiunge na EAC kivyake!
 
Hii ni kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ibara ya 64 inayozungumzia - Madaraka ya
Kutunga Sheria:

64 (1) Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo mengine yote yahusuyo TANZANIA BARA, yatakuwa mikononi mwa Bunge.

(2) Mamlaka yoyote ya kutunga sheria katika TANZANIA ZANZIBAR juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano yatakuwa mikononi mwa Baraza la Wawakilishi.

Swali: Je, wapo wanao ona kiini macho katika maneno ya kijani na buluu?
 
Hii ni kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ibara ya 64 inayozungumzia - Madaraka ya
Kutunga Sheria:

64 (1) Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Bunge.

(2) Mamlaka yoyote ya kutunga sheria katika Tanzania Zanzibar
juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano yatakuwa mikononi mwa Baraza la Wawakilishi.

Swali: Je, wapo wanao ona kiini macho katika maneno ya kijani na buluu?

Ni makosa ya makusudi! Akili ni nywele!!!
 
Kwa kweli nimependa style yako ya uandishi na kuwa mkweli kwa mtazamo wako. Mimi na wewe naweza kusema tuko katika same page pengine route tu tafauti. Mungano huu umedumu sio kwa sababu ya uakinifu wa swerikali zote katika kutatua kero za muungano, naamini ni werevu wa wananchi wenyewe both visiwani na bara na udugu uliojengeka ndio uliosaidia muungano huu kufika miaka hii 48/49 ya sasa. Ukitazama kwa undani wanasiasa au viongozi wa nchi hii wamekuwa ndio chanzo cha kero zote za muungano kwa kuenda kinyume sio tu na mkataba wa muungano bali matashi ya wananchi.

Tulipofika hapa ni kwa sababu ya udanganyifu wa CCM juu ya muungano hasa mabadiliko yanayofanywa pande zote mbili kimnya kimnya bila ya ushirikishwaji wa mwenziwe ili kupata suluhisho la kudumu. Kwa sasa credibility ya Mzee Warioba ipo katika balance depending na outcome ya result zake juu ya ukusanyaji wa maoni. Tatizo moja kubwa ninaloliona kwa viongozi waliopita ni kuendekeza maoni binfasi badala ya kulinda demokrasia ya hoja za wananchi walio wengi. Katiba ijayo inaweza ikawa ndio nguzo ya kudumu ya muungano mpya yenye nguvu ya wananchi au ikawa ndio threat kubwa ya sio muungano tu bali hata amani na uutulivu tunaojivunia.

Katika miungano iliofanikiwa duniani ni hii ambayo imetowa uhuru mkubwa wa nchi husika kujiamulia mambo yake huku ikijengwa zaidi kwa huduma za wananchi, uimarishaji wa demokrasia, haki na sheria. Kama hatujakaa chini na kuwasikiliza wadau wanasemaje hasa juu ya muungano hatutafika na ubaya zaidi tutakuja jikuta tukiwa maadui wakubwa baina ya ndugu mkubwa na mdogo kama ilivyo Eritrea na Ethiopia. Tujenge muungani wa heshima baina yetu, maelewano, na upendo sio wa kuwanufaisha wanasiasa wachache huku azma nzima ya muungano ambayo lngo kuu ni maendeleo kwa wananchi ikawekwa nyuma.

hakuna Mzanzibari alie na akili timamu atakaepinga kuwepo kwa Tanganyika, Fact! Haikuwahi kutokea kwamba wazanzibari wakapinga kurejeshwa kwa Tanganyika na ukiangalia wengi ambao walicommit political assasination kutoka Zanzibar ni kwa sababu ya kudai kurejeshwa kwa Tanganyika. Ni tafauti kwa Bara ambapo hoja zote zinajengwa kwamba lazima tuwe nchi moja regardless maoni ya wananchi yanasemaje. Huku ndio kutapotuingiza katika janga kubwa zaidi la mifarakano ya kudumu kwa sababu hakuhitaji kuwa rocket scientist kujuwa mtazamo wa serikali moja unabebwa vipi na wazanzibari au kwa nini attempts zote za kuweka nchi moja kwa miaka 48 zimegonga mwamba.

Ulioyasema mengi nimekubaliana nayo, naamini muungano huu kutoka waasisi wenyewe walikuwa na interest tafauti wakati wakikubaliana kuungana, na ndio maana ukiangalia article of union iko wazi na haikuwa na mashaka, kila mmoja akijuwa mipaka yake ya utawala na uhuru wake, lakini ubabaishaji umeanzwa kwa kuizika tanganyika kwanza, then katiba iliokuja ikiwa na agenda tafauti na makubaliano ya awali na mwishowe haya tunayoyaona sasa.
 
Hivi kuna haja gani kwa nchi mbili disproportinal in size population na resources kama tanganyika na zanzibar kuungana kama sio kuzusha mgogoro usiomalizika? Kama moja haikubali kumezwa hapa ni kuzua mgogoro usiokwisha. Mimi naona utaratibu wa sasa ambapo zanzibar inakua na partial autonomy ni the best model, vinginevyo kama wazanzibari hawataki basi tupeane talaka tatu, yaani hakuna rejea. Wazanzibari wapewe kura ya maoni ili ku determine kama kweli hawataki muungano au ni hila za mabwana zao wa zamani kurejea kutawala. Hii mambo ya muungano inatupotezea muda tu. Sisi bara tunadhani hawa jamaa wako salama kwenye muungano kuliko wakiwa peke yao, lakini kama wanaona tofauti tuwaache tu waende zao. Msemo mzuri wa kiswahili..'Mtoto akililia wembe mpe'
 
Huyu jamaa nimemkubali.... anakwenda kwenye ukweli na uwazi
Hawa wanasiasa wetu kama hawakulitatua hili tatizo la mungano kiukweli na uwazi basi Tanzania tutaadthirika sana na huu mungano
 
Hivi kuna haja gani kwa nchi mbili disproportinal in size population na resources kama tanganyika na zanzibar kuungana kama sio kuzusha mgogoro usiomalizika? Kama moja haikubali kumezwa hapa ni kuzua mgogoro usiokwisha. Mimi naona utaratibu wa sasa ambapo zanzibar inakua na partial autonomy ni the best model, vinginevyo kama wazanzibari hawataki basi tupeane talaka tatu, yaani hakuna rejea. Wazanzibari wapewe kura ya maoni ili ku determine kama kweli hawataki muungano au ni hila za mabwana zao wa zamani kurejea kutawala. Hii mambo ya muungano inatupotezea muda tu. Sisi bara tunadhani hawa jamaa wako salama kwenye muungano kuliko wakiwa peke yao, lakini kama wanaona tofauti tuwaache tu waende zao. Msemo mzuri wa kiswahili..'Mtoto akililia wembe mpe'

Kwanini Tanganyika waone kuwa Zanzibar wako salama kwenye Muungano dhana hiyo ya kuwa Tanganyika ina jua lipi baya na lipi zuri kwa Zanzibar, ndio wazanbari hawaitaki, wanataka usawa kama nchi mbili zilizokuwa na uhuru kamili ambazo zimekubali kuungana zina sauti sawa katika muungano

Munganao wa kuwa mmoja mume na mwengine mke,mmoja anaweza kuamua mwengine aamuliwe huo sio muungano bali ni ukoloni,Tafakari
 
Chabuso usichukulie kama offense; kuwa mkweli na kuona hali halisi. Watu milioni 50 na watu milioni moja. Kama zanzibar ingekua na utajiri mkubwa pengine isingeuhitaji hata huo muungano ila hali ya zanzibar wakati wa muungano ilihitaji uhakika wa ulinzi. Sasa tumekua nchi moja kwa miaka 50 kwa nini tusiendelee kuvumiliana kwenye umaskini au utajiri kama ilivyokua tangu awali? Zanzibar siku zote imebakia na serikali yake inayoongozwa na rais ili kuendeleza utambulisho wake ndani ya muungano.
 
Mkuu, Hii ni hatma ya nchi na watu wake,ukichukulia kuvuliana Zanzibar imeshashavumilia mengi,mfano mdogo tu hizi zinazoitwa "kero za mungano",wazanzibari wameshapiga kelele sana kwa serikali ya Mungano lakini hakuna kilichofanyika.

Ule wakati wa "cold war" haupo tena Mrusi ameshasalim amri hakuna siasa za magharibi na mashariki, Zanzibar haitaki ulinzi tena,kama zanzibar itavamiwa basi itavamiwa na Tanzania bara au Kenya, na hicho kitu hakiwezekani kwa sasa kwani kuna mungano wa nchi za east Africa

Mkuu, Zanzibar ilipoungana na Tanganyika 1964 ilikuwa ni nchi tajiri katika afrika na Kati,hata Karume baba raisi wa kwanza wa Zanzibar alikuwa akigamba kwenye mikutano yake kuwa Zanzibar haidaiwi na kila mzanzibari hata wale wanaozaliwa wana dolla 5000 za kimarekani

Wazo zuri ni kwa Tanganyika kuwa na dola yake kamili na Zanzibar Dola yake,wanasiasa wanakaa mezani wanaweka mikataba nchi zetu ziishi vipi kiuchumi na kisiasa,hapo ndio mafanikio yatapatikana kwa nchi zote mbili Tangayika na Zanzibar
 
Hakuna tabu mkuu hata sisi Watanganyika tunaipenda nchi yetu sana kama Wazanzibari wanataka nchi yao hatupungukiwi kitu ila utulivu wa roho kwa kelele za kero za muungano.
 
Baada ya Lissu kuwasilisha, wabunge toka Zanzibar walisimama mmoja baada ya mwingine wakimshambulia kwa matusi, mengine ya nguoni!
 
Ni makala ndefu ngonja nipite kwanza na nitarudi kwa wakati muafaka kuisoma vizuri.
 
Baada ya Lissu kuwasilisha, wabunge toka Zanzibar walisimama mmoja baada ya mwingine wakimshambulia kwa matusi, mengine ya nguoni!

Itakuwa ni wabunge wa ccm,au hujui kama muungano huu ndio itikadi yao inavyotaka?
 
hoja ya kujadili upya muungano ni nzuri,maana ni kweli kuna vugu vugu la chini chini,ambalo tukilifumbia macho litaleta madhara kwa muungano wetu,ni vuzuri tujadili,ili kuuboresha zaidi.
Mwalimu nyerere alikuwa na nia nzuri kuhusu muungano wetu hilo halipingiki,ila lazima tuelewe pia,kwa wakati ule inawezekana pia hawa kuweka into concideration kwamba population za both,tanganyika na zanzibar zitakuwa zikiongezeka.
Tunawapongeza sana nyerere na karume kwa jitihada zao za dhati kabisa za kuleta muungano,ila tujaribu kutafutia ufumbuzi ufa zinazojitokeza kwa hivi sasa,na haya maswala hayapaswi kutatuliwa kisiasa.
 
Back
Top Bottom