Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kama Serikali ya CCM inapinga kweli ushoga basi ikafute kipengele cha Katiba kinachoinyima Serikali kuingilia faragha ya mtu

Alichojibu ndio msimamo wake Lisu.Mwandishi wa habari kazi yake kamaliza katimiza wajibu wake wa kiuandishi vizuri kabisa kama mwandishi wa habari proffessional kauliza swali professiona na amajibiwa na LIsu msimamo wake kwenye hilo.Muuliza swali wala hana kesi yoyote na hakuna wa kumushambulia kwa nini aliuliza.Ni haki yake kuuliz

Lisu Aliyejibu huyo ndie mumiliki na mwenye hatimiliki ya hilo jibu alilojibu
Alitoa ufafanuzi jinsi sheria inavyojieleza.
 
Kwa wajinga tu ndio wanaona kasema point

Ukisoma Katiba kile kipengele cha HAKI YA MTU utaona kana kwamba mtu an uhuru wa kufanya chochote.

Lakini mshike mtu makalio ndio utajua huna haki kikatiba pia.
Kama kufilana ni sehemu ya katiba yetu aseme ila asirushe ngumi
Jifunze kuelewa kuelewa kabla ya kuanza kubisha, kufanya vile ni kosa la shambulizi la aibu.
 
Tundu Lissu akiwa Arusha leo asubuhi imeibuliwa tena hoja ya ushoga na huu ndiyo msimamo alioutoa

"Wanaleta vihoja kuwa naunga mkono ushoga, katiba ya JMT inasema kila mmoja ana haki ya kulindiwa faragha yake, naunga mkono msimamo huo wa Katiba, siyo kazi ya Serikali kuchungulia kwenye vyumba vya watu, kama kweli wanapiga vita ushoga wafute hayo maneno."

Ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kama wataanza kuingilia mambo ya vyumbani kwa watu itafikia kipindi mtu ataulizwa "Wewe mbona hufanyi sawasawa"

MY TAKE: WANA CCM IFIKIE HATUA MUACHE SIASA ZA KIPUUZI
Rais yeyote anayechaguliwa anaapa kuilinda katiba. Na isitoshe ni lazima uelewe kuwa kila kinachoandikwa kwenye katiba lazima kifuatwe na Rais mteule na ndiyo maana anaapa.

Kwenye katiba nchi yetu haijauzungumzia ushoga kwa kuwa hawana kipimo cha kumjua shoga ili waliweke kuwa ni kosa. Mfano hao kina James hakuna mahali unaweza ku prove kuwa ni shoga.

Isipokuwa sheria imewekwa kuzuia usambazaji wa video na picha chafu ikiwemo za ngono na hiyo sheria waliipitisha kina Lissu bungeni. Hilo linabakia kama maadili ya mtu binafsi na Mungu wake. Sasa huwezi kumtuhumu Lissu kwa mapenzi ya jinsia moja wakati ndoa yake aliyofunga imehusisha jinsia mbili tofauti. Pia ana watoto na hajawahi popote kutamka hata mzaha tu kuhusu ushoga.

Nikupe mfano. Hivi Magufuli alipokuwa Dodoma kisha akamjibu yule baba kuwa aliyedai kuwa anamuota akamuuliza "Unaniota tukiwa kitandani au? Angekuwa amesema hivyo Lissu hata kwa mzaha tu nyie muda huu si mngekuwa mnamnyea kabisa!

Au leo Magufuli alipomuomba Sugu amsugue ingekuwa kasema hivyo Lissu si mngepeleka hadi malalamiko NEC? Mbona wao Chadema wala hata hawana ishu na hayo aliyosema Magufuli?

Ifikie mahali nyie CCM muache hizi siasa za kipumbavu!
Kama kuna watu wanaopaswa kuacha upumbavu ni hao Chadema na mgombea wao
 
Huu ni msimamo wa serikali ya Tanzania
 

Attachments

  • 2534685_IMG_20200929_104345.jpg
    2534685_IMG_20200929_104345.jpg
    45.6 KB · Views: 1
..kulawiti watoto sio ushoga?
Kaulize mahakama kuu kwanini waliachiwa ukutane na ushahidi mpya wa wale watoto waliotumika kusema uongo. Ukitoka hapo muulize Tundu wakati lowasa anatangazia umma kuwa angemuacha huru alikua na ushahidi gani na kwanini Tundu alishabikia?

Hii sio nchi ya kunyanyasa wanyonge tena
 
Complicated gani bwana wewe hebu acha siasa za kilevi!

It is either black or white!! Hiyo "complicated" wewe umeitoa wapi?

Kesi zote za jinai mimi nashughulika nazo lakini sikuwahi kuona shoga kashtakiwa popote!!

Unadhani wewe mataga una akili sana kuliko serikali?
Basi mkuu tusibishane sana Lisu kawaruhusu endeleeni hatawabughudhi
 
Ama kweli ukistajabu ya Musa utashsngaa ya firauni Leo hii tundu unaunga mkono ushoga kweli tutakuamini kweli hatuwezi kumpa nchi mtu Kama wewe
 
Mkuu inajulikana wazi ushoga hapa tz ni kitendo haramu, hakifai kwanza hata kutamka tu ni aibu kubwa.

Sasa anapotokea muhuni mmoja kisa kakutana na wahuni wenzie huko ubelgiji na kuanza kusema eti ni siuala la faragha inatia hasira sana.

Hizo haki za faragha huyo muhuni wenu inaonekana hajui.
Unaweza ukamtambua shoga kwa kumtazama?
 
Ametoka kwenye nchi ambazo zinazoruhusu iyo kitu hawezi kuacha watanzania tumfundishe kwa kutokumpa kura hata moja asije tupeleka kwenye ushoga
 
Kama huwezi kumtambua mwizi kwa kumtazama ni halili kusema ni ruksa kwao kufanya wanavyotaka?
Siwezi kujadili hizi hoja mfu. Nyie endeleeni na siasa zenu za maji taka. Nimekuuliza, ulimsikia Magufuli alivyomwambia yule mwanaume pale Dodoma?
 
Yani CCM wana hila sana wanataka kuwaambia watu eti kwa sasa Tanzania tatizo lililopo ni ushoga na wanataka mtu wa kupambana nalo. Hoja za kipuuzi na kilaghai ili kutaka tu kuwapumbaza watanzania na kuendelea kuwatesa na dhiki.
Ndiyo maana tunapaaza sauti zetu kupingana nao kuhusiana na hoja ya Ushoga.Propaganda hii ndiyo karata waliyobakiwa nayo kuwajaza Wananchi Hofu ili wajishebedue kuwa wao ni watetezi na wapinga Ushoga.Tuwaulize swali;CCM mtuambie mbinu gani mtatumia katika kupambana na Ushoga.
 
Yani CCM wana hila sana wanataka kuwaambia watu eti kwa sasa Tanzania tatizo lililopo ni ushoga na wanataka mtu wa kupambana nalo. Hoja za kipuuzi na kilaghai ili kutaka tu kuwapumbaza watanzania na kuendelea kuwatesa na dhiki.
Chadema mna mapungufu mengi sana pamoja na mgombea wenu, mnajaribu kutushawishi kwamba; mtaruhusu sera ya kuigawa nchi vipande vipande a.ka. majimbo, mkaenda mbali na kusema nyie hamtakusanya kodi isipokuwa mtaweka madini na rasilimali zingine ili kupata mkikopo ya kuendeshea shughuli za maendeleo na uendeshaji serikali.Leo mmekuja na mpya ya karne ya kuruhusu ushoga kwa kuubariki kama faragha. kwa haya madhambi; R.IP CHADEMA
 
Ndiyo maana tunapaaza sauti zetu kupingana nao kuhusiana na hoja ya Ushoga.Propaganda hii ndiyo karata waliyobakiwa nayo kuwajaza Wananchi Hofu ili wajishebedue kuwa wao ni watetezi na wapinga Ushoga.Tuwaulize swali;CCM mtuambie mbinu gani mtatumia katika kupambana na Ushoga.
Sheria zipo ndiyo maana shoga hawezi thubutu kujitangaza hadharani au kufunga ndoa hadharani, wanachofanya ni kuiba gizani na siku wakikamatwa hawatakua tofauti na majambazi yanayoendelea kupora kinyume cha sheria. Lakini chadema leo mmeithibitishia dunia kuwa hilo kwenu ni ruksa. Ndiyo maana mmeshindwa pia hata kuutambua muungano wa Tanzania na zanzibar mnadai hamna maslahi nao duuuuuuu mnahitaji kuombewa peo mchafu awatoke.chadema ni debe la petroli
 
Ama kweli ukistajabu ya Musa utashsngaa ya firauni Leo hii tundu unaunga mkono ushoga kweli tutakuamini kweli hatuwezi kumpa nchi mtu Kama wewe
COMRADE POLEPOLE amekwisha onya kwamba; something, some where is wrong with this man(LISSU)
 
Siwezi kujadili hizi hoja mfu. Nyie endeleeni na siasa zenu za maji taka. Nimekuuliza, ulimsikia Magufuli alivyomwambia yule mwanaume pale Dodoma?
Sasa hapa mwenye hoja mfu ni nani?

Magufuli alisema huyo mwanaume ni shoga?

Mkuu mshaurini Lisu kama katumwa, kashashindwa
 
Back
Top Bottom